MASUALA IBUKA

Magonjwa

Aina

  • malaria
  • mafua
  • macho
  • ngozi
  • meno
  • kifua kikuu
  • homa ya mapafu
  • kifaduro
  • zinaa (kaswede/syphilis)
  • kipindupindu
  • homa ya matumbo
  • homa ya mapafu
  • shinikizo la damu
  • ugonjwa wa moyo
  • matumbwitumbwi/machapwi
  • saratani
  • utapia mlo
  • ukambi/surua
  • tetewanga
  • homa
  • malale

Jinsi ya Kujikinga na Magonjwa

  • Kula chakula chenye virutubisho vyote na madini
  • Kutotumia chumvi, sukari au mafuta mengi
  • Kufanya mazoezi
  • Kupimwa mara kwa mara
  • Kupika vyakula vizuri
  • Kunawa mikono na macho
  • Kuchemsha maji au kuyatia dawa kabla ya kuyanywa
  • Kutozini au kutumia kinga
  • Chanjo kwa watoto
  • Kutochangia vifaa kama vitana na nyembe na mavazi ili kujikinga na magonjwa ya ngozi.
  • Kulala ndani ya neti iliyotiwa dawa
  • Kufyeka nyasi karibu na nyumba na kutupa mikebe iliyo na maji
  • Kuweka dawa kwenye vidimbwi ili kuua mbu
  • Kutotumia vileo kama vile pombe na sigara
  • Kuzuia kunyeshewa na mvua na kuvaa mavazi mazito wakati wa baridi au usiku
  • Kukohoa au kupiga chafya mtu akiwa ameziba pua na midomo na kutotema kikohozi ovyo
  • Kutubu dhambi, kujua Mungu na kuomba kwa afya ya kiroho

Ukimwi

  • Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya HIV unaofanya mwili kupungukiwa na kinga dhidi magonjwa.

Njia za Maambukizi

  • Uzinzi, ubakaji au ulawiti
  • Tohara ambapo ngariga anatumia kisu kimoja kwa watahiriwa wote
  • Kuchangia vifaa vyenye ncha kali k.v. nyembe, vinyoleo n.k.
  • Utumiaji wa sindano moja na vifaa vya upasuati ambavyo havijatiwa dawa au kutokoswa ili kuua viini
  • Wanawake kuambukiza watoto wakijifungua
  • Kuongezewa damu ambayo haijapimwa au haijapimwa vizuri.
  • Utumiaji wa dawa za kulevya kwa kujidunga kwa sindano moja
  • Ulevi kumfanya mtu kupotewa na utambuzi kisha kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa.
  • Kubusu mtu aliye na virusi ukiwa na vidonda kinywani
  • Wakati wa ajali watu walio na viini wanapojeruhiwa na kutokwa na damu na inafikia majeraha katika miili ya wasio na hivyo viini

Dalili

  • Kukohoa kwa muda mrefu
  • Kuendesha kwa muda mrefu
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Kukonda au kupoteza uzani wa zaidi ya kilo 10 kwa muda mfupi
  • Mwili kudhoofika/unyonge
  • Kunyonyoka nywele
  • Jipu lmwilini
  • Mwasho mkali katika ngozi
  • Vidonda kinywani na kooni
  • Homa na kutokwa na jasho jingi usiku
  • Magonjwa ya kifua kikuu na homa ya mapafu
  • Saratani ya ngozi
  • Kuvimba shingoni
  • Utaahira wa akili k.v. kusahau na kutokumbuka mambo

Madhara

  • Jamaa kuathirika kisaikolojia wakiona mtu wao akiteseka na ugonjwa
  • Vifo kwa kuzidiwa na ugonjwa
  • Huzuni baada ya mgonjwa kuaga dunia
  • Watoto kuachwa wakiwa mayatima baada ya wazazi kufa
  • Gharama kubwa ya kugharamia matibabu
  • Unyanyapaa/kutengwa/kubaguliwa
  • Ndoa kuvunjika kutokana na lawama
  • Ubakaji wa watoto wa kike ili kujitakasa
  • Kuathiri uchumi wa nchi pesa nyingi zinapotumiwa kununulia dawa za kupunguza makali hata za kifua kikuu
  • Serikali kupoteza wataalamu iliyogharamia elimu yao kulazimika kuajiri wataalamu kutoka nje kwa gharama ya juu sana

Jinsi ya Kujikinga

  • Kutofanya zinaa kabla na nje ya ndoa
  • Walioambukizwa kutumia dawa za kupunguza makali (A.R.Vs)
  • Aliyebakwa kupewa dawa za A.R.V kabla ya saa 72
  • Kuwapa mama waja mzito wenye virusi dawa kabla ya kujifungua kukinga mtoto
  • Ngariba kutotumia kisu kimoja kwa watahiriwa wote
  • Kutumia sindano mpya hospitalini na matumizi ya dawa za kulevya
  • Kupima damu vizuri kabla ya kuwaongezea wagonjwa
  • Kupimwa kabla ya ndoa na mara kwa mara ili kujua hali ili kujikinga dhidi ya maambukizi au kujitunza kama mtu ameambukizwa
  • Kutumia mipira
  • Walioambukizwa kutofanya mapenzi bila kinga ili wasipate virusi aina tofauti na sugu au magonjwa mengine ya zinaa
  • Kula chakula vinavyofaa na kufanya mazoezi
  • Kupata matibabu wakati ufaao mtu anapougua magonjwa mengine
  • Kumjua Mungu ili kumwamini na kumtumainia ili kuondoa uoga na mahangaiko na hivyo kumwezeha mtu kuishi siku zaidi

Unyanyasaji/Udunishaji wa Wanawake na Utamaduni/Taasubi ya Kiume

  • Kutorithi mali
  • Wanawake wajane kunyang’anywa mali na kufukuzwa
  • Ndoa za wake wengi (uke wenza)
  • Kupata watoto wengi
  • Kurithi wanawake
  • Kupashwa tohara
  • Kutawishwa au kunyimwa uhuru wa kutoka
  • Kutoelimishwa eti kwa akiolewa hatafaidi familia, atapanda wanaume vichwa au atakuwa malaya
  • Ndoa za mapema/lazima zinazosababisha kukatiza elimu yake (mahari haiwezi kurudishwa)
  • Kulazimishwa kuolewa na mtu asiyempenda
  • Kunyimwa haki ya kusema
  • Kupigwa na kutusiwa
  • kubakwa
  • Kutalikiwa
  • Wanaume kutokuwa waminifu kwao hata kuwanyima mahitaji na kuwapa mahawara zao
  • Wanaume kupuuza majukumu ya kukimu familia
  • Ubadhirifu wa wanaume na hali wake zao ndio walifanya kazi za kupatia hizo pesa
  • Kubughudhiwa
  • Kulaumiwa mtoto akikosekana hata mke mwingine kuolewa
  • Mahali pa mwanamke kuwa nyumbani au haruhusiwi kufanya kazi ofisini au kuongoza
  • Kulazimishwa kuvaa mavazi aina fulani na kukatazwa kuvaa aina mengine
  • Kufanyishwa kazi za nyumbani kama mtumwa
  • Kudhibitiwa na wanaume zao kwa sababu ya vivu.
  • Kunyimwa ajira kwa vile akipata mimba atajikokota kazini na atahitaji likizo baada ya kujifungua.
  • Ajira ya mtoto wa kike ambapo anafanyishwa kazi ya sulubu na kupewa mshahara duni

    Suluhisho

  • Hatua kali za kisheria kwa wanaowapiga, wanaowabaka na wanaotekeleza mila ya tohara na ndoa za mapema
  • Kufanya kampeni dhidi ya mila zinazochangia udunishaji wa wanawake
  • Kuwashauri watoto wa kike badala ya kuwapasha tohara
  • Kuanzisha makao ya watoto wa kike wanaotishiwa na mila mbaya
  • Kumwelimisha mwanamke kuhusu haki zake
  • Kuhimiza wanawake kupigania haki zao
  • Serikali kutenga pesa za kuelimisha watoto wa kike ili kuwapa uwezo wa kiuchumi kwani wengi hunyanyaswa kutokana na umaskini na ujinga.
  • Mashirika ya kutetea haki za wanawake kama FIDA na Maendeleo ya Wanawake.
  • Hazina ya kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake k.v. K.W.F.T
  • Kuwapa wanawake nafasi sawa za ajira na katika uongozi.
  • Kupunguza alama ambazo wasichana wanazopaswa kufikisha ili kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
  • Kubuni sheria za kuwawezesha kumiliki mali

    Jinsi Wanaume Wanavyodhulumiwa

  • Kupigwa
  • Kuchomwa kwa maji moto
  • Kukatwa sehemu nyeti
  • Wanawake kutokuwa waminifu kwao
  • Kutusiwa
  • Kutofuliwa nguo
  • Kunyimwa chakula
  • Kunyimwa unyumba kama njia ya kulipiza kisasi au kumwadhibu
  • Kufanyishwa kazi fulani k.v. kufulishwa nguo na kupikishwa mke akiwepo hata mbele ya wageni
  • Kuzomewa/ kugombezwa
  • Kunyimwa pesa kama hana ajira

    Ufisadi

    • Uovu, ubaya au uharibivu.

    Aina

  • Wanafunzi kudanganya katika mtihani
  • Kufanyiwa mtihani na watu wa nje
  • Kutoza mwanafunzi wa kidato cha kwanza pesa au chakula kama nyama ili kuwalinda.
  • Kujipakulia chakula kingi.
  • Waalimu wakuu kuitisha hongo ili kuruhusu wanafunzi wajiunge na shule zao
  • Kupita wengine katika foleni wanapokwenda kupata chakula au chai hata benki
  • Kurudishiwa bakaa/chenji nyingi dukani na kutoirejesha kwa muuza duka.
  • Kuokota pesa njiani na kutoulizia ni za nani
  • Kughushi stakabadhi za mtihani, hati za umiliki shamba
  • Kunakili kanda za muziki za wengine na kuziuza
  • Waajiri kuajiri watu wa familia zao au makabila yao
  • Daktari kuitisha hongo ili amhudumie mgonjwa
  • Polisi kuitisha hongo ili aruhusu magari ya huduma kwa umma yasiyofaa kupita
  • Kutohoa maziwa au kuyaongezea maji ili yawe mengi
  • Wenye maduka kuuza bidhaa kwa bei ghali
  • Kuuza bidhaa kama sukari, nyama, nafaka, gesi na mafuta ya petroli ambazo hazijatimiza uzani unaotakikana
  • Madereva wanaoendea mafuta ya petroli kuuza kiwango fulani cha hayo mafuta na kuongezea ya taa au diseli
  • Kuuzia watu dawa bandia zisizotibu magonjwa
  • Ulanguzi wa dawa za kulevya
  • Kuiba pesa kwa kutumia risiti bandia au kufuruisha bei za bidhaa ili pesa zilizo juu wahusika wagawane
  • Kutoa ushahidi wa uongo
  • Kunyang’anya wajane na yatima mali zao
  • Uporaji wa mali ya umma k.v. nyanja za kuchezea watoto na misitu
  • Hakimu kuchukua hongo aididimize kesi
  • Madaktari kutoza wawele ada ya juu hata kuwafanyia upassuaji wasiouhitaji ili wapate pesa.
  • Wafanyakazi wa halmashauri za miji kujificha wanapomwona mtu akiegesha gari ili wadai anakwepa kulipa ada ya uegeshaji ili wahongwe au walikokote gari wapate pesa zaidi.

    Sababu Ya Watu Kuushiriki Ufisadi

    ecolebooks.com
    • Tamaa ya kutajirika
    • Kutofahamu madhara/matokeo yake
    • Kukosa njia za kukimu mahitaji
    • Mishahara au mapato duni yasiyomwezesha mtu kukimu mahitaji yake au ya familia
    • Kutotosheka kwa kile mtu alichonacho
    • Hofu ya kupata hasara au kukosa ajira
    • Kutomjua mungu hivyo hawana imani
    • Kuzugwa au kutekwa nyara kimawazo na kuwa mtumwa na shetani
    • Wengine hulichukulia kama jambo la kawaida tu au hali ya maisha
    • Imani kuwa siku hizi mtu hawezi kupata chochote bila kutoa hongo

    Madhara

    • Vifo kutokana na aajali barabarani au kutotibiwa bila hongo
    • Majeruhi wa ajali za ajalini wengine hulemaa wasiweze kujifanyia kazi zao
    • Kufutiliwa kwa matokeo ya mtihani
    • Kufukuzwa shuleni au chuoni
    • Umaskini kutokana na utoaji hongo ya pesa nyingi kisha kutopata kazi na ununuzi wa bidhaa kwa bei ghali
    • Kushuka kwa viwango vya elimu wasiohitimu ipasavyo wanaporuhusiwa kujiunga na shule ama vyuo fulani
    • Kushuka kwa viwango vya huduma kwa umma kutokana na kuajiriwa kwa watu ambao hawajahitimu vizuri.
    • Afisi za serikali kuchomwa wafisadi wakijaribu kusitiri ushahidi wa ufisadi
    • Nchi kurudishwa nyuma kiuchumi na kimaendeleo kutokana na pesa za miradi au ambazo zingewekezwa katika vitega uchumi kuporwa
    • Kupoteza ajira baada ya kufutwa kazi kutokana na ufisadi
    • Familia kuteseka baada ya kupoteza ajira
    • Kufungwa jela kwa wanaopatikana na kosa la ufisadi
    • Uharibifu wa mazingira na madhara yanayoendana nao kutokana na ufyekaji wa misitu
    • Kudidimiza haki pale kesi inakatwa vibaya kutokana na hongo hata asiye na makosa aweza kufungwa
    • Viongozi wafisadi katika mashirika na asasi kupoteza nyadhfa

    Suluhisho/Njia za Kuukabili Ufisadi

    • Hatua kali kisheria kwa wafisadi
    • Kulipa wafanyakazi mishahara mizuri
    • Kuelimisha kuhusu madhara ya usisadi
    • Kufuta kazi wafisadi
    • Kunyang’anywa pesa au mali walizopata kifisadi
    • Watu kutangaza mali zao k.v. kwa kujaza fomu kudhihirisha hayo
    • Shirika la kukagua vipimo na ubora wa bidhaa
    • Majina ya wafisadi kutangazwa hadharani
    • Ukaguzi wa hesabu za matumizi ya pesa katika asasi za serikali
    • Shirika la kupambana na ufisadi
    • Kufumania wafisadi
    • Kupiga picha kwa kamera ya video wafisadi k.v. polisi wakichukua hongo
    • Kujifunza kutosheka kwa kile mtu alichonacho na kuishi maisha ya kiwango chake.
    • Kuarifu polisi au shirika la mkupambana na ufisadi kuhusu visa vya ufisadi
    • Kumjua na kumcha Mungu

    Dawa za Kulevya/Mihandarati

    • Dawa ambazo huathiri utendakazi wa mwili.

    Sababu za Kutumiwa

    • Masurufu au kuwapa vijana pesa nyingi za matumizi
    • Kujipa burudani
    • Shinikizo la rika kwa vijana
    • Ukosefu wa ushauri/kutojua madhara
    • Matangazo ya biashara
    • Shida k.v. ukosefu wa ajira na mahitaji ya kimsingi
    • Marafiki wabaya
    • Kukaa katika mazingira zinamotumiwa
    • Malezi
    • Kuvunjika kwa ndoa
    • upweke
    • Kujitoa haya k.m. makahaba
    • Shida kazini
    • Kudanganywa zina manufaa k.m. kumpa mtu nguvu ya kufanya kazi au kuerevusha
    • Kujipa hisia za kuwa huru na ujitambuaji

    Madhara

    • Magonjwa k.v. saratani na ya zinaa
    • Vifo kutokana na ajali, magonjwa au dawa zenyewe
    • Kuiba ili kupata pesa za kununulia dawa za
    • Ubakaji
    • Hufilisi watu kwa kutumia pesa nyingi hata kuuza au kuzikodisha mali zao ili kuzigharamia
    • Jamaa kuathirika kisaikolojia wanapoona mwenzao akiKushindwa kuendelea na masomo.
    • Visa vya ubakaji.
    • Kupotoka kimaadili k.m. kuwa mwenye matusi, kupiga wengine, kuwa mgomvi hata mzinifu.
    • Kuwa mchafu kama fungo k.m. kutooga, kutofua nguo, kutochanua nywele n.k.
    • Kuhisi mambo yasiyokuwepo (hallucination).
    • Wengine kushindwa kuolewa na kutoweza kupata watoto k.m. watumiaji wa miraa.
    • Kuvunjika kwa ndoa kutokana na kupiga mke, kutumia pesa vibaya.
    • Kufutwa kazi k.m. kutokana na ulevi.
    • Wazimu
    • Uhalifu
    • Jamaa ya mtumizi kuteseka ikimwona mwenzao akiangamia kutokana na kuzitegemea dawa za kulevya
    • Mhusika huathirika kimwili na kisaikolojia
    • Huathiri ukuaji wa mwili na akili
    • Wazimu
    • Huathiri uwezo wa kufikiri kwa kuua seli za ubongo
    • Hufanya mtu kupotoka kimaadili k.m. upyaro, vita, uchoyo, uzinifu
    • Kuvunjika kwa ndoa
    • Kufukuzwa shuleni
    • Kufungwa jela
    • Kuzaa watoto ambao hawajatimiza uzani wa wastani
    • Kufa kwa neva na viungo kukatwa

    Suluhisho

    • Kuelimisha watu kuhusu madhara ya dawa za kulevya
    • Watu kumjua Mungu
    • Matibabu ya kurekebisha watumwa wazo
    • Kujitenga na marafiki wabaya
    • Kutoingia katika mandhari zinamotumiwa
    • Maelekezo kuhusu dawa za matibabu kufuatwa ipasavyo
    • Kutotumia dawa za matibabu kwa matumizi mengine yasiyo ya kutibu
    • Ukaguzi wa wageni na mizigo katika viwanja vya ndege
    • Hatua za kisheria kwa walanguzi, wauzaji na watumiaji
    • Kuongeza nafasi za ajira
    • Kukomesha matangazo ya biashara ya dawa hizo
    • Kuandika matahadharisho katika chupa na pakiti za vileo

    Uhalifu/Utovu wa Usalama

    Chanzo

    • Umaskini kusababisha wizi na uisadi
    • Dawa za kulevya kusababisha wizi au kubaka
    • Marafiki wabaya
    • Malezi mabaya
    • Malezi mabaya k.m. mtoto akiiba na kupelekea wazazi, wazazi hawamuulizi alikotoa vitu hivyo.
    • Tamaa ya mali kufanya watu kuiba, kushiriki ufisadi, n.k.
    • Hasira au kushindwa kujidhibiti kusababisha kumpiga na kumuumiza mtu hata kumuua
    • Tamaa kubwa au uchu kusababisha ubakaji.
    • Chuki na wivu huweza kusababisha mauaji

    Suluhisho

    • Hatua kali za kisheria
    • Kuongeza askari kwani idadi yao ni dogo ikilinganishwa na raia
    • Kuunda vikundi vya kujilinda
    • Vituo vya polisi kuongezwa
    • Vitu vya thamani kuwekwa mahali salama k.m. benki
    • Kutotembea nyakati za usiku
    • Kutoendea mahali kusikofaa k.v. vichochoroni
    • Kuweka ua na lango
    • Mavazi yanayofaa kuzuia ubakaji
    • Kutoa mafunzo ya kujikinga
    • Nambari za simu za dharura za kuripotia uhalifu
    • Kumjua Mungu
    • Kuongeza nafasi za ajira

    Haki za Binadamu

    • Kuishi
    • Kuingiliana/kutangamana
    • Uhuru na usawa
    • Elimu
    • Makazi
    • Afya
    • Kiwango cha kurithisha cha maisha
    • Chakula
    • Kuabudu
    • Ajira ya watoto
    • Kufanya kazi
    • Kumiliki mali
    • Kutunzwa uzeeni/ hifadhi ya jamii/wasio na uwezo
    • Kupiga kura
    • Kutobaguliwa
    • Kutoteswa kuminya habari
    • Uhuru wa kuongea/usemi
    • Kutembea na kuishi popote
    • Kesi kuendeshwa kwa haki
    • Kujitetea
    • Kuoa au kuolewa na unayemtaka
    • Utulivu k.m. mtoto au mke asipigwe ama kuteswa
    • Huduma za matibabu
    • Jina na utaifa wakati wa kuzaliwa
    • Mtoto mlemavu apewe huduma maalum
    • Alindwe kutokana na mateso, kazi ya sulubu na kuhusishwa vitani
    • Alindwe dhidi ya mila na tamaduni zisizofaa
    • Haki ya kupata burudani
    • Haki ya faragha/ kuhifadhi siri zake
    • Asiajiriwe
    • asiteswe

    Jinsi ya kuwalinda na kuwatunza watoto

    • Sheria kubuniwa za kuwalinda
    • Hatua kali kisheria kwa wanaodhulumu watoto
    • Shirika la kupigania haki za watoto
    • Makao ya watoto wanaokimbia wa dhuluma
    • Hazina ya wizara na maeneo bunge ya kufadhili watoto maskini (bursary)
    • Watoto kuelimishwa kuhusu haki zao
    • Kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda mtoto
    • Elimu ya bure ili watoto maskini wafaidi
    • Shule maalum kwa watoto walemavu
    • Wananchi kuchanga kusaidia watoto maskini
    • Makanisa kusaidia watoto yatima
    • Shule kuwapa watoto maskini ufadhili

    Mazingira

    • Hali au mambo yanayomzunguka kiumbe katika sehemu anakoishi.

    Jinsi Yanavyoharibiwa

    • Kufyeka misitu ili kupata mahali pa makazi ama kulima
    • Kufuga mifugo kupita kiasi
    • Kutupa taka ovyoovyo
    • Moshi kutoka katika magari na viwanda huchafua hewa
    • Dawa na mbolea za kemikali za kilimo huchafua udongo na maji.
    • Migodi kuacha mashimo ardhini ambayo hujaa maji na kuwa hatari kwa binadamu na kizalio cha mbu.
    • Kelele za vyombo vya mziki, viwanda, honi za magari na ndege
    • mafuriko kuchanganya choo pamoja na maji safi
    • Taka kutoka nyumbani na viwandani kuelekezwa mitoni.

    Madhara

    • Ongezeko la joto duniani
    • Mvua za gharika
    • Uhaba wa mvua
    • Ukame na njaa
    • Uhaba wa maji
    • Kufa kwa wanyama wa majini kama samaki
    • Magonjwa na vifo kutokana na kuathiriwa na maji machafu
    • Magonjwa ya mapafu kutokana na hewa chafu

    Suluhisho

    • Kupanda miti kusiko na miti na kule misitu imefyekwa
    • Elimu kuhusu madhara ya kuharibu mazingira na jinsi ya kuyatunza Uhaba wa maji.
    • Kukagua viwabda na hatua za kisheria kama vinavyoachilia taka katika mazingira
    • Kutumia samadi badala ya mbolea za kemikali na dawa za kiasili kuua wadudu katika mimea na mifugo
    • Kutaifisha misitu
    • Askari wa kulinda misitu
    • Kutumia kawi mbadala na ambazo hazichafui mazingira k.v. kutokana na maji na jua
    • Mashimo na mapipa ya kutupa taka
    • Kuweka mifugo kulingana na eneo la malisho
    • Kutolima kando ya mito
    • Kutia choo cha binadamu dawa kabla ya kukiachilia mitoni
    • Kutumia magari ya umma
    • Kutumia taka kama malighafi na kutumia vile vitu vyaweza kutumika tena

    Usalama Barabarani

    Vyanzo vya ajali

    • Madereva kutohitimu vizuri
    • Magari mabovu
    • Kutotii sheria za barabarani
    • Njia mbovu
    • Kubeba abiria na mizigo kupita kiasi
    • Kuendesha magari kwa kasi
    • Waabudu shetani kusababisha magari kupoteza mwelekeo
    • Kupita magari mengine bila uangalifu
    • Ulevi
    • Wenda miguu kutokuwa waangalifu wanapovuka barabara
    • Kutodhibiti usukani vizuri
    • Uchovu kusababisha usingizi
    • Dawa za matibabu
    • Abiria kutolalamika au hata kumwambia dereva aendeshe kwa kasi wafike haraka
    • Kuchanganyikiwa

    Suluhisho

    • Hatua za kisheria kwa wakiukaji kanuni za barabarani
    • Kuondoa polisi wafisadi barabarani
    • Kukarabati barabara
    • Ukaguzi wa magari ili kuhakikisha yafaa kuwa barabarani
    • Kufunza madereva upya
    • Mikanda au mishipi ya kujifunga kuzuia kujeruhiwa vibaya na vifo ajali ikitokea
    • Kuweka vidhibiti mwendo
    • Vifaa vya kutambulia madereva walevi na kasi ya magari
    • Uangalifu wakati wa kupita magari mengine
    • Kuwa mwangalifu wakati wa kuvuka barabara

    Sayansi na Teknolojia

    • Uvumbuzi wa umeme unaotumiwa kuangazia na kuendesha vyombo vingi
    • Matibabu kuwezesha watu kuishi kwa muda mrefu k.m. dawa,chanjo, upasuaji, upachikwaji viungo, miale ya kutibu saratani, n.k.
    • Kurahisisha na kuharakisha usafiri k.m. magari, pikipiki, ndege, k.m.
    • Kurahisisha na kuharakisha mawasiliano kunakosaidia wakati wa dharura k.m. rununu, mtandao, nukulishi, n.k.
    • Upashaji wa habari kuwezesha kupata habari kutoka kote duniani k.m. satalaiti, mtandao, redio, runinga, n.k.
    • Utengenezaji bidhaa viwandani kuharakishwa kutokana na mitambo inazoendesha na tarakilishi
    • Mimea na mifugo wanaokomaa haraka na walio na mazao mengi
    • Roketi inayowezesha kwenda katika mwezi na sayari nyingine
    • Silaha kama bunduki za kupambana na maadui na wahalifu
    • Burudani bora k.m. sidi, video, mtandao, n.k.

    Madhara

    • Uavyaji mimba
    • Mauaji ya huruma
    • Tishio la dunia kuangamia kutokana na silaha za nuklia na viini vinavyotengezezewa maabarani
    • Uhalifu kuongezeka kutokana na wingi wa bunduki, simu na mtandao
    • Vyakula kutokana na mimea ina mifugo iliyokuzwa kisayanzi kudhuru afya
    • Wizi wa viungo vya mwili hata kuhasiwa bila hiari
    • Ajali za barabarani na za ndege zinazoua watu wengi
    • Upotoshaji kimaadili kama vile filamu chafu katika mitandao na sidi
    • Kutumia vijusi kutengenezea viungo
    • Ongezeko la joto duniani kutokana na uchafuzi wa hewa
    • Ugaidi kutokana unaotekelezwa kwa mabomu

    Simu za Rununu

    Faida

    • Kurahisha na kuharakisha mawasilano
    • Kupunguza gharama za usafiri
    • Mtandao huelimisha na hufahamisha habari
    • Kutuma pesa
    • Kuweka pesa/akiba
    • Burudani k.m. nyimbo, michezo
    • Kupiga nduru uhalifu unapotokeo
    • Ajira kwa wauzaji na watengenezaji
    • Ushuru kwa serikali
    • Shajara, kalenda, kamera, kikokotozi

    Madhara

    • Burudani kusababisha ajizi
    • Uhalifu
    • Gharama kubwa hasa kuweka chaji na malipo kabla ya kutumia kuongea au mtandao
    • Mtandao kupotosha kimaadili
    • Hutoa miale ambayo yaweza kusababisha saratani
    • Kudanganya katika mitihani
    • Kufungwa jela kutokana na arafa za vitisho na matusi

    Runinga/magazeti

    • Burudani
    • Habari
    • Ajira kwa wanahabari na watangazaji
    • Matangazo ya biashara
    • Kufunza maadili k.m. michezo ya kuigiza na vichekesho.
    • Kutuwezesha kufahamu sehemu nyingine za nchi na dunia
    • Kuelimisha k.v. vipindi vya fasihi
    • Utalii
    • Kuangazia sehemu na watu wenye shida
    • Kukuza lugha
    • Kukuza uzaleno

    Madhara

    • Ajizi
    • Kupotosha kimaadili
    • Filamu ziazohimiza watu kuwa wazinifu.
    • Matangazo ya vileo
    • Kuenezea chuki na propaganda
    • Kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa k.v. mavazi, talaka
    • Gharama ya kununulia
    • Kutopata muda wa kushauri watoto na kuomba
    • Wanafunzi kutosoma jioni
    • Mke na mume kutoongea kujadili mwelekeo wa familia
    • Wanaume kuchelewa kurudi nyumbani usiku wakitazama mpira
    • Migogoro kwa kutaka kutazama vipindi tofauti
    • Kelele na usumbufu kwa waliolala

    Utalii

  • hali ya kusafiri mbali ili kuvinjari au kufurahia mandhari

    Faida

    • Fedha za kigeni
    • Ajira katika hoteli, udereva, n.k.
    • Uhifadhi wa mazingira
    • Kuboreshwa kwa miundo msingi
    • Mapato kwa serikali kutokana na ada ya kuingilia mbugani na kodi za mikahawa
    • Amani na maelewano nchini na duniani
    • Kuhifadhi mila na tamaduni zetu
    • Kupa nchi umaarufu duniani
    • Maeneneo kame kuweza kutumiwa ipasavyo kama kivutio chao
    • Soko kwa mazao ya kilimo
    • Kuwapa wauzaji vinyago mapato

    Ubaya

    • Magonjwa k.v. ya zinaa
    • Matumizi ya mihandarati
    • Tabia zisizofaa k.v. Usenge zinazovunja ndoa na kueneza magonjwa kama ukimwi
    • Upuuzaji wa miradi ya maendeleo serikali ikijengea watalii hoteli za kifahari na viwanja vya ndege ambavyo hutumika kwa nadra sana
    • Kusababisha watoto kuacha shule ili wawe wanawaelekeza wapate pesa
    • Kuhimiza mauaji wa wanyama kwa kununua pembe na ngozi
    • Kelele za magari yao husumbua wanyama na kukanyaga na kuharibu lishe yao

    Jinsi ya kuvutia watalii zaidi

    • Kudumisha usalama
    • Kuimarisha miundo msingi
    • Kutangaza nchi na vivutio nje
    • Kupunguza malipo katika hoteli za watalii
    • Kufahamisha wananchi kuhusu vivutio kupitia vyombo vya habari
    • Kuongezea wafanyakazi mishahara ili kuweka akiba waweze kuzuru maeneo yenye vivutio
    • Kuwapa wafanyakazi likizo ya kutosha

    Umaskini

    Suluhisho

    • Kuongeza nafasi za ajira
    • Kutoa mikopo rahisi kulipa
    • Kupunguza bei ya pembejeo
    • Elimu ya bure
    • Kupigana na ufisadi
    • Upangaji uzazi ili kupunguza idadi ya watu
    • Bei bora ya mazao ya kilimo
    • Kazi kwa vijana

    Ukeketaji

    Sababu

    • Kupunguza tamaa
    • Njia ya kukomaa
    • Mila na tamaduni

    Madhara

    • Kifo kwa kutokwa na damu sana
    • Uenezaji wa magonjwa
    • Shida wakati wa hedhi na kujifungua
    • Ndoa kuvunjika
    • Kibali cha kujiingiza katika myenendo isiyofaa
    • Utengano kati ya waliotahiriwa na ambao hawajatahiriwa -migogoro
    • Kuzua utabaka baina ya waliopashwa na wasiopashwa tohara

    Suluhisho

    • Hatua za kisheria
    • Elimu kuhusu madhara
    • Mawaidha kwa wasichana
    • Makao ya watoto

    Njaa

    • Kilimo cha unyunyizaji maji
    • Kupunguza bei za pembejeo
    • Njia bora za kuhifadhi mazao
    • Mimea na mifugo inayokomaa haraka
    • Utumizi wa samadi na mbolea
    • Kuelimisha wakulima kuhusu kilimo bora
    • Kutayarisha mashamba mapema
    • Serikali kununua mazao ya wakulima na kuyahifadhi

    Dini

    Uzuri

    • Kufunza maadili
    • Kusaidia maskini
    • Kuanzisha shule na hospitali
    • Ajira kwa padri, kasisi n.k.
    • Kuandaa watu kwa maisha baada ya kifo
    • Kufariji/kuliwaza wenye dhiki

    Ubaya

    • Tamaa ya pesa
    • Biashara
    • Ubakaji wa watoto
    • Kuuza uponyaji
    • Nyingine kutosaidia wenye shida
    • Vita/jihadi
    • Kuruhusu waovu bora watoe pesa
    • Kutoenda hospitalini
    • Kuendeleza maovu k.v. uzinifu, ushirikina, uabudu shetani, n.k.

    Maasi ya vijana

    • dawa za kulevya
    • shiniko la kikundi
    • filamu mbaya
    • kudhibitiwa kupita kiasi
    • kukosa nidhamu
    • malezi mabaya/udekezaji
    • kubomoka kwa msingi wa jamii
    • Ufukara kusababisha kujiunga na makundi haramu
    • Kukata tamaa
    • Kutumiwa vibaya na wanasiasa

    Suluhisho

    • Kujiondoa kundini
    • Kuimarisha uchumi
    • Kuwashauri vijana
    • Kujenga udhabiti wa jamii
    • Kuwaadhibu kulingana na makosa yao
    • Vijana kujisaka na kujikosoa
    • Vijana kumjua mungu
    • Uhuru wa kadiri
    • Uongozi bora
    • Malezi bora
    • Kuongeza nafasi za ajira

    Umoja na Utangamano katika Familia

    • Kuheshimiana
    • Utiifu na unyenyekevu
    • Kuwa na usemi
    • Kuvumiliana na kusameheana
    • Uaminifu na kuaminiana
    • Kutochagulia watoto taaluma na wachumba
    • Wazazi kutolazimisha watoto taaluma au kozi wasizotaka
    • Kutumia pesa vyema bila ubadhirifu
    • Kutopendelea na kulinganisha watoto kiuwezo
    • kutotumia dawa za kulevya
    • Kuomba pamoja
    • wazazi kutopendelea watoto fulani
    • Baba kutimiza majukumu yake ya kukimu jamii
    • Kutodhibiti mke na watoto kupita kiasi
    • Uadilifu
    • Kushiriki kazi

    Mambo yanayoathiri utaifa/umoja na utangamano/amani

    • Ufisadi k.v. kuajiri watu kimapendeleo
    • Ukabila
    • Viongozi kueneza chuki
    • serikali kutoakisi uwakilishaji wa taifa zima
    • Usalama kukosekana
    • Ukosefu wa ajira
    • Matamshi mabaya ya viongozi
    • Kupanda kwa gharama ya maisha
    • Majanga ya kiasili
    • Kutojenga miundo msingi kwa usawa
    • Kupendelea maeneo fulani katika ugawaji wa raslimali
    • Ukimbizi wa ndani kwa ndani
    • Ubomoaji wa nyumba

    Suluhisho

    • Lugha ya taifa
    • Kukabiliana na ufisadi
    • Usawa katika ugawaji wa raslimali
    • Kuelimisha kuhusu umoja wa kitaifa
    • Tamasha za kitamaduni
    • Kutalii sehemu nyingine za nchi
    • Ndoa za makabila tofauti
    • Serikali ya muungano
    • Viongozi wachochezi kuchukuliwa hatua kisheria

    Matatu

    Faida

    • Kurahisisha na kuharakisha usafiri
    • Ajira
    • Ushuru
    • Biashara
    • Huduma za dharura

    Madhara

    • Ajali
    • Wizi
    • Ufisadi wa polisi kuongezeka
    • Kuongeza nauli ghafla
    • Ujeuri wa madereva na mataniboi
    • Kuchelewesha watu njiani

    Magazeti

    • Habari za taifa na kimataifa
    • Kuelimisha k.m. kuhusu afya
    • Kuburudisha k.m. vibonzo
    • Matangazo ya biashara
    • Ajira k.m. wahariri, wauzaji
    • Mapato kwa serikali
    • Kutangaza nafasi za ajira
    • Elimu k.m. uchambuzi wa vitabu vya fasihi na mashairi
    • Hutumiwa kufungia bidhaa

    Ubakaji

    • Sura mbaya
    • ulevi
    • Ulemavu
    • Unyonge wa kiakili
    • Kushindwa kudhibiti jicho na tamaa za mwili
    • Njaa ya kimapenzi
    • Kisasi
    • Kujihisi duni
    • Kisomo duni
    • Mavazi

    Athari

    • Waliobakwa huathirika kisaikolojia
    • Kujikosea heshima na kujihisi mchafu
    • Magonjwa ya zinaa
    • Mimba zisizotakikana
    • Vifo
    • kujeruhiwa
    • Kupoteza imani na wanaume/wanawake
    • Kutengwa
    • Kufungwa jela

    3. UTUNGAJI WA KISANII

    • Mashairi mepesi (huru/arudhi)
    • Hadithi fupi
    • Vitendawili
    • Mafumbo/chemshabongo
    • Vitanza ndimi
    • Michezo ya kuigiza

    Mambo ya Kuzingatia katika Uadishi wa Insha

  • maagizo
  • Usijibu swali usilolielewa
  • Uandishi mzuri wa nambari ya swali unalofanya
  • Kuandika vidokezi
  • Kuandika kila hoja katika aya yake
  • Kuanzia aya kwa njia tofauti
  • Lugha sahili
  • Miundo tofauti ya sentensi
  • maudhui
  • muundo
  • Kichwa kwa herufi kubwa, kipigwe mstari na kisizidishe maneni sita
  • Upatanisho/uwiano za kisarufi
  • Tahajia/hijai
  • Kuakifisha
  • Mtiririko
  • Uhalisi
  • tafsiri ya moja kwa moja k.m. kurudisha mlango, mguu wa gari, kutoa/kuweka nguo
  • Maadili (lugha na mawazo safi na mtazamo wa kusaidia taifa)
  • Urefu
  • Uasilia (utungo wako si kurejelea vitabu vya fasihi)
  • Usafi (mwandiko unaosomeka na ambao haujapigwapigwa mistari na kufutwa)
  • Tamathali za usemi
  • Msamiati na tamathali zinazokubalika wala si za kupachika. Usitumie msamiati wa kishairi k.v. mtima, ja, n.k.
  • Kutofupisha k.v. k.m., n.k., Bi.
  • Kutumia kistari ikiwa neno linaendelea katika mstari wa pili na kutokata silabi
  • Herufi f, u, i, j, m, l
  • Kutaja na kueleza kikamilifu
  • Kukamilisha maneno
  • Kutotenganisha sehemu za neno k.m. walilo zungumzia, walioenda
  • Kutounganisha maneno k.m. kwasababu, ni mimi
  • Mdokezo kuoana na maneno yako.
  • Usiongeze maneno kwenye dondoo la kumalizia.
  • Kutoweka dondoo ni kupotoka
  • Kusoma insha baada ya kuandika

    4. UANDISHI WAKAWAIDA

    Ufahamu

  • Kuelewa
  • Kuandika idadi ya hoja kulingana na alama
  • Hoja kwa muhtasari
  • Andika hoja ulizo na uhakika nazo kwanza
  • Kuorodhesha hoja kwa nambari wala si kistari
  • Jibu lililokamilika
  • Kutoa majibu kutoka katika ufahamu si fikra zako
  • Maana za maneno kama yalivyotumiwa kwa muundo ule ule

    Muhtasari/Ufupisho

  • Kutoa mawazo makuu huku kiini cha taarifa kikidumishwa.

    Hatua

    • Andika nambari za aya
    • Soma makala
    • Elewa swali
    • Andika mambo muhimu ukizingatia swali ukiondoa maneno yasiyo muhimu
    • Usibadilishe chochote hata kama unatakiwa kutumia maneno yako
    • Andika hoja kikamilifu
    • Andika nakala safi ukizingatia mtiririko
    • Epuka viunganishi vingi
    • Zingatia idadi ya maneno uliyopewa
    • Zingatia kanuni za uandishi
    • Piga mshazari nakala chafu

    Matumizi ya lugha

    • Kuzingatia sehemu za swali
    • Sehemu zinazobadilika
    • Kuzingatia neno moja moja
    • Kuzingatia hatua au mbinu
    • Kutojibu maswali kwa pupa
    • Kusoma jibu ili kusahihisha makosa
    • Kuelewa swali k.m. tunga sentensi moja, eleza maana
    • Tunga sentensi fupi
    • Kuonyesha neno, fungu la maneno au kiambishi unachotumia kutunga sentensi
    • Kubainisha (eleza kikamilifu kwa kuandika neno au maneno na jina lake)
    • Tahajia k.m. yabwa, kitendo

    Isimu jamii

    • Kutaja, kueleza na kutoa mifano

    Fasihi

    • Kufikiri ili kuelewa swali
    • Usijibu maswali zaidi ya manne. Kama jibu halikuridhishi, lipige mshazari
    • Maagizo (swali la kwanza ni la lazima, usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
    • Chagua maswali utakayoweza kujibu na kupata hoja nyingi
    • Andika nambari vizuri
    • Usiandike hoja nyingi kuliko alama
    • Andika hoja ulizo na uhakika nazo kwanza
    • Hoja kwa aya moja
    • Kutaja, kueleza kikamilifu na kuthibitisha kwa mifano kutoka kitabuni (kutaja alama moja, kueleza mbili)
    • Usirudie hoja kwa njia tofauti
    • Kutochanganya wahusika
    • Kusoma vitabu mara nyingi ili kujua dondoo limetolewa wapi
    • Maswali ya dondoo (msemaji, anayeambiwa, wapi, lini)
    • Maswali ya kujadili
    • Swali la methali
    • kulinganisha



');}
Bc0138c3d2dab0944d91d638547c2715

subscriber

2 Comments

  • 36152a58b3eb97f8e463bbe18882371e

    Sheldine, April 9, 2025 @ 9:49 amReply

    This is good for the students i bet now they would understand more about ushairi and insha

  • 36152a58b3eb97f8e463bbe18882371e

    Sheldine, April 9, 2025 @ 9:47 amReply

    T

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*