Share this:

UTANGULIZI

Katika somo hili la matamshi, tutashughulikia vitate na vitanza ndimi.Vitate ni maneno yanayotatiza kimatamshi.Utatanishi huu unatokana na;

 • kukaribiana kimatamshi kwa sauti fulani.Mfano. posa –poza.
 • Mtamkaji kuathiriwa na lugha ya kwanza au lugha nyingine;Mfano. mahali /mahari

Vitate

Vitanza ndimi 

Sikiliza vitanza ndimi vifuatavyo kisha uvitamke.
 

 1. Sitasitasita kusisitiza kuwa sita na sita si sita.
 2. Vazi alilovua alivaa baada ya kulifua likamfaa sana.
 3. Makoti Alikoti alipohukumiwa, alipiga magoti na kulivua koti kortini.
 4. Juzijuzi mjuzi jasusi alikutana na mjusi akienda kumuona mchuuzi akichuuza mchuzi.

Himizo

Muundo ni sura au namna kitu kinavyoonekana kwa nje .
Soma mahojiano yafuatayo kati ya mwandishi wa habari na mwanariadha huku ukizingatia muundo wa mahojiano yenyewe.
Mwandishi: Hujambo dada?
Mwanariadha: Sijambo.
Mwandishi: Mimi ni Philip Okelo mwanahabari wa Shirika
Utangazaji la Mambo Leo.Ningependa
Utangazaji la Mambo Leo.Ningependaa
kukuhoji kuhusu kukuhoji kuhusu la ushindi
wako.Waeleze wasikilizaji majina yako.
Mwanariadha: Jina langu ni Janet Jelimo. Kwa jina la utani
naitwa Risasi.
Mwandishi: Kwa nini wanakuita Risasi?
Mwanariadha: Kwa sababu ya kasi yangu katika mbio.
Mwandishi: Hongera kwa kushinda medali ya dhahabu
katika michezo ya Olimpiki.
Mwanariadha: Asante!
Mwandishi: Je, mipango yako ya siku za usoni ni ipi?

Mwanariadha: Ningependa kupata medali nyingi zaidi za dhahabu na kuvunja rekodi nyingi zaidi kabla ya kustaafu. 
Mwandishi: Mbali na riadha, unashiriki mambo yepi mengine?
Mwanariadha: Tayari nimejiunga na Chuo Kikuu cha Fujihama ili kujiendeleza kielimu.
Mwandishi: Unasomea nini?
Mwanariadha: Nasomea Uhandisi wa Tarakalishi.
Mwandishi: Una ujumbe gani kwa vijana?
Mwanariadha: Ningependa kuwahimiza vijana wajitolee na kukuza vipawa vyao. Kila mtu amebarikiwa na kipawa fulani. Lakini watu wengi hupuuza vipawa vyao na kukosa kuvikuza. Ni muhimu vijana kujipa muda na kutambua vipawa walivyo navyo. Baada ya kuvitambua, wapaswa kujitolea na kutia bidii ili waweze kunufaika kutokana na vipawa hivyo.

mu wa nyimbo hutokana na ujumbe uliomo katika wimbo wenyewe. 
Endelea kufanya utafiti zaidi kuhusu nyimbo.
Ni nyimbo ambazo huimbwa na mlezi wa mtoto kwa sauti nyororo na mahadhi taratibu ili kumtuliza mtoto,kumwongoa au kumfanya alale. 

Sarufi ya lugha huwa uwanja mpana ambao unashirikisha mada kama vile aina za maneno katika lugha na matumizi yake kisahihi na kimaana kwa kufuata utaratibu uliokubalika na wanajamii wa lugha husika. Hali kadhalika, huhusisha uakifishaji. 
Somo hili linahusisha ufundishaji wa kila aina ya maneno katika lugha na matumizi ya maneno hayo kisahihi, kimaana na kisarufi. Somo hili litakuwezesha kukuza kiwango chako cha msamiati na matumizi ya istilahi mbalimbali.

Sarufi na matumizi ya lugha hushirikisha shughuli za kimawasiliano na kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha tofauti tofauti na mazingira halisi. Ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi na matumizi ya lugha humpa mwanafunzi nyenzo za kuwasiliana kikamilifu.

Mwandishi: Asante kwa kutembelea Idhaa hii. Vijana wamepata kujifunza mengi kutoka kwako. Tunakutakia kila la heri.
Mwanariadha: Asante sana.

Tanbihi
Inadhihirika kuwa mahojiano huwa na maswali elekezi ya kudadisi undani wa jambo fulani.
Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha.
Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha. 
Shughuli
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uwe na uwezo wa:
i) kueleza maana ya mazungumzo
ii) kutambua muundo na sifa za mazungumzo
iii) kubainisha miktadha mbalimbali ya mazungumzo
iv) kutambua umuhimu wa mazungumzo

Tazama na kusikiliza mazungumzo A na B katika video hii. Tambua matukio yote katika shughuli hizi mbili.

Video A Marafiki wawili wamekutana mtaani baada ya muda mrefu. Haya ni mazungumzo ya kirafiki kuhusu maisha yao ya hapo awali na ambavyo yameendelea.
Video B Kuna mazungumzo kati ya wakulima wawili wanaokutana katika kituo cha malipo. Wanazungumza juu ya mavuno haba na malipo duni waliyopata kutokana na hali mbaya ya anga.

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Mwalimu na mwanafunzi wako nje ya sebule ya walimu)
Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu.
Mwalimu : Marahaba! U hali gani ?
Mwanafunzi: Sina neno mwalimu ila ningependa kuomba msaada wako kuhusu hotuba na mazungumzo.
Mwalimu : Shida yenyewe ni ipi?
Mwanafunzi: Aaa;Aa;nimeshindwa kubaini tofauti kati ya vipengele hivi viwili.
Mwalimu : (Akionyesha kushangaa) Lo! Kwani jana hukuwepo darasani tukijadili mambo haya?
Mwanafunzi: Samahani mwalimu nilikuwa hospitalini kwa matibabu.
Mwalimu : Pole, Utapata nafuu.
Mwanafunzi : Ahsante, nishapoa.

Mwalimu : Tofauti kuu kati ya hotuba na mazungumzo ni kwamba hotuba huwasilishwa na mtu mmoja kwa hadhira fulani nayo mazungumzo ni maongezi kati ya watu wawili au zaidi. Hotuba huchukua umbo la maelezo kuhusu jambo fulani ilhali mazungumzo huchukua umbo la kitamthilia.
Mwanafunzi : Ahsante mwalimu, kunazo tofauti zingine?
Mwalimu : Ndiyo, lugha inayotumiwa katika hotuba huwa na urasmi fulani, mazungumzo hutegemea muktadha. Lugha inayotumika hotelini haina urasmi ilhali ile itumikayo ofisini huwa na urasimu. mazungumzo katika hoteli,hospitali,kituo cha polisi na kadhalika. Mwanafunzi : (Anatabasamu) Nashukuru sana Mwalimu. Hakika umenitoa gizani.
Mwalimu : Karibu. Nenda darasani udurusu zaidi.

ecolebooks.com

SIFA ZA MAZUNGUMZO

Nyimbo
Wimbo ni utungo ulioundwa kwa maneno au sauti zilizoteuliwa kisanii na zenye utaratibu wa kimuziki.Sauti hizo hupanda na kushuka na kuibusha hisia fulani kwa mwimbaji na msikilizaji. Nyimbo hazizingatii kaida zote za ushairi kama ilivyo katika mashairi halisi. 
WIMBO WA TAIFA 

Umesikia na kuona nini ?
Huu ni wimbo wa Taifa la Kenya, unaoimbwa katika shughuli rasmi za kitaifa kama vile :
-katika sherehe na shughuli za kitaifa na kimataifa
-wakati wa kupandisha bendera katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali 

umuhimu wa wimbo wa taifa la Kenya 
hutambulisha taifa letu
huibua hisia za uzalendo
hukuza umoja
hukuza na kuendeleza utamaduni
ni ombi kwa Maulana
hufunza maadili
huzindua wananchi 

AINA ZA NYIMBO

Kuna aina mbalimbali za nyimbo kama vile: 
-nyiso
– hodiya/vave/wawe
– sifo
– mbolezi
– nyimbo za kidini
– nyimbo za kisiasa
– nyimbo za mapenzi
– nyimbo za kizalendo na kadhalika 

Ni nyimbo ambazo huimbwa na mlezi wa mtoto kwa sauti nyororo na mahadhi taratibu ili kumtuliza mtoto,kumwongoa au kumfanya alale.
Nyimbo hizi hudhihirisha hisia za mlezi kwa mtoto.

BEMBEZI
Soma wimbo huu. 
Ukimpenda mwanao
Na wa mwenzio umpende
Wako ukimpa chenga
Wa mwenzio chenjegele
Humjui akufaaye

Akupaye maji mbele
Kilengelenge cha boga
Kuti nazi kunoga
Roho yataka kunoga 
Mkono wafanya woga

Nyamaa mama nyamaa
Nyamaa usilie mno
Ukilia waniliza
Wanikumbusha ukiwa
Ukiwa wa baba na mama

(Kutoka Kiswahili Fasaha Oxford University Press Waititu Francis, Ipara Isaac, Okaalo Bilha, Amina Vuzo)

Umejifunza nini kuhusu sifa za wimbo?

Nyiso
Ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa tohara na shughuli zingine za jandoni.
Umuhimu wa Nyiso 
-hujasirisha
-hukuza ukakamavu
-hukuza maadili na kusuta
-hukuza na hudumisha utamaduni
-hukuza umoja
-huburudisha
-huhamasisha
-hufaharisha
Hodiya
Hodiya ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa kazi kwa mfano wawe/ vave huimbwa na wakulima, kimai huimbwa na wavuvi.
Umuhimu wa Hodiya
-Humtia shime anayefanya kazi
-hubeza wavivu-
-huonyesha jinsi wahusika wanavyoonea fahari kazi
– huonyesha mtazamo wa jamii kuhusu kazi

Sifo huimbwa kwa lengo la kusifu wahusika kwa sababu ya umaarufu unaotokana na ushujaa, cheo, kipawa cha pekee na mambo ambayo wameweza kayatekeleza.Sifo huhimiza wanajamii kuiga matendo yanayosifiwa, kufunza maadili na amali za jamii.

NYIMBO ZA KIZALENDO

Nyimbo za kizalendo ni nyimbo zinazoimbwa kudhihirisha uzalendo wa wananchi kwa taifa lao.
Nyimbo hizi huhimiza upendo kwa taifa lao na ombi kwa Maulana kubariki nchi.Huhimiza maadili na amali za kijamii

Mbolezi
Nyimbo zinazoimbwa wakati wa matanga au maombolezi. 

Umuhimu wa Mbolezi
-kufariji/kuliwaza waliofiwa, 
-huwapa tumaini walioachwa, 
-huonyesha imani ya jamii husika kuhusu maisha na kifo,
-kumsifu mwendazake,na kutoa ushauri. 

Nyimbo za mapenzi
Ni nyimbo zinazohimiza mapenzi.Nyimbo hizi zinaweza kuchukua mikondo mbalimbali.

Wapendanao huimba ili kuimarisha na kudumisha penzi lao. 
Hali kadhalika huwasilisha hisia za kimapenzi. 
Fauka ya hayo, hutumika kuwasilisha matarajio aliyo nayo mpenzi mmoja kwa mwingine. 
Zinaweza pia kutumiwa ili kumsifu mpenzi.
Mpenzi asiyeridhika na maisha ya kimapenz humlalamikia mpenziwe kwa mateso ya kimapenzi anayompa. 
Hali kadhalika humrai arekebishe ili hali iwe jinsi ilivyokuwa hapo awali.
Wanaotengana ambao wameshindwa kabisa kuvumiliana kwa hivyo hawana budi kuwachana. 
Aghalabu huelezea maisha yalivyokuwa na namna hali ilivyo sasa baada ya penzi kunyauka.
Nyimbo za chekechea 
Nyimbo za chekechea ni nyimbo zinazoimbwa na watoto wanapocheza.
Umuhimu
kujiburudisha 
kuwaleta pamoja
kufunza maadili
kusaidia katika kunyoosha viungo na kuimarisha afya
kukuza ukakamavu na uwezo wa kujieleza
hufunza lugha

NYIMBO ZA KIDINI

Nyimbo za kidini huimbwa ili kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Umuhimu wa Nyimbo za Kidini
Hudhihirisha imani ya wahusika kutegemea muktadha
nyenzo muhimu za kupitisha amali za kidini.
Maadili
Hutoa mafunzo kuhusu dini husika/ huelimisha
Hukuza imani ya wahusika
Huhamasisha waumini/ Humpa mwumini tumaini
Huliwaza
 


NYIMBO ZA HARUSI
Nyimbo za harusi huimbwa wakati wa sherehe za harusi.
Umuhimu wa nyimbo za harusi 
Husifu maharusi
Huwahamasisha maharusi kuhusu majukumu ya unyumba 
Huhimiza umoja wa jamii husika
Huburudisha
Huhimiza heshima kwa asasi ya ndoa
NYIMBO ZA KISIASA
Nyimbo za kisiasa huimbwa ili kushawishi watu kisiasa.
Umuhimu wa Nyimbo za Kisiasa
Kusifu au kushtumu viongozi wa kisiasa
Kusambaza cheche au mwamko wa kisiasa na propaganda hivyo kushawishi watu kufuata mkondo Fulani
Kuonyesha utesi dhidi ya dhuluma na ukandamizwaji
Kuleta watu pamoja kwa misingi ya kisiasa
Kuzomea uongozi mbaya
SIFA ZA NYIMBO
Ni wazi kuwa nyimbo huwa na sifa mbalimbali kwa mfano :

 1. Kuwa na mapigo ya sauti( huchukua muundo wa ushairi) ambapo kuna beti, mishororo,vina, mizani
 2. Hutumia tamathali za usemi kama vile mafumbo, jazanda, ishara (taashira),takiriri kwa mfano nyamaa mama nyamaa
 3. Nyimbo huweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi
 4. Nyimbo huambatana na ala za muziki
 5. Waimbaji aghalabu huwa na maleba
 6. Huambatana na miondoko
 7. Nyimbo kutegemea umri, jinsia,mazingira na muktadha

Nyimbo hutumiwa kuburudisha na kufurahisha
Nyimbo hufunza maadili
Uhifadhi utamaduni
Nyimbo huelimisha
Huhifadhi historia ya jamii
Nyimbo huliwaza na kufariji
Nyimbo hukuza umoja
Nyimbo husifu na kukashifu matendo. 
TANBIHI
Umejifunza kuwa nyimbo zina umuhimu katika jamii. Aina za nyimbo hugawika kulingana muktadha, jinsia,na lengo .UmuhiMU

MATUMIZI YA NOMINO KATIKA SENTENSI

Soma sentensi zifuatazo:
i) Wazee wamekuja kwetu.
ii) Kenya ni nchi nzuri.
iii) Upole wake ni wa kupigiwa mfano.
iv) Kuimba huko kulimfikisha mbali.
v) Biwi la takataka lilitiwa moto na topasi.
vi) Sukari ya mpishi imekwisha.
vii) Kikosi cha askari kinapiga gwaride uwanjani.
viii)Nairobi ni mji mkubwa.
ix) Kufagia sakafu kumechukua muda gani?
x) Mafuta yaliyoletwa yana bei ghali.
Kutokana na sentensi tulizosoma, tumejifunza kuwa nomino hutumiwa kutungia sentensi. 

Kipindi hiki kimetuwezesha kubainisha aina za nomino na matumizi yake.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa tunazitumia vyema nomino hizi. 
Ni bora tutalii matumizi yake zaidi . 

shughuli 
Kufikia mwisho wa kipindi, unatakiwa uweze:
i) kueleza maana ya kivumishi
ii) kubainisha aina za vivumishi
iii) kutumia vivumishi katika sentensi ipasavyo. 

Vivumishi 

Haya ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu nomino ilivyo kwa mfano ndogo,nzito,laini,nyororo na kadhalika.
Tazama kibonzo hiki na usikize sauti.Ni sifa zipi zinazojitokeza? 

a) Mtu mrefu
b) Mtu nadhifu
c) Mtu mnene
d) Mtu mweusi
sifa zilizojitokeza
mtu mrefu,mtu nadhifu,mtu mnene,mtu mweusi 

Tazama vibonzo hivi na usikilize sauti. Ni sifa zipi zinazojitokeza? 

Hivi hutoa maelezo kuhusu pale nomino ilipo. Nomino ikiwa karibu inaonyeshwa kwa kivumishi-kionyeshi cha karibu kama vile huyu, hiki, hawa, hivi, kutegemea ngeli. Iwapo nomino iko mbali kabisa, inaonyeshwa kwa kivumishi kionyeshi cha umbali kabisa kama vile, yule, kile, wale, vile, kutegemea ngeli.

Vivumishi vionyeshi hubadilika kulingana na ngeli. Kwa mfano:
Ngeli ya A-WA: Tunasema-
Mtu huyu
Mtu huyo
Mtu yule 
Ngeli ya LI-YA : Tunasema-
Tunda hili
Tunda hilo
Tunda lile
Ngeli ya Mahali: Tunasema-
Pahali hapa
Pahali hapo
Pahali pale


VIVUMISHI VYA IDADI
Tazama picha hizi. 
Je umetambua idadi ya vinavyofanana katika kila picha?
Kuna picha usiyoweza kutambua idadi yake?
Picha 1-Machungwa matatu
Picha 2 -Watoto wanne
Picha 3- Maji mengi
Picha 4-Majani tele

Idadi inaweza kuwa kamili au ya kukadiria kwa mfano: mtu mmoja, sahani mbili, shilingi ishirini ni mifano ya idadi kamili. Maji mengi, majani tele, watu wachache ni mifano ya idadi za kukadiria.
Vivumishi vimilikishi
Soma jedwali ulilopewa na utambue vivumishi vimilikishi vilivyotumiwa.

Vivumishi hivi huchukua mianzo kutegemea ngeli husika.Vivumishi vimilikishi ni maneno yanayoonyesha kitu ni cha nani au kimehodhiwa na nani. Hujikita katika mashina sita: 
i. -angu iv) -etu
ii. -ako v) -enu
iii. -ake vi) -ao

Mifano: Umoja Wingi
a) Shule yangu imepata mfadhili Shule zetuzimepata wafadhili 
b) Mtoto wako amefuzu Watoto wenu wamefuzu
c) Tunda lake limeliwa Matunda yao yameliwa 

Soma jedwali lifuatalo

Jedwali hili linaonyesha mizizi ya viulizi pamoja na baadhi ya mifano ya matumizi. Kivumishi kiulizi hutumiwa kudadisi au kuhoji kuhusu nomino. Vivumishi viulizi ni vya aina tatu, -pi – ngapi – gani
Mifano

 1. Ni wanafunzi wangapi wamo darasani?
 2. Unataka chakula gani?
 3. Ukuta upi umebomoka?

Kivumishi a-unganifu huhusisha nomino mbili. Huonyesha nomino ya kwanza inamilikiwa na ya pili. Kiambishi hubadilika kulingana na ngeli kama inavyoonekana katika jedwali.

Tazama vibonzo hivi. Unaweza kutambua tofauti yake na vivumishi vionyeshi?
Vivumishi visisitizi huundwa kutokana na vivumishi vionyeshi. Hutumika kutilia mkazo kinachoashiriwa.
Mifano:
i) Mche uu huu/ huu huu ndio utakaopandwa.
ii) Wanafunzi wawa hawa/hawa hawa ndio waliopita mtihani.
iii) Kucheza kuko huko/huko huko ndiko kulikomfanya ateuliwe katika timu ya raga ya taifa . 
iv) Maji yale yale ndiyo yaliyotekwa na kijakazi.
v) Werevu ule ule ndio uliomwezesha kuvumbua mtambo ule.

VIVUMISHI VYA PEKEE

Soma majedwali yafuatayo

Majedwali haya yanashughulikia vivumishi vya pekee. Vivumishi hivi vinarejelewa kama vya pekee kwa sababu kila mojawapo ina matumizi yake ya kipekee. Vivumishi hivi hubadilika kutegemea ngeli husika. Kila kivumishi hubeba wazo fulani kama ifuatavyo: 
Kivumishi Wazo
-enye kumiliki
-enyewe kusisitiza
– ote ujumla
-o-ote bila kuchagua
-ingine ziada au badala ya
-ingineo nyongeza au badala ya

.
SHABAHA:
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uwe na uwezo wa :
(i) kueleza maana ya vihusishi
(ii) kubainisha aina za vihusishi
(iii) kutumia vihusishi katika sentensi ipasavyo.
Vihusishi ni maneno yanayotumiwa kuonyesha uhusiano uliopo baina ya neno na neno au fungu la maneno na lingine.

Tazama kwa makini matendo katika kibonzo hiki.

Maelezo
Kibonzo kinaonyesha :
i) Gari limegeshwa kando ya mti
ii) Mbwa yuko chini ya gari
iii) Ndege ametua juu ya gari
iv) Kondoo yuko mbele ya gari
v) Paka yuko nyuma ya gari
vi) Dereva yumo ndani ya gari
Maneno yaliyopigiwa mstari ni vihusishi
Tazama hivyo vibonzo. Unaona nini?

Katika kibonzo cha kwanza kihusishi ni –
i) kabla ya 
ii) baada ya.
Katika kibonzo cha pili kihusishi ni :
i) hadi
Vihusishi hivi vinaitwa vihusishi vya wakati.
Tazama picha na vibonzo vifuatavyo. 

Katika picha na vibonzo ulivyotazama, vihusishi vilivyotumika vinaonyesha viwango kwa mfano:
i) Kutoka Nairobi hadi Mombasa ni kilomita 500.
ii) Mtu wa kwanza ni mrefu kuliko mtu wa pili.
iii) Mtu wa kwanza amebeba vitabu vingi zaidi ya mtu wa pili.
Kihusishi hutumika baina ya nomino mbili na huonyesha uhusiano baina ya nomino hizo.
Ni muhimu kuwa makini tunaposhughulikia vihusishi katika sentensi kwani baadhi ya vihusishi huweza kutumika kama viunganishi.
Tazama vibonzo na picha. Kuna tofauti gain katika matukio hayo?
Vitendo ulivyoona vinaonyesha vitenzi na vinyume vyake. 
i) keti-simama
ii) pakia-pakua
iii) anika-anua
iv) funga-fungua
v) paa- tua
vi) tembea haraka- tembea polepole
i) Furahi- huzunika
ii) Tia- toa

Vinyume ni maneno yaliyo na maana inayokinzana na maana ya maneno yaliyotolewa. 

shughuli

Maneno haya ni mifano zaidi ya vitenzi ambavyo ni vinyume.

Inabainika kuwa vinyume vikiundwa huchukua viishio oa,ua au ia na ambapo haiwezekani neno lingine lenye maana kinzani hutumika.
Pia ufahamu kuwa baadhi ya vitenzi huwa havina kinyume kwa mfano,saga, sema, zaa, soma,kula.Vitendo hivyo vikishatendeka haviwezi kutenduliwa.

Tazama vibonzo ulivyoonyeshwa. Umetambua kuwa kutokana na vibonzo hivyo vitenzi vifuatvyo vimejitokeza?
i) unapigwa
ii) anasomewa
iii) umejengekaka
iv) wanapigana
v) waalipiana
vi) anabebeshwa
vii) kimbizana
viii) anamkaribishia
Kutokana na vibonzo ulivyotazama umetambua kuwa mnyambuliko wa vitenzi unahusu hali ya kurefusha kitenzi kwa kukipa kiambishi tamati ili kuleta maana nyingine kutokana kitenzi asili.
Kwa mfano
i) piga- pig-wa
ii) soma- som-ewa
iii) jenga- jengeka-ika
iv) piga- pig-ana
v) lipa- lip-iana
vi) beba- beb-eshwa
vii) kimbia- l-ishana
viii) karibisha- end-eshea
Sehemu zilizovutwa baada ya mzizi wa kitenzi zinaonyesha mnyambulika wa vitenzi katika kauli mbali mbali.

Kufikia mwisho wa kipindi hiki unatakiwa uwe na uwezo wa:
i) kueleza maana ya mnyambuliko wa vitenzi 
ii) kunyambua vitenzi katika kauli mbalimbali
iii) kueleza maana kutokana na vitenzi vilivyonyambuliwa katika kauli husika. 

Mnyambuliko ni hali ya kurefusha kitenzi kwa kukipa kiambishi tamati ili kuleta maana nyingine tofauti na kitenzi katika hali yake ya kawaida.

tendewa

tendeshwa

tendana

Katika kauli hii huonyesha mtu au kitu kimepokea tendo husika moja kwa moja.
Vitenzi hivi huishia wa. kwa mfano, pigwa,limwa, limwa, somwapia baadhi huwa na miisho liwa au lewa. mfano -chukuliwa,-nyolewa 

miwa imekatwa 

Huonyesha tendo limefanywa na mtu kwa niaba ya mwingine au kwa ajili ya mtu huyo. Kwa mfano somewa, imbiwa,itiwa, tobolewa, dhulumiwa, kataliwa
Vitenzi katika kauli hii huishia kwa-iwa,-ewa,-liwa,-lewa

Huonyesha namna ya kutendeka kwa jambo mfano, mpini unashikika.
Huonyesha kuwezekana kwa jambo kutendeka kwa mfano ,ukuta unabomoleka.Pia huonyesha kukamilika kwa jambo. kwa mfano, Mlango umefungika.
Vitenzi katika kauli hii huishia na -ika,-eka,-lika na -leka 

chupa imevunjika 
Huonyesha kitendo kimetendwa na kitu, mtu au mnyama kwa mwenzake naye mwenzake anamtendea tendo lile lile kwa wakati uo huo.
Kwa mfano pishana, juana, pambana 
Vitenzi katika kauli hii huishia na -ana 

fahali wanapigana 
Tendeana
Tendo limetendwa na wahusika wawili kwa niaba yao wenyewe, mfano someana, pikiana, choreana.
Vitenzi katika kauli hii huchukua kiishio -iana/eana

Tendeshwa 
Ni hali ya kusababisha au kulazimisha kitendo fulani kutendwa. Anayetenda hana hiari.Vitenzi katika kauli hii huishia na -shwa,-zwa kwa mfano,
-bebeshwa
-pikishwa
-tembezwa
-pendezwa.

tembezwa

Vitendo katika kauli hii vina dhana fiche ya kulazimishana au kuhimizana kutenda. Vitenzi katika kauli hii huchukua viishio hivi eshana,-ezana,-ishana,
kwa mfano, pokezana, pendekezana, pikishana, furahishana, potoshana, 

Mbwa na Paka wanachezeshana. 
Tendo hutendwa kwa ajili ya mtu ili kumsaidia.Vitenzi katika kauli hii huchukua viishio -eshea, ishia, izia.
kwa mfano,endeshea,

AINA ZA VIELEZI


Kuna aina nne za vielezi. 
i) Kielezi cha namna ,kwa mfano, vizuri, kinyama, haraka, ovyo,polepole ii)Kielezi cha Wakati,kwa mfano, jana, sasa, jioni, mwaka ujao, usiku,alfajiri iii)Kielezi cha Mahali,kwa mfano,Limuru,darasani, nje,barabarani, iv)Kielezi cha Idadi ,kwa mfano. Mara tatu, sana, kiasi,chache, mara kwa mara, 
Mifano katika sentensi

 1. Alipigwa kinyama
 2. Wanafunzi wanacheza Uwanjani.
 3. Mama ananunua matunda matamu sasa.
 4. Alifanya kazi pole pole mno.

Maneno yaliyopigiwa mstari ni vielezi. 

Tazama vibonzo hivi na kusikiliza sauti.
anatembea polepole

anatembea kasi

anatembea kijeshi

katika sentensi ulizosikia, vielezi vya namna vimetumika kwa vile vinaeleza namna vitenzi vilivyofanyika.kama vile,maneno yaliyopigiwa mstari ni vielezi vya namna. 

VIELEZI VYA WAKATI

i)nimeamka asubuhi

ii)Ninakula saa saba.

iii) Nitasoma usiku 

Tazama kibonzo hiki na usikize kinachosemwa. Yaani 
i) Nimeamka asubuhi.
ii) Nitakula saa saba
iii) Nitasoma usiku
iv) Nilizaliwa 1995
v) Nitajiunga na kidato cha tatu mwaka ujao
Vielezi vinavyojitokeza ni vya wakati. Hueleza kitendo kilitendwa lini au wakati gani mfano asubui, saa saba, 1995, na mwaka ujao.

Tazama picha hizi.

Unaona nini katika picha hizi? Picha ulizoona zinaonyesha vielezi vya mahali, kama vile:
wanacheza uwanjani
kagevera amewasili Nairobi
Karema amesimama nje
Parachichi limeanguka chini 

Maneno yaliyopigiwa mstari ni vielezi vya mahali. Hivi huonyesha kitendo kilitendekea wapi.

Tazama vibonzo hivi na usikilize kwa makini yanayosemwa.

Ameruka mara tatu. 

Maji yamejaa pomoni. 

Huenda shule kila siku 

Husali mara kwa mara 
Umeona nini? Umesikia nini?
Maneno:mara tatu,mara mbili,kila siku,mara kwa mara ni vielezi vya idadi.
Kuna vielezi vya idadi kamili na idadi ya jumla.
Vielezi vya idadi kamili hutoa idadi kamili ya kitendo kutendeka kwa mfano, mara tatu, mara tano.
Vielezi vya idadi ya jumla havitoi idadi iliyo kamili bali jumla. kwa mfano kila siku,Pomoni.

 1. Gichomo ameruka mara tatu.
 2. Maji yamejaa pomoni.
 3. Jibo huenda shule kila siku.
 4. Abubakri husali mara tano kila siku


Kufikia mwisho wa kipindi hiki unatarajiwa uwe na uwezo wa:
i) kueleza dhana ya wastani,ukubwa au udogo wa nomino
ii) kubainisha nomino katika hali ya ukubwa au udogo
iii) kubadilisha nomino katika hali ya wastani,ukubwa au udogo
iv) kutumia nomino katika wastani,ukubwa na udogo ipasavyo katika sentensi
Nomino huweza kuchukua hali tatu tofauti-wastani, ukubwa na udogo. Hali hizi tatu huathiri maana na matumizi ya nomino. 
Unaona tofauti gani katika picha zinazoonyeshwa katika kila orodha?

Tofauti ulizoona zinadhihirisha kwamba nomino zinaweza kuchukua hali tatu tofauti
-udogo,wastani na ukubwa.
Mtu kijitu jitu
Kiti kijiti jiti
Uso kijuso juso
Nyumba kijumba jumba
Kiambishi kiji huongezwa katika mzizi ili kuunda hali ya udogo. Kama inavyojitokeza hapa mizizi ya maneno haya yanapoteza viambishi awali na kuchukua kiji
M-tu Kiji-tu
Ki-ti Kiji-ti
uso kij-uso
Ny-umba kij-umba

Kiambishi ji huwekwa kwa mzizi ili kuunda hali ya ukubwa. Mfano:
Mtu Jitu
Kiti Jiti
Uso Juso
Nyumba Jumba

Nomino zikibadilika hali, huathiri sentensi yote katika upatanishi wa kisarufi.Hii ni kwa sababu udogo huchukua ngeli ya Ki-Vi na ukubwa Huchukua Li-Ya. 
Mtoto alimwona nyoka mkubwa njiani.
Udogo
Kijitoto kilikiona kijoka kikubwa mbugani.
Vijitoto viliviona vijoka vikubwa mbugani

Ukubwa
Jitoto lililiono joka kubwa mbugani.
Majitoto yaliyaona majoka makubwa mbugani.
Kisu kilichotumiwa kumkata kuku kimechukuliwa na kijana
Kijisu kilichotumia kukikata kikuku kimechukuliwa na kijijana
Vijisu vilivyotumika kuvikata vikuku vimechukuliwa na vijijana
Jisu lililotumika kulikata jikuku limechukuliwa na jijana
Majisu yaliyotumika kuyakata majikuku yamechukuliwa na majijana

Kufikia mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uwezo wa: 
i) kueleza maana ya muhtasari
ii) kueleza umuhimu wa muhtasari
iii) kufafanua hatua za kuzingatia uandikapo muhtasari
iv) kuandika muhtasari wa kifungu.

MUHTASARI
Muhtasari ni ufupisho wa habari bila kupoteza maana iliyokusudiwa.
Muhtasari huwezesha mtu kutoa habari ndefu kwa maneno machache na kwa muda mfupi ili kurahisisha mawasiliano.

Ufupisho una manufaa mengi katika shughuli za kila siku.
Hutumiwa hususan katika mawasiliano na matangazo 
mbalimbali kama vile ya kibiashara na vifo, uandishi wa habari na makala ya magazeti, uandishi wa ripoti na kumbukumbu, maandalizi ya mitihani,uandishi wa arafa.

Ufupisho husaidia kutumia wakati vyema na pia kuokoa fedha na rasilimali.
Ujuzi wa kuandika muhtasari ni jambo la lazima maishani. 

Hatua za kuzingatiwa katika kuandika muhtasari
i) kusoma na kuelewa makala.
ii) kuchagua au kuteua mambo muhimu au kiini cha habari huku tukijiepusha na maelezo ya ziada, mifano, vielezi au tamathali za usemi. 
iii) Palipo na orodha ya mambo au vitu, ni muhimu kutumia maneno ya kijumla.
iv) kuandika kwa mtiririko mambo muhimu tuliyoyateua kwa hati nadhifu.

Ufupisho wa hotuba
Sikiliza kwa makini hotuba zifuatazo
Hotuba A
Wananchi hamjambo! Hamjambo tena. Na baada ya salamu hizi, nimesimama mbele yenu kuwasalimia. Jambo lingine nimekuja kwenu leo kuwaomba kura zenu. Ninataka niwe mwakilishi wenu katika eneo hili la bunge
Hotuba B
Wananchi hamjambo, niko hapa kuwaomba kura ili niwe mbunge wenu.

Hotuba ya kwanza ina maneno mengi kuliko ya pili lakini ujumbe ni uleule.

Soma kifungu kifuatacho kisha 
Visa vya utapeli vinaendelea kuongezeka humu nchini kwa kasi mno. Wananchi wengi wametapeliwa kiasi kikubwa cha pesa na watu ambao hujidai kuweza kutatua matatizo waliyo nayo. Idadi kubwa ya vijana wameingia katika mtego huu wanaposhawishiwa kwa kupewa ahadi za ajira ambayo imekuwa nadra kupatikana. Wengine ni wananchi wanaotafuta nyumba za kukodisha au viwanja vya kujengea. Hawa hutapeliwa na mawakala ambao hujifanya wanawakilisha mashirika fulani. Mawakala hawa huchukua pesa na kutoroka. Inasikitisha kuwa matapeli wengine wanatumia dini. Wao huwadanganya watu kuwa, wakipewa pesa na kuziombea zitaongezeka maradufu, jambo ambalo haliwezekani.
Ili kukabiliana na tatizo hili, ni muhimu kwa wananchi kuwa makini zaidi wanapojihusisha na watu wasiowafahamu vyema. Vijana wanaotafuta ajira wanapaswa kuwajibika, kuchunguza vizuri ili kubaini mashirika yanayotangaza kazi yapo au ni ya kufikiria tu. Serikali inaweza kusaidia katika kuwasaka, kuwanasa na kuwachukulia hatua matapeli. Vile vile vyombo vya habari viangazie visa vya aina hii ili kutahadharisha na kuwawezesha wananchi kuwa makini zaidi.

 1. Dondoa hoja muhimu katika aya ya kwanza. (maneno 25)
 2. Fupisha aya ya pili.

MAJIBU

 1. Visa vya utapeli vimeongeka. Walioathirika ni vijana wanaotafuta ajira, watu wanaotafuta nyumba na viwanja na wale wenye tamaa ya pesa.
 2. Ili kutatua tatizo hili, wananchi wanapaswa kumakinika, vijana wanaotafuta kazi wawe na subira na uangalifu, seriksli iwaadhibu wahusika na vyombo vya habari viangazie visa hivi ili watu zaidi wasihadaiwe.

Utungaji wa kiuamilifu 
Utungaji wa kiuamilifu ni stadi zinazohusu maarifa na ujuzi wa tungo ambazo mwanafunzi ye yote atahitaji katika maisha yake ya kila siku hata baada ya mafunzo ya shuleni.
Utungaji wa kiuamilifu huwa na taratibu ambazo lazima zifuate.
Maarifa haya yanahusu tungo kama , insha za ripoti, hotuba, barua, kumbukumbu, hojaji, resipe, shajara na kadhalika. 
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uwe na uwezo wa: 
i) kueleza maana ya tungo za kiuamilifu
ii) kufafanua maana ya hotuba
iii) kubainisha umuhimu wa hotuba
iv) kueleza muundo wa hotuba
v) kuandika hotuba ipasavyo
Hotuba
Hotuba ni taarifa inayotolewa na mtu mbele ya hadhira kwa nia ya kuwasilisha ujumbe mahususi, kutoa msimamo au kuelekeza.
Muundo wa hotuba huwa na sehemu tatu.
Sehemu ya kwanza ni ya utangulizi ambao ndio mwanzo wa hotuba. Utangulizi hushirikisha kuwatambua wale waliohudhuria.Utambulishaji huu,hufanywa kwa kutaja wadhifa wa juu. Vile vile ni katika utangulizi ambapo maamkuzi hufanywa.
Utangulizi hufuata na mwili ambao ndio kiini cha hotuba yenyewe. Mhutubi huelezea mada, kiini ,mapendekezo au ushauri wake. 
Hotuba hukamilika kwa hitimisho ambapo mhutubi hutoa shukrani zake na kuagana na hadhira yake.

Tazama video hii na usikilize kwa makini.

je umeona na kusikia nini?
Katika video kuna hadhira. Mbele ya hadhira, kuna mtu anayezungumza. Aliyesimama mbele ya umati anatoa hotuba. 
Hotuba aghalabu huweza kupitisha ujumbe ili kuelimisha, kushawishi, kushauri, kutahadharisha na kuhimiza
.Ujumbe wa hotuba hutegemea muktadha husika. 

Tazama na kusikiliza video hizi mbili.

Wahutubi hawa wana tofauti zipi katika hotuba zao?

Inadhihirika kwamba mhutubi wa kwanza ni bora kuliko wa pili.Hatibu bora anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
i) ana ukakamavu 
ii) sauti nzuri na inayosikika vizuri
iii) anatumia viziada lugha kama vile masaja,ishara za mikono na kadhalika.
iv) anahusisha hadhira yake kikamilifu
v) hutumia lugha fasaha na ya adabu
vi) ana mawazo yaliyopangwa kimantiki
vii) anatumia lugha ya kusisimua na kuteka urazini wa hadhira
viii) hajirudii bila sababu
ix) ana uwezo wa kushawishi na kuhamasisha hadhira
x) kuelewa hadhira yake vilivyo

Umealikwa kama mgeni wa heshima katika hafla ya siku ya vijana. 
Andika hotuba ukayoitoa kuhusu nafasi na majukumu la vijana katika jamii,
changamoto zinazowakabili vijana, namna vijana wanaweza kuimarisha maisha yao
na ya wakenya wengi. 
i) kueleza maana ya Resipe
ii) kueleza umuhimu wa Resipe
iii) kueleza muundo wa Resipe
iv) kutambua msamiati wa mapishi mbalimbali
v) kuandika Resipe 
Resipe ni maelezo ya namna ya kutayarisha chakula mahususi.Hushirikisha orodha ya viungo na kiasi kinachohitajika kwa vyakula hivyo kutegemea idadi ya walaji. Resipe hutegemea walaji mathlaani watoto, wazee, wagonjwa, wachezaji, wajawazito na kadhalika.

RESIPE YA KITOWEO CHA KUKU

Kulingana na video uliyoitazama umetambua wazi kwamba utayarishaji wa kitoweo cha kuku hufuata utaratibu ufatao:
Mahitaji

 1. Idadi ya walaji 4.
 2. Vinavyohitajika na vipimo vyake

i. Kuku 1.
ii. Mafuta ya kukaanga vijiko 2 vikubwa.
iii. Kitunguu maji 1 (kikubwa).
iv. Nyanya 3 mbivu.
v. Chumvi kijiko kidogo.
vi. Bizari iliyosagwa kijiko 1 kidogo.
vii. Pilipili hoho 1.
viii. Maji vikombe vidogo 3
ix. Dania fungu 1
x. Biringanya 

3. Utaratibu

Osha vipande vya nyama ya kuku,biringanya,dania,pilipili hoho,nyanya na vitunguu 
Teleka sufuria juu ya moto
Chemsha mafuta kwa dakika moja
Katakata vitunguu na kuviweka ndani ya mafuta.
Vikigeuka rangi kahawia, weka nyanya na pilipili hoho kisha tumbukiza vipande vya nyama ya kuku ndani ya mafuta.
Tia chumvi na bizari na kukoroga.
Funika kwa dakika 20.
Punguza kiwango cho moto kwa dakika 10.
Kitoweo kimeiva na chaweza kuandaliwa pamoja na kachumbari na kuliwa kwa sima au wali.

RESIPE YA UGALI

Maelekezo ya kutayarisha

Mahitaji

 1. Idadi ya walaji 4
 2. Viungo

maji lita 1
unga kilo 1
Chemsha maji hadi yatokote
Weka unga
Koroga mchanganyiko kwa mwiko hadi ushikamane.
Baada ya dakika 5 punguza kiasi cha moto halafu funika.
Epua sufuria kisha tia sima kwenye sahani halafu andaa mlo.

RESIPE YA UJI
Jinsi ya kutayarisha
a) kikombe kimoja cha unga wa wimbi
b) vikombe viwili vya maji
c) sukari
d) kijiko kimoja cha siagi 

Utaratibu
a) Tekeleka maji kwenye sufuria hadi yatokote
b) tengeneza mchanganyiko wa unga wa wimbi na maji kwenye bakuli kando
c) mwaga mchanganyiko huo kwenye maji yaliyotokota halafu ukoroge.
d) acha mchanganyiko huo utokote kwa dakika kumi
e)ongeza sukari
f)sasa epua sufuria, na utie uji kwenye vikombe halafu uandae. 

UANDISHI WA RESIPE
Tazama vibonzo kwa makini. Umetambua kuwa kuna hatua maalum za kuzingatiwa katika kuandika Resipe?

 1. Kuchagua na kutaja aina ya lishe kama vile asusa, ugali, wali, kitoweo na vyakula vinginevyo.
 2. Kuonyesha idadi ya walaji.
 3. kuandika orodha ya vipimo vya viungo-andika idadi ya vipimo kwa nambari.
 4. Kueleza jinsi ya kupika
 5. kuandaa

andika resipe ya chapati kwa kitoweo cha maharagwe


UMUHIMU WA RESIPE

i) hutusaidia kutoa lishe bora kwa jamii
ii) husaidia kujua namna ya kupika chakula kizuri
iii) Hutuelekeza katika kujua kiasi cha chakula kwa idadi fulani ya walaji.
iv) Kupitia Resipe, tunajua aina mbalimbali za mapishi kulingana na tamaduni mbalimbali).
Imedhihirika kwamba Resipe ni muhimu kwa kuwa:
iii) hutuelekeza katika kujua kiasi cha chakula kwa idadi fulani ya walaji.
iv) kupitia Resipe, tunajua aina mbalimbali za mapishi kulingana na tamaduni 
mbalimbali.

Utungaji huu hujikita katika uandishi wa kisanaa yaani ufundi na urembo unaotokana na mbinu ya uwasilishaji.
Insha hizi zinahusu jinsi lugha inavyotumiwa. 
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unahitajika:
i) kueleza maana ya michezo ya kuigiza
ii) kueleza umuhimu wa michezo ya kuigiza
iii) kufafanua muundo wa mchezo wa kuigiza
iv) kuandika mchezo wa kuigiza ukizingatia kanuni za utungaji ipasavyo

Tazama hii video kwa makini.

i) Umeona nini?
ii) Waigizaji wamevaa vipi?
iii) Wako wapi?
v) Lugha yao inaandamana na nini ?
Huu ni mchezo wa kuigiza. Mchezo unaigizwa jukwaani. Waigizaji huwa na mavazi maalum-maleba yanayooana na nafasi wanazoigiza. Mazungumzo yao yamejaa ishara, hisia na huambatana na utendaji. Aghalabu lugha hii husheheni matumizi ya tamathali za usemi ili kuteka urazini wa hadhira

Soma kisehemu hiki cha mchezo.
(Jukwaani. Ni nyumbani. Baba anaingia jioni. Anamkuta mwanawe anayesomea shule ya bweni nyumbani
Baba : (Akishtuka) Unafanya nini hapa mwanangu?
Mwana: (Akilia) Ni-niki kuambia u- ta-nirudi.
Baba : Kwani umefanya nini?
Mwana : Nilipatikana 
Baba : ( kwa ukali)Ulipatikana na nini?
Mwana : na ..na.. na Simu tamba.
Baba : (akimkaribia na kumkaripia)Simu ya nani?
Mwana : ( Huku akitetemeka)Ni..li..pewa na..na.. rafiki yangu na…na…. sikujua alikuwa ameiba.
Baba : Unajua ni hatia kuwa na simu tamba shuleni na kuwa na mali ya kuiba?
Mwana : (Akiogopa) Nisamehe baba.
Baba : (Akitikisa kichwa)Sasa imekuwaje ?
Mwana : (Kwa mkono unaotetema)Mwalimu mkuu amenituma nyumbani na kunipa barua hii nikuletee.
Baba : ( Akiipokea , kuifungua na kuisoma barua) Kesho tutaandamana hadi shuleni.

Tazama video hii.
Michezo ya kuigiza huwa na umuhimu gani katika jamii?
i) kuburudisha
ii) kufunza
iii) kuadilisha
iv) kukuza vipawa vya wasanii
v) kutafakirisha
vi) kuliwaza
vii) kuonya na kutahadharisha
viii) kuhamasisha
ix) njia ya kujipata riziki
x) hukuza staid za lugha
xi) kustawisha utamaduni
xii) kukuza umoja
Utungaji wa mchezo wa kuigiza huzingatia kaida zifuatazo:
i) kuteua mada ya kutungia
ii) kutumia lugha yenye mnato na mchomo ya hisia wa kutumia tamathali za usemi zinazokubalika kama tasifida, mafumbo, chuku, taharuki
iii) kuchagua mandhari yafaayo 
iv) kuzingatia ufaafu wa waigizaji
v) kuchagua maleba yatakayoafiki nafasi na hadhi za waigizaji
vi) kugawa mchezo katika maonyesho mbalimbali kulingana na mtiririko wa matukio

Kufikia mwisho wa kipindi uweze:
i) kusoma kwa ufasaha
ii) kufurahia kusoma maandishi katika lugha ya Kiswahili
iii) kuzingatia mafunzo na maadili yatokanayo na maandishi katika lugha ya Kiswahili.
iv) kudondoa na kueleza maana ya msamiati na istilahi zilizotumiwa katika makala
v) kufafanua ujumbe unaojitokeza katika makala

Mada hii inahusu usomaji wa majarida, magazeti vitabu vya ziada na makala yanayozingatia maswala ibuka.
Hukusudiwa kufurahisha na kukufunza maadili 
Maagizo kwa Mwanafunzi.
Sikiliza kwa makini wasomaji hawa wawili wanaposoma.

KUSOMA DONDOO

(Provide two interesting story features for example Dondoo from Taifa Leo which will promote positive values which the learner will read on the screen.)
Soma makala haya kwa ufasaha.
Je, umeyafurahia? Kwa nini?
Ili kuzidi kupata uhondo katika usomaji wa Kiswahili huna budi kutafuta na kusoma
matoleo ya majarida, magazeti, na vitabu vya Kiswahili. 

(Type the short play on page 80 of Chemichemi za Kiswahili Kidato cha 2 ,By G. Waihiga and Wamitila, Longhorn Publishers.)
Tazama na sikiliza yanayosomwa na kufanyika katika vibonzo hivi

Je,umeona na kujifunza nini?(clickable button)
Kutokana na matukio katika kipindi hiki ni wazi kuwa ni vizuri kusoma kwa mapana bila kushurutishwa. 
Utaimarisha ufasaha wako wa kusoma na kukuza msamiati. Utajua mambo mengi kuhusu maswala ibuka na utapata weledi katika mambo mbalimali yanayoshughulikiwa katika magazeti, majarida na vitabu malimbali. 

SHABAHA: 
i) kubainisha aina za nomino
ii) kueleza sifa za kila aina ya nomino
iii) kutumia kila aina ya nomino katika sentensi ipasavyo.

choma -katika kitenzi choma tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume chomoa
komea- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume komoa
shona- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume shonoa
tia- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume toa
fuma- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati u katika mzizi ili kupata kinyume fumua
kunja- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati ukatika mzizi ili kupata kinyume kunjua
hama- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati i katika mzizi ili kupata kinyume hamia
fukia- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati ukatika mzizi ili kupata kinyume fukua
nuka- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati i katika mzizi ili kupata kinyume nukia

funika-katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati u katika mzizi ili kupata kinyume funua

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uweze:
i) kueleza maana ya vinyume
ii) kubadilisha kitenzi hadi kinyume chake
iii) kutumia vinyume ipasavyo katika sentensi.

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA 

Kusikiliza na kuzungumza ni stadi zinazoshirikisha shughuli za kimawasiliano na kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha tofauti tofauti na mazingira halisi.Katika kusikiliza na kuzungumza, matamshi yafaayo ni muhimu. 
Ufunzaji na ujifunzaji wa stadi hizi humpa mwanafunzi nyenzo za kuwasiliana, kuingiliana na kutagusana ili kutimiza mahitaji mbalimbali. 

Kwa mfano:
1. Kujuliana hali 
2. Kupasha ujumbe
3. Kuelimisha
4. Kuelekeza
5. Kuzindua/Kuhamasisha 
6. Kuonya/kutahadharisha
7. Kuhimiza/kushawishi
8. Kuliwaza
9. Kutatua mizozo katika jamii
10. Kutumbuiza 

Hitimisho Imetambulika wazi kuwa stadi ya kusikiliza na kuzungumza itakufaa sana maishani!


 
Share this:


EcoleBooks | Kiswahili Form 2 All Notes

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*