Share this:
 • Utungo unaoundwa kwa mfululizo wa sentensi zinazozungumzia jambo, tukio au kitu fulani

Aina

 1. INSHA ZA KAWAIDA
 • Insha ya Picha
 • Ambapo mwanafunzi amepewa picha kadha na kutakiwa kutunga kisa na kueleza yote yanayotokea kwenye picha hizo. Chunguza vizuri ujue kinachotokea katika hizo picha.
  • Kichwa kiafikiane na picha ulizopewa. Kila picha ipangwe na kuwa na aya moja.
 • Insha ya Methali
 • Insha inayosimulia kisa kinachoonyesha ukweli au uongo wa methali Fulani.
  • Wazia methali nyingine za kutilia mkazo methali uliyopewa.

Muundo

 • Kichwa
 • methali yenyewe
 • Utangulizi
 1. Maana ya juu/wazi
 2. Maana ya ndani/batini
 • Mwili
 • kisa kinachofungamana na methali cha kweli au cha kubuni
 • Hitimisho
 • funzo/maadili
  • Insha ya Maelezo
 • Inayohusu kutoa ufafanuzi kuhusu mahali, kitu au jambo fulani kama vile ugonjwa wa ukimwi, umuhimu wa maji, n.k.
  • Insha ya Masimulizi
 • Ambapo unatakiwa kusimulia hadithi, kisa au tukio kuhusu jinsi mambo fulani yalivyotokea. Huweza kuanzia kwa ‘Ilikuwa…’
  • Insha ya Mdokezo
 • Ambapo umepewa mdokezo wa kuanzia (xxx…) au kumalizia (…xxx) k.m. ‘…tangu siku hiyo alikula yamini kutopuuza ushauri wa wazazi wake tena’
  • Insha ya Mjadala
 • Ambapo unatakiwa kujadili suala fulani k.m. ‘Shule za mabweni zina manufaa’ au ‘Kujiajiri ni bora kuliko kuajiriwa’ Jadili.

  Unapaswa:

 • Kuunga
 • Kupinga
 • Kutoa uamuzi kutegemea upande ulio na hoja nyingi au nzito.
  • Insha ya Mawazo
 1. Inayohusu mambo ya kuwaza kuhusu jambo fulani k.m. ‘MIMI NYUKI’
 • Ni nani asiyenifahamu mimi nyuki.
 • Insha ya Mazungumzo
  • Maongeo ya kawaida ambayo huandikwa kama tamthilia
  • MAZUNGUMZO BAINA YA…

Muundo

 • Kichwa
 • Jina la msemaji kwa herufi kubwa likifuatwa na koloni
 • Maneno ya msemaji
 • maelezo ya mandhari na vitendo vya msemaji kwenye mabano
 • Wazungumzaji wasikike kama watu wa kawaida
 • Pawepo na sentensi ndefu na fupi
 • Matumizi ya vihisishi
 • Ukatizaji wa maneno…
 1. TUNGO ZA KIUAMILIFU
 • Ambazo hutekeleza kazi maalum na huwa na muundo maalum.

Dayalojia

 • Mazungumzo kati ya watu wawili au zaidi kuhusu jambo au mada fulani
 • DAYALOJIA BAINA YA…
 • Huwa na utangulizi, mwili na hitimisho

  Mahojiano

  • Mazungumzo yanayoendeshwa kwa muundo wa maswali na majibu
 • (MAHOJIANO BAINA YA…)

  Barua ya Kirafiki

  • Inayoandikwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

  Muundo

 • Anwani ya mwandishi (wima au mshazari. Jina lisiwekwe!)
 • Tarehe ya kuandikwa barua (22 Februari, 2011)
 • Mwanzo wa barua (kwa … mpendwa/kwenu…
 • utangulizi (salamu, kumjuliana hali)
 • mwili/yaliyomo (ujumbe)
 • Hitimisho (Kwa leo sina mengi. Wasalimie jamaa wote. Ni mimi wako/wenu, Jina (wima au mshazari)

  Barua Rasmi/Kwa Mhariri

 • Barua ambazo huandikwa na kutumwa ofisini kwa kutaka kuomba kazi, kuomba msaada, malalamiko, kutoa maoni gazetini, n.k.

  Muundo

  • Anwani ya mwandishi (wima au mshazari)
  • Tarehe ya kuandikwa (usiweke jina).
  • Marejeleo k.m. REJ: SUD/MSS/054/009 (nambari ya kumbukumbu, faili au nambari ya barua)
  • Cheo na anwani ya mwandikiwa k.m. Mkurugenzi, Kiwanda cha majani chai cha Kangaita, S.L.P, 12000, Kerugoya au Mhariri wa Gazeti la ‘Nation’, S.L.P 89000, Nairobi au KWA ANAYEHUSIKA
  • Kupitia kwa: MWALIMU MKUU, anwani
  • Mtajo k.m. Kwa Bwana/Bibi/Profesa/Daktari/Mhubiri
  • Kichwa cha barua k.m. MINT: OMBI LA KAZI YA UALIMU/MAPENDEKEZO KUHUSU JUMA MRISHO/ MWALIKO WA KUHUDHURIA KONGAMANO LA KISWAHILI
  • Utangulizi (Mintaarafu ya tangazo mlilochapisha…naandika kuomba…jinsia…ahadi kufanya kazi kwa bidii)
  • Mwili (matatizo, madhara, mapendekezo (naomba, paswa, stahili, naonelea ni bora)
  • Hitimisho (Natumai, Nitashukuru…Wako mwaminifu/mtiifu, sahihi, jina /cheo, Chama cha Kiswahili. Nakala kwa: (i), (ii) (wima au mshazari)

  Barua ya Gazetini Iliyohaririwa

  • Kichwa (kwa herufi ndogo na usemi halisi)
  • mtajo (Mhariri,)
  • Utangulizi (Naandika kueleza…)
  • Mwili (malalamiko, maoni, maombi, mapendekezo)
  • Hitimisho (Natumai…) jina na anwani ya mwandishi)

  Tahariri

 • Maelezo mafupi ya mhariri wa gazeti kutoa mawazo, maoni au msimamo wa chombo cha habari anachowakilisha kuhusu suala maalum na muhimu.

  Muundo

  GAZETI LA MZALENDO

  Februari 24, 2011

  ecolebooks.com

  HATIMA YA WATAHINIWA

  Yaliyomo

  Imeandikwa na…

  Hotuba

  • Maelezo yanayotolewa mbele ya watu.
  • Hutolewa kwa usemi halisi na huanzia na kuishia kwa alama za usemi.

  Muundo

  • Anwani (HOTUBA KUHUSU…)
  • Utangulizi (kutaja hadhira kuanzia walio mashuhuri, kuwasalimu, kujitambulisha na kuwakaribisha na kutambulisha kiini cha hotuba)
  • Yaliyomo (kutaja na kufafanua hoja)
  • Hitimisho (shukrani na kuwatakia mema katika shughuli zao za kila siku)

  Ratiba

  • Mpangilio wa jinsi shughuli fulani inavyofanyika kulingana na wakati fulani uliotengwa k.m. sherehe ya arusi, mazishi, siku ya michezo, kutoa zawadi n.k.

  Muundo

  • Kichwa (Ratiba ya shughuli gani, ya nani, mahali na tarehe, mgeni wa heshima: …Wageni mashuhuri: 1….2….3….)
  SAATUKIOMHUSIKA
  Asubuhi/adhuhuri Ku…/watu…
  • Makaribisho
  • Maombi
  • Kutoa tuzo
  • Kutoa shukrani
  • Kufungwa kwa maombi
  • Kuondoka/kufumkana

  Shajara

 • Daftari ambayo huhifadhiwa matukio yanayofanyika kila siku. Yaweza kuwa ya siku moja, wiki au mwezi mmoja.

  Aina

  • Ya kibinafsi

  JUMANNE 30/8/10

  Leo tulizuru…

  • Rasmi (hutumiwa katika ofisi)

  SHAJARA

  JUMANNE MEI 7, 2008

 1. asubuhi

Ku…

Onyo

 • Makatazo.
  ONYO!

  USISIMAMISHE WALA KUEGESHA GARI KWENYE ENEO HILI!

  Tahadhari

 • Julisho kuhusu jambo la hatari.
  TAHADHARI!

  DARAJA HILI LINA KASORO

  TAFADHALI USILITUMIE

  Ilani

 • Julisho, tangazo au notisi.
  ILANI

  TAFADHALI USITUMIE SIMU

  YA MKONO NDANI YA BENKI

  ILANI YA SERIKALI KUHUSU KUZUKA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

  Serikali imetoa ilani kwa wananchi kuhusu kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu. Kila mwananchi anatakikana kuzingatia mambo yafuatayo ili kudhibiti maambukizi.

 1. Mtu asinywe maji kabla kuyachemsha
 2. Kupika chakula hadi kiive vizuri
 3. Kutoenda haja nje bali kutumia vyoo vya mashimo
 4. Mtu anawe mikono yake kwa sabuni baada ya kutoka msalani
 5. Mtu asile matunda au mboga za majani bila kuziosha kwanza
 6. Anayeonyesha dalili ya ugonjwa wa kipindupindu apelekwe katika kituo cha afya mara moja.
 7. Uchuuzi wa vyakula umepigwa marufuku
 8. Ufuliaji nguo motoni pia umepigwa marufuku

Watakaokaidi maagizo katika (g) na (h) watachukuliwa hatua kali za kisheria ya kutozwa faini ya shilingi elfu tano au kifungo cha miezi miwili gerezani.

Matangazo

 • Majulisho kuhusu jambo fulani.
  • Arifa

   SHULE YA UPILI YA GATWE

   Anwani, tarehe

   USAJILI WA …

   Sahihi

   Jina

   Cheo

  • Kibiashara

  Sifa

  • Lugha kwa kifupi
  • Chuku
  • Takriri
  • Alama ya (!) na (?)
  • Michoro
  • Maonyo
  • Maelezo kukihusu
  • Kinavyotumika
  • Ubora wake
  • Watengenezaji
  JINUNULIE UNGA WA MAHINDI WA
  JAMBO SIKU YA LEO. UNGA WA JAMBO UMEONGEZEWA VITAMINI NA MADINI MUHIMU. BEI IMEPUNGUZWA KUTOKA SHILINGI 120 HADI SHILINGI 90. JIPAPIE PAKITI YAKO LEO KABLA BEI HII KUACHA KUTUMIKA
  • Kifo

   TANGAZO LA KIFO

   Tunasikitika kutangaza kifo cha …Alikuwa…

   Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi

  • kazi

   SHULE YA UPILI YA GATWE

   Anwani, tarehe

   NAFASI YA KAZI YA UHASIBU

   SIFA ZA MWOMBA KAZI

   JINSIA

   Awe wa jinsia ya kike.

   UMRI

   Awe na umri wa miaka isiyopungua25 na isiyozidi 40.

   ELIMU

 1. Awe na shahada ya uhasibu kutoka chuo kikuu au awe na shahada ya diploma ya juu ya uhasibu
 2. Awe amepata alama ya c katika kingereza

KAZI

 • Kuidhinisha hati za malipo za shirika
 • Kusimamia shughuli za uhasibu katika idara inayohusika

UZOEVU/TAJRIBA

Awe na uzoevu wa kazi usiopungua miaka 5 kwenye shirika au taasisi kubwa.

DINI

Awe muumini wa dini ya kikristu na awe ameokoka.

MUDA WA KAZI

Kuanzia saa mbili hadi saa kumi na moja jioni na masaa mengine ikibidi.

MSHAHARA

Mshahara utategemea elimu ya anayehusika lakini utakuwa baina ya ksh 24,000 na ksh 45000.

MAELEZO YA ZIADA

 • Maombi yote yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 30 mei 2010.
 • Maombi yatumwe kwa:

  Katibu,

  Halmashauri ya shule ya upili ya Gatwe,

  Anwani

 • Maombi yatakayopelekwa baada ya muda wa mwisho hayatajibiwa.
 • Maombi yaandamane na hundi ya shilingi elfu moja ambazo hazitarejeshwa.

Maagizo/Maelekezo

 • Maelezo kuhusu namna ya kufika mahali kutoka kituo fulani au maelezo kuhusu njia ya kutumia kitu au huduma fulani.

Sifa

 • Maelezo wazi
 • Michoro au ramani
 • Dira
 • Huhusika maonyo
 • Tarakimu k.m. 1×3
 • Matumizi ya herufi nzito.

Mifano

 • Maagizo ya daktari kwa mgonjwa wa kisukari.
 • Maelekezo ya kutoka nyumbani hadi shuleni mwenu.
 • Jinsi ya kutumia dawa za wadudu

Kujaza Fomu

 • Karatasi ambayo ina nafasi ya kuandika maelezo ambayo yanatakiwa.
 • Soma fomu kwa makini kabla ya kujaza chochote.
 • Andika maelezo kwa muhtasari.
 • Usijaze kama huna hakika kwenye sehemu Fulani.
 • Usifutafute.
 • Itumie alama inayostahili wakati wa kujaza fomu.

MAELEZO YA KIBINAFSI

TAREHE…………………………………………………………………………………………………………………..

JINA……………………………………………………………………………………………………………………….

JINSIA……………………………………………………………………………………………………………………

UMRI………………………………………………………………………………………………………………………

TAREHE YA KUZALIWA……………………………………………………………………………………………

URAIA…………………………………………………………………………………………………………………….

NAMBARI YA KITAMBULISHO…………………………………………………………………………………

KAZI……………………………………………………………………………………………………………………….

MKOA…………………………………………………………………………………………………………………….

WILAYA………………………………………………………………………………………………………………….

SIMU……………………………………………………………………………………………………………………..

SAHIHI………………………………………………………………………………………………………………….

TAREHE…………………………………………………………………………………………………………………

Hojaji

 • Maswali ambayo hutumiwa kama msingi wa kufanyia utafiti na huelekezwa kwa mhojiwa.

Aina

 • Hojaji Wazi
  • Hojaji yenye maswali ambayo mhojiwa anaruhusiwa kuyajibu kwa maneno yake mwenyewe.

  UCHAGUZI NA VIONGOZI

 1. Una maoni gani kuhusu uchaguzi wa kila baada ya miaka mitatu? …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 2. Kwa nini una maoni hayo? …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 3. Wewe ungependelea utaratibu gani wa uchaguzi? …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 4. Je ni kweli viongozi hung’ang’ania mamlaka? ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
 5. Je viongozi hung’ang’ania uongozi kwa sababu zipi?
 • …………………………………………………………….………………………
 • ……………………………………………………………………………………
 • ……………………………………………….….…………………………….….
 • Hojaji Funge
 • Hojaji ambapo mhojiwa anapewa majibu kadha ambayo anatakiwa kuchagua mojawapo bila kuwa na uhuru wa kuandika atakayo.
 • MATATIZO YA KIJAMII

  Tia alama kwenye jibu unaloafiki

 1. Jamii yetu inawakandamiza wanawake?

  Ndiyo ( ) La ( )

 2. Tatizo kubwa la jamii yetu kwa sasa ni umaskini na ugonjwa.

  Kweli ( ) Si kweli ( )

Mialiko

 • Barua ambayo hupeleka taarifa kwa mtu kumuomba ahudhurie sherehe fulani.
 • Rasmi (kadi au barua rasmi)

Muundo

 • Jina la mwalikaji/waalikaji (Bwana/mabwana/bibi/kasisi/daktari
 • Jina la mwalikwa
 • Sherehe (ndoa, mchango wa pesa, Kuna aina mbili za mialiko.
 • Kusherehekea/kuadhimisha…)
 • Kuhusu nani
 • Mahali pa kukutanika
 • Tarehe
 • Wakati
 • Anwani na nambari ya simu ya mwalikaji ambapo jibu litapelekwa kushoto chini (Majibu kwa…wima)
 • Kirafiki (barua ya kirafiki)
 • Sehemu ya mwili itoe habari zote muhimu katika mwaliko.

  Risala

 • Taarifa inayotoka kwa mtu au watu inayoeleza haja fulani k.m. risaala ya rambirambi, risala ya heri njema, ya waajiriwa kwa mwajiri au kinyume.

  RISALA YA RAMBIRAMBI/HERI NJEMA KWA…KUFUATIA

  Mimi wako…

  Resipe

 • Jumla ya hatua na kanuni ambazo hufuatiwa na mtu anayenuia kupika au kuandaa kitu fulani.

  UPISHI WA PILAU

  Walengwa/walaji

  Mipakuo mine (kwa watu wanne)

  Viambata

 1. Vikombe viwili vya mchele
 2. Gramu 25 za mafuta ya majimaji
 3. Vijiko viwili vidogo vya pilau masala
 4. Nusu kilo ya nyama
 5. Vitunguu vinne vya ukubwa wa wastani
 6. Vikombe vinne vwa maji

Hatua za Upishi

 • Kaanga vitunguu katika mafuta hadi rangi yake ikaribie rangi ya udhurungi
 • Chemsha nyama pekee hadi ilainike
 • Ongeza nyama kwenye sufuria yenye vitunguu na upike kwa dakika tano
 • Ongeza mchele na uchanganye kwa mwiko
 • Ongeza maji na uache mchanganyiko utokote kwa dakika kumi na tano
 • Pakua pilau ikiwa tayari

Orodha Ya Mambo

 1. Mlolongo wa vitu vilivyoandikwa.

  MAHITAJI MUHIMU YA KURUDI SHULENI TAREHE 5/1/2010

 • Sukari kilo mbili
 • Dawa ya meno ya gramu hamsini
 • Koko gramu 500
 • Sabuni sita za kipande
 • Kalamu nne za rangi
 • Penseli moja
 • Rangi ya viatu ya gramu 40

Tahakiki

 1. Maandishi ya kuchambua maandishi ya fasihi.

  USASA WAKUTANA NA UKALE

  Anwani: Kitumbua Kimeingia Mchanga

  Mwandishi: Said A. Mohamed

  Mchapishaji: Oxford University Press

  Mhakiki: Amina Fuzo

  Maudhui

  Meme

 2. Barua ambazo huhusisha matumizi ya ya vifaa vya umeme kama talakilishi, kiepesi/nukulishi/faksi au simu ya mkonono/tamba/rukono.

  Barua za Mdahilisi/Pepe

 3. Ambazo hutumwa kwa tarakilishi kwa njia ya mtandao.

  Ijumaa Machi 30, 2007 saa 08:09:19

  Kutoka: [email protected]

  Kwa: ahmed@african online.ke

  Nakala kwa: amina @ mwananchi.com

  MINT/KUH:

  Barua ya kawaida

  Hitimisho: Aisha Kizito Makwere

  Memo

 4. Taarifa fupi ambayo huandikwa ofisini kuhusu mambo ya ndani kutoa maelekezo, maelezo au kukumbusha kuhusu jambo fulani. Ujumbe huwa mfupi na huhusu suala moja tu.

  SHULE YA UPILI YA GATWE

  Anwani

  MEMO

  REJ: km/01/06

  KUTOKA: Mwalimu Mkuu

  KWA: wafanyakazi wote

  MADA: likizo fupi

  TAREHE: 28/2/2011

  Ujumbe

  Sahihi

  Jina

  Cheo (mwalimu mkuu)

  Taarifa

 5. Kuarifu kuhusu habari mpya

  UCHOCHEZI

  Hitimisho

  Mariga Mununga

  Mwanahabari

  Wasifu

 6. Maelezo ya mtu kuhusu mtu mwingine tangu kuzaliwa mpaka alipo au kufa kwake.

  WASUFU WA NDUGU YANGU JUMA

  Tawasifu

 7. Maelezo ya mtu kujihusu

  TAWASIFU YANGU

  Vidokezo

 • Jina lake/lako
 • Jinsia
 • Anakotoka
 • Umri
 • Kuzaliwa
 • Maumbile
 • Elimu
 • Kazi
 • Hadhi ya ndoa
 • Lugha
 • Lakabu na sababu
 • Umaarufu
 • Uraibu

Wasifutaala/Wasifu Kazi

 • Maelezo rasmi kuhusu mtu binafsi ambayo huambatanishwa na barua ya kuomba kazi.

WASIFUTAALA WANGU

MAELEZO BINAFSI

Jina : Farida Almasi Juma

Tarehe ya Kuzaliwa : 7-6-1980

Umri : miaka 22

Mahali pa kuzaliwa : Voi

Jinsia : mwanamke

Hadhi ya ndoa : Nimeolewa/kapera

Nambari ya kitambulisho : 12345678

Uraia : Mkenya

Lugha : Kiswahili, Kingereza, Kikuyu

Anwani ya kudumu : S.L.P. 1600, Voi

Barua pepe : [email protected]

Simu tamba : 9876543210

ELIMU

 1. Chuo Kikuu cha Maseno (Shahada ya Uhasibu)
 2. Shule ya upili ya Shimoni (Shahada ya KCSE)

  1978-1987 Shule ya Msingi ya Umazi (shahada ya KCPE)

  TAJRIBA

  Mpaka sasa Mhasibu katika shule chekechea ya Mtakatifu Yohana

  HABARI ZA ZIADA

  URAIBU

 • Kusoma vitabu vya sarufi na fasihi
 • Kutembelea wajane, mayatima na wagonjwa
 • Kuandika mashairi

AZIMIO LANGU

 1. Kupaa kitaaluma kwa kuendeleza masomo yangu hadi kiwango cha uzamifu
 2. Kuwa mhasibu bora zaidi nchini kwa matendo na kuwapa wananchi huduma za kufaa

WAREJELEWA

 • Profesa Hassan Muoso,

Chuo Kikuu Kenyatta,

S.L.P.43844,

Nairobi.

 • Maimuna Njavu Mukota,

Shule ya Upili ya Alliance,

S.L.P. 1 234,

Nairobi.

Kumbukumbu

 • Maelezo kuhusu yaliyojadiliwa na kuafikiwa katika mkutano.

Muundo

 • Kichwa (kumbukumbu za mkutano wa kamati/jopo gani, uliofanyika wapi, tarehe gani, saa ngapi hadi gani na majira)
 • Waliohudhuria (mwenyekiti, katibu, mweka hazina, wanakamati)
 • Waliotuma udhuru kwa kutohudhuria
 • Waliokosa kutuma udhuru wa kutohudhuria
 • waalikwa
 • Ajenda
 • Kufunguliwa kwa mkutano (KUMB 3/2OO9)
 • Kufunguliwa kwa mkutano, mwenyekiti kuwakaribisha na kuwashukuru waliohudhuruia na kumwomba … aongoze kwa maombi.
 • Kusoma na kudhibitisha kumbukumbu za mkutano uliotangulia
 • Kusomwa na katibu, aliyependekeza na aliyedhibitisha.
 • Masuala yaliyotokana na kumbukumbu hizo
 • (a) KUMB 8/2008 ununuzi wa miti
 • Shughuli nyinginezo
 • Kufunga mkutano (KUMB 7/2009)
 • Mkutano uliisha saa ngapi, maombi yaliongozwa na nani, na mwingine ukapangwa kuwa wa siku gani.
 • Maneo kama walikubaliana, waliafikiana, alipendekezwa, ilisemekana, waliambiwa, ilionelewa ni bora, walishauriwa, ilidaiwa, aliomba, n.k.

THIBITISHO

KATIBU TAREHE…………… SAHIHI ……………

MWENYEKITI TAREHE ……………. SAHIHI ……………

Ripoti

 • Maelezo kuhusu mtu, kitu au tukio
 • Ripoti ya Kawaida
 • Swali huanzia kwa ‘Wewe kama katibu wa chama…’

  Muundo

  • Kichwa (ripoti ya kamati/jopo gani)
  • Utangulizi (maelezo mafupi ya jumla kuhusu chama)
  • Shughuli za chama (i, ii, iii)
  • Hitimisho (matumaini, mwito kwa wengine wajiunge, wajitahidi)
  • Ripoti imeandikwa na (jina, cheo/katibu, sahihi, tarehe)
   • Ripoti Maalum
  • Kichwa (ripoti ya jopo la kutathmini usalama barabarani)
  • Utangulizi/Hadidu za rejea (ripoti ilihitajika na kamati gani, uchunguzi ulifanywa kubainisha nini, matokeo kuelezewa chini pamoja na mapendekezo kutolewa)
  • Jopo (majina na vyeo vya wanajopo waliohusika)
  • Utaratibu/ hatua za utafiti (wanakamati walifanya nini (kamati iliwahoji…ilifanya ukaguzi wa magari, iliwapa baadhi ya wasafiri hojaji wakajaza, ilipiga picha za video, mashauriano)
  • Matokeo (kamati iligundua kuwa: (a)
  • Mapendekezo (suluhisho la shida)
  • Hitimisho (ripoti imeandikwa na, sahihi, jina, cheo/katibu, tarehe 21 Machi 2011.
 1. UTUNGAJI WA/INSHA ZA KISANII
  1. michezo ya kuigiza
  2. hadithi fupi
  3. mashairi
  4. mafumbo
  5. vitanza ndimi

USHAIRI

Istilahi za Kishairi

 • arudhi
  • sheria za jadi zzinazofuatwa na watunzi wa mashairi:
 1. kugawa shairi katika beti
 2. beti kugawika katika mishororo inayolingana kiidadi
 3. mishororo kugawika katika vipande
 4. mishororo kuwa na mizani zinazolingana kiidadi (urari wa mizani)
 5. kuwa na vina vya kati na vya mwisho vinavyotamkika kwa namna sawa (urari wa vina)
 6. mtoshelezo wa beti au beti kutoa wazo kamili
 • bahari
  • aina tofauti tofauti za mashairi k.m. ukara
 • ubeti/beti
 1. kifungu katika shairi kinachojitosheleza kimaaa
 • mshororo
  • mstari katika ubeti
 • mwanzo
  • mshororo katika ubeti
 • mloto
  • mshororo wa pili katika ubeti
 • mleo
  • mshororo wa tatu katika ubeti
 • kimalizio
  • mshororo wa mwisho ambao haurudiwi katika kila ubeti
 • kibwagizo/mkarara/kipokeo/kiitikio
  • mshororo wa mwisho ambao hurudiwarudiwa katika kila ubeti na hubeba maudhui au kiini cha shairi.
 • kipande/mgao
  • sehemu katika mshororo ambayo huonyeshwa na koma na huwa na kina
 • ukwapi
  • kipande cha kwanza katika mshororo
 • utao
  • kipande cha pili katika mshororo
 • mwandamizi
  • kipande cha tatu katika mshororo
 • mizani
  • silabi zinazotamkika katika mishororo
 • urari wa mizani
  • kuwepo kwa idadi sawa ya mizani katika mishororo
 • kina/vina
  • silabi zinazotamkika kwa namna sawa zinazopatikana katikati na mwishoni mwa sentensi.
 • urari wa vina/vue
  • kuwepo kwa silabi zinazotamkika kwa namna sawa

Aina za Mashairi

 • mashairi la arudhi/ushairi wa kijadi
 1. Ambayo huzingatia sheria za jadi za utunzi wa mashairi.
 • mashairi huru
  • Ambayo hayazingatii sheria za jadi za utunzi wa mashairi.

Mashairi ya Arudhi

 • Aina
  • tathmina (mshororo mmoja katika kila ubeti)
  • tathnia (miwili)
  • tathlitha (mitatu)
  • tarbia (minne)
  • takhmisa (mitano)
  • tasdisa (sita)
  • ushuri (kumi)
 • Bahari
  • mtiririko (mfanano wa vina vya kati na vya mwisho katika shairi zima)
  • ukara (vina vya mwisho kufanana na vya kati kutofautiana)
  • ukaraguni (vina vya kati na vya mwisho kutofautiana katika shairi zima)
  • kikwamba (mishororo kuanza kwa neno fulani katika shairi zima)
  • pindu (neno au maneno mawili ya mwisho ya kila mshororo kutumiwa kuanzia mshororo unaofuata) k.m. kicha changu wachezea. Wachezea kichwa changu.
  • Tenzi/tendi (mgao mmoja, kina kimoja)
  • Mathnawi (migao miwili, vina viwili)
  • Ukawafi (migao mitatu, tumbuizo 8,8,8)
  • Ngonjera (majibizano)
  • Malumbano (kujinaki/kuonyesha ugwiji akimdunisha mshairi mpinzani ili kutaniana)
  • Msuko (mshororo wa mwisho mfupi kuliko inayotangulia)
  • Sakarani (mchanganyiko wa bahari)
  • Dura mandhuma (kauli/swali katika ukwapi na mjalizo/jibu katika utao k.m. shida zikishinda, hazishindiki. Unalolipenda, halipendeki. Unapopaenda, hapaendeki)
  • Gungu (mizani 12, kina kimoja cha mwisho)
  • Upeo (mishororo inayozidiana ki mizani)
  • Kikai (mizani 12, 4:8 au 8:4, hakuna ulinganifu wa mizani katika ukwapi na utao)
  • Zivindo (hutoa maana tofauti za neno k.m.
  • Sumbila (kila ubeti una kimalizio tofauti na beti nyingine)
 • Muundo/Umbo/Sura ya Nje
  • Kutaja idadi ya beti
  • Mishororo mingapi katika kila ubeti
  • Vipande vingapi katika kila mshororo-aina
  • Mpangilio wa mizani na jumla k.m. ukwapi 8, utao 8, jumla 16.

   8 8

   8 8

   8 8

   8 8

  • Mpangilio wa vina au kufanana, kutofanana katika shairi zima au vina vya mwisho kufanana na vya kati kutofautiana-bahari

   na ma

   na ma

   na ma

   ka ba

Vina na Mizani

8a 8b

8a 8b

8a 8b

8c 8b

 • Kibwagizo(linacho au halina. Kinakili kama kipo)
 • Majibizano (ngonjera)
 • Malumbano (majinaki)
 • Uhuru/Idhini za Kishairi
 1. kibali mshairi alichonacho kukiuka sheria fulani.
 • Inkisari (kufupisha ili kuwe na urari wa mizani na vina. Aghalabu huonyeshwa kwa matumizi ya ritifaa k.m. ‘sikate-usikate)
 • Mazda/mazida (kurefusha neno ili kuwa na urari wa mizani na vina)
 • Tabdila (kubadilisha tahajia ya neno bila kuzidisha au kupunguza mizani k.m. siachi-siati)
 • Utohozi
 • Kuboronga/kufinyanga sarufi (kubadili mpangilio wa maneno katika sentensi k.m. upesi jielimishe)
 • Kiswahili cha kikale/ujadi (mtima, ngeu, insi, mja)
 • Lahaja k.m. ficha-fita
 • Matumizi ya ritifaa
 • Lugha ya Nathari
  • lugha ya kawaida na kimtiririko
   • Kutotumia koma au vipande
   • Kutumia maumbo ya kawaida ya maneno
   • Ubeti kutengewa aya moja
   • Kuondoa uhuru na kusanifisha lahaja na kikale
 • matumizi ya lugha/fani
 • matumizi ya maneno (kama yalivyotumiwa)
 • ujumbe
 • maudhui
 • dhamira
  • kusimanga, kusuta, kudharau, kusifu, kufunza, n.k.

Mashairi Huru

Sifa/Mbinu

 • urudiaji
  • wa neno (takriri neno)
  • wa kifungu (usambamba)

  Umuhimu

 1. kusisitiza ujumbe
 2. kutia ridhimu/mapigo fulani katika usomaji
 • mishata
 1. mishtari ambayo haikamiliki. Mistari toshelezi ni mistari iliyokamilika.
 • sehemu za beti kuingizwa ndani

Umuhimu

 • ili kusisitiza
 • kuzifanya zionekane wazi

Ulinganishaji wa Shairi la Arudhi na Shairi Huru

Kufananisha

 1. yote mawili ni sanaa ya ushairi
 2. mishororo kupangwa katika beti
 3. yametumia mbinu za lugha za namna moja
 4. alama za kuakifisha zinazofanana
 5. kufanana kimuundo
 6. uhuru wa kishairi

Kutofautisha

 1. moja ni la arudhi jingine ni huru
 2. mishata
 3. sehemu za beti kuingizwa ndani
 4. kuwa au kutokuwa na urari wa mizani
 5. kuwa au kutokuwa na urari wa vina
 6. tofauti kimaudhui
 7. idadi ya beti
 8. idadi ya mishororo katika beti
 9. vipande
 10. kutumia alama za uakifishi tofauti
 11. uhuru wa kishairiShare this:


EcoleBooks | INSHA na ushairi wa Kiswahili Notes

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*