Share this:

 

1. TUMBO LISILOSHIBA

 

Historia ya Mwandishi.

 

Hadithi hii imeandikwa na Prof. Said Mohammed, mwandishi mtajika ambaye amewahi pia kuandika vitabu vingine vitajika kama vile Riwaya ya Utengano. Mwandishi huyu bila shaka ni gwiji katika ulingo huu kwani amewahi kuandika kazi zingine za fasihi andishi zikiwemo tamthilia, mashairi na hadithi fupi.

 

Dhamira

 

Dhamira ni funzo kuu litokanalo na kazi ya sanaa au lengo kuu la mwandishi. Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshoba alidhamiria kufunua uozo unaoletwa na ubinafsi na tamaa katika jamii. Aidha anawajasirisha wanaoathiriwa kuwa wanaweza kukubali madhila wanayofanyiwa ama kupinga dhulma hizo na kusimama wima na kutetea haki zao.

 

Ufupisho wa Hadithi.

 

Hadithi hii inaangazia maisha ya watu wanaoishi katika mtaa wa Madongoporomoka, mtaa ambao umepakana na jiji linalokuwa kwa kasi mno. Jiji hili limeshiba kwa wingi wa mijengo iliyojengwa k i a s i c h a k u a n z a k u t i s h i a u we p o wa m t a a d u n i wa Madongoporomoka. Uvumi unawakia wanamadongoporomoka kwamba mtaa wao utanyakuliwa ili upanuzi wa mji ukie eneo hilo. Mwanzoni ulianza kama tu uvumi uliokuja na kupita bila ya wanamadongoporomoka kuwa na uhakika nao. Ingawa uvumi huo u l i i s h i a k u t ow e k a , M z e e M a g o k a t u h a k u wa r u h u s u wanamadongoporomoka kutupilia mbali wazo la uvumi huo kutimia na wao kuishia kufurushwa. Anawaleta pamoja wanakijiji wenzake ili kutafuta suluhishi kwa tatizo lililokuwa limewakodolea macho. Kwa pamoja wanakijiji wote wanakubaliana kutoondoka na liwe liwalo. Hata ikiwa watafurushwa, wanaamua kutetea mtaa wao na kusalia.

Kisadfa, bwana mmoja mwenye tumbo kubwa anawasili kwenye

ecolebooks.com

mkahawa wa Mzee Mago na kutaka kupewa chakula chote kilichoandaliwa. Ajabu ni kuwa anapokabidhiwa chakula hicho,

 

1.

anafyeka chote fyuu! Ni ajabu kwani huyu jamaa ana “Tumbo lisiloshiba“. Baada ya kula na kutoa bweu kubwa lenye harufu mbaya, jitu linalipa na kuahidi litarejea siku iliyofuatia.

Siku iliyofuata wanamadongoporomoka wanagutushwa na maporomoko yanayotokana na vibanda vyao kubomolewa na mabuldoza. Wanafurushwa wote kwa nguvu. Vibanda vyao vinabomolewa na wao kuishia kufukuzwa. Ajabu ni kwamba “Bwana Tumbo” anarejea kama alivyoahidi. Ila wakati huu yuko ndani ya gari kubwa na dereva anayemwamrisha. Hivyo amerudi kula kila kitu kama alivyoahidi ila wakati huu amekuja kula m a s h a m b a y a o . M z e e M a g o a n a w a s h a w i s h i wanamadongoporomoka kutoondoka, licha ya dhulma hizo. Umoja wa wanakijiji hawa unawaokoa kwani muda mfupi baadaye, vibanda vyao vinaanza kuota tena. Wanafaulu kuzuia tamaa ya tumbo kubwa lisiloshiba la mji kutokula mashamba yao.

 

 

MAUDHUI

 

 

Baadhi ya maudhui yanajitokeza katika hadithi hii ni kama vile:

a) Ubinafsi na tamaa b) Unyanyasaji

c) Utetezi wa haki d) Umaskini

e) Utabaka

f) Migogoro

 

 

a) Ubinafsi na tamaa (Tumbo lisiloshiba)

Haya ndiyo maudhui makuu katika hadithi hii. Maudhui haya yanajengeka kwa kutazama jinsi ambayo wahusika fulani hawatosheki na mengi waliyokuwa nayo na hivyo basi kutamani vidongo vya wengine na kutaka kuwahini. Wakubwa wa jiji wanadai kwamba jiji limejaa tayari hadi Pomoni. Halijaacha hata nafasi ya mtu kuvuta pumzi.

 

2.

Jiji lenyewe limekuwa limesheheni usa, ujumi na tamaduni mbali mbali. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmental stores, casinos, viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpira wa vikapu, raga, kabumbu, vyuo vikuu, mahakama, hospitali, majumba ya osi na mengine mengi. Haya yote yamekuwa yamesimama wima jijini. Hapajasalia hata nafasi kidogo ya kuvuta pumzi. Hivyo basi wakubwa wa jiji waonelea vyema kwa ardhi ya watu wa Madongoporomoka kutwaliwa. Hii ni tamaa ya hali ya juu. Wanataka wajenge majumba ya kifahari huko. Hawataki kuwalipa wenye ardhi hiyo dhamana inayofaa bali wanataka tu kuwafurusha wanamadongoporomoka.

Mhusika “Bwana Tumbo” anaingia kwenye mkahawa wa Mzee Mago. Ukubwa wa tumbo lake unashangaza wengi. Ni dhahiri kuwa huyu mtu ni mlaji hodari. Jamaa huyu anaishi kuulizia chakula kilichopo kwenye mkahawa na kukila. Anakula chakula chote kilichoandaliwa kwa walaji wengine wote. Anamaliza chakula na kuongezewa kingine. Anakula nyama ya kuchoma, mchuzi wa nyama, wali wa nazi, samaki wa kukaanga, chapatti kadhaa na kuishia kuteremshaa na chupa mbili za Coca cola. Anafagia mkahawa wote. Anaahidi kurejea siku itakayofuata na kutaka chakula kipikwe mara mbili Zaidi ya kile kilichopikwa siku hiyo. Hii ni tamaa ya ajabu. Watu waliokuwepo kwenye mkahawa wanabaki kushangaa ni vipi mtu anakula chakula chote kilichoandaliwa walaji wote kwenye mkahawa?

Bwana mwenye tumbo ana tamaa ya mashamba. Anajaribu kuwafurusha wanamadongoporomoka kutoka kwenye makaazi yao. Anawarausha asubuhi na mapema kwa mabuldoza yanayobomoa makaazi yao. Inakusudiwa kuwa majengo yatajengwa katika ardhi hii inayotamaniwa sana na wenye jiji. Anwambia Mzee Mago kuwa amekuja kula mashamba yao. Hii ni

tamaa ajabu ya mashamba yaliyo na wenyewe.

 

 

3.

Jiji lina tumbo ambalo halishibi. Jiji hili limepambwa vyema na majumba ya kifahari. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmental stores, casinos, viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpira wa vikapu, raga, kabumbu, vyuo vikuu,mahakama na hata hospitali. Ajabu ni kuwa jiji hili halijatosheka kwa usa wake. Jiji l i n a t a k a k u p a n u a t u m b o l a ke h a d i k a t i k a m t a a wa Madongoporomoka.

 

a) Unyanyasaji

 

Hii ni hali ya wahusika kuhiniwa haki ambayo wanastahili na badala yake wengine kupewa haki hiyo kwa haramu. Wanamadongoporomoma wananyanyaswa na viongozi wa jiji. Lic ha ya wao kuwa wamiliki halisi wa mashamba yao, wanapangiwa hila ya kunyang’anywa vipande vyao vya ardhi. Ardhi hiyo inapangiwa njama ya kunyakuliwa bila ya wao kulipwa

dia inayostahili. (Uk 4)

WanaMadongoporomoka pia wananyanyaswa kisheria. Ni mujibu

wa sheria kuwatetea watu wote ambao wamehiniwa au kutendewa

isivyo haki. Mzee Mago anafahamu vyema kwamba kuna

uwezekano mkubwa wa wao kupokonywa mali zao ilhali sharia

itumiwe kuwakandamiza yeye na maskini wenzake.Anaomba

waishie kumpata hakimu ambaye ni mpenda haki ili haki isiuliwe na

asiyestahili kuishia kutetewa na sharia mbovu. (Uk 2)

Majengo makubwa yaliyoko jijini yananuia kuwanyanyasa

wanamadongoporomoka na kumeza vipande vyao vya ardhi.

Vipande hivi vya ardhi vinanuiwa kutumika ili kuwahi kujenga

majengo bora Zaidi.

 

b) Utetezi wa haki

 

Mzee Mago ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha mtetezi wa haki ya wakaazi wa kijiji wa madongoporomoka. Mhusika huyu anawatetea madongoporomoka kutokana na maonevu ya wakuu wa jiji.alijitahidi kuzuia njama ya watu wakubwa kutaka kuchukua ardhi za watu wadogo. Mzee Mago aliwafuata wengine ili kuzungumza kuhusu haki ya unyang’anyaji wa mashamba yao. Yeye hupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia haki isiangamizwe. (Uk 2)

 

4.

Kwa kuwa Mzee Mago anafahamu kwamba haki inauzwa na kupewa watu wasiostahili. Anajua kuwa haki itauzwa. Anafahamu kwamba haki itapewa wengine wasiostahili. Hivyo basi anamtafuta wakili mzuri ambaye hatasaidiana na viongozi dhalimu ili kuwahini mashamba yao.

Mzee Mago anawahamasisha wanamadongoporomoka kutokubali kufurushwa kutoka maeneo yao. Hawaruhusu watu kusahau uvumi wa wao kufurushwa. Anawaita katika kikao na kuwakumbusha uwezekano wa hao kufurushwa. Anawaongoza kutokubali kufurushwa ikiwa wakubwa wa jiji watakuja kuwaondoa kwenye makaazi yao. Baadaye wanamadongoporomoka wanapovamiwa, wanakataa kuondoka hadi wiki tatu baadaye ambapo makaazi yao yanarudi kuchomoza kama uyoga. (Uk 11)

 

 

a) Umaskini

 

 

Ni hali ya kukosa mali/hali ya ufukara au ukata. Umma wa Madongoporomoka unaishi katika hali mbaya ya kimaskini. Mandhari ya kijiji hiki ni ya kimaskini na kufedhehesha mno. Kuna mashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwara vinavyozungukwa na uoza na bubujiko la maji machafu. Kuna uvundo unaopasua mianzi ya pua. (Uk 4). Bila shaka, mandhari haya sio ya mahali ambapo mtu anaweza kufurahia kuwa. Ni mandhari ya mahali ambapo ni masikini tu ndio wanaishi.

 

 

b) Utabaka

 

Hii ni hali ya wahusika kugawika katika makundi tofauti tofaauti kulingana na uwezo wao wa kiuchumi. Kuna tabaka la matajiri na masikini. Kila tabaka limejikita katika shughuli zao wenyewe za kutetea matumbo yao. Masikini wanapigania kutetea makaazi yao ya kimaskini. Wanakataa kata kata kuhiniwa na wachache matajiri ambao wanamiliki mali nyingi. Kwa upande mwingine, matajiri wana matumbo yasiyoshiba. Wananyakua mashamba ya masikini kwa minajili ya kutaka kuendeleza ujenzi wa majumba ya kifahari. Hivyo basi, matajiri wanaishi kuwafurusha masikini kutoka kwenye makaazi yao. (Uk 10-11)

 

5.

a) Migogoro

 

 

Katika hadithi hii panazuka migogoro mbali mbali baina ya wahusika tofauti. Kuna tofauti nyingi ambazo zinazuka kati ya wahusika mbali mbali katika hadithi. Baadhi ya migogoro hii ni kama vile:

a) Mgogoro baina ya Wakuu wa Jiji na wanakijiji wa

Madongoporomoka.

 

 

Mgogoro huu unatokana na hali ya jiji kupanuka na kusheheni kila aina ya majumba kiasi cha kukosa nafasi ya mtu kuvuta pumzi. (Uk 4)Kutokana na hali hii, wakuu wa jiji wanaonelea kuwa mahali pazuri pa kupanua shughuli za jiji lile ni huko Madongoporomoka. Huko ndiko kuna vijishamba ambavyo havina kazi. Vishamba ambavyo vinapaswa kupambwa na majumba mazuri ya kifahari. Kwa upande mwingine, maskini hawa wanaenzi vijumba vyao pamoja na mazingira yao na hawako tayari kuondoka kwa njia yoyote ile. Hali hii inazua mgogoro kati yao na wakuu wa Jiji.

 

 

b) Mgogoro baina ya Bwana mwenye tumbo na wana- Madongoporomoka.

 

 

Bwana Mwenye tumbo ananuia kula mashamba ya wana- Madongoporomoka. Kwa upande mwingine, wanakijiji hawa wanakaidi amri ya kuondoka, pamoja na madhila ya kubomolewa makaazi yao wanamoishi. Licha ya mateso yote wanayoelekezewa wana-Madongoporomoka, wanakataa kuondoka katika mashamba yao na kuruhusu ujenzi wa majumba ya kifahari kutekelezwa. Ni wazi kuwa huu ni mwanzo tu wa mgogoro kati ya wahusika hawa hawa na mporaji huyu wa ardhi.

 

6.

MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.

 

 

Hizi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ili kuleta mvuto katika kazi yake. Mbinu za uandishi ni sawa na mtindo wa mwandishi. Hizi zinahusu upekee wa mwandishi kwa namna anavyoichora kazi yake. Mbinu za uandshi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ili kutupa sisi wasomaji ujumbe wa ziada. Mbinu hizi ni kama vile matumizi ya ndoto, barua, mbinu rejeshi,n.k. mbinu zilizotumiwa katika hadithi hii ni pamoja na:

 

 

1. Takriri

 

 

Takriri ni mbinu ya kifasihi ya kurudiarudia neno au kifungu cha maneno ili kusisitiza au kulitilia mkazo. Mifano ya takriri ni kama ifuatayo:

a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong’ono. Nong’ono zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawa hofu… (Uk 1).

b) …gwa sahau hiyo ni tokeo la lile lile la umoja katika uwili. (Uk 1)

c) Mzee Mago kajifunza kutosahau. Kutosahau hamkumpi hata kidogo… (Uk 2)

d) Itikadi ya wakubwa ilikuwa bado ni ile ile. (Uk 2)

e) Hawawezi…hawawezi, hawawezi, kabisa hawawezi! (Uk 5)

 

 

2. Kinaya

 

 

Kinaya ni hali ambayo mhusika anasema au kutenda kinyume na matarajio. Mifano ya kinaya ni kama ifuatayo:

a) …maana siku hizi wanasheria waaminifu ni adimu kama haki yenyewe. (Uk 2)

b) Ilishikilia kwamba jiji halina nafasi tena. Yaani limejaa kila pahala. Limejaa hiki na kile, hili na lile. Limejaa hadi pomoni. (Uk 3-4)

 

7.

c) Halikuacha hata nafasi ya kuvuta pumzi. (Uk 4)

d) “sharia gani hiyo iko mikononi mwetu?” Aliuliza Mzee

Mago. “Sheria kila wakati iko mikononi mwao.” (Uk 6)

a) “Nitakula chakula chako chote ulichopika kuwauzia wateja wako leo.” (Uk 8)

 

 

1. Taswira

 

 

Taswira ni maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili za msomaji. Mifano ya taswira ni kama ifuatayo:

a) Kuna mashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwara vinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu. Kuna uvundo unaopasua mianzi ya pua. (Uk 4).

b) Wakati huu ndipo pua za wazungumzaji hawa ziliponasa harufu za vyakula vilivyotoka jikoni. Harufu mchanganyiko zilizowaingia puani na kukaanza kulambatia na kukaza mate vinywani mwao. (Uk 6)

c) Jitu lilikuwa limevaa suti nyeusi na shati jeupe. Limekabwa shingoni na tai ya buluu iliyozama kwenye misuli ya shingo fupi nene…(Uk 7)

d) Naam. Vyakula vilipakuliwa. Wali na nazi. Mchuzi na nyama.

Nyama ya kuchoma kwa mkaa na bakuli la kachumbari. Samaki wa kukaanga. Chapatti kadhaa za duara… (Uk 8)

 

 

1. Maswali
ya
Balagha

 

 

Balagha ni mbinu ambapo mwandishi huuliza maswali yasiyohitaji majibu. Maswali haya hulenga kumfanya mhusika au msomaji kukiri kwa kina. Kwa mfano:

a) Aaa, kuna jabu gani lakini mvua ikinyesha? Si kila siku huanguka kupunguza joto …? Si huanguka kuburudisha nafsi zinazohaha na kukata tamaa? (Uk 1)

b) Nani angewashauri wao mburumatari? Sauti zao hazikustahi kusikika, seuze kusikizwa? (Uk 3)

 

 

8.

c) Kwani si kila mtu anafaa kujua kuwa kimya kirefu kina mshindo mkuu? (Uk 3)

d) Tuondoke twende wapi? (Uk 5)

e) Kuwe na mazungumzo gani hasa yatakayomchangamsha kila mtu wakati huu kuliko uvumi ulioanza tena kuvuma? (Uk 5)

f) Aaa, nani anayejua hatimaye? Kesho yenyewe haijazaliwa seuze fumbato ndani ya kesho yenyewe?

g) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo?

(Uk 8)

h) Wakawa wanatazamana kwa wakionyesha hawaamini nini kinachotokea. Itawezekanaje?

 

 

1. Kuchanganya
Ndimi

 

 

Hii ni mbinu ya uandishi ambapo wahusika huzungumza kwa kutumia lugha zaidi ya moja ili kuonyesha hali yao na hisia zao katika mazungumzo. Mbinu hii humwezesha mhusika kujieleza vyema Zaidi kwa kutumia msamiati ambao hauko katika lugha fulani. Kwa mfano:

 

 

a) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo? (Uk 8)

b) Jitu hilo lilikuwa limeketi nyuma ya gari kubwa aina ya Audi

 

Q7…(Uk 10)

 

c) Simama kidogo Chauffer… (Uk 11)

 

 

 

 

 

 

9.

2. Taharuki

 

Taharuki ni mbinu inayotumiwa na waandishi ili kuteka hisia na hamu ya wasomaji kutaka kuendelea kusoma zaidi. Katika kufanikiwa kujenga taharuki, mwandishi husuka matukio yalito na mshikamano na mtiririko ambao humvutia msomaji asiiweke chini kazi hiyo pindi aanzapo kuisoma hadi akie kikomo chake.

a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong’ono. Nong’ono

zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawa hofu… (Uk 1). Msomaji anajiuliza, Ni jambo gani hili ambalo linatarajiwa kutendeka?

b) Kwa Mzee Mago, iliyobaki sasa ni kutazamia siku ya kulipuka mambo…(Uk 3)

Ni mambo yepi yatalipuka? Hii inasalia kama taharuki.

c) Kesho nitaka hapa tena. Niwekee chakula mara mbili kuliko hiki cha leo…(Uk 9)

Tunashangaa ikiwa jitu hilo kweli litarudi.

 

 

1. Jazanda/
Istiari.

 

 

Jazanda ni mbinu ambayo inaonyesha fumbo lililotumiwa na mwandishi kurejelea hali fulani kwa njia che. Istiari kwa upande mwingine inalinganisha moja kwa moja kitu au hali na nyingine lakini bila ya kutumia maneno ya ulinganisho. Mifano:

a) Angepoaje na ule moto unaomlipukia kila mtu pale mtaani umeacha mpaka sasa kovu bichi moyoni…? (Uk 2)

 

 

 

 

 

10.

b) Wakubwa hawatambui kuwa kwamba jambo hilo la kuwafanya wao takataka tu ndilo linalowakasirisha… (Uk 3)

c) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango ya wasiwasi vichwani mwa watu… (Uk 5)

d) Bweu likapasuka na kutoa uvundo wa mnyama aliyeoza… (Uk 9)

Hii ni ishara ya jinsi jitu hili litawahangaisha wanakijiji hawa baadaye.

 

 

2. Tashbihi/Mshabaha

 

 

Tashbiha/Tashbihi/Mshabaha ni maneno yanayofananisha kitu, jambo au kitendo na kingine kwa kutumia vihusishi kama vile ‘kama’,

‘mithili’, ‘ja’, ‘mfano wa’ na kadhalika. kwa mfano:

a) …maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kama maziwa ya kuku! (Uk 2)

b) Ulikuwa ukitukuta ndani kwa ndani kama moto ya makumbi. (Uk 3)

c) Umebaki tu ukining’inia hewani kama mvua inayotarajiwa kunyesha…(Uk 4)

d) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtu aliyechapwa na bakora. (Uk 7)

e) Lilipokula, lililamba sahani zote kana kwamba lilikuwa na jukumu la kuziosha.(Uk 9)

f) …vibanda vya Madongoporomoka viliota tena hapo kama

uyoga. (Uk 11)

 

 

 

 

11.

1. Tashihisi/Uhuishaji

 

Hii ni mbinu ya lugha ya kuweka hisia na uhai katika vitu visivyokuwa na uhai. Pia kuna uwezekano wa kuwapa wanyama uwezo na hulka za binadamu. Mifano:

a) Nong’ono zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. (Uk 1)

b) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukaba koo akina sisi! (Uk 1)

c) Yeye hupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia haki isiangamizwe…(Uk 2)

d) Mzee Mago lakini hairuhusu sahau iketi na kutawala kichwani mwake. (Uk 2)

e) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kila mtu…(Uk 2)

f) Kesho yenyewe haijazaliwa, seuze fumbato…(Uk 5)

g) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango ya wasiwasi vichwani mwa watu… (Uk 5)

h) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtu aliyechapwa na bakora. (Uk 7)

i) Haikuchukua muda mrefu akili zilipowaamsha kuwapeleka maana ya kile…(Uk 10)

 

 

2. Chuku

 

 

Ni mbinu ya kutilia mazungumzo chumvi ili kuyafanya yavutie

Zaidi. Kwa mfano:

a) K w a m i u j i z a , n d i p o j i t u l a m i r a b a m i n e

lilipoingia…halikujulikana lilipotoka. Liliingia tu ghaa..(Uk

6)

b) Lile tumbo lake limezidi kufura na ndani ya tumbo, ugomvi wa

vyakula ukawa unapwaga kwa mingurumo ya radi iliyosikika

hadi nje. (Uk 9)

 

 

 

 

12.

c) Mstari huo ulikuwa umefuatana na mpasuko mkali wa radi na umweso uliomulika mpaka ndani ya mioyo ya watu. (Uk 10)

d) Jitu hilo lilimwaga tabasamu mfululizo iliyoenea eneo lote la

Madongoporomoka. (Uk 10)1. Nidaa

Ni mbinu ya kuonyesha hisia aliyo nayo mhusika. Hujulikana kwa kutumia alama ya hisi. Kwa mfano:

a) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukaba koo akina sisi! (Uk 1)

b) …maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kama maziwa ya kuku! (Uk 2)

c) Pale lilipoketi, lilionekana kupapa jasho ovyo! (Uk 7)

d) Halikubakisha hata chembe moja ya chakula chochote alichopewa! (Uk 9)

e) Hazitatuhamisha kabisa hizi fujo zenu! (Uk 11)

2. Tanakuzi.

Ni mbinu ya kutaja vitu viwili ambavyo sifa zao zimepingana. Kwa mfano:

a) “Hata hivyo, kila mtu, mdogo kwa mkubwa, kike kwa kiume… (Uk 2)

b) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini au tajiri. (Uk 2)

c) Lile jitu lilimkata maneno Mzee Mago, Wakubali, wasikubali…(Uk 8)

d) Watu wanakimbia huku na huku, huku na kule, mbele na nyuma…(Uk 10)

e) Kike kwa kiume, vijana kwa wazee, watoto kwa watu

wazima…(uk 10)

 

 

 

 

13.

WAHUSIKA
NA
UHUSIKA

 

 

a) MZEE MAGO

 

 

Huyu ndiye mhusika mkuu ambaye ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha watetezi wa haki. Ametumika kuwatetea wanyonge kutokana na madhila ya matajiri wanaotaka kuwapokonya mashamba yao. Sifa zake ni kama zifuatazo:

 

 

i) Ni mtetezi wa haki.

 

 

Anakataa kutazama huku wanakijiji wakihiniwa mashamba yao. Anamtafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki ya w a n y o n g e . I s i t o s h e , a n a k a t a a k u w a r u h u s u wanamadongoporomoka kusahau uvumi uliokuwepo hapo awali kuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.

 

 

ii) Ni mwenye hekima/busara.

 

 

Anafahamu vyema matokeo ya wingu linalotarajiwa kutua. Hivyo anajiandaa na pia kuwaandaa wanakijiji ili yatapowasili madhila, wawe tayari wameungana kupigania haki zao.

 

 

iii) Ni mwenye bidii.

 

 

Ni yeye tu aliye na mkahawa pale madongoporomoka, ishara ya kwamba ni mtu mwenye bidii ya mchwa.

 

 

 

 

14.

iv) Ni mwenye ushawishi

 

 

Anafaulu kuwahamasisha wanakijiji wote kujiandaa ili kukabiliana na vita vinavyokuja vya kunyang’anywa vipande vyao vya ardhi. Isitoshe anawaandaa wanamadongoporomoka kupinga hila zitakazokuja na kukataa kuondoka kwenye mtaa wao. Hatimaye wanapovamiwa na kubomolewa makazi yao, wanakaidi na kukataa kuondoka, jambo linalowapa ushindi baadaye.

 

 

v) Amepevuka

 

 

Anafahamu ka uzito wa kesi na ubishi unaotokana na ardhi. Isitoshe ana ufahamu mzuri wa namna ambavyo haki haipatikani kwa urahisi. Hivyo anaamua kumtafuta wakili aliye mwaminifu ambaye hatimaye anawaokoa kutokana na makucha ya matajiri wenye tamaa. Wanarudia kujenga vibanda vyao upya.

 

 

a) JITU LENYE TUMBO

 

 

Mhusika huyu hatujapewa jina lake halisi ila matendo yake ndiyo yanashangaza. Sifa zake ni kama zifuatazo:

 

 

i) Ni katili

 

 

Hana huruma anapobomoa makazi ya maskini. Anawafumania asubuhi na mapema na kuwafurusha. Anabomoa makazi ya watu ambao hawana pahala pengine pa kuita kwao, huku akiangua kicheko akiona namna wanavyohangaika.

 

 

 

 

 

15.

ii) Mwenye tamaa

 

 

Anatamani ardhi za maskini wa Madongoporomoka na kuwapangia njama ya kuwafurusha kutoka makwao. Ingawa ana uwezo wa kutumia buldoza na polisi, anaishia kushindwa katika wizi wake na maskini hawa kurejelea makaazi yao.

 

 

iii) Mwenye dharau/Kiburi

 

 

Anawazungumzia Mzee Mago na wenzake pale kwenye mkahawa kwa dharau na mabezo.

 

 

iv) Ni Mla

 

 

Anafyeka vyakula vya aina mbali mbali bila kusaza chochote. Vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja pale kwenye mkahawa vinaliwa na yeye pekee. Mwishowe anatoa bweu kubwa linalochafua hewa yote pale.

Mhusika huyu ametumiwa kama kielelezo cha watu wenye tamaa mbaya ya mali, waliojawa na ukatili na wanaoweza kutenda ukatili wowote ili kupata mali.

 

 

Kabwe, Bi.Suruta na Bi. Fambo.

 

 

Hawa ni wana-Madongoporomoka ambao wanaoshirikiana na Mzee Mago ili kujiandaa kwa wingu ambalo lingeanguka hapo baadaye. Ni wazi kwamba wahusika hawa ni wenye hekima na waliomakinika kwa mambo yajayo. Wahusika hawa wametumiwa kama kielelezo cha viongozi wenye mioyo ya ujasiri wa kupigania jamii zao.

 

 

 

 

 

 

 

16.

2.MAPENZI YA KIFARAUNGO Historia ya Mwandishi.

 

 

Mwandishi wa hadithi hii anaitwa Kenna Wasike. Ni mwandishi ambaye yuko katika harakati zake za mwanzo katika ulimwengu wa uandishi. Yeye ni mwalimu aliyesomea chuo kikuu cha Nairobi.

 

 

Dhamira

 

 

Mwandishi amekusudia kutahadharish wasomaji wake dhidi ya kugawanywa kwa misingi ya utabaka. Analenga kukashifu migawanyiko ya watu kwa kuzingatia uwezo wao wa kiuchumi.

 

 

Ufupisho wa Hadithi

 

 

Mwandishi anatumia nafsi ya kwanza katika masimulizi yake. Anatupa hadithi yake mwenyewe akiwa chuo kikuu. Ingawa amefaulu kuka chuo kikuu, maisha sio mepesi kwa namna yeyote. Wazazi wake ni maskini hohe hahe wanaopigania mikono kuka kinywani tu. Bidii yake ndiyo ilimkisha katika chuo kikuu. Msimulizi anapoka katika chuo kikuu, anashangaa namna ambavyo wanafunzi wengi wanaandamana kwa mapenzi. Ingawa anatamani, haimpitii mawazoni mwake ya kwamba naye pia angeweza kuwa na mpenzi huko chuoni. Masomo chuoni ni magumu na ambayo hayaeleweki kwa wengi wa wanafunzi hao, ingawa wanajitahidi. Mwalimu anayewafunza ni Dkt. Maboga ambaye anatema dhana nzito nzito za fasihi. Wanafunzi wengi wanauliza maswali ilikuelewa Zaidi anavyomaanisha mwalimu huyu. Bila shaka hawaelewi mambo anayosema huyu mwalimu, lakini nani atadhubutu kumuzomea daktari mzima?

 

17.

Siku moja baada ya msimulizi kupika uji wake na kujiandaa kunywa, anasikia mtu akibisha mlangoni. Anapofungua, anamkuta binti mmoja mrembo ambaye baadaye anagundua kwamba ni mwanafunzi mwenzake nye darasa moja anayeitwa Penina. Penina anadai kwamba anampenda Dennis bila kujali umaskini wake. Ajabu ni kuwa Penina ni binti wa Waziri. Ni kinaya kwa msichana wa haiba yake kumpenda maskini kama Dennis. Baada ya masomo yao, Dennis na Penina wanaishi pamoja huku wazazi wa Penina wakilipa kodi ya nyumba na matumizi yao yote. Dennis anajaribu kutafuta kazi bila mafanikio. Anapata fursa katika shirika la uchapishaji wa magazeti. Anapopatikana katika chumba cha udodosi, anashindwa kufungua kinywa chake na kujitetea ni kwa nini anahitaji kazi ile. Dennis anafurushwa kutoka chumba cha udodosi kwa haya nyingi usoni na majuto mengi moyoni.

 

 

Anaporejea nyumbani, anamkuta Penina ameketi akitazama televisheni. Anataka kupewa chakula ila anaariwa kuwa hakuna chakula chochote kile. Penina anamwarifu kuwa chakula hakipo kwani yeye Dennis hakuwacha chochote cha kuliwa. Kisha Penina anataka kujua ikiwa Dennis amefaulu kupata kazi. Dennis anapojibu kwamba hakufaulu, jibu la Penina linamshangaza. Penina anamwambia kwamba anajutia uamuzi wake kuolewa kwake. Anajuta kutowasikiliza wazazi wake kwani walimwonya kutokana na Dennis. Anadai kuwa anataka kuolewa na mtu mwenye kazi nzuri na pesa. Kisha Penina anishia kumfukuza Dennis kutoka kwake. Anamwamrisha afunge virago vyake na kuondoka. Dennis anapomdadisi kuhusu mapenzi yao, anamhakikishia kuwa yeye hataki kuolewa na maskini kama yeye. Ni ajabu kuwa mapenzi ya Penina yameyeyuka.

 

 

18.

Ni mapenzi ya kifaraungo. Dennis akiwa anaondoka na begi lake, anasikia sauti ikimwamuru nyumba ile aione paa na asiwahi kurejea. Hali hii inamletea majuto si haba. Kweli mapenzi ya Penina yalikuwa

na kifaraungo. Yaguzwapo tu na wimbi ndogo yananyauka.

 

 

MAUDHUI

 

 

Baadhi ya maudhui yanajitokeza katika hadithi hii ni kama vile:

a) Elimu

Hii ni hali ya mhusika kupata maarifa yanayonuiwa kumpevusha kimawazo. Kuna aina mbili kuu za elimu:

 

 

i) Elimu ya Vitabu.

 

 

Hii ni elimu ambayo wahusika huipata kwa kuhudhuria madarasa shuleni na kuelimishwa katika masomo mbalimbali. Baadhi ya masomo haya ni kama vile kemia, hisabati, bayolojia, Kiswahili, kingereza, na masomo mengine mengi mno. Elimu hii hutumika kuwasaidia wanafunzi kuingia katika taaluma mbalimbali kama vile udaktari, ualimu, uhandisi na kadhalika. Penina na Dennis wanakutana pale kwenye chuo kikuu wakiwa wanafunzi wa fasihi. Wanatafuta elimu hii ili kuwahi kupata ajira bora baadaye. Ni elimu hii ambayo Dennis anaitumia kutafuta kazi katika shirika la uchapishaji wa magazeti. Watu wote wanaoendelea na kufanikiwa kwenye elimu hii huishia kufaulu sana maishani katika kupata taaluma wanazozipenda wao wenyewe. Wanafunzi wote katika chuo kikuu wanatia bidii masomoni ili waweze kupata kazi za aina mbali mbali.

 

 

 

 

19.

ii) Elimu ya Maisha.

 

 

Elimu hii haihisiani na elimu ya vitabu. Haya ni maadaili anayokuzwa nayo mtu. Ni mkusanyiko wa tabia na itikadi njema ambazo mja hukabidhiwa katika aushi yake ili kuweza kutangamana vyema na umma. Dennis alikuzwa vyema na kufundishwa kuwaheshimu watu. Isitoshe, ni mvulana aliye na tabia nzuri. Anapoenda chuo kikuu, hajihusishi na tabia zinazoelekeza kupotoka kwake kwa maadili. Anawaheshimu wote. Kwa upande mwingine, Penina amelelewa kwa kuwabagua watu kwa misingi ya pesa uchumi wao. Ni wazi kuwa muda wote huu, alikuwa ameyacha makucha yake tu.

 

 

a) Mapenzi

 

 

Mapenzi ni hali ya kumkubali mtu wa jinsia tofauti na kumuenzi pamoja na kujihusisha naye katika mahaba. Mapenzi yanayoonekana katika muktadha huu ni ya aina mbili:

 

 

i) Mapenzi ya kifaraungo.

 

 

Penina ndiye anadhihirisha mapenzi haya. Anampenda Dennis ingawa kwa masharti. Licha ya wao kuishi pamoja, anamwambia Dennis ya kwamba hawezi kuolewa na mtu asiye na pesa. Ni wazi kuwa mapenzi yake hayaamuliwi na uzuri wa penzi bali kiwango cha pesa alichonacho mtu. Punde tu penzi lao linapoguzwa na upepo mdogo tu (ukosefu wa ajira) linanyauka na kupotelea mbali.

 

 

 

 

20.

ii) Mapenzi ya dhati.

 

 

Dennis anampenda Penina kwa keweli. Anaishia kumpenda na hata kumtambulisha kwa wazazi wao. Ingawa alikuwa anashuku ukweli wa Penina kumpenda maskini kama yeye, anajitolea na kumpenda Penina kwa dhati. Anatazamia kumuoa haswaa pindi atakapopata kazi.

 

 

b) Utabaka

 

 

Hii ni hali ya jamii kugawika katika makundi tofauti kulingana na uwezo wa kifedha. Mahusiano yote kati ya wahusika yanaongozwa na fedha walizo nazo mfukoni. Penina anaonywa na wazazi wake kujihusisha na Dennis kwani yeye ni maskini. Ingawa anakataa mawaidha ya wazazi wake hapo awali, anaishia kumfurusha Dennis kwani anamwona kama maskini asiyefaa kumwoa.

 

 

c) Umaskini

 

 

Msimulizi wa hadithi hii (Dennis) ndiye kielelezo cha maskini wanavyoishi. Alisoma kwa shida kwani karo ilikuwa kero kubwa. Ni wazi kwamba jamii yake inamtazamia yeye kuikomboa kutokana na umaskini wao. Ingawa amefaulu kuka chuoni, chumba chake Dennis ni kitupu kisichokuwa na chochote cha kutamaniwa. Anapohisi njaa, anagutukuka kuwa hana chochote cha kupika. Anaamua kupika uji. Baadaye anagundua kwamba hata sukari ya kutia kwene uji wake mweupe hana. Anaishia kunywa uji hiyo bure kwa kujihurumia.

 

 

 

21.

Ingawa Dennis anafaulu kumpata mpenzi anayempenda, anajitegemeza kwake kwa kiasi kikubwa. Wanaishi pamoja lakini ni wazaziwe Penina wanaowakimu mahitaji yao yote sio Denniskwani yeye ni maskini. Baadaye, Penina anapochoshwa na Dennis anamfurusha. Ni ajabu kuwa Dennis anabeba kila kilicho chake kwenye begi moja tu! Anatembea akijutia masomo yaake ambayo hadi sasa hayajamsaidia kustawisha misuli yake ya kiuchumi. Anashangaa jinsi ataweza kuwaokoa wazazi wake na umaskini uliowagubika.

 

 

a) Ukosefu wa Ajira

 

 

Ajira ni adimu katika nchi anayoishi Dennis. Ametembea katika makampuni mengi na mashirika mengi akipeleka nyaraka za kuomba kazi. Amebisha huku na kule akiwacha tawasifu yake na ya Penina lakini tangu kumaliza masomo ya chuo kikuu, miaka mitatu baadaye hajafaulu kupata kazi. Dennis anaishia kufurushwa na mpenziwe kwani hana uwezo wa kukimu mahitaji yao ya kifedha.

 

 

a) Majuto

 

 

Dennis anachorwa kama mhusika anayejutia maisha yake. Anajutia umaskini wake kwani Penina anamfurusha kwa kisingizio kuwa yeye hawezi kutoa hela zozote za chakula na matumizi ya pale nyumbani. Anajutia kisomo chake kwani anatumaini kuwa kitampa ajira lakini ng’o! Anajuta akiwakumbuka wazazi wake na kukiri jinsi ambavyo anaweza kuwasaidia ili kuwaondoa katika umaskini. Anajutia bidii yao ya kumsomesha kwani sasa hivi hawafai wazazi inavyostahili.

 

 

22.

Anajutia fumbo ya maisha kuwa kinyume naye katika kila jambo analofanya. Anajutia kuonewa na maisha.

 

 

MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI. a) Tashihisi

 

 

i) Ninafuta chozi linalochungulia machoni. (Uk 13)

ii) Njaa inanitafuna kama mbwa anvyoguguna mfupa. (Uk 17) iii) Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa hatimaye. (Uk 20)

iv) Mapenzi yasiyujua kufa. (Uk 20)

v) …bado bahati yangu haijasimama. (Uk 22)

 

 

b) Tashbihi

 

 

i) …kumuibia bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutajaria kuyapata maziwa kutoka kwa kuku. (Uk 13)

ii) …sasa anaanza kututamkia maneno machungu kama shubiri. (Uk 14)

iii) Mapenzi ni matamu kama uki…(Uk 26)

iv) Njaa inanitafuna kama mbwa anvyoguguna mfupa. (Uk 17) v) Almuradi maskini na matajiri wametengana kama ardhi na mbingu. (Uk 17)

 

 

vi) Mwili mzima unaanza kutetemeka kama ndama aliyenyeshewa…(Uk 17)

vii) Waamatunaapendana kama ulimi na mate. (Uk 21)

viii) Wanafanana kama riale kwa ya pili. (Uk 23)

ix) Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa… (Uk 25)

 

 

23.

a) Kuchanganya ndimi

 

 

i) Wanabeba vipakatalishi na Ipad zao mikononi, sa kabisa! ii) Hatimaye nimeka kwenye ghorofa ya tatu katika jumba la makazi ya Mastura Hall. (Uk 16)

iii) Mimi na Penina tunaishi katika mtaa wa New Zealand. (Uk

22)

iv) …basi ni wazi kuwa your competence is doubtful. (Uk 25)

v) Unajua tangu nianze tarmacking sijawa nikitazama runinga. (Uk 26

 

 

b) Nidaa

 

 

i) Wanabeba vipakatalishi na Ipad zao mikononi, sa

kabisa! (Uk 13)

ii) Laiti mama yangu angeliweza kunisomesha hadi shule ya kitaifa! (Uk 13)

iii) La hasha! (Uk 14)

iv) Looh! Kwani swali langu vipi? (Uk 15)

v) Lo! Nitakula nini? (uk 17) Lo! Mlangoni yuko msichana mmoja mrembo. (Uk 18)

vii) Ah! Pengo gani ilhali una mapenzi ya kweli…? (Uk 19)

 

 

a) Misemo na nahau.

 

 

i) Nikatupa macho huku na kule. (Uk 12)

ii) Analaza damu usiku na mchana. (Uk 14)

iii) Licha ya uchechefu wa pesa, nimejikaza kisabuni. (Uk 21)

iv) Mama na baba wanakula mwata. (Uk 28)

v) Lakini sitakata tamaa. (Uk 28)

 

 

24.

a) Uzungumzi nafsia.

 

Mbinu hii imetawala kote kwenye hadithi kwani haya ni masimulizi katika nafsi ya kwanza. Mifano michache ya mbinu hii ni kama:

i) “Kwa nini ninalia sasa?” (Uk 13)

 

b) Kinaya

 

i) Unajua watu waliosoma sana kama Daktari Mabonga hawajui lolote wala chochote. (Uk 14)

ii) Utajifundishaje kula na chakula hukitafuti? (Uk 15)

iii) Masomo ya chuo kikuu si masomo, ni madubwana

yasiyojulikana yalikotoka.(Uk 15)

iv) Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi.

Sina majibu. (Uk 25)

 

c) Maswali ya Balagha.

 

i) Itakuwaje wewe ufundishwe kujinadhishia kesho yako? (Uk 15)

ii) Utajifundishaje kula na chakula hukitafuti? (Uk 15)

iii) Lo! Nitakula nini? (uk 17)

iv) Nifunge mlango au nifungue? (Uk 17)

v) Mbona asiketi kitini?…kwani ni lipi alilojia humu? (Uk 18)

vi) Kabwela kama mimi nina faida gani? (Uk 23)

 

a) Chuku.

 

i) Darasa zima linangua kicheko. Msichana mmoja amecheka hadi ameanguka. (Uk 15)

ii) Mtazamo wake unaweza kumwamsha mbwa aliyelala. (Uk 18) iii) Ukimtazama machoni, machozi ya furaha hayaachi kukutonatona. (Uk 18)

iv) …kitambo kirefu kilichatawaliwa na kimya- kimya cha kuanguka pamba uusikie mlio wake. (Uk 18)

v) Wasikilizaji wako watacheka mpaka midomo ianguke. (Uk 22)

vi) Akanyagapo chini ardhi inatetemeka. (Uk 22)

 

 

 

 

25.

a) Methali.

i) Mzungu wa kula haufunzwi mwana. (Uk 15)

ii) Ujapokosa la mama, hata la mbwa huamwa. (Uk17)

iii) Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezi. (Uk 20)

iv) Mume ni mume hata akiwa gume gume. (Uk 21)m

v) Mgomba changaraweni, haupandwi ukamea. (Uk 27)

 

 

WAHUSIKA NA UHUSIKA.

1. Dennis (Msimulizi)

 

 

Huyu ni mvulana aliyesoma kwa bidii licha ya umaskini wake na kuka chuo kikuu, ni mpenziwe Penina. Ana sifa zifuatazo:

 

 

a) Mwenye bidii.

 

 

Licha ya umaskini uliopo pale nyumbani, anatia bidii masomoni. Anasoma na kufanya vyema kuanzia shule ya msingi, shule ya upili hadi chuo kikuu. Pia ana bidii ya kutafuta kazi ili aweze kuwasaidia wazazi wake na pia kumwoa mpenzi wake Penina.

 

 

 

b) Mwenye mapenzi.

 

 

Anampenda Penina kwa dhati. Anamuenzi na kutaraji kuwa siku moja atamwoa Penina. Anamwonyesha kwa wazazi wake ambao wanafurahia sana kumwona mwanao akiwa na mpenzi akama Penina.

 

 

 

 

 

26.

a) Mwenye matumaini.

 

 

Ana matumaini ya kupata kazi ndiposa anatia bidii masomoni. Anaahidi kumwoa Penina endapo angepata kazi ambayo ingemwezesha kukimu mahitaji yao. Ana matumaini kwamba ingawa hana kazi sasa hivi siku moja bahati itamfungulia milango na mambo kumwendea vyema akapata kazi nzuri.

 

 

b) Ni mwoga.

 

 

Anapopewa fursa ya kuzungumza katika udodosi wa kazi katika shirika la uchapishaji wa magazeti, anaogopa kufungua kinywa chake. Kijacho chembamba kinamtiririka huku akitetema na kukosa maneno. Anafurushwa kutoka chumba kile bila kutamka chochote.

 

 

a) Mwenye majuto.

 

 

Licha ya yeye kutia bidii maishani na masomoni, anajuta kwamba bahati inakataa kumfungulia milango ya heri. Anajuta kutokuwa na kazi kwani anafurushwa kutoka chumbani na mpenziwe. Pia anajutia kutowasaidia wazazi wake baada ya wao kumsomesha kwa shida mno. Anajuta kumwamini Penina na kukubali mapenzi yake ya kifaraungo.

 

 

 

 

 

27.

1. Penina

 

 

Huyu ni mpenzi wa msimulizi ambaye walikutana kule chuo kikuu wakisoma katika darasa moja. Anampenda msimulizi na kuahidi kuoana naye watakapokuwa matajiri.

 

 

a) Ni mzembe.

 

 

Anaketi chumbani mchana kutwa bila kufanya kazi yoyote ile.Kazi ni kutazama televisheni tu. Tawasifu zake zinapelekwa maosini na Dennis. Hana bidii ya kutafuta kazi. Anaamini kuwa Dennis ndiye anafaa kutafuta hela.

 

 

b) Mwenye unaki.

 

 

Licha ya yeye kudai kumpenda msimulizi, ni wazi kuwa penzi lake ni la kifaraungo. Upendo wake unaongozwa na tamaa ya pesa na utajiri. Anajifanya kumpenda Dennis lakini ukweli ni kwamba alitazamia ya kwamba Dennia angepata kazi ili waweze kuoana.

 

 

a) Mwenye tamaa.

 

 

Tamaa yake ya pesa inadhihirika wakati ambapo utulivu wake unakia kikomo. Anamfurusha Dennis kwa umaskini wake. Anadai kuwa hawezi kuolewa naye kwani Dennis hana pesa. Anaweza tu kuolewa na mtu mwenye pesa.

 

 

 

 

 

 

 

 

28.

b) Mwenye mawazo ganda.

 

Penina anaamini kuwa ni mwanaume tu ambaye anapaswa kutafuta hela. In

gawa wote wawili wameelimika, Penina hana bidii ya k u t a f u t a k a z i . A n a m wa c h i a j u k u m u h i l o D e n n i s anayezunguka katika maosi mengi bila mafanikio.

 

1. Daktari Mabonga.

 

Ni mwalimu wa fasihi katika chuo kikuu cha Mavuko. Ni wazi kuwa yeye ni mwalimu asiyependa kudadisiwa kwa vyovyote vile. Ni chanzo cha namna ambavyo mafunzo yanatendeka katika vyuo vikuu.

 

a) Mwenye hekima

 

Anatema maneno yaliyojawa na hekima na maarifa anapozungumza na wanafunzi wake. Anawapa maarifa kuhusu maisha ambayo yanawasubiri baada ya masomo yao. Anawanoa wanafunzi wake vilivyo.

 

b) Mwenye kiburi/mabezo.

 

Licha ya yeye kufundisha vizuri wanafunzi wake hawamwelewi. Anatumia lugha ngumu inayowashangaza wanafunzi. Wanafunzi wake wanapomtaka atumie lugha nyepesi ili waweze kuelewa, anawajibu kwa kiburi na mabezo.

 

c) Mwenye mapuuza.

 

 

Anapuuza maswali anayoulizwa na wanafunzi wake na kuyaona ya kitoto. Anatupilia mbali maswali yote yanayoibuliwa na wanafunzi wake wa fasihi.

 

 

29.

1. Shakila

Huyu ni msichana ambaye walisoma pamoja na Dennis kwenye chuo kikuu. Mamake ni mkurugenzi mkuu katika shirika la uchapishaji wa magazeti. Ametumiwa na mwandishi kuendeleza maudhui ya ubaguzi.

 

 

a) Mwenye dharau.

Anapomkuta Dennis osini akisubiri kufanyiwa udodosi, anazungumza naye kidogo na kisha kutoa cheko kubwa lenye dharau linalomkera Dennis. Hii ni ishara tosha kwa Dennis kwamba hatapata kazi yoyote pale.

 

 

b) Mwenye unaki.

Anapomkuta Dennis osini, anamsalimu na kumzungumzia vyema. Ajabu ni kwamba anapoingia oni kwa mhazili, anatoa cheko kubwa pamoja na mamake. Anamcheka Dennis bila shaka.

 

 

2. Mamake Shakila.

Mhusika huyu ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha watu wenye mitazamo hasi kwa wenzao, wenye mabezo na kujishaua. Ingawa ni mkurugenzi hana utu wa ukurugenzi. Sifa zake ni panmoja na:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

30.

3. SHOGAKE DADA ANA NDEVU

 

Historia ya Mwandishi.

Mwandishi ni mojawapo ya waandishi chipukizi wenye uwezo wa

kipekee wa kubuni kazi za fasihi. Ni mwalimu aliyewahi kuandika

Makala mbalimbali ya Kiswahili. Isitoshe ana tajriba ya muda

mrefu wa kufundisha Kiswahili katika shule mbali mbali.

 

Dhamira

Mwandishi wa hadithi hii amedhamiria kuwaonya vijana dhidi ya

kujihusisha na mapenzi ya kiholela. Anawatahadharisha vijana

kuhusu hatari za kushiriki mapenzi ovyo ovyo. Hatari hizi ni mimba

za mapema pamoja na kukumbana na mauti wakati wa kuavya

mimba.

 

Ufupisho wa Hadithi

Hadithi hii inawasawiri wazazi wawili ambao wamejukumika

kuwalea wanao vyema. Bwana Masudi na Bi. Hamida

wamejukumika vilivyo na kumlea binti na mwana wao kwa

uangalifu mkubwa. Wamemfunza dini na tabia njema.

Wanamlinganisha binti yao na wasichana wengine pale kijijini na

kuwona bora zaidi kuwaliko. Jina la msichana huyo ni Saa.

 

Saa anawaomba wazazi wake ruhusa ya kumleta shogake anayeitwa Kimwana ili waweze kusoma kwa pamoja. Wazazi wake Saa hawana pingamizi kwa ombi hilo kwani wanamtakia binti yao fanaka katika masomo yake na ikiwa kuna shogake ambaye wanaweza kufaana katika kudurusu, basi hawaoni tatizo lolote. Kimwana anakuja siku baada ya nyingine na kudurusu pamoja na Saa kwenye chumba chake Saa. Kila anapokuja, mama mtu anawaruhusu kujifungia chumbani ili nduguye Saa asiwasumbue wakiwa katika shughuli za kudurusu.

 

Ajabu inayokuwepo ni kuwa wazazi wa Saa hawajawahi kumsikia huyo shogake Saa akizungumza. Ni “Marahaba” tu ndiyo inamtoka kila anapokuja kusoma pamoja na Saa na kisha wanaandamana na kujifungia kwenye chumba cha Saa ili kuendeleza masomo yao. Hakuna anayewasumbua, iwe ni mama, baba au ndugu, kwani wanahitaji muda wao wa kutosha ili kusoma ipasavyo! Wazazi hawamwoni Kimwana kuwa na ila yoyote ile.

 

31

Baada ya miezi sita hivi, tatizo linaingia. Mama saa anaanza kuona mabadiliko katika mwili wa bintiye. Habaini ikiwa ni mawazo yake tu ama ni kweli kwamba mambo yalikuwa yakitendeka. Anapomdadisi bintiye, Saa anakana kuwepo kwa jambo lolote lile lenye utofauti katika mwili wake. Ila mamake anatambua ya kwamba kuna jambo. Lakini ushahidi atautoa wapi vile? Hajui. Anatulia tuli ila moyoni anasalia na done chungu la tuhuma kwa bintiye. Anapomuuliza babake Saa, mume anamzomea na kumhujumu kwa kumtuhumu bintiye.

 

 

Siku ya siri kujulikana inapowadia, wanakuwa wameketi baba, mama na ndugu mdogo wa Saa. Ndugu anamweleza mamake jinsi ambavyo yeye na rakiye walikuwa wakicheza. Walicheza mchezo wa kujicha. Ila alipatikana kila mahala alipojaribu kujicha. Ndipo Lulua akaamua kujaribu kujicha katika chumba cha dadake. Akafungua mlango na kuona aliyoyaona. Aliwapata Saa na shogake wamelala kitandani. Walikuwa wamelala lakini huyo shogake ambaye muda wote huvalia buibui na kudhaniwa ni mwanamke, alikuwa na ndevu. Mama anagutuka na kudhihirisha tuhuma zake za siku nyingi.

 

 

Kwa sadfa wakati huo, simu inalia. Baba Saa anapojibu, huyo anayempigia simu anampa habari zinazomkata maini. Saa amekuwa maiti. Saa anakuwa kaaga baada ya kujaribu kuavya mimba. Sasa inabainika wazi kwamba yule Kimwana anayeruhusiwa na wazazi wa Saa kuja kusomea hapo nyumbani pamoja na Saa hakuwa mwanamke, bali mwanamume anayejihusisha kimapenzi na Saa, mapenzi ya siri yanayoishia kumsha saa.

 

 

 

32.

MAUDHUI

Maundhui mengi yameangaziwa katika hadithi yakiwemo:

 

 

a) Unaki

Saa ni msichana anayeaminika kwa wazazi wake. Wazazi wake wanajiamini wakijua kwamba binti yao ameshika maadili mema ya jamii. Isitoshe, anakuwa kajiweka na kuwekeka vyema. Anakuwa msichana mwenye tabia na heshima zake. Saa anapowaomba ruhusa ya kumleta raki yake pale nyumbani kwa madhumuni ya masomo, hakuna anayeshuku. Ajabu ni kwamba Saa anawadanganya wazazi wake. Yule anayedhaniwa kuwa msichana alikuwa mwanamume mwenye ndevu ambaye wanalala pamoja kule chumbani muda wote ule wanaodhaniwa wanasoma. Matokeo ya siri hiyo ni mimba ya mapema inayoishia kumkatizia saa masomo yake na pia kumletea mauti. Huu ni unaki wa hali ya juu.

 

 

b) Majuto

Wazazi wa Saa wanajuta kumruhusu binti yao kumleta mgeni nyumbani kwao kwa madhumuni ya kusoma, jambo ambalo halikutendeka hivyo. Badala ya kusoma, Saa anajihusisha kimapenzi na Kimwana na kwenda kinyume na maadili aliyofunzwa na wazazi wake.

Ni wazi kwamba Saa pia anajutia vitendo vyake. Anapozungumza na mamake, anaonekana kuwa mwingi wa haya kwa kujutia vitendo vyake. Ni fedheha hiyo inayomwelekeza kutaka kuavya mimba, jambo ambalo

linamwangamiza.

 

 

 

 

33.

c) Malezi

Bwana Masudi na Bi. Hamida wamejukumika kumlea binti na

mwana wao kwa uangalifu mkubwa. Wanamkuza Saa na

kumpanda katika maadili. Wanamfundisha akujiwelka vizuri kama

mtto wa kike. Wanampa ushauri mwema utakaomfaa maishani.

Isitoshe elimu ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwao.

Wanahakikisha kuwa wamemwelimisha binti yao. Ni furaha na

shauku ya wazazi hawa kushuhudia saa akipaa na kuendelea

masomoni. Wanapomwona akiwa na raki anayeweza kumsaidia

kuimarika masomoni, wanampa nafasi yao kusoma kwa makini bila

kusumbuliwa hata kidogo. Wanamruhusu Saa kujifungia

chumbani na rakiye ili waweze kusoma kwa pamoja. Haya ni

malezi mema kwa watoto hawa.

 

 

 

a) Mapuuza

 

Wazazi wake Saa wana mapuuza. Wanapoambiwa ya kwamba Saa na Kimwana wanasoma huko chumbani walikojifungia, wanaamini tu. Hakuna yeyote anayeshuku ikiwa ni uwongo. Hata hawashangai ni kwa nini shoga huyu Kimwana hapendi kuketi sebuleni au hata kuzungumza nao. Wazazi hawa wanafungia macho uwezekano wa Kimwana kuwa samba anayevamia zizi la kondoo.

Kando na hapo, hakuna aliyewahi kujaribu kudhibitisha ukweli wa vijana hawa wawili kusomea chumbani. Wazazi h a wa wa n a p o a m b i wa n i m a s o m o ya n ayo k u wa yakiendelea, hawatilii shaka ukweli huo bali wanaamini moja kwa moja. Haya ni mapuuza ya hali ya juu. Mapuuza ya wazazi hawa yanaishia kumuangamiza Saa kwani

anaaga baada ya kujaribu kuavya mimba.

 

34.

b) Mapenzi

 

Kuna aina mbili za mapenzi yaliyoangaziwa karika hadithi hii:

 

i) Mapenzi ya dhati.

 

ii) Mapenzi ya uwongo.i)

 

 

 

Mapenzi ya dhati.

Haya ni mapenzi ya kweli kati ya wahusika. Mapenzi haya yanaweza kuwa kati ya ndugu wawili au kati ya mzazi na mwanawe au kati ya wahusika wawili wenye jinsia tofauti. Bwana Masudi na Bi. Hamida wanampenda binti yao. Upendo huu unadhihirika kwa namna ambavyo wanamlea kwa makini. Wanahakikisha kwamba binti huyu amekuzwa kwa maadili mema, amefundishwa kujiweka sawasawa. Akilinganishwa na wasichana wengine pale mataani, hakuna msichana wa kifuu chake. Huu ni upendo wa kweli. Isitoshe, wazazi hawa wanadhamini masomo ya binti huyu na kumpa msaada wotote kadri ya uwezo wao. Wanamtakia Saa mema maishani.

 

 

Bwana Masudi na Bi. Hamida wanapendana kwa dhati. Hawa ni wazazi wawili wenye mapenzi ya dhati kati yao. Wanazungumza mambo mazito na ya ndani kila jioni wakisubiri usingizi uwachukue. Wao huzungumza mambo yote yaliyopo ndani ya nafsi zao. Haya ni mapenzi ya dhati.

 

 

 

 

 

 

 

 

35.

ii) Mapenzi ya uwongo.

 

 

Mapenzi haya ni yale ambayo huibuka tu kwa mshawasho wa ujana na tamaa za mwili. Mapenzi haya yamejitokeza katika uhusiano uliopo kati ya Saa na Kimwana. Matokeo yake ni mimba haram u ambayo inamtia Saa mashakani. Wanapojaribu kuitoa wanamletea Saa mauti. Waama, mapenzi haya huwaletea wahusika majuto.

 

 

a) Elimu.

Elimu ya vitabu ni muhimu kwa maisha ya baadaye. Saa anahimizwa kutia bidii masomoni ili aweze kupata nafasi katika shule ya upili. Wazazi wake Saa, Bwana Masudi na Bi.Hamida wanamsaidia binti yao kwa lolote atakalo mradi tu apite mtihani huo wa shule ya upili. Katika kumsaidia Saa kupita mtihani, wanamruhusu kumwalika rakiye ambaye anamsaidia katika masomo yake. Wanasaidiana ili wote wawahi kupita mitihani yao na kuelekea katika shule za upili.

 

 

MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI. a) Majazi

i) Bwana Masudi-

ii) Kimwana- Hili ni jina ambalo linapendekeza jinsia ya mtu huyu anayedhaniwa kuwa mwanamke. Yeye ni Mwana (MVULANA) bali sio msichana.

iii) Saa- jina hili linapendekeza kuwa mhusika huyu ni sa wa tabia. Ni kweli kwamba yeye ni sa lakini mwisho tu ndio anatia doa hulka yake.

iv) Lulua- hiki ni kitu cha thamani mno. Mwana huyu anapendwa mno na wazazi wake.

 

 

36.

b) Tashihisi

i) …wanapokuwa kitandani wakingojea usingizi mtamu uwachukue.. (Uk 29)

 

 

c) Maswali ya balagha

i) Wangapi wanaozaa watoto wazuri kama au kuliko Saa wetu. Na watoto hao hutokezea kuwa na balaa tupu? (Uk 29)

ii) Ya nini ushungi huo? (Uk 31)

iii) Si hubaki humo mpaka wamalize kusoma na kujadiliana? (Uk

32)

iv) Itakuwaje waamini kila kitu anachesema Saa? (Uk 32)

v) Kweli? Uongo? Kweli au uongo yale maneno ya binti yake?

 

a) Nidaa

i) …lakini matendo yake afadhali ya mbwa, tena mbwa koko! (Uk 29)

ii) Saa mama, umo ndani mwenu ‘vyo! (Uk 31)

 

 

b) Methali

i) Lisemwali lipo, kama halipo linakuja. (Uk 30)

ii) Siri ya kata iulize mtungi. (Uk 30)

iii) Kidole kimoja hakivunji chawa. (Uk 31)

 

 

 

 

c) Tanakuzi

i) Saa halindwi, hujilinda yeye mwenyewe. (Uk 31)

 

 

d) Taharuki

i) Ni kwa nini Kimwana alijifunika buibui?

ii) Ni kwa nini Kimwana hakuzungumza mambo yoyote?

iii) Mbona Kimwana na Saa walijifungia mle ndani kwenye chumba? (Uk 32)

 

 

37.

e) Mdokezo

i) Tena haishi kutapikatapika… (Uk 33)

ii) Pamoja na kujilinda kwangu… (Uk 33) iii) Kumbe mlango haukufungwa… (Uk 34) iv) Ameshakufa…ameshakufa… (Uk 35)

 

 

f) Kinaya

g) Mfano mzuri mpaka leo ni kwamba wao wazazi hawajapata hata neno lake, ila “Shikamoo” inayotoka midomoni nyuma ya buibui kama kata ya maji mtungini. Ni ajabu kuwa wazazi wa Saa hawajui ni nani anahusiana na binti yao.

 

 

a) Misemo na nahau

i) Kwa hivyo watakuwa wanaongozana na kuzibana nyufa…(Uk

31)

 

 

b) Tashibihi.

i) …ila “Shikamoo” inayotoka midomoni nyuma ya buibui kama kata ya maji mtungini.

 

 

c) Takriri.

i) Juzi…juzi… (Uk 34)

ii) shogake…shogake…(Uk 35)

iii) Ameshakufa…ameshakufa…(Uk 35)

 

 

WAHUSIKA NA UHUSIKA.

1. Saa

Huyu ni msichana mdogo aliye katika shule ya msingi. Ni bintiye Bwana Masudi na Bi.Hamida. Anatarajia kujiunga na shule ya upili hivi karibuni ikiwa atapita mtihani wake wa shule ya msingi. Sifa zake ni pamoja na:

 

 

 

 

38.

a) Ni msiri

Anafaulu kumcha raki yake wa kiume na kumvisha buibui ili kuwapumbaza wazazi wake kumdhania kimwana kuwa mwanamke. Wanaendelea na mchezo wao kwa siku nyingi hadi Saa anaishia kupata mimba. Isitoshe, anacha mimba yenye na kuikana mamake anapomdadisi ikiwa kuna jambo lolote mbaya limemtendekea. Anacha mimba yake na kujaribu kuiavya. Hapo tu ndipo wanazi wanabaini yaliyokuwa yakiendelea kwa muda wote huu.

 

 

b) Mwenye Unaki

Anawadanganya wazazi wake kwamba anasoma pamoja na rakiye wa kike ilhali Kimwana ni mvulana. Wanadanganya kwamba wanasoma ilhali ni mapenzi yanaendelea kule chumbani mwa Saa. Huu ni unaki wa hali ya juu.

 

 

a) Msaliti

Saa anasaliti uaminifu ambao wazazi wake walikuwa nao kwake. Wanamwamini wakijua yeye anasoma ilhali wakati huo, yuko kwenye mahaba ya Kimwana.

 

 

b) Ni mwenye bidii.

Anapokuwa nyumbani yeye hufagia, hupika, huosha vyombo, hufua, hupiga pasi na kutandika kila siku.

 

 

c) Mwerevu.

Katika kila mtihani, Saa aliibuka wa kwanza kabisa katika darasa. (Uk 30)

 

 

 

 

39.

1. Kimwana

a) Mwongo

 

 

Anajifunika buibui na kujifanya kama mtu wa jinsia ya kike. Kwa uwongo huu, anafaulu kuingia nyumbani kwa Saa na kuandamana naye hadi chumbani mwake wanakodhaniwa wanaendelea masomo.

 

 

b) Mwenye unaki

Katika mawazo ya wazazi wa Saa, Kimwana ni msichana ambaye ni raki ya Saa. Wanadhaniwa kusaidiana katika kudurusu kazi ya shuleni. Ajabu ni kwamba Kimwana ni simba anyemnyemelea kondoo na kumla mzima mzima akiwa zizini.

 

 

2. Bwana Masudi

a) Mwenye mapenzi.

Anampenda mkewe na watoto wake. Ni baba mwenye upendo.

 

 

b) Mwenye Bidii.

Anajibidiisha kuhakikisha kuwa jamii yake inaishi vyema. Isitoshe anajibidiisha kumuelimisha Saa.

 

 

a) Mwenye mapuuza.

Anapoelezewa kuhusu mabadiliko yanayotokea kwa bintiye, anakana na kuyatupilia mbali.

 

 

 

40.

1. Bi. Hamida

 

 

a) Mwenye mapenzi.

Anampenda mumewe kiasi cha kumfungulia moyo wake wote. Isitoshe anawaenzi watoto wake na kuwapenda mno. Anamtakia Saa mema na hivyo kumfunza maadili mema.

 

 

b) Mdadisi.

Umakini wake unamfanya kugundua kuwa kuna jambo baya na bintiye. Anagundua kuwa bintiye ana tatizo na umbo lake limeanza kubadilika kwa kiwango fulani. Udadisi wake ndio unamuelekeza kugutukia hali mpya ya bintiye.

 

 

1. Lulua

a) Ni mkweli.

Anapoulizwa maswali kuhusu dadake, anasema ukweli wote bila kucha chochote, jambo linalowapa mwangaza wazazi wake kuhusu tabia za dadake saa.

 

 

4. SHIBE ITATUMALIZA Historia ya Mwandishi.

Mwandishi ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Tanzania. Ni msomi na mwalimu wa Kiswahili. Amechangia pakubwa katika Isimu na lugha.

 

 

Dhamira

Mwandishi amedhamiria kuwaonya hasaa mataifa ya Afrika kuhusu tabia za ula na uroho.

 

 

41.

Ufupisho wa Hadithi

Sasa na Mbura ni watoto wa mwanasiasa, Mzee Mambo. Mzee Mambo anawaandaa wanawe kuingia katika harakati za unyonyaji wa mali ya umma katika nchi husika. Anawataka wanawe pia waingie katika siasa na wizi wa mali ya umma.

 

 

Baada ya uteuzi, sherehe zinaandaliwa za kufana ili kusherehekea ufanisi wa wanasiasa. Sherehe zinaandaliwa na matangazo yake kupeperushwa kwenye runinga. Watu wote nchini wanashuhudia jinsi ambapo wanasiasa wanasherehekea. Magari ya kifahari yanatumiwa na wanasiasa ili kujishaua na kuonyesha fahari ya wanasiasa.

 

 

Kisadfa, wakati huo huo wa sherehe, wanasiasa wakiwa kwenye sherehe wakila, wananchi hawana chakula. Wananchi hawana dawa hospitalini. Pia kuna uhaba wa chakula. Wanasiasa wanafurahia shibe, ilhali wananchi wanateseka na kuumia kwa kukosa mahitaji ya kimsingi. Wanasiasa wanapeana makandarasi kwa kujuana

.

Katika sherehe, inadhihirika kuwa Dj alipewa kandarasi kuuza dawa ambazo zilistahili kuwasaidia wananchi. Dawa ambazo zilistahili kupewa wananchi zinafujwa na kupewa Dj ili aziuze.

 

 

MAUDHUI

a) Uongozi mbaya

Uongozi mbaya unapelekea wananc hi kukosa huduma wanazostahili. Umma hauna dawa kwani viongozi wamejinyakulia madawa ambayo yanapaswa kuwa kwenye hospitali za umma na kisha kuwapa watu binafsi wanaojifaidi kama vile Dj (Uk 43).

 

 

42.

a) Ubinafsi na tamaa.

Dj ananyakua dawa za wagonjwa na kuziweka kwenye duka lake mwenyewe, kuuza na kujifaidi huku mamia ya watu wengine wakiumia kwa kukosa dawa hizo.

 

 

b) Usadi

Sasa na Mbura ni watoto wa mwanasiasa, Mzee Mambo, na hawakustahili kupewa kazi yoyote kwenye serikali. Ajabu ni kwamba wanapewa nyadhifa ili kusimamia Mipango na Mipangilio. Nyadhifa hizi haziwafai hata kidogo kwani hakuna kazi yoyote wanayotekeleza. Isitoshe, Dj na wenzake wanavuna mabilioni ya pesa kwenye sherehe kwa njia za udanganyifu.

 

 

MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI. a) Mdokezo

i)hata yeye mwenyewe hujikuta kimya kimya huku akisema nafsini mwake…(Uk 36)

ii) Kwenye kioo cha taifa, fesibuku, gazeti la… (Uk 45)

 

 

b) Methali

i) Wajinga Ndio waliwao. (Uk 37)

 

 

c) Utohozi – haya ni maneno yaliyoswahilishwa. i) Fesibuku (Uk 38)

ii) Wasapu (Uk 38)

iii) TV (Uk 38)

iv) Monokotilidoni (Uk 43)

v) Kwenye kioo cha taifa, fesibuku, gazeti la… (Uk

45)

vi) …mabomu, presha, obesity, sukari, …(Uk 44)

 

 

d) Tashibihi

i) …matumbo yao matupu yalishindana kunguruma kama radi. (Uk 39)

 

43.

e) Misemo na nahau

I) Magari yanapina vikumbo kuingia na kutoka kwa Mzee

mambo. (Uk 38)

 

 

a) Tashihisi

i) Jingine linamimina jamaa na mzee Mambo shereheni. (Uk

39)

ii) Njaa inawatafuna. (Uk 39)

iii) Upepo unawapuliza na kuwabembeleza… (Uk 41)

iv) Swali nalo linagoma kupuuzwa namna hii. (Uk 41)

 

 

b) Tanakuzi

i) Vyakula vyeupe. Vya rangi. Vitamu. Vikali. Vichachu. Baridi. Haya tu. (Uk 39)

 

 

c) Matumizi ya mashairi

i) Shairi 1- Uk 43- Shairi hili ni la kuwagutusha wanasiasa wanaolala. Ni shairi linalokusudia kuwazindua wanasiasa na kuwagutua wawe watu wa kujukumika.

 

 

d) Matumizi ya nyimbo

i) wimbo wa kwanza-Uk 37. Wimbo huu unatumika kuwaponza wahusika Sasa na Mbura ili kuwagutusha na kwamba Mola aliyewapa wao mali anaweza pia akawapa wengine.

Wimbo wa pili– Uk 43. Wimbo huu ni jibu kwa ule wimbo wa kwanza. Viongozi dhalim u wanawajibu wananc hi wakiwaambia wananchi kwamba hawajali wala kubali lawama zozote zile wanazopewa.

 

 

a) Takriri

I) Kunywa na kunywa na kunywa tena.

ii) Huiga kwa jamii. Huiga…huiga. (Uk 40)

 

44.

WAHUSIKA NA UHUSIKA.

Wahusika wakuu katika hadithi hii ni wawili: Sasa na Mbura. Sifa zao zinafanana. Sifa hizi ni pamoja na:

 

 

a) Ni wala.

Wanapohudhuria sherehe, kazi yao ni kula na kula tu bila kujalli. Wanatunga foleni mara tatu tatu na kujaza vyakula kwenye masahani yao hadi pomoni. Wanakula na kumaliza vyakula vyote vilivyojaa kwenye masahani yao hadi pomoni

.

b) Ni sadi.

Wamepokea kazi katika asi za serikali. Wanapewa nyadhifa za mipango na mipangilio kama wakuu lakini wanaishia kutofanya lolote. Kazi zenyewe hawakuzipata kwa njia halali. Ulikuwa ni usadi uliowaingiza katika osi hizo.

 

 

c) Ni wazembe.

Baada ya kula sahani tatu tatu za vyakula kwenye sherehe, wanalala usingizi mzito badala ya kwenda kazini.

 

5.
MAME
BAKARI

 

Mohammed Khelaf Ghassany ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mshauri na mwandishi wa hadithi fupi. Kwa sasa ni mwanahabari katika idhaa ya Kiswahili ya Redio Welle Ujerumani.Sena ni mwanafunzi,alibakwa akitoka masomo ya ziada.Kitendo hiki kinamsababishia uchungu moyoni,ukiwa na unyonge.Mara anaamua kubadilisha mtazamo wake kuhusu maisha .Anaamua kukabiliana na dunia,anaamua kutolia tena wala kujilaumu tena.Lazima maisha yaendelee .Anaamua kutoavya mimba

,kutojiua na hata kutokimbia pao.Ujasiri huu unamwelekeza kumfunulia moyo wake rakiye Sarina.Sarina anaahidi kumsaidia kubeba mzigo ule.Waliamua kuucha ujauzito chini ya Jilbabu(vazi pana linalifunika mwili ili kuweka heshima).Waliamua pia kuwa sehemu ya kujifungulia kuwa shamba kwa wazazi wake Sarina.

45.

 

Beluwa dadake Sarina alimhudumia Sara nyumbani ili kucha siri.Hatimaye anawaeleza wazazi wa Sara yaliyompata Sara.Wanapokutana pale hospitalini Sara anashtuka kwani hakutarajia kuwapata wazazi wake pale na zaidi ya hayo,alishtushwa na utu wa mapenzi waliyodhihirisha wazazi wake.Mimba ya Sara inaishia kuwa jambo la kawaida kwenye nyumba yao na mipango yote ya awali ikawa haina maana tena.

 

Sara anajifungua mtoto wa kike ambaye alikuwa Mke wa babake mpya.Sara bado ana nia ya kulipiza kisasi kwa huyu mbakaji.Akiwa kwao anasikia ghasia na fujo huko nje.Ina sadfu kuwa fujo hiyo ilihusiana na Yule mbakaji.Alikuwa amelala huku anataka kutapia roho yake iliyokaribia kumtoka kutokana na kichapo alichokuwa amepata.Anapigwa kwa mvua ya matufali hadi anafariki.

 

DHAMIRA

a) Mwandishi anakusudia kukashifu tabia ya wazazi ya kuwadidimiza wanao na kutowaelewa.Inafanya watoto waogope sana wazazi wao na wanashindwa kuwaambia wanayopitia.

 

b) Mwandishi alidhamiria kuonyesha umuhimu wa kuwajibika kazini.fano: Alivyowajibika Sakina na hatimaye anasaidia kupatanisha Sara na wazazi wake.

c) Mwandishi alikusudia kukashifu tabia ya ubakaji kwa kuonyesha athari zinazotokana na tabia hii.

d) Mwandishi pia alikusudia kukashifu taasubi ya kiume katika jamii

 

WAHUSIKA: Baba Sara

Katili

Kulingana na Sara,babake angemchinja na kumlaumu kwa kubakwa. Hangemwamini Sara.Badala angemdidimiza zaidi pia angemfukuza toka nyumbani.

 

a) Mkali

Ni kutokana na kuwa mkali ndio sababu Sara anashindwa kumweleza kilichompata.

 

 

 

46.

Mama Sara

Dhaifu/mnyonge

Hawezi kujitetea mbele ya mumewe. Hawezi kutetea bintiye.Ni

dhaifu kwa sababu ni mwanamke.

Sara

Mnyonge/dhaifu

Baada ya kubakwa na kupata ujauzito aliishi kulia.Hakuwa na

njia ya kujitetea .Aliamua kulia tu.

Mwenye kisasi

Hakuweza kumsamehe yule mbakaji,alitaka kulipiza kisasi.Hata

baada ya kupata mtoto wake Sara bado alitamani kulipiza.

Msiri

Anaamua kutomwambia yeyote kuhusu kubakwa na hata kuhusu

ujauzito wake.

Mwenye Imani

Alikuwa na imani na raki yake Sarina.Aliamini kuwa Sarina

angemsaidia katika hali hii ngumu. Mtani

Anamtania Sarina kuwa ni zamu yake kubakwa.

 

Mcha mungu

Tokea hapo awali alijulikana kama mcha mungu.Hata kuvalia

jilbabu halikuwa jambo la kushangaza.

 

 

BELUWA. Amewajibika

Yeye ni mlezi wa Sakina .Pia anaahidi kumpa kila msaada uliohitajika kuhusu ujauzito.

 

Mshauri mwema

Alimshauri Sara aende hospitalini ujauzito ulipotimia miezi sita kwani vipimo vya sasa vingelishirikisha mambo mengine ambayo hayangeweza kufanyika nyumbani.

 

Ni Mpatanishi

Anawapatanisha Sara na wazazi wake.Baadaye wanakuwa na uhusiano mzuri .Ujauzito uliokuwa mzito Sara unakuwa mwepesi.

 

Jasiri

Anawaelezea wazazi wa Sara kuhusu ujauzito wa Sara na anapanga kuwakutanisha Sara na wazazi wake pale hospitalini.

 

47.

.MAJIRANI. i.Ni wadaku.

Walikuwa wameanza kumsema Sara walipojua kuhusu ujauzito wake.

 

 

 

MBINU ZA UANDISHI

 

1. Mbinu Rejeshi(kisengere nyuma).

 

Mwandishi hurudi nyuma na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa(ashback).

 

a)UK 47..Aliendelea kuliona lile janadume asilolijua likimvamia na kumbaka ghaa.Kisha likambamiza ardhini na ardhi ikashuhudia ukatili na udhalimu ule.

 

b)UK 47…Anakumbuka vyema siku ile….ilikuwa ni jumatano moja ya bahali mbaya kwake majira ya saa tatu unusu usiku,akirudi darasani.

 

2)Takriri

 

Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani(Repetition). UK 47

 

a).Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia,kulia na kushoto.

b).UK 46 Ndiyo mbo yake,mbo yamnyonge na mnyonge ni yeye sasa.

c).UK 49-50 Nimekosa nini? Nini? Nini hasa?

d).UK 49 Dunia we dunia,Dunia na mwenye nguvu.

 

3Tashihisi/Uhuishaji(pensonication)

Ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye

uhai(sifa za kibinadamu). (UK 47)

 

 

48.

a).UK 47….Kisha likambamiza ardhini na ardhi ikashuhudia ukatili na udhalimu ule

b).UK 48….Bwana Yule mwenye masikio makaidi c)UK 50……Kioo hakikumpa makini kamwe. d)UK 50…. Akili imehama chumbani mwake. Inaranda huku na huko kutafuta la kufanya.

e)UK 50…. Kila wazo likatangaza suluhisho mwafaka.

f)UK 53…. Kilio kikachukua nafasi.

 

 

4.Taswira

Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali/jambo fulani kwa msomaji.

a). UK 47…Kisha likambamiza ardhi na ardhi ikashuhudia ukatili na udhalimu ule.

b) UK 47…..Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia,kulia na kushoto kama mdungo wa mshikaki juu ya tanuri la makaa.

 

 

5.
TASHBIHI

a). UK 47…Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia, Julia na kushoto kama mdungo wa mshikaki juu ya tanuri la makaa.

b). UK 52…Waliubeba kishujaa hata wakauhisi mwepesi kama

vunge la pamba.

c). UK 49…Kutengwa kama mgonjwa wa ukoma.Waliubeba kishujaa hata wakauhisi mwepesi kama vunge la pamba.

d). Sara anabadilika kutoka msichana na kuwa mama.

e). Jina lake Sara linabadilika na kuwa mama Sara. f). Baba aliyekuwa mkali anabadilika.

g). Uhusiano kati ya baba na mamake anabadilika na kuwa mzuri.

 

49.

6 MASWALI BALAGHA.

Maswali yasiyotarajia kujibiwa.

a).UK 49-50

Udhaifu na unyonge si ndio maana ya uanauke? Si ndio unaotumiwa kutimiza unyama wao?Nimekosa nini? Nini? Nini

hasa? Kipi kipya kilichotokea?

 

 

7. Ritifaa.

Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo)kana kwamba yuko pamoja nawe.

UK 51…Sitakuua mwanangu kamwe,alikiahidi kijanacho.

 

 

8. Jazanda.

Matumizi ya maneno yenye maana che. a).UK 47….Muhuzi mpya(ule ujauzito) b)UK 47…Ukanda wa picha

c)UK 48…Ukurasa(maisha mpya)

 

 

9. UZUNGUMZI NAFSI.

Mhusika hujizungumzia,ama kwa kuongea au kuwaza,bila kukusudia kusikika na yeyote.

a). UK 47….Aaa,maskini Sara miye,maisha yangu ndiyo yameshakunjwa hivi! Alijiambia kimoyomoyo.

b).UK 49…Lakini kwa nini?na kwa nini hasa? Sena aliendelea

kujiuliza ilivyopasa.Je!Nimetendewa hayo kwa sababu

ya

udhalifu wangu.

 

10.SADFA.

Ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa,japo havikuwa vimepangwa. (coincidence)

 

 

 

50.

UK 51…Shauri la usiniuwe la Abdulaif Abdalla ambalo Sena alikuwa amelisoma siku mbili kabla ya mkasa huo kusudia kilichompata Sena;ule ubakaji na kushika ujauzito.

 

UK 54….Wakati Sena alipokuwa akikiri atakavyo mwadhibu baba wa mtoto wake? Ilisadifu kuwa wakati huo kukawa na ghasia pale nje kwao.Ikawa aliyekuwa akipigwa na watu alikuwa ni Yule mbakaji.Hatimaye akafa.

 

UK 52…Wakati Sena alipata ujauzito,kisadfa,babake akaanza kumwita mama Sena.

Chuku:Kutilia chumvi.

 

UK 47…Hadi sasa pua yake imejaa ile harufu kali ya kutuzi iliyompa kipalizi na kumkolizo.

 

MAUDHUI. Mabadiliko.

1. UK 46…kuna mabadiliko katika mwili wa Sara… Sara alishtuka wakati mkono wake uligusa tumbo lake, alihisi mabadiliko ya kitumbo chake kilichokwishaanza kufura.

2. UK 50…Baada ya Sara kulia kwa muda mrefu, alitambua kuwa kilio chake hakikumsaidia .Anaamua kutulia tena , kutojijutia na kutojilaumu tena.Anaamua kutafuta suluhisho la tatizo lake kwa kuikabili dunia moja kwa moja.

3. Ujauzito uliokuwa mzigo mzito kwa Sara unabadilika na kuwa mwepesi baada ya Sara kumweleza Sarina.

 

Ukatili

Ukatili ni kule kukosa utu /ubinadamu.

 

Lile janadume lililombaka Sara halina utu .Halikuwa na huruma lilimkabamiza ardhini kwa ukatili na udhalimu (uk

47). Pia ni ukatili kwa jamii kumlaumu na kumtenda aliyebakwa badala ya kumhurumia.

 

 

 

51.

ELIMU

Elimu imetiliwa maanani katika jamii hii na ndio sababu kuna

mpango wa masomo ya ziada ..twisheni.

 

NAFASI YA MWANAMKE.

 

a) Mwanamke anaishi katika ndoa ambapo hajui kujitetea nafsi yake mbele ya mumewe kutokana na udhaifu wake.

b) Kama aliyewakulaumiwa kila kulipokuwa na visa vya ubakaji.Yeye alionekana kuwa ndiye shetani.Kama chombo cha kutimiza uchu wa mwanaume,kama aliyetumiwa kutimiza unyama wa wanaume.Mwanamke ametengwa kutokana na kosa la mwanamume.Baada ya kubakwa na kupata ujauzito,mwanamke anatengwa shuleni,nyumbani na kila mtu.

 

MAJUTO.

Sara alipobakwa hakumweleza yeyote kilichomfanyikia.Alienda nyumbani na kukoga.Baadaye akawa anajuta kwa nini hakutoa taarifa kuhusu kubakwa na kwa nini akakoga.

 

UNYONGE/UDHAIFU.

Sara alipobakwa alijawa na unyonge na ukiwa.Ni mnyonge kwa sababu hata baada ya kubakwa hangepata haki,hangeweza kujijitea,hangeweza kuaminiwa.Kilichobaki ni kulia na kulipiza tu.Mamake pia ni dhalifu kwa kuwa hawezi kujitetea nafsi yake mbele ya mumewe.

 

Sara anabakwa kwa sababu nimnyonge,unyonge unaotokana na yeye kuwa mwanamke.Anasema Udhalifu na unyonge ndio unaotumiwa na wenye nguvu zao.

 

TAASUBI YA KIUME.

 

Jamii hii inamuona kama mwanamume ni bora kuliko mwanamke. Katika jamii hii,mwanamke alilaumiwa ndiye shetani kila kulipotokea visa vya ubakaji.

 

 

 

52.

MASWALI.

Nimekosa nini ?nini ? Nini hasa ?

a) Eleza muktadha wa maneno haya.(AL4)

b) Ni mbinu gani za uandishi zinazojitokeza katika dondoo hili ?

 

(Al 2)

a) Jadili maudhui ya udhalifu na unyonge kama yalivyojitokeza katika hadithi hii(AL 14)

“Thibitisha ukweli wa methali.Hakuna siri ya watu wawili. Siri si siri inapotolewa kwa mtu mwingine”.

Sara alipomwelezea Sarina kuhusu kubakwa na ujauzito wake.Waliamua kuwa wangeiweka kama siri.

Wakapanga kuwa Sara avalie vazi ambalo litaweza kuucha ule ujauzito.

Wakapanga pia kuwa sehemu ya kujifungulia itakuwa shamba kwa wazazi wake Sarina.

Walimhadithia dadake Sarina,Beluwa ambaye alikuwa daktari wa uzazi.

Beluwa naye alipaswa kuweka siri hii.Mwezi baada ya mwezi alichukua vifaa vya kupima mimba na kuvipeleka nyumbani kumhudumia Sara,maana walitaka iwe siri kubwa. Ujauzito ulipotimia miezi,Beluwa akamtaka Sena aende hospitalini kwani vipimo vya wakati huo vingelishirikisha mambo mengi ambayo hayangeweza kufanyika nyumbani.Sara alipoka katika chumba cha daktari,kumbe baba na mama yake Sara walikuwemo wanamsubiri ,kumbe Beluwa alikwisha waeleza wazazi wake kuhusu ujauzito wake. Siri ikawa si siri tena.

 

6. MASHARTI YA KISASA.

Na Alifa Chokocho

Msuko

Hadithi masharti ya kisasa ni hadithi fupi iliyoandikwa na Alifa

Chokocho. kwa mapana na marefu amezungumzia suala la

mapenzi. Anayalinganisha mapenzi na ugonjwa usiokua na dawa.

Mwandishi anaelezea mapenzi kupitia kwa mhusika Dadi njia hasi,

kuwa mapenzi ni mateso, utumwa, ukandamizaji, udunishaji na

ushabiki usio na maana.

 

53.

 

Dadi ni mchuuza samaki, licha ya hayo amezaliwa na kukulia mjini. Dadi alikuwa amelemazwa na tamaa yake kwa Kidawa na alikuwa akimwinda mara kwa mara. Kidawa alimwekea ukuta ili kuyakata mawasiliano, mara kwa mara akajifanya kuwa hataki kuzungumza.

 

Siku moja, Kidawa alimkujia Dadi na kwa wakati huu akawa mwingi wa maneno. Dadi alishangaa nakutoamini aliyokuwa akiyasikia. Mkururo wa maswali uliompikita Dadi kwa mshangao na wasiwasi mwingi kwa maana hakuamini.

 

Jambo moja ambalo Kidawa alikariri mara si moja ni usasa. Hili halikumwia wazi dadi alilokuwa akimaanisha likawa ni fumbo ambalo hata Dadi mwenyewe hakuweza kulifumbua. Katika ukurasa 58, “nimekupimanisha Na kukuona mtu wa maana. Ila tu, Zaidi ya hayo, nataka ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa na mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamme wa kisasa, mwenye mapenzi ya kisasa. Huba ya Dadi kwa Kidawa ilimziba macho asipigikamae msasa maneno yenyewe. Alisikia neno kisasa kama mapigo yenye mahadhi mazuri.

 

Mwandishi anasema kuwa hii ingekua ndoa ya ajabu kama Dadi angefahamu masharti ya ndoa. Lakushangaza ni kuwa alikubali basi kuelewa mzigo ulioambatana na masharti hayo.

 

Bi Zuhura anamfanyia Dadi stihizai na kumtania sana.Baada ya kufanyiwa mzaha, anaamua kutomuuzia Bi Zuhura samaki.

Tatizo la Dadi lilikua kumshuku mkewe kuwa ana uhusiano na mwalimu mkuu.Hali hii inampeleka kumpeleleza. Anafululiza hadi shulleni mahali ambapo mkewe alifanya kazi ya umatroni. Huko anagundua kuwa wasiwasi wake ulikua wa bure katika shuguli yake anatambua kuwa mkewe alikuwa radhi kuiacha kazi kwa hofu yakuwa mmewe hakuwa anamwamini. Dadi anapofumanishwa akichungulia anaanguka chini na kupoteza fahamu.

 

MAUDHUI.

1. MAPENZI

Mwandishi anayaona mapenzi kama kitendawili, anayalinganisha na ugonjwa usiokua na dawa. Kupitia kwa mhusika Dadi anayaelezea kwa njia hasi anayafasili kuwa mateso, utumwa, ukandamizaji, udunishwaji na ushabiki. Hata hivyo, Dadi anajitumbukiza katika mapenzi haya bila kuyatalii. Kidawa anapendekeza mapenzi ya kisasa na kusema kuwa atakuwa mke wa kisasa. Dadi hakuwa na mtazamo huo. Mtazamo wake ulikuwa kupenda na kupendwa bila masharti yoyote. Jambo hili linamfanya kumshuku mke wake.

 

 

54.

1. USASA.

Mwandishi kupitia kwa mhusika dadi anaonyesha jinsi usasa

unavyoathiri maisha ya mwanadamu. Usasa ulikuwa na

maana ya kuchukua majukumu kwa zamu. Kidawa

alipendekeza wasaidiane katika majukumu ya kinyumba

kwa mfano; iwapo ameenda kazini. Dadi apike na kupiga

deki.Kidawa anasema kuwa yeye ni mwanamke wa kisasa.

Dadi alikiri kuwa mizani kwa kuwa amezaliwa na kulelewa

mjini anaelewa barabara. Hivyo basi, anayakubali yote

aliyoambiwa na Kidawa bila kuyatia kwenye mizani.

 

2. UTABAKA.

Kuna matabaka mawili. Tabaka la juu ambalo linawakilisha

mwalimu pamoja na Kidawa. Dadi ndiye anayejiweka katika

tabaka la chini na kujidunisha. Utabaka huwa ni zao la watu

wenyewe mfano utabaka unajitokeza pale ambapo tuna

m a k u n d i m a w i l i k a t i ya wa l e wa l i o n a v y o n a

wasiokuwanavyo. Dadi anaingiwa na kiwewe kutokana na

hali hii ambayo inamlemaza na kuulemaza uhusiano wao.

 

3. ELIMU.

Dadi ndiye anatufahamisha kiwango cha elimu ya Kidawa.

Yeye mwenyewe hatuambii alipokia anataja tu kazi yake.

Hata hivyo tunaskia kuwa kiwango chake cha elimu kilikua

chini kikilinganishwa na kile cha Kidawa.

 

4. NDOA/KUTOAMINIANA.

Ndoa inastahili kujengwa katika msingi unatokana na

kuaminiana. Hata hivyo, ndoa baina ya Dadi na kidawa ina

mushki kwa sababu Dadi ana wasiwasi . Wasiwasi huu

unatokana na kujidunisha kwake. Kwa upande wa Kidawa,

hana tatizo lolote. Kabla ya kuoana alikuwa ameyatoa

mashrti ambayo yangekuwa mwongozo wa ndoa yao. Kila

wakati ilipotokea hali ya swintofaham u Kidawa

alimkumbusha masharti.Ndoa hii inapata msukosuko pindi

Dadi anapoamu kumfuata mkewe akimshuku kuwa ana

uhusiano na mwalimu mkuu.

 

 

 

55.

6.MASHARTI.

Mashar ti yanayoambatana na tatizo linalotokana na

makubaliyano mara nyingi huweza kusuluhisha migogoro fulani.

Hata hivyo mojawapowa yale mawili anapokosa kuyatimiza, basi

huwa kunatokea mvutano na mgongano. Dadi aliingia katika

makubalioano kwa pupa bila kuyawazia hali hii inasababisha

matatizo makubwa, pindi anapofanya kosa, anakumbushwa

masharti.

 

Dadi aliingia katika makubalioano kwa pupa bila kuyawazia hali hii inasababisha matatizo makubwa, pindi anapofanya kosa, anakumbushwa masharti.

 

WAHUSIKA

1. DADI

Dadi ni mchuuza samaki kama tunavyofahamishwa katika

utangulizi wa hadithi. Licha ya hayo Dadi mwenyewe anadhibitisha

hayo anaposema kuwa mimi ni muuza samaki tu. UK. 58.

Ingawa kidawa ameelimika dadi hataki kubaki nyuma, anasema

kuwa amezaliwa mjini. Kulingana na Dadi kuwa usasa unaweza

kulinganishwa na maisha ya mji.

 

SIFA.

a) Mwenye bidii.

Dadi ni mtu mwenye bidii kazini. Kuzaliwa na kukulia mjini

kumemfunza namna ya kuyakabili maisha. Dadi hakutegemea

kazi ya kuajiriwa bali aliweza kujiajiri mwenyewe. Kazi ya

kuuza samaki inahitaji mtu mwenye jitihada, kuwatafuta samaki,

kuwatafutia soko kama tunavyoelezwa na mwandishi anapita

akitembeza samaki wa mwishomwisho. Uk 59.

 

b) Mwenye hamaki.

Msanii amewasiri Dadi mwenye hamaki pindi anapolazimishwa

kufanya hivyo. Hapendi kuingiliwa masuala yake ya ndani

sana.Bi. Zuhura anapomwingilia kwa hamasa, Dadi alitamka ”

ukiwanunua utafanya heri” ukr 62. Bwana Dadi anachujia

baiskeli yake anamweleza peupe ” wewe hutaki samaki,

unataka umbeya na kujua mambo ya watu” Uk 63.

 

 

56.

c) Mwenye kujidunisha.

Dadi anajiona duni mbele ya Kidawa. Ana mawazo nyu

kuhusu hali yake na kazi yake. Anasema kuwa” mimi ni muuza

samaki tu” uk 58.

d) Mwenye kushuku

Kutokana na hali yake ya kujidunisha, Dadi anakosa kujiamini

kiasi kuwa hamwamini ata mkewe. Hali hii inafanya amfuate

mkewe hadi mahali pa kazi akimshuku kuwa na uhusiano na

mwalimu mkuu. Nusura hali hii inasababisha maafa makubwa.

Wasiwasi wake haukuwa na mashiko.

e) Mwenye pupa

Kiini cha matatizo yake ni kutokana na pupa yake katika

maamuzi. Kama angekua amemakinika asingeingilia ndoa

bila kutafakari masharti aliyowekewa na kidawa. Kilichokuwa

kimemzuga Dadi ni neno “kisasa”. Kiasi kuwa hangeweza

kuona chochote wala kusikia lolote lile.

 

UMUHIMU WAKE.

 

Ni kiwakilishi cha watu ambao hufanya maamuzi bila kujali matokeo yake. Dadi ni mfano wa watu ambao hufanya maamuzi yanayoadhiri maisha yao kwa kiasi kikubwa.

 

KIDAWA

Hili ni jina la kimajazi amabalo linawakilisha dawa katika

moyo wa kisasa ambaye anataka mambo yafanywe kwa

usasa. Anafanya kazi katika shule kama matroni.

 

SIFA

a) Mwenye dharau

Mwandishi anasema kuwa hawangeweza kupataan

anatumia fumbo kwa kusema” wakati wa zile siku ngumu

yeye alipotembea ardhini, kidawa aliruka hewani” ukr 56.

kidawa anadhihirisha dharau kutokana na viwitabia vyake

mfano

a) Uk 56 a) kuiburia midomo kumbeza

b) kidawa kumwambaa dadi

c) kumpa dadi mgongo

 

 

57.

 

(ii) uk 57 a) nimefuatwa na wanaume wengi walionitaka uchumba.

b) “wenye uwezo na wasio nao”

 

(b) mwenye masharti

Ndoa yao ilijengwa kwenye masharti magumu ambayo hatimaye

yanaiadhiri kidawa alikuwa na mpango wake wa awali kuhusu

maisha ambayo angetaka waishi lakini dadi hakuyaelewa

masharti yale.

Masharti yale yalikuwa mpango wa awali wa ndoa yao na kama

dadi angeyaelewa ndoa yao ingekua ya kupigiwa mfano.

 

a) Mwenye mapenzi ya dhati

Kidawa alikua mwenye mapenzi ya dhati ni kutokana na

hali hii ambayo anayaweka mashrti ili asivunjwe moyo.

Alipomuuliza dadi kama mapenzi ni dhahiri kuwa

hakutaka kuvunjwa moyo. Alipokua akitafutwa

alionyesha kana kwamba hakutakauhusiano lakini ilikua

njia ya kukadiria kiwango cha mapenzi ya dadi kwake.

Kuandaa chakula ni ithibati kuwa alimpenda dadi. Hata

hivyo alikua tayari kuacha kazi yake ili kuonyesha penzi

yake kwa mmewe.

(d) mwenye mapato

Kidawa anasema kuwa alitafutwa na wanaume

waliosoma nna wasiosoma wenye uwezo na wasio nao.

Hii ilikua ni njia mojawapo ya kujigamba kuwa sio dadi

pekee aliyemtaka.

 

MWALIMU MKUU

a) Mwenye bidii

Mwandishi kupitia kwa mkewe mwalimu mkuu anaonyesha

jitihada za mwalimu kazini hasa tukizingatia kuwa ilikua ni

wakati wa jioni. Anazidi kusema kuwa huwa anfanya hivyo

kila siku kazi inapozidi. Wakati kidawa alipoenda

kwenye osi ya mwalimu mkuu alimpata akiwa kazini. Na

hata sauti yake ilishauri uchovu. Hii inaonyesha kuwa

mwalimu ni mchapa kazi.

 

 

58.

a) Mwenye hekima

Kidawa alipoenda osini akiwa na wazo la kutaka kuacha

kazi, mwalimu mkuu alimuuliza kama amekiria, anaonyesha

kuwa mbali na kuwa na hekima ni mshauri bora kwa sababu

anamwambia kuwa ni magumu. Anajali maisha yake na jamii

yake kwani hangependa ataabike na maamuzi ya haraka.

 

ZUHURA

(a) Mwenye dharau

Jinsi anavyomzungumzia dadi ni ithibati kuwa ana dharau.

Anaingilia masuala yasiyomhusu hasa yanayoingilia jamii.

Kumuuliza dadi kama wameshaoza ni kiwango cha juu cha

madharau.

(b) Mdaku

Bi zuhura anajiingiza kwenye mambo ya watu wengine. Alitaka

kujajua masual ya ndani ya kidawa na dadi

© Mjeuri

Anaposimamisha dadi anamuliza kama ana samaki wa kuuza au

anao wa kumkaangia bi kidawa, lake lingekua la kununua

samaki wala si mengine

 

MBINU ZA KUGHA

1. Maswali ya balagha.

Maswali ya balagha au tashtiti ni maswali yanayoulizwa na

msimulizi au mhusika ambayo yanahitaji jibu.

(i) Uk 56……kwa nini misumari ya nyuki inamuuma sasa ila si wakati ule wa tamaa ya ushindi. Ilipokuwa mabli mbingu na ardhi.

(ii) Uk 57……(a) bwana wewe unataka mapenzi utayaweza a) Tuseme kisasanini

b) Ameshatuliza moyo wake c) Nani angeangamini?

(iii) Uk 60…..(a) kwani dadi engewezaje kupuuza yale masharti ya ndoa ya kisasa?

(b) yale masharti yanaendelea kumtamiriria

(c) dhana au ukweli?

(d) hata wepesi wa kufahamu kibinadamu hanao?

59.

 

(e) huyu mwanamke asiyechoka kujipodoa akiingiliana ndani? (iv) uk 62…….a- kwa nini limkere mtu

b- watu inawahusu nini

c- mbona nawaona laini namna hii?

d- au wameshaoza?

a) Unaona mashavu ya samaki yalivyo mekundu hivi?

 

1. NIDAA

Ni usemi unaoonyesha kushangazwa na jambo Fulani na huambatanishwa na alama hisi

(i) Uk 56…ni ugonjwa usio na dawa

(ii) Uk 57…..dawa ya ugonjwa wangu’ (b)………sikiliza dadi

(iii) Uk 58….ladha ya ajabu

(iv) Uk 60……eti dhana

(v) Uk 61…..masharti ya ndoa ya kisasa

(vi) Uk 62……Jamani

(vii) Uk63…….biashara haigombi hivyo

 

2. KUCHANGANYA NDIMI

Msanii anapoyaweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili, msanii anweza kufanya hivi kwa kusudia au bila kusudia. Anafanya hivyo kuonyesha ana ya mhusika anayehusishwa na uneni ule.

 

Uk 65 (i) ‘stop your gaze’

a) my dress, my choice’

b) Celeb ama socialite

 

1. UTOHOZI

Hii ni mbiu ya kuswahilisha maneno ya kiingereza na kufanya yawe na mapigo ya silabi ya Kiswahili.

a) Uk 60… fasheni b) Uk 61… umetroni c) Uk 66…friji

d) Uk 67….paipu

e) Uk 69…. Ambulensi

 

 

 

60.

1. TASHBIHI

Huu ni mlinganisho wa kitu na kingine kwa kutumia kiunganishi

kama :mfano wa, mithili ya , kama na ja

1. uk 56….(i)akimwinda kama kunguru

(ii)kuambaa kama ugonjwa wa tauni

2. uk 57…..maskio kuwa wazi kama anga

 

 

2. TAKRIRI

Hii ni mbinu ya kurudiarudia neon moja au kifungu cha maneno

ili kusisitiza ujumbe Fulani;

(i) Uk 57…. Nani angeamini? Baada ya visa vyote vile dadi alivyofanyiwa nani angeamini?

(ii) Uk 58…..(a) na mapenzi ya kisasa yana shuruti za kisasa

(b) lazima ufanye wajibu wa kisasa kwa mimi

nitakayekuwa mkeo wa kisasa

(iv) ) uk 59…..kwa hatua, kipembe baada ya kipembe

…….pom pom pom poom poom pom poom

 

3. MDOKEZO

Msanii hukatiza maneno au anaamua kuachia maneno bila

kutaja kitu. Mdokezo huwa ni mbinu ya kumfanyia msomaji

awze kujijazia kwa njia ya ubunifu

(i) Uk 59… pom poom pom poom pom poom

(ii) Uk 66,,,,,na tazama

(iii)Uk 67……lakini leo ni leo

(iv)Uk 68….labda anachungulia wasichana

 

MIFANO MINGINE

 

4. SADFA

5. UZUNGUMZI NAFSIA

6. MAJAZI

7. MSEMO

8. NAHAU

 

 

 

 

61.

7.
NDOTO
YA
MASHAKA

 

Ali Abdulla ndiye mwandishi wa hadithi Ndoto Ya Mashaka. Yeye ni mzawa wa Pemba. Ameondokea kuwa mwandishi stadi wa hadithi fupi. Amechangia pia mkusanyo wa Damu Nyeusi na hadithi Nyingine.

Mashaka alikua kijana aliyeishi maisha yaliyojaa mashaka. Alizaliwa na baada ya muda akaitwa yatime. Mamake alifariki alipomzaa kishaa babake akafuata,akashindwa kuvumilia upweke. Biti Kidete akamchukua Mashaka na kumlea. Biti Kidete daima alilalamika kuhusu miguu yake ambayo haikusikia dawa. Ilimbidi Mashaka atafute vijibarua ili wapate riziki.

Baada ya Mashaka kumuoa Waridi,maisha yao yalijawa na shida na umaskini. Jambo ambalo halikuwafurahisha wazazi wa Waridi hawakulipenda.

Waliishi katika chumba kidogo ambacho hakikuwatosha. Walipata watoto saba, sita kati yao walizaliwa kwa pacha tatu na mmoja pekee. Waliishi katika mazingira yaliyokuwa duni na machafu. Siku moja Waridi alishindwa kuvulia na akarudi kwao na watoto wote. Mashaka aliyempenda Waridi sana alijawa na upweke na ukiiwe. Alijitahidi kuwasaka lakini hakuwapata.

Kuna utabaka ambao unadhihirika wazi. Matajiri walio wachache wanazidi kuwa matajiri zaidi. Nao maskini walio wengi walizidi kuwa maskini zaidi . Ndotoni Mashaka anawaona maskini (wasakatenge) wakiandawana na hatimaye maisha ya wanabadilika na kuwa bora

 

Anwani

Anwani ‘Ndoto ya Maisha’ ni faafu kwa sababu hadithi nzima ni

ndoto. Kuwapo kwa Waridi na maisha yao, ni ndoto. Mashaka

anasema “Aaaa, kumbe ii yote ilikua ndoto, ndoto yangu Mashaka,

ndoto ya mashaka yangu , ndoto ya Mashaka isiyo Waridi wala

tamaa ya maisha kuboreka. Heri nisingeota.”

 

Dhamira

1.Mwandishi alikusudiwa kukashifu mfumo wa utabaka katika jamii.

2.Mwandishi alidhamiria kuonyesha athari za umaskini katika jamii.

3. Alitaka kuthihirisha ukweli wa methali, “Mapenzi ni majani,

popote penye mbolea hujiotea.”

 

62.

MAUDHUI
Umaskini

Watu wengi katika jamii hii wameathirika na umaskini. Kutokana na umaskini wa Biti Kidete , Mashaka alilazimikakutafuta vijikazi ili apate riziki. Aliweza kwangulia watu nazi au kwenda pwani kurambaza au kuokota kombe na chanje.

Mashaka alipomuoa Waridi maisha yao yalizidi kuwa na shida nyingi. Waliishi katika chumba kimoja kwa miaka mingi katika mazingira duni. Kuliponyesha, michinzi ya maji lilionekana kwani paa lilikua likifuja.

Chumba chao kilik]ua hakiwatoshi. Usiku binti zao walibanana na mama yao kwenye kijichumba chao na wavulana wakalala jikoni kwa chakupewa, jirani yao. Chumbani mlikua na vitu vichache tu. Hawakua na sababu ya kuvinunua na pia hawakua na pesa za kuvinunua. Mkewe alilalia mayowe na watoto wa kike wakalala chini kwenye mbacha.

Wasakatenge waliathirika mno na umaskini hadi wakatamani wafe.

 

Uchafu

Mazingira walimoishi wasakatenge yalikua machafu kupindukia.

Kwa mfano, chuma cha Mashaka kilikumbatiana na choo cha jirani.

Harufu yote kutoka chooni uliingia hadi chumbani mwa Mashaka.

Upande mmoja wa kile chumba kukawa na mfereji wa maji

machafu. Mvua uliponyesha , mfereji ule ulifurika na kwote kukawa

na uvundo. Wakati mwingine hawa wasakatenge walitumia

karatasi za plastiki kufanyia haja ndogo na kubwa kasha kutupa

huko nje.

 

Utabaka

Kupitia kwa Mashaka , tunaelewa pengo ulilopo kati ya watu wa

tabaka la juu na watu wa tabaka la chini ni pana sana (uk. 78)

Mashaka anauliza , “Na je , hizo fedha hupatikana wapi ?Nini

kinaleta tofauti hizi?kwa nini pengo hili kuzidi kukua na kupanuka

kila uchao?…”Matajiri wanazidi kuwa matajiri na fukara wakizidi

kufukarika na kudidimia

 

 

63.

Mapenzi
ya
dhati

Waridi anampenda Mashaka kwa kweli bila ya kuangalia uduni

na utupu wa Mashaka,alimpenda katika umaskini wake.

Mashaka pia alimpenda Waridi ‘kufa’. Alimpenda kwa hamu na

ghamu.Alipoachwa na Waridi hakua na dhamani ya maisha tena.

Alijitahidi kuwasaka bila ya mafanikio.

 

Ajira
kwa
watoto

M a s h a k a a l i t a f u t a v i j i k a z i a l i v yo v i we z a . A l i c h u m a

karafuu,akaangulia watu nazi. Alienda pwani kurambaza au

kuokota kembe na change. Pia alisaidia mtu kijikazi chake mkono:

kufyeka majani usoni pa nyumba yake ,kuyachanja kuni magogo

yake na hata kufua na kupiga pasi nguo zake… yote kwa lengo la

kutafuta riziki.

 

Kifo/Mauti

Kuna vifo vya watu tofauti. Mamake Mashaka alifariki alipomzaa.

Babake naye aliposhindwa kuvumilia upweke baada ya kifo cha

mkewe naye akafa. Hatimaye Biti Kidebe naye akaeafuata.

Urembo

Mashaka anaeleza kuhusu urembo wa Waridi. Anamlinganisha na

ua lenye hauba iliyotukuka na aliye na harufu nzuri.

 

WAHUSIKA
Mashaka

Ndiye muhusika mkuu

Mwenye mapenzi

1.Uk 74: Mashaka anasema alimpenda Waridi Kufa .

Anapowakosa Waridi na wanawe pale nyumbani alijitahidi

kuwasaka bila ya mafanikio.

2.uk 77: Mashaka alipoachwa na Waridi hakuona thamani ya

maisha tena.

3.uk 79: Mashaka anasema “Nilimpenda mno bila shaka,

nilimpenda kwa hamu na ghamu.”

4.uk 80: Waridi aliporejea, Mashaka alifurahi sana na hata

akasahau yote yaliyokuwa yamepita.

 

 

 

64.

Upweke na Ukuwe

1.Uk 87:Alikua mwenye upweke na ukuwe Waridi alipomtoka

katika maisha yake.

2.Babake Mashaka aliposhindwa kuvumilia upweke baada ya kifo

cha mkewe . Huo upweke ndio ulisababisha kifo chake.

 

Mwenye Mashaka

Maisha ya Mashaka ni mashaka matupu. Alipozaliwa, mamake

akafa na baadae babake akamfuata kwa kushindwa kuvumilia

upweke.Biti Kidebe aliyemchukua baada ya vifo vya wazazi wake

akawa naye hajiwezi kiafya na kimali. Mashaka yakamzidia

Mashaka. Huyo akawa anafanya vibarua ili apate riziki.

Hatimaye naye Biti Kidebe akafa.Baada ya kumuoa Waridi

matatizo yakawa chungu nzima. Yalipozidi Waridi akashindwa

kuvumilia na akamuacha Mashaka pekee. Akabaki akiwa na

umaskini.

 

Kufa moyo

Uk 79: Nikaona kira za nafsi yangu zinaendana na zile za moyo

wanguuliokwisha tamauka.

Uk 79: Mashaka anasema “Nimelioka hata naradua kufa kuliko

kuishi.”

Uk 80:Wanyonge wa tabaka la chini waliandamana huku

wakipiga kelele , “Tunataka Tufe!Bora Tufe!”

Waridi anashindwa kuvumilia maisha ya Mashaka na anaamua

kurudi kwao.

 

Maskini

Uk 74:Waliishi katika chumba kile kile kibovu kwa miaka mingi na

shida zikawa zinawatamirira kila upande. Kazi yao kubwa ikawa

ya kijungu-meko,kazi ya kupigania tumbo.Walilala chini na hata

kuomba nafasi kwa jirani. Hawakuwa na vitu chumbani kwani

hawangeweza kununua.

 

 

 

 

 

 

 

 

65.

Waridi

Mwenye mapenzi ya dhati

Uk 74: Waridi alimpenda Mashaka kwa dhati. Hakuangalia hali

duni ya Mashaka .Alimpenda katika umaskini wake.

Mapenzi hayachagui fukara wala tajiri kwani mapenzi huota

popote.

 

Mvumilivu

Aliweza kuvumilia maisha hayo ya umaskini kwa miaka mingi.

 

Mrembo

Uk 70: Mashaka anafananisha urembo wa Waridi na ua ambalo

hupendeza macho na kumfurahisha mtima.

 

Wasakatange

Ni watu maskini wa tabaka la chini. Walitamani kutokana na hali

yao duni.

 

Mzee
Rubeya

Alikua babake Waridi.

Alikua na asili ya Yemeni.

Alikua tajiri ambaye alihuzunishwa na ndoa ya Mashaka na bintiye

Waridi kwa sababu Mashaka alikua maskini.

 

MBINU
ZA
UANDISHI
Jazanda

1.Ua la Waridi limetumika kijazanda kulinganisha Waridi mke wa

Mashaka.(uk 70)

2.Mashaka analinganisha mshahara wake na mkia wa mbuzi.( uk

76)

3.Nitaramba na kulmbatua asali yake tamu kama nyuki (uzuri

wako).

 

Maswali
Balagha

Ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo

hayahitaji jibu (rhetorical question).

 

 

 

 

66.

Uk 70: Na harufu yake je?

Leo harufu tu ina sifa hiyo, waridi lenyewe je?

Ni Biti Kidebe mamangu, au waja tu na dharau zao?

Uk 76:Wamekwenda wapi watu hawa?

Uk 78: Na je ,hizo fedha hupatikana vipi? Mbona kuna pengo

kubwa kati ya walionazo na wasiokuwa nazo? Nini kinaleta tofauti

hizi?

 

Nyimbo

Uk 77: Wimbo uliopigwa na redio Tanzania Dar ulipendwa sana na

Waridi. Wimbo huu unaonesha hisia za kutamauka. Mtu aliyekufa

moyo

 

Methali

Uk 70: Baada ya dhiki faraja

Jungu kuu halikosi ukoko

Uk 75: siri ya mtungi iulize kata au kitanda usichokilalia hujui

kunguniwe

Uk 78: Subira ni ufunguo wa heri.

Uk 79: Ngoja ngoja huumiza matumbo

 

Chuku

Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe Fulani

au kusia kitu.

Uk 71: Nikalienzi ua langu kuliko hata mboni za macho yangu

Uk 74: Nampenda kufa

 

Uk 76: Dhiki ndio ilikua nguo na harufu yetu.

Uk 80: karne nzima imepita sasa pasi na kuliona ua langu. Ndio

kwanza leo nilitie jichini baada ya miaka mia. (muda mrefu

sana)

 

Tabaini

Matumizi ya kikanushi ‘si’

Uk 72: Si maisha si wazimu

Uk 71:Si ya sasa si ya baadae

 

 

 

 

67.

Tashihisi

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai(binadamu)

Uk 74: Harufu yote itapikwayo na domo la choohicho

Uk 74:Nao hutema uchafu wao katika mto Msimbazi.

Uk 76:Katika maisha hayo siku zilijisotora zikapita kama hazitaki. Uk 82:Rangi ya urujuani ulichungulia katika nyufa

Uk 88: Mwili wangu niliuhisi mtamu. Ulinitafuna kama kidonda

Uk 79: Haukutoka (msemo) na wala haukutaka kamwe kutoka

 

 

Utohozi/Kuswahilisha

Uk 74: Plastiki

 

 

Takriri

Ni mbinu ya kurudia rudia neon moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. (repetition}

Uk 81: Ilikua radi iliyopiga kila mahali. Ilika kila mahali. Kila mahali uliingia.

Uk 79: “Hadi lini lakini…hadi lini…”

 

 

Tashbihi

Hii ni mbinu ya lugha inayo linganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha:kama, mithili ya,sawa na,je.

Uk 72:Akaiga dunia bado mbichi kama jani la mgomba

Uk 73:Rubaa ya watu wane ikajitema chumbani kama askari wa

fanya fujo uone

Uk 74:Choo chenyewe kimeinuka juu kama ghorofa

Uk 75: Wavulana walilala jikoni kama nyau…

Uk 76: Katika maisha hayo siku zilijisotora zikapita kama hazitaki

Uk 77:Ilikua tamu kama ya ndege wa peponi.

U k 7 7 : N i l i k u a k a m a n d e g e k a t i k a t u n d u

uk 88: Ni maadamano yale walikua wamefwua na kufwuana kama

unga

 

 

68.

Majazi

Ni pale tabia za wahusika zinaambana na majina yao halisi

Uk 73:Waridi: Mashaka anasema jina lake lilipige ndipo bila shaka. Linaelezea urembo wa Waridi

Uk 74:Wasakatenge (maskini)

Uk 75:Chakupewo ?(anawapa mahali pa kulala)

 

Misemo

Uk 72:Kusalimu amri

Uk 72:Maji yalipozidi unga

Uk 72:kupiga kite

Uk 76:Ziligonga mwamba

 

Uzungumzi
nafsia

Mhusika hujizungumzia, ama kuwa au kuongea bila kukusudia kusiko na yeyote.

Uk 76:Nilijiuliza lakini jibu sikupata

Uk 77:Niliwaza mengi zaidi. Nikawaza ya laity ningekua na maisha mazuri.

Uk 78:Nafsi yangu uliniambia “subira ni ufunguo wa heri.”

Uk 79:”Hadi lini lakini…hadi lini. Subira hiyo?” Moyo uliuliza

 

Maswali

1.Mashaka, Waridi na wasakatenge ni majina ya majazi. Thibitisha kutoka kwa hadithi

2.Onesha jinsi mwandishi wa hadithi ya Ndoto ya Mashaka amefaulu katika matumizi haya

a)Chuku b)Tashisi c)Tashbihi d)Nahau

 

Chuku

ni kutia chumvi katika jambo ili ufafanuke zaidi au lieleweke waziwazi.

Uk 71:Nikalienzi ua langu kupita hata mboni za macho yangu. Uk 74:Nilimpenda kufa

Uk 76: Sura zetu zilitosha kuwa sura za kusemea

Uk 76: Dhiki ulikua ndio nguo na harufu zetu

Uk 80:Karne nzima imepita sasa pasi na kuliona ua langu.Ndio kwanza leo nilitie jichoni baada ya miaka mia.

 

69.

8. KIDEGE

ROBERT
W
EDUOR

Msuko

Hadithi hii imejikita katika mazingira ya bustani.Bustani ya ilala ni

mahali ambapo wapenzi walikuwa wakikutana.

Taswira inayojitokeza ni ya watu wanaopendana.Ili kusisitiza

jambo hili,mwandishi anazungumzia rangi.Rangi inapotumika

kisanaa huweza kuwasilisha wazo Fulani.Msanii anasema kuwa

,’Nyasi zilikuwa zimepiga umanjano na kukaribisha binadamukwa

hali za kila aina’uk83.

Msimulizi anasema kuwa mahali hapa ni mandhari ya

wapendanao.Ni mahali ambapo waja huzungumzia mambo mengi

na wengine wakiwa na mambo mengi.Tunaelezewa kuwa mahali

pale ni mahal I pa kuanzisha uhusiano.

Msimulizi anasema kuwa,kati ya waliokuwa wakizuru Bustani ile ni

Joy na Achesa,Siku hiyo walikuwa na mchezo wa kitoto.Wakiwa

katika mchezo,mawazo ya Achesa yanatekwa na ndenge

mmoja.Ndenge Yule alimfanyia mambo ya ajabu,akawa ni

mhusika muhimu katika masimuluzi haya.Pamoja na ndenge Yule

inasadifa kuwa Mose alikuwa amejibanza………

 

Jina halisi la mose ni Musa.Mose alikuwa mapenzi makuu kwa samaki waliokuwa kwenye kidimbwi.Kutokana na mapenzi yale akawa na mazoea ya kuwasilisha na kuwatunza.Mose alikuwa na raki yake kwa jina Shirandula.Shirandula alikuwa mtani mkubwa wa mose,alimtegea mose kitendawili ambacho kilimlemea.

Mose aliota ndoto usiku wa kuamkia jumamosi,ndoto ilikuwa juu yan midege ya ajabu.Katika uhalisia anaamua kuelekea kwenye bustani.

 

MAUDHUI

a) Uhusiano mwema.

Uhusiano mwema hudhihirika kutokana na mahusiano na

mwingiliano barua ya watu.Katika hadithi kidege

unadhihirika kati ya Joy na Achesa.Wanaonyesha hali hii

kwsa kucheza pamoja mchezo wa kitoto.

Mose anataniana na maraki hawa bila kuwaudhi UK85

wakabaki wanachekeana,ama wanachekacheka ovyo.

 

 

 

70.

a) Mapenzi

Mapenzi yanadhihirishwa na wanadamu wanapojituliza chini kwenye vipimbe vilivyowacha wakiendeleza mining’ono ya mapenzi.Mapenzi yanayolengwa ni ya m wa n a m ke. M wa n d i s h i a n a s e m a k u wa m a h a b a yamewafura.Anamaanisha kuwa mapenzi yamekita mizizi katika jamii hii,mwandishi anatutilea taswira ya ndege wanaotazama wanadamuwakiwa katika haba.

 

b) Utunzaji
wa
mazingira
na
viumbe.

Mose alijipatia wajibu wa kuwatunza samaki na ndege.Aliwatupia samaki kipande cha sima bila kuwasahau ndege.

B u s t a n i ya i l a l a i l i k u wa i m e h i f a d h i wa v i z u r i . Mwandishianasema kuwa uzuri………………??????????? h a wa k u wa wa n aya h a r i b u m a z i n g i r a ya l e . H a t a samakiwaliokuwa kwenye kidimbwi hawakudhuriwa na wanadamu.

 

c) Uraki

Uraki unajitokeza kwenye hadithi Joy na Achesa ni miongoni mwa maraki waliokuwa wakijituliza kwenye bustani.Ni maraki tu ambao wanaweza kuwa na mchezo uliokuwa ukichezwa.Licha ya hao wawili,kulikuwa na Jozi nyingine ya maraki nao ni Mose na Shirandula.

 

d) Starehe

Katika hadithi hii,mwandishi anatupeleka kwenye mazingira ya bustani.Bustani ya ilala ilikuwa na uzuri wake ndio maana watu walikuywa wakienda mahali pale ili kustarehe.

 

WAHUSIKA

Hawa ni watu,vitu au viumbe wanaoishi katika kazi ya kisanaa kwa lengo nla kubeba dhamira mbalimbali na kuiwasilisha kwa wanajamii.Mwandishi wa hadithi kidege amewatuma wahusika wa aina mbalimbali.Amewatuma wahusika wanadamu,ndege na samaki wote kwa lengo la kuwasilisha madhumuni yake.Kuna wale aliowadokeza na hawa kuendelea zaidi wakawapokeza wengine majukumu ya kuendeleza maudhui.

 

71.

1) MUSA

Jina la utani ni Mose,jina hili linaendelezwa hadi mwisho wa hadithi.

 

SIFA

a) Mwenye bidii

Licha ya kuwa na shughuli zake aligeuza uhusiano wake na samaki kuwa wajibu.Vipande vya sima alivyokuwa akivibeba havikuwa vyake bali vilikuwa vya kuwalisha samaki na ndege.Hata katika ndoto yake anapovamiwa na midege,kra zake zinampeleka mfukoni kwani yalikuwa ni mazoea yake kuwalisha.

 

b) Mwenye mapenzi makubwa kwa samaki.

Mose aliwapenda samaki na kuwafanya uraki nao.Aliwatunza samaki hata kama haikuwa kazi yake,alichukua wajibu wa kutenda hayo (uk86).Samaki walimjua na kumzoea, hii inatokana na hali ya kuwatupia vipande vya sima.

c) Mtani

Mose alitaniana na shirandula ndio shirandula alimtegea mose kitendawili.Kitendawili ambacho aliomba siku mbili ili akitegue.

d) Mkarimu

Aliweza kuwatunza na kuwalisha wale viumbe.Iwapo angekosa siku mbili au tatu,siku ya nne angefanya juhudi kuwatembelea.Hali hii inaonyesha ukarimu wa muda wake na kidogo alichokuwa nacho…..ni yeye tu ambaye angeweza kuwatembelea kwa madhumuni ya namna hii.(UK 89)

e) Mtabiri

Ndoto yake inakuwa ni utabiri wa mambo ambayo yangetokea.Ndoto ni kioo cha yaliyojiri baadaye.

f) Anamlahaka mwema

Mhusika huyu anaonyesha jinsi wanavyoingiliana na maraki zake.Hii ndiyo sababu iliyomfanya ajibanze mahali akiwatazama Joy n AchesA.Yeye na shirandula hawakuwa na utofauti.

 

 

72.

1) Shirandula:

a) Mtani

Mwandishi anatuelezea kuwa Shirandula alizoea

kumtania mose kila wakati kutokana na utani wake

hakosi la kusema anavyoeleza kuwa c hoo

kinachimbwa kasha kinajengwa..(UK87)

b) Mbunifu

Mtu mbunifu hakosi la kusema pindi tu anapojipata

katika hali ya kujitolea.Shirandula hakukosa la

kusema katika kitendawili.Mfano wanapozungumzia

kuhusu choo na kuelezwa kuwa choo hakijengwi

kinachimbwa…(UK86)

Anatoa jibu mara moja…(UK87)

 

 

c) Mcheshi

A n a p o p a t a j i b u l a m o j a k wa m o j a . Awa l i

anazungumzia kuhusu vijisamaki ambavyo anasema

huwezi kuvila na anauliza ni vya faida gani.

d) Mshamba

Watuwa mji wanamwita mshamba kwa kuwa yeye

alizaliwa kijijini.Mbali na kuzaliwa kijijini,tabia zake

zinadhihirisha hali hii kutokana na mawazo yake

kuhusu samaki.

 

 

2) JOY NA ACHESA.

Hawa ni baadhi ya wale waliokuwa wakizuru bustani ili

kujituliza.

 

 

SIFA

a ) Wenye mapenzi ya dhati.

Hawa wawili wanaonekana kuwa na mapenzi ya muda

,kama tunavyoelezwa na mwandishi kuwa walikuwa na

mazoea ya kuzuru mahali pale.

 

 

 

 

73.

b) Watani

Kutokana na mchezo wanaocheza wa kitoto ni bayana kuwa lazima wawe wametaniana.Joy kumrukia Achesa na wote kujikuta wakiwa chini.

c). Wacheshi

Kila mmoja anaangua kicheko kutokana nay ale wanayoyashuhudia.

 

MBINU ZA LUGHA.

1. Uhuishi/Tashihisi.

Hii ni tamathali ya usemi ambayo msanii huvipatia vitu sifa walizonazo binadamu kutenda na kufanya kama wanadamu..

a)Ndege walijibizana,mmoja huku na mwengine kule wakizungumza(UK83).Ingawa ndege wana uhai huwa hawazungumzi,msanii amewapatia sifa ya kuzungumza.

b) Ndege naye pale mtini akaona na kushangilia..(UK

85)

C) Ndege akaamua kuwafunganisha ndoa…(UK85)

d) Fikra zikamtuma mfukoni (UK89)

2. Tabaini

Ni tamathali ya usemi ambayo msanii hutuma usemi unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani

a) Jua si jua,baridi si baridi(UK 83)

b) Si wakubwa ,wala si wadogo(UK89)

c) Mwewe si mwewe,tai si tai(UK89

 

3) Takriri

Ni mbinu inayotumiwa na msanii ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno kwa lengo la kusisitiza : Mfano

i. Wakabingiria,Wakabingiria ….UK 84

ii. Samaki kumvutia mose,mose kumvutia ndege,Ndege

n a y e k u m v u t  a n a n i ? M o s e n a

Ndege,………………UK88

iii. Vuta,Vuta ………….….UK92

Shika, shika……………….UK86

 

 

 

 

74.

1) Nidaa

Huu ni msemo unaotumiwa na msanii kuonyesha kushangazwa na

jambo Fulani na huambatana na alama ya hisi au mshangao.

a) Poa! UK 83

b) Usivue! UK 86

c) Lakini wapi! UK 89 d) Lo! UK 94

e) Hawa watu na matamshi yao! UK 87

 

 

1) Tashbihi

Tamathali ya usemi ambayo msanii anavilinganisha vitu viwili

au zaidi, kwa kutumia maneno kama vile

Mfano wa mithili ya,kama na ja.

i. Alifuata desturi kama ibada…UK 89

ii. Midomo kama panga….UK 91

2) Tanakali za sauti

Hii ni mbinu ambayo msanii hutumia kuiga sauti za milio

mbalimbali. Milio inaweza kuwa ya vitu,wanyama n.k

i. Ndege alitoa sauti chwi!UK 84

ii. ………alikuwa keshamrukia pu !UK 84

iii. Kikalenga kwenye pua, chwa !UK 85

iv. ………Sauti yake ya kawaida chwi!UK 90

Chwi!……Chwi!……Chwi! UK 92

 

 

MTINDO WA UANDISHI

Msanii ametumia mtindo wa fasihi simulizi.Ameweza

kuingiza tanzu za fasihi simulizi katika masimulizi

yake.Lengo la kufanya hivi ni kuendeleza dhamira yake

na kuyakuza maudhui:

a) Utanzu wa maigizo

Mwandishi ametumia kipera cha kitendawili UK

90Kitendawili!Tega! Anayejenga choo na anayejenga?

 

 

75.

8. NIZIKENI PAPA HAPA

Ken walibora ni mkaazi wa Kenya, na mwandishi maarufu wa

Kiswahili. Ni mwandishi mtajika wa kazi ya fasihi ya Kiswahili.

 

MUHTASARI

Nizikeni papa hapa .Haya yalikuwa maneno ya otii mwenyewe. Otii alikuwa akisakatia kandanda timu ya Bandari FC Kwenye uwanja wa manispaa na kote inchini.Wakati huo alikuwa na siha yake na aliishi Mombasa.

 

Anakutana na Rehema Wanjiru msichana aliyekuwa mrembo Zaidi. Rehema alimwambukiza Otii ugonjwa.Akawa anaendesha akakonda sana na akawa na kikohozi kisichokoma .Ugonjwa huu unampeleka hadi kaburini .

 

Kabla ya kifo chake ,wanachama wa chama cha nyumbani wananza kukutana kwake kupanga mipango ya mazishi .Walihitaji kuchangisha fedha za kukondisha magari yakuchukua maiti na waombolezi kutoka Mombasa hadi sidindi karibu na Kisumu.Otii hakuona umuhimu wa safari hii ya kutoka Mombasa hadi sidindi

.Anapendekeza azikwe hapo Mombasa.

 

Hakuna anayesikiza ombi la Otii .Wanasisitiza lazima

{azikwe]maiti ya Otii angepelekwa Kisumu kulingana na mila na desturi zao. Jamaa na maraki na watu wa nyumbani lazima waandamane kupeleka maiti Kisumu. Walipoka mtito Andei wanakabiliana na Lori refu ambalo lilikuwa likija kasi huku linayumbayumba barabarani. Dereva wa matatu iliyokuwa imebeba maiti alijaribu kukikwepa kichwa cha lori lakini hakufanikiwa. Watu arubaini walifariki hapo papo . Wengine kumi na watatu walijeruhiwa ,baadhi yao vibaya sana.

 

Yote haya yalisababishwa na kupuuza . wangemsikiliza otii mambo hayangeishia vile;

 

ANWANI

Anwani ya hadithi hii nizikeni papa hapa inaoana na yale yaliyomo. Hili lilikuwa ni pendekezo la Otii kuwa akifa maiti yake isisarishwe hadi Kisumu lakini azikwe papo hapo Mombasa.

 

 

 

76.

DHAMIRA (LENGO)

1. Mwandishi anakusudia kuonyesha umuhimu wa uhusiano

katika kufanya mambo

2. Anadhamiria kukashifu mapenzi ya kiholela na kutuonyesha

athari zake. Mf uhusiano kati ya Otii na Rehema Wanjiru.

3. Mwandishi alidhamiria kuonyesha ukweli wa methali

asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

 

MAUDHUI MILA NA DESTURI

Wananchama cha watu cha nyumbani wanasisitiza kuwa lazima otii(maiti) ipelekwe Kisumu kulingana na mila na desturi. Wanasema katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si chochote, si lolote, muhimu ni kwmba sharti mtu wa kwetu azikwe nyumbani.

 

USHIRIKIANO/ UMOJA

Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani wanatangamana na kupinga mipango ya mazishi ya oti. Baada ya kifo cha otii, jamaa na maraki wa watu wa nyumbani ya mazishi walikjumuika kwa wingi, katika kitongoji duni cha Kisumu ndogo kupanga mazishi. Kwa pamoja wanachangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti nyumbani, siku ya kupeleka maiti nyumbani wanajitokeza kwa wingi.

 

UJEURI NA ATHARI ZAKE

Wanachama wa chama cha watu wa nyumabani walipoanza mipango ya mazishi na hata kufanya michango ili kugharamia mipango ya kupeleka maiti nyumbani.Otii aliwaambia mara kadhaa wamzike papo hapo Mombasa laikini hawakumsikiza. Walipokuwa safarini kuelekea Kisumu, kunatokea ajali mbaya ambayo inawaangamiza wengi na wengine wanapata majeraha mbaya.

 

(uk100) rakiye Otii anamtahadhirisha Otii dhidi ya kuwa na uhusiano na wasichana wazuri Zaidi kama Rehema Wanjiru. Otii hakutilia makini hayo. Alisema “pana hasara gani nzi kua kidondandani?”Aliendelea na uhusiano huu. Akapata ugonjwa uliompleka kaburini.

 

 

 

77.

SIFA ZA WAHUSIKA

OTII

Otii ndiye mhusika mkuu

 

Mchezaji hodari.

Aliyechezea timu ya Bandari FC kwenye uwanja wa manispaa na

kote nchini. Alichezea timu ya taifa Harambee stars wakati

alipotambaa jijini Mombasa .UK98 anakumbuka mataifa mengi ya

kigeni alikosari kwenda kusakata Kabamba kwa niaba ya taifa

lake na jukumu la kupeperusha bendera ya nchi yake.Alipokuja

tamko la michezo lililonukuliwa gazeti lilikisi kira za wengi. Pengo

la Otii haliwezi kuzibwa.

 

MBADHIIFU

Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipokutana

kupanga mipango ya mazishi, walikusudia kuchangisha fedha za

kununua jeneza, mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za

kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombolezaji hadi sindindi

yeye hakutaka hayo alisema, ‘ gharama zote hizo za kunipelka

sidindi za nini? Lakini wenzake wakasisitiza kuwa gharama hizo ni

zao si zake{UK97]

 

UJEURI/MWENYE MAPUUZA

Alipotahadharisashwa dhidi yakuwa na uhusiano na huyo msichana

mrembo Rehema Wanjiru alipuuza.Hatimaye akaambukizwa

ugonjwa uliompeleka kaburini.

 

CHAMA CHA WATU WA NYUMBANI

1.Umoja/ushirikiano

Wanashirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kupanga

mazishi ya Otii wanachanga pesa, wanakutana kwa Otii na

wanafuatana kuelekea sidindi kuhudhuria mazishi ya Otii.

 

2.Wanamapuuza

Otii alisisitiza kuwa yeye angetaka azikwe palepale Mombasa

lakini wakapuuza. Hatimaye wakapata ajali mbaya sana wakiwa

safarini kwenda sidindi kuhudhuria mazishi.

 

 

78.

3.WATAMADUNI

Wanasisitiza lazima wamzike otii nyumbani kulingana na mila zao.

Ni kinyume cha mila na ada zao kumwadia mwenzao kutupiliwa

mbali kana kwamba hana kwao.

 

WAKARIMU

Wanahakikisha wamechanga pesa za kutosha kugharamia mazishi

ya otii.

 

REHEMA WANJIRU

Ni msichana wa aina yake, mwenye urembo wa kutikisa jiji zima,

urembo wa kulikausha bahari, urembo uliompa wasichana wenziwe

husuda na wanaume mshawasha Fulani.

 

MZINIFU

Kuna uwezekano kuwa ugonjwa huu aliupata kupitia tabia ya

uzinifu.

MBINU ZA UANDISHI Chuku(hyperbole)

Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbefulani au

kusifu.

 

Uk 96…. kituamepotelea kwenye kitanda chake( mdogo Zaidi)

Uk 97…..Alipokua anakanyaga ardi mpaka inatetemeka( kwa

nguvu kutokana na afya nzuri)

Uk 100.. urembo wa kulitikisa jiji zima( mrembo sana)

Uk 101.. pengo aliloacha otii haliwezi kuzibwa( mchezaji stadi)

Uk 102.. wanahabari waliotiwa mbinu ya kupiga picha

hawakuweza kula nyama tena mazishini mwao.

 

Istiara

Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja.

Uk 96….. kabakia sindano (ameendelea sana)

Uk 96 wanamwita mbu ( mdogo Zaidi)

 

 

 

79.

Tashbihi (simile)

Ni mbinu ya lugha unayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa

kutumia maneno ya kulinganisha, kama mithili ya, sawa na ja;

Uk 98. Hakuweza kunyanyuka pale chini alikoabwagikie kama

gunia la chumvi.

Uk 99…. Alikuwa ametupwa kama masimbi yabuzaa

Uk 102…. Akajaribu kukwepa kichw acha hari kilichokua

kimemkodolea macho kama simba wa Hifadhi ya Wanyama ya

Tsavo.

 

Jazanda:

Kutumia maneno yaliyo na maana che.

 

Uk 96…jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahali pa kununua mwavuli..(jeneza)

Uk 98…. Alikua mwibe.

Uk 97,,, mbwa( kitu kisicho na thamani)

Uk 100… pana hasara gani nzi kua kidondani.

 

 

Utohozi

Ni mbinu ya kuwahilisha maneno ya lugha yatamkike kama ya

Kiswahili.

 

Uk 98…. Manispaa(Municipal) Uk 98…..mechi(march)

Uk 99 eksirei(xray) Uk 99… klabu (club) Uk 96 fremu

 

MSEMO

UK 97… Anapiga chafya.

Uk 99…. Akichungulia kaburi.

Uk 99…..Hawakujali hawakubali.

Uk 99….kufumba na kufumbua.

Uk 100..akapigwa na butwaa.

 

 

 

 

 

80.

Tashhisi/ Uhuishaji.

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye

UK100 urembo wa kulikaulisha bahari.

Uk.101.sifa za kibroda waombolezaji na kutapika wengine.

102 akajaribu kukikwepa kic hwa c ha lori kilic hokuwa

kimemkondolea macho.

 

METHALI

Uk.99. Mwacha kile hanacho na chema kimpotele.

Uk.99.aliyeumwa na nyoka akiona ungongo hushtuka.

 

Tabaini

Ni tamathali ya semi ambayo kwayo maneno/mawazo

yanayokinzana hutumiwa katika sentensi ili kuleta msisitizo wa

wazo.

 

UK99.si barabara ya mlango wa papa ,si barabara ya Nkrumah, si barabara ya jomo Kenyatta, si ya Digo

UK100..Si kuendesha, si kukonda, si vipele si si kukichwa kukikokome….

 

Mbinu rejeshi

UK96….Ukutani kumetundikiwa fremu yenye picha yake alipokuwa

bado na siha yake alipokuwa akisakatia kandanda timu ya

bandari FC.

Uk95…anakumbuka jinsi alivyokuwa akiwala chenga wachezaji

wa timu pinzani.

 

MASWALI

1. Anwani Nizikeni papa hapa ni mwafaka kwa hii

hadithi.Fafanua.[al 20]

2. Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusarisha

maiti.

a] Eleza muktadha wa dondoo hili. [al 4]

Haya ni maneno ya mwenyekiti wa chama watu wa nyumbani

walikuwa kwa Otii kando ya kitanda cha Otii ili kupanga mikakati

ya mazishi. Hii ilitokea baada ya daktari kuwaeleza wamrejeshe

Otii nyumbani kwa kuwa hakukuwa na matumaini ya kupata afueni.

 

 

81.

b] Walihitaji pesa za nini? [al 4]Walipaswa kununua jeneza,mavazi ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombolezaji kutoka hapa

Mombasa hadi Kisumuasilia.

c)Kwa kurejelea hadithi ya nizikeni papa hapa , eleza maafa

yanayotokana na ujeuri na mapuuza.

Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipoaanza

mipango ya mazishi na kufanya michango ili kugharamia mipango

ya kupeleka maiti ya Otii nyumbani.Otii alipendekeza azikwe pale

Mombasa lakini hawakumsikiza kabla ya Otii kukata roho. Pia

aliwakumbusha pendekezo lake la kuzikwa pale Mombasa,lakini

bado hawakutilia pendekezo lake maanani. Walipokuwa safarini

kuelekea Kisumu walipata ajali mbaya ambayo iliangamiza wengi

na wengine wakapata majeraha mabaya.Wangemsikiliza Otii

hawangepanga safari ya kwenda Kisumu na basi hakungekuwa na

ajali hii ambayo ilileta maafa Zaidi.

UK100….Rakiye Otii anamtahadharisha Otii dhidi ya kuwa na

uhusiano na wasichana warembo kama Rehema Wanjiru lakini Otii

alipuuza .

Aliendelea na ule uhusiano akaambukizwa ugonjwa uliompeleka

kaburini.

 

MASWALI

Methali ni nini? taja na ufafanue

Methali zilizotumwa katika hadithi ya mama bakari.

 

 

10.TULIPOKUTANA
TENA ALIFA CHOKOCHO

Hadithi hii inasimuliwa na Sebu,Msimulizi akiwa mkewe pamoja na rakiye Kazu aliyekuwa na mkewe pia,walikuwa kwenye Hoteli

 

 

Rombeko. Maraki hawa walikuwa na mazoea ya kukutana kila mara walipopata wakati,kwa lengo la kubadilisha mazingira Kutokana na mazungumzo yao,ni bayana kuwa maraki hawa ni watani.Utani wao unawajumuisha wote wanne bila kuudhika huku wakijihusisha jamii zao.

 

 

82.

Siku hiyo walizungumzia kuhusu uchawi.Vicheko vyao vilidhihirisha uhusiano mwema,hali hii inaonyesha mlahaka uliokuwepo baina wane hao.

 

Mazungumzo yalibadilika pale msimulizi alirejelea maisha yake ya awali ambapo alikuwa na kumbukizi ya raki yake wa utotoni kwa jina Bogoa.Msimulizi anasema kuwa yeye Bogoa waliyafanya mengi ya utotoni lakini walitengana baada ya kuhitimu miaka 19 mwaka wa1966.

 

Kazu anazungumzia kuhusu Bogoa aliyetoka sehemu za mate.Anaelezea kuwa Bogoa alijifuza usonari na alikuwa akikifahamu kitinya kama lugha Yake mwenyewe.Inasadifu kuwa Bogoa wanaye mzungumzia ni yuyo huyo mmoja.

Hofu ya Sebu ilikuwa uwezekano wa Bogoa kukubali mwaliko kwa sababu anavyotueleza msimulizi ni kuwa aliipuuza nchi yake na hata kuwasahau wazazi wake.

 

Miradi yao ilikuwa wakutane club Pogopogo,kwa watu wa kupata cha chini.Bogoa alimtambulisha mkewe Sakina kwa raki yake Sebu naye akamtambulisha Bogoa kwa mkewe Tunu.

Bogoa anaturejesha katika maisha yake kwa uc hungu mwingi.Ilikuwa ni hadithi ambayo hakuwa amemsimulia yeyote hata mkewe.Anayakumbuka maisha aliyoyapitia kwa mlezi wake.Alinyimwa hata uhuru wa kucheza na badala yake akafanya ngumu.

Wazazi wa Bogoa wanaonyesha hali ya kutoajibika majukumu yao kama wazazi.Hawakuwa na wakati na mtoto wao hata baada ya kumuachia mle hawakufaidia maisha yake .Bogoa anabaki kuwa na kisasi kuwa na kisasi na wakazi wake.

 

DHAMIRA

Mwandishi anawakashifu wazazi ambao hawayatekelezi

majukumu yao ya uzazi.Wengi wa wazazi wanawaachia walezi

majukumu yote bila kujali hisia za watoto wao.

 

 

 

83.

Bogoa utotoni anayapitia maisha magumu na hakuwa na wakumwelezea madhila aliyoyapitiaila ila tu aliangalia ndani kwa ndani.Hali hii inapalilia kisasi dhidi ya wazazi wake.

 

 

 

MAUDHUI.

1. Ulezi

Jukumu la kila mzazi ni kumlea mtoto kwa njia ifaayo na

kuyatekeleza mahitaji ya huyo mtoto.Jambo la msingi ni

kumwelimisha na kumpatia mashauri.

Wazazi wa Bogoa waliyakwepa majukumu yao na kumtwika

mlezi ambaye alimdhulumu mwanao.Malezi hayo yanamfanya

Bogoa kulipiza kisasi dhidi ya wazazi wake hata wanapoaga

dunia hakuhudhuria mazishi yao..

2. Ukatili

Sinai alimtendea ukatili Bogoa kwa kumnyima fursa ya kucheza na

wenzake.Fauka ya hayo alimpiga pindi tu alipochelewa

kurudi.Babake Bogoa aliutenda unyama kwa kumpeleka

mwanawe kwa mlezi bila kufuatilia maisha yake yalivyokuwa

kwa mfadhili wake.

3. Elimu

Elimu ni mwanga kwa kila mja.Njia moja ya kuelimika ni kwa

kupelekwa shule.Hata hivyo kuna elimu inayopitishwa na

wanamrika(peer);mfano:Sebu alimfunza Bogoa kusoma mpaka

akaweza kusoma hadithi nzima.Kulikuwa na mtazamo hasi

kuhusu watoto wa kimaskini ambao ilisemekana kuwa hawastahili

kusoma shuleni.Mtoto ambaye hakwenda shule alidhaniwa kuwa

mtoro.

4. Umaskini

Sababu kuu ya umaskini kulingana na mwandishi ni idadi kubwa ya

watoto.Wazazi wa Bogoa walikuwa na watoto takribani kumi na

sababu ya kumpeleka Bogoa kwa mlezi ilikuwa ni kutowamudu.

Ishara ya umaskini inadhihirishwa na vazi alilovalia msimulizi

a n a s e m a . ” K i l i k u wa n i k i v a z i p e k e e c h a m t u n g i n i

kwangu”.Hawakuwa na fedha hata za kununulia viatu.Vile vile

hakuwa na pesa za kulipia nauli ndiyo maana walitembea kutwa

hadi jijini.

 

 

84.

1. Uraki

Uraki wa maraki haya ni wa dhati.Maraki hawa walikuwa wanakutana si mara moja kwani anasema kuwa …….`tulipenda kuja seka kubadilisha mazingira na kuonana na maraki z e t u . ” … ( U K 1 0 4 ) . K w a k u w a w a l i k u w a m a r a  k i wakubwa,waliwahusisha wake zao.Ni kutokana na mojawapo wa mikutano yao. Kazu anapomtaja Bogoa. Kutajiwa Bogoa kunaleta kumbukumbu katika mawazo ya Sebu.Anamkumbuka raki yake wa utotoni.Kutokana na mjadala ule ndipo wanapokutana tena.

 

 

Maudhui mengine:

1. Ukandamizaji wa watoto

2. Uchawi

3. Bidii

4. Uwajibikaji

5. Uhuru wa watoto

6. Nafasi ya wazazi katika malezi.

 

 

WAHUSIKA. a) SEBU

Huyu ndiye msimulizi, jina lake halisi tunalitambua kutoka kwa wahusika wengi kama Kazu na Mkewe.

a) Mtani

Sebu pamoja na rakiye wanataniana kwa kiwango kikubwa bila kuudhika .Ni watani wa muda mrefu kwa sababu wanataniana kuhusu jamii zao.

b) Ana mlahaka mzuri

Kutokana na mazungumzo yao tunaelewa kuwa uhusiano wao ni mzuri.Anatueleza kuwa huwa wanakutana pindi wanapopata upenyo .Hali hii ndiyo iliyomfanya kuwa na uhusiano mwema.

c) Mwaminifu

Bogoa alimwaamini tangu wakiwa watoto.

 

 

85.

a) BOGOA.

Raki wa utotoni wa msimulizi.

Sifa:

Msiri;

Hakumwelezea Sebu shida alizokuwa akizipitia kwa mlezi

wake.Hakuwaelezea wazazi wake madhila aliyokuwa

akiyapitia.Wanafunzi wenzake hawakujua asili yake kwa maana

hakuwaelezea walibaki tu kukisia.(UK 116)

 

Mvumilivu;

Aliyavumilia mateso kutoka kwa mlezi wake.Katika umri wake

mdogo alifanyishwa kazi nyingi zilizopita umri huo.Kama

anavyoeleza ni kuwa angechelewa,alitafutwa na kupigwa vibaya

sana..(UK 116).

 

Mwenye Bidii;

Licha ya kupitia madhila hayo,Bogoa alikuwa mwenye

bidii.Alijifunza kazi ya usonara na kuajiriwa.

 

Ameajibika;

Aliwajibikia jamii yake na ndoa yake ilikuwa imesimama imara,

zaidi ya hayo ni kuwa watoto wake walikuwa wamekomaa.

 

Mwenye Kisasi;

Alikasirika kiasi cha kutorudi kwao tena,Hata mazishi ya wazazi

wake hakuhudhuria.Alikuwa na kisasi na wazazi wake.

 

MATUMIZI YA LUGHA

a) Tashbihi

Tamathali ya usemi ambayo msanii huvilinganisha vitu viwili au

zaidi kwa kutumia maneno ya kulinganisha kama vile:Mithili

ya,sawa na,ja,na mfano wa:

· Kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga(UK

109)

· Kumtoka kama maji yanavyotiririka bombani.

 

 

 

86.

a) Uhuishi

Uhuishi/Tashihisi/Uhaishaji ni tamathali ya usemi ambayo msanii huvipatia vitu visivyokuwa na uhai sifa walizonazo binadamu na kutenda kana kwamba vina uhai.

a) Vicheko vilivyovuma na kuparamia kuta.(UK 107).Vicheko

vinapatiwa sifa ya binadamu ya kuparamia kuta.

b) Kuikimbiza furaha na kuileta huzuni(UK 109)

c) Ukweli wenye makali yanayochinja bila huruma (UK 117)

b) Nidaa

 

 

Ni msemo unaoonyesha kushangazwa na jambo Fulani na huambatana na alama ya mshangao.

 

 

a) …….na kuwatema watu hao huko magharibi!(UK 105)

b) ……mimi ni binadamu mwenzako!(UK 105)

c) …..hatukupata hata fununu ya kuwepo kwake(UK 110)

c) Maswali ya balagha

Haya ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika na hayahitaji majibu ya moja kwa moja.

a) …..huoni kwamba unaniumiza?(UK 105)

b) …..uchawi si sayansi?(UK 106) c) ……kabadilika vipi? (UK 111) d) Semi

Haya ni mafungu ya maneno ambayo yanapotumika,hutoa maana nyingine badala ya ile ya maneno yaliyotumika.Hutumika ili kuipamba lugha .Kuna:

NAHAU

Huu ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la

k u l e t a m a a n a i l i y o t o f a u t i n a m a n e n o h a y o

yaliyotumiwa.Tofauti na msemo huwa na vitenzi.

a) Napiga funda (UK 106)

b) Kupiga funda (UK 114)

 

 

 

87.

MISEMO

Hizi ni semi fupi fupi zinazotumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalum.Mfano;

Pua na mdomo(UK 108)

 

 

 

11.MWALIMU
MSTAAFU

Dumu Kayanda ni mwandishi chipukizi mwenye uwezo wa kubuni hadithi ilio na upeo usiokadirika. Amekuwa mwalimu wa somo la Fasihi kwa muda katika shule mbalimbali.

Mwalimu Mesi ndiye mhusika mkuu katika hadithi hili. Anwani hii inafaa kwa sababu hadithi inaelezea kuhusu maisha ya Mwalimu Mesi Kabla na baada ya kustaafu.

Kutokana na kuwajibika kama mwalimu,Mwalimu Mesi alipewa sifa chungu nzima. Aliweza ‘kuwanyanga’ wanafunzi wake mpaka hatimaye wakawa watu wa kutajika. Wengine wakawa mawaziri,wabunge,marubani,wahandisi,madaktari na wengine wahasibu.

 

Siku ya sherehe ya kumuaga shuleni,wazazi wa wanafunzi wa zamani na wampya walihudhuria na kumletea zawadi za aina tofauti tofauti. Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa isipokuwa hotuba ya Jairo iliyokuwa ya kumlaumu tu Mwalimu Mesi.Jairo alikuwa zuzu hata darasani , anamlaumu mwalimua eti alimpotezea muda wake na ndio kwa sababu yeye ni maskini. Mwalimu anampa Jairo zawadi zote lakini Jairo hana shukrani. Anakiona hicho kitendo cha kupewa zawadi kama kuaibishwa na Mwalimu. Jairo anawaleta mke na watoto wake kwa mwalimu kama zawadi. Mke wa Jairo alipewa nyumba kwenye kichumba cha mwalimu na akakaa na watoto wake.

 

Jairo hakuwapitia kwa Mwalimu Mesi kuwaona jamaa yake hadi siku alipokiwa na tetesi kuwa mwalimu amemwoa bintiye. Kumbe ilisadifu kuwa mwalimu na kile kisichana walipoandamana kwenda kununua kitabu mjini, mwalimu akawa mgonjwa na Yule msichana akapelekwa shule ya bweni. Ilikua ni sababu tosha ya wenye umbeya kueneza uvumi kwa mwalimu na bintiye Jairo. Hawakuonekana na ni kwa sababu wameanza kuandika kurasa mpya za maisha yao pamoja.

 

 

88.

Anwani.

Anwani hii MWALIMU MKUU inafaa kwa sababu hadithi mzima

inazungumza kuhusu maisha ya Mwalimu mstaafu Mesi .

 

 

Dhamira

1.Mwandishi alikusudia kuonyesha umuhimu wa kuwajibika kazini

kama alivyowajibika Mwalimu na mazao ya kazi yake

yanaonekana.

2.Mwandishi pia anadhamiria kuonyesha tofauti ya watu wa elimu

maishani. Kuna tofauti ya watu waliosoma na wale ambao ni zuzu

kama Jairo.

 

 

WAHUSIKA
Mwalimu

Mesi

1.Amewajibika

Kutokana na kule kuwajibika, anapewa sifa chungu nzima .

Wanafunzi wanaishia kuwa madaktari,, mawaziri, marubani n.k.

Wengi wanahudhuria sherehe yake ya kumuaga na kumletea

zawadi nyingi kama ishara ya shukrani.

 

 

2.Karimu

Anampa Jairo zawadi Zote alizoletewa katika sherehe ya

kumuaga.

Anakubali mke na watoto wa Jairo waishi kwake.

Kisichana cha Jairo kilipofukuzwa shuleni kwa kukosa kitabu,

waliandamana hadi mjini kukinunulia kitabu.

 

 

3. Mwenye utu/ubinadamu

Anaamini watu wote ni sawa, hakuna mtu nusu mtu. Anasisitiza watu

ambao hawakuja kwa magari mazito pia wapewe nafasi ya kutoa

hotuba walivyopewa wengine wa tabaka la juu. Jairo anapotoa

hotuba yake, alimlaumu tu Mwalimu lakini hilo halikumkera

Mwalimu.Anampa Jairo zawadi zote , anaamini jairo alizihitaji

zaidi.

 

 

89.

4.Mwenye sifa tele

Uk 120…Wanafunzi wake wote hao hawamsahau kwa nasaha

zake, kwa insafu yake, kwa huruma yake, kwa hekima yake,kwa

ustaarabu wake,kwa uadilifu wake ,kwa uwajibikaji wake, kwa

nemsi yake,kwa ucheshi wake.

Hotuba zao zilijaa sifa tele.

 

JAIRO

Alikua mwanafunzi wa Mwalimu msaafu ambaye mambo

hayakumwendea vizuri.

 

1.Mwenye Kulaumu

Jairo alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Mwalimu Mstaafu. Yeye ni

tofauti na wengine wengi, aliishia kuwa mtu ovyo . Hali yake ya

umaskini inamfanya amlaumu Mwalimu eti alipotezea wakati kwa

kumueka darasani na kumpa tumaini za uongo.

 

2.Zuzu

Hata baada ya kuwa shuleni kwa miaka yote ile hakuweza kuunga

moja na moja. Pia alipata sufuri masomoni.

 

3.Mcheshi

i)Haelewi kwa nini Mwalimu alimshauri asilewe ilhali anaamini

tembo inampa raha ya kuishii. Alisema kuwa alipolewa hata

akitembea bila viatu na kujikwaa au kudungwa na miiba, hakuhisi

kitu.

ii)Hakuelewa pia kwa nini kuepukana na ulevi, kusubiri hadi ndoa

ndipo ‘kuchana ngazi.’

iii)Anapeleka mkewe na wanawe kwa Mwalimu na kumpa kama

zawadi.

 

MKE
WA
MWALIMU

1.Mwenye utu

Anakubali mke wa Jairo na wanawe waishi kwao. Anamtunza kama

bintiye. Anamwambia , “Hapa paite nyumbani. Upaone hapa

kwenu kama si nyumbani pako. Ukae upumzike. Ukae uone raha ya

kuishi.”

 

 

90.

2.Mwenye bidii/Anauhusiano mzuri na watu

Wanaandamana na mke Wa Jairo kwenda kondeni kupanda

mbegu, kupalilia, kumwagia mazao kondeni mbolea. Pia walienda

k u t e k a m a j i n a k u t a f t a k u n i . Wa l i c h u m a k u n d e n a

mchacha,mabenda kondeni wakiziambua na kuzikata mboga hizo

pamoja pale uani.

 

MKE
WA
JAIRO

1.Mvumilivu

Mwandishi anaeleza maisha ambayo mkewe Jairo ameyapitia.

“Katika maisha yake na Jairo, ameonja ladha zote za dhiki, thakili,

bughudha na kero. Hakuna mwanamke anayejua kumezamate

machungu kama Mke wa Jairo.”

 

2.Mtiifu

Anapopelekwa kwa Mwalimu kama zawadi, Mwalimua

anamshauri arudi kwake lakini anakataa. Anasema “sharti ni mtii

mume wangu. Mume ni mume hata akiwa gumegume.” Mwalimu

aliposisitiza, mke wa Jairo alimweleza kuwa hawezi kwenda

kinyume na amri ya Jairo mume wake.

 

 

 

3.Mwenye bidii

Waliandamana na mke wa Mwalimu kondeni kupanda, kupalilia,

kuteka maji vijitoni na kutafta kunikuni.

 

WANAFUNZI
NA
WAZAZI

1.Ni wenye shukrani

Wanaka katika sherehe ya kumuaga Mwalimu kwa wingi wakiwa

na zawadi chungu nzima.

 

2.Karimu

Wanamletea Mwalimu zawadi chungu nzima.Wanaendesha

magari makubwa na ni waadilifu kwa sababu walifuata ushauri wa

walimu wao. Wale ambao hawakupata elimu wameishia kuwa

maskini , walevi ambao hawana mbele wala nyuma. Pia hawana

maadili mema.

 

 

91.

3.Uzuzu/Ujinga

Hata baada ya kuhudhuria shule ya msingi, Jairo hawezi kuunga

moja na moja. Haoni umuhimu wa elimu. Anamlaumu Mwalimu Mesi

eti alimpotezea muda wake bure shuleni kwa kumwambia kila

uchao kwamba ataimarika na hakuwahi imarika. Anamlaumu

Mwalimu kwa kumshauri asinywe tembo ilhali anaamini hiyo tembo

ndio humpa raha ya kuishi. Anaamini kinyume cha nasaha za

Mwalimu ndio utamu na uhondo wa maisha. Uzuzu unamfanya

awapeleke mke na watoto wake kwa Mwalimu kama zawadi.

Anaona soni kupokea zawadi kutoka kwa Mwalimu. Haelewi

mbona akapewa zile zawadi ilhali alizihitaji zaidi.

 

MAUDHUI
Kuwajibika

Hii inadhihirika zaidi siku ya sherehe za kumuaga Mwalimu Mesi pale shuleni.

 

Waliohudhuria sherehe hii walikua wengi mno. Mwandishi asema “walika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano wa soka wa kuwania kombe la dunia kutokana na kazi nzuri ya Mwalimu, wanafunzi wake waliishia kuwa madaktari, wabunge n.k. Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa kwa Mwalimi Mesi.

 

Elimu

Mwandishi anatuonyesha umuhimu wa Elimu.watu waliomakinika

k a t i k a e l i m u h a t i m a y e w a l i k u w a ‘ w a t u ‘ , w a k a w a

mawaziri,wabunge, marubunu n.k. Wakawa pia wanaendesha

magari ya nguvu. Elimu unawafanya watu kuwa watu wa maana

,watu bora kwa hadafu. Lakini wale ambao hawakumakinika,

hutumia yao duni, maisha ya umaskini. Pia wana mitazamo hasi

kuhusu maisha.

 

Utabaka

Utabaka unasababishwa na kupata au kukosa elimu. Waliosoma

na kufaulu katika elimu, wanaishi kama ‘watu’. Wanapata kazi

nzuri, zinzwapa mshahara.

 

92.

Ukarimu

ukarimu unajitokeza wakati Mwalimu Mesi anampa Jairo zawadi zake zote, anasema “mimi nimeamua kwa hiari yangu kukupa wewe zawadi hizi.”

Mwalimu na mkewe (Bi Sera) ni karimu,wanawakaribisha mke na

watoto wa Jairo kwao.

 

MBINU
ZA
LUGHA
Kuorodhesha

Mwandishi anatumia mbinu ya kuorodhesha mfano;

Uk 120: Wanafunzi waje wote hao wanafunzi wake hawamsahau

kwa nasaha zake,kwa insafu yake, kwa huruma zake ,kwa hekima

zake, kwa ustaarabu wake, kwa uadilifu wake…

Uk 121:Wanafunzi wake waliokuwa bado wanasoma kwenye shule

hiyo waliimba tele, nyimmbo za jamii mvbalimbali, wakacheza

zeze,mariamba, lelemama, mdundiko, violoni.

 

Uk 122:…sikwambii haya madude makubwa waliokuja kututisha nayo akina Bariki,Festo, Mshamba ,Nangeto na hali kadhalika.

 

Tabaini

Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzola mchanga,si

makubadhi ,si meza na samani aina aina, si fedha

Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzolea mchanga,si

makubadhi,si meza na samani aina aina,si fedha.

 

Takriri/Uradidi

Uk 126:Wanafunzi wako wote hao wanafunzi wake.

Uk 128:Jairo aliambiwa , akaambiwa na kuambiwa na wajuao.

 

Tashbihi

Uk 120:…mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji kwenye mlima

Kilimanjaro.

Uk 121:…walifurika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki

wa mchuano.

 

 

 

 

93.

 

Uk 122:Kichwa chake chenye upana killing’aa utosini kama sufuria kwenye duka la Buniani.

Uk 125:…wakapokeza hotuba hio kama huizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Uk 129:…kimenawiri kama ua linalotimbuka kudamu.

Uk 129:Aliona madodo yamesimama kifuani kama kanzi mbili za mwanamasumbwi.

Uk 129:…kiuno kimechukua umbo mduara kama cha nyigu.

 

Tashhisi

Uk 120:Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake kidogo.

 

Methali

Uk 121: Anayo maneno ya kuweza kumtoa nyoka pangoni. Uk 123: : Kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.

Uk 128:Alikuwa ametuma jongoo na mti wake.

 

Jazanda

Matumizi ya maneno yenye maana che.

Uk 121:…wenzao hao waliokuwa wamekua watu.

Uk 121:…lakini nadhani ni jambo la busara kutotia mchanga kitumbua.

Uk 129:Walitafuta kitabu cha maisha na kuanza kuandika kurasa mpya za maisha yao pamoja.

Uk 124:…kusubiri hadi ndio ndipo kuchuna ngozi.

 

Kinaya

Kinyume cha matarajio

Uk 123: Ni kinaya kwa Jairo hakuona sifa nzuri ya Mwalimu Mesi. Yeye anamuona kama kikwazo kikubwa kwake. Kama yeye Jairo anaishi maisha duni kwa sababu ya Mwalimu Mesi.

Uk 126:Ni kinaya Mwalimu Mesi kumpongeza Jairo kwa hotuba yake kumhusu ambayo ilijaa kumlaumu Mwalimu kisha Mwalimu Mesi anamueleza akifa mwanzo azungumze siku ya mazishi yake. Uk 126:Ni kinaya Jairo anapopeleka mke wake na watoto kwa Mwalimu Mesi kama zawadi.

Uk 127:Ni kinaya kwa mkewe Mwalimu Mesi (Bi Sera)kumkaribisha mke na watoto wa Jairo kwao “Mwachie akae huyu binti na watoto wake, tutawatunza.”

 

 

94.

Msemo

Uk 121:Wanafunzi wake wa zamani waliopewa kisogo na dunia

Uk 126:Hakuna mwanamke anayejua kumeza mate machungu.

 

Mdokezo/Kauli
isiyokamilika

uk 120:kisa na maana ni huyo Mwalimu Mesi.

uk 123:kwamba kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.

UK 125:…umefanya makosa makubwa sana.

Uk 125:…hamna mwendawazimu wala mahaka kati yetu.

Uk 126: “Badala ya ngojera nyingi za huyo anayemwita si siri au

siri sijui.

 

Sadfa(matukio mawili yanayotokea kwa pamoja).

Inasadifu kuwa baada ya Mwalimu kuondoka na kile kisichana

kununua kitabu hakuonekana tena. Watu wakakiri eti Mwalimu

alikua amekioa kile kisichana. Kumbe wakati huu Mwalimu alikua

akiugua na alikua ndani(nyumbani) wakati wote huo na ndio

sababu hakuonekana.

 

Maswali

1.Onyesha umihimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya

Mwalimu Mtaafu.

i)Mwalimu Mesi

ii)Jairo

iii)Mkewe Jairo

iv)Wanakijiji

(al 20)

2.Fafanua maudhui yoyote manne katika hadithi hii. (al 20)

 

Ukarimu

Mwalimu Mstaafu ni mkarimu. Hii inadhihirika anapopokea zawadi

kutoka kwa wazazi na wanafunzi na kumpa Jairo zote.

Pia Mwalimu na mke wake ni wakarimu kwa mke wa Jairo na watoto

wake. Waliwapa nyumba akae na watoto wake. Waliwachukua

kama binti yao. Bintiye Jairo alipofukuzwa shuleni kwa kukosa

kitabu, Mwalimu Mstaafu alimnunulia.

 

 

 

95.

Utabaka

Utabaka umesababishwa na kupata au kukosa elimu. Waliopata elimu walipata kazi nzuri kama za uwaziri ,ubunge, udaktari, urubani n.k. kazi zilizo na mshahara mzuri. Wakawa wanaishi maisha mazuri na kuendesha magari ya nguvu. Wale nao ambao walikosa elimu, waliishi kuwa maskini na walevi.

 

Kuwajibika

Hii inadhihirika zaidi siku ya sherehe za kumuaga Mwalimu Mesi. Kutokana na kuwajibika kwake kama Mwalimu,wanafunzi wake wa n a f a u l u m a i s h a n i . Wa n a p a t a k a z i n z u r i k a m a z a udaktari,ubunge,uwaziri n.k. Hii ndio sababu walikuja kwa wingi kumshukuru Mwalimu Mesi. Hotuba zao pia zilijaa sifa tele.

 

Bidii

1.Mwalimu anajibidiisha katika kuwafunza na kuwashauri wanafunzi wake.

2.Wanafunzi walifanya bidii na kufaulu mitihani yao.

3.Mkewe Mwalimu na mkewe Jairo wana bidii pale kondeni wanapo panda mbegu,wanapalilia,wanateka maji.

 

12.MTIHANI
WA
MAISHA

Eunice Kumaliro ni mzaliwa wa Kenya. Mshauri na mtaalam wa elimu aliyeandika vitabu kadhaa.

 

Muhtasari

Je,Samueli alikuwa amepita mtihani wake wa Elimu? Kuanguka mtihani wa elimu ni kuanguka pia mtihani wa maisha?

Samueli ambaye ni mhusika mkuu katika hadithi anaenda shuleni kuchukua matokeo yake ya mtihani. Akiwa pale foleni nafanya moyo wake kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa alikuwa amepita mtihani wake vizuri.

 

Kule ndani ya osi , Mwalimu Mkuu ameketi pale na anapuuza kuwepo kwake osini humo. Hatimaye anamtupia Samueli stakabadhi ya matokeo yake.

Samueli anapotambua alivyokuwa amefeli mtihani wake, anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo yake kwa dai ya kutokamilisha kulipa karo ya shule.

Samueli haoni haja ya kuishi tena. Anakata kauli kujitosa majini afe. Hakuwa tayari kupata aibu kutokana na matokeo yake mabaya.

 

 

96.

Mamake Samueli ana matumaini kuwa kuanguka mtihani wa elimu si kuanguka mtihani wa maisha. Anamshika Samueli mkono na wanaelekea nyumbani.

 

Anwani

Anwani ya hadithi hii, MTIHANI WA MAISHA inaoana na yale yaliyomo. Kupitia kwa mamake Samueli, mwandishi anaonyesha kuwa kuna maisha hata baada kuanguka mtihani wa elimu. Kuanguka mtihani wa elimu sio kuanguka mtihani wa maisha.

 

Dhamira

Mwandishi alikusudia kuonyesha;

1.Kuanguka mtihani wa elimu sio mwisho wa maisha. Bado kuna

matumaini.

2.Umuhimu wa kumakinika katika masomo kwani athari za

kuanguka mtihani ni hasi.

 

MAUDHUI
Ukatili

Samueli analinganisha babake na hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Samueli alipofeli mtihani wake, anavunjika moyo na kuona maana ya kuishi. Anakata kauli ya kujiangamiza kwa kujitosa majini. Babake hata baada ya kumuona mwanawe katika hali ya kuvunjika moyo, hakumhurumia, badala yake anaamrisha watu wamuache ajitose majini afe. Pia anampa kamba atumie kujitia kitanzi.

 

Ucheshi

Samueli ni mcheshi. Anachekesha anaposema udongo uliowaumba

babake na mamake ni tofauti na ndio sababu mama angeweza

kuelewa kidogo atakapojua amefeli mtihani lakini baba hawezi.

Anapomwangalia Mwalimu Mkuu, anamwona ni kama aliyezidiwa

na maumivu au anayepaswa kufanyiwa oparesheni ya ubongo na

anayehitaji maombi.

Anapoamka kuchukua hatua ya kujiangamiza ,anatazama juu

kumpasha Muumba wake ujumbe kuwa alikuwa njiani akielekea

mbinguni. “Naja huko juu mbinguni mapena kidogo Baba.

Nitengee nafasi. Nimeruka foleni…”

 

 

97.

Nafasi
ya
Mwanamke

Mwanamke anapuuzwa katika jamii hii. Inathibitishwa na mtazamo

wa baba kupitia elimu. Ingawa baba aliyaonea fahari mafanikio

ya binti zake, aliwaona kama wanawake tu. Fahari yake ya dhati

ilikuwa katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Samueli

haamini vipi angeweza kushindwa katika mtihani na dada zake

ilhali ni wanawake.

Mwanamke kupitia kwa mhusika mama amechorwa kama aliye na

utu na matumaini. Anamshika Samueli mkono na kumwambia

waende nyumbani na kumweleza maneno ya kumpa tumaini. Pia

anapenda amani na ni mshauri mwema. Anamshauri mumewe

aende shuleni wasuluhishe sintofahamu kuhusu karo.

 

Kufa
moyo/kuvunjika
moyo

Samueli alipoanguka mtihani hakuona haja ya kuendelea kuishi na

anaamua kujitosa majini afe. Anasema, “Acha nijiondokee duniani

niwaachie wafanisi wafanikiwe.” Katika ujumbe wake na Muumba

anasema itabidi aende mbinguni kwa sababu stahamala

zimekwisha.

 

Elimu

Elimu ni muhimu maishani. Wasichana katika jamii hii wanafanya

vizuri kuliko wavulana. Wavulana wanamchezo shuleni (Mahoka)

unaochangia kuanguka kwao. Hakuna anayepewa matokeo yake

ya mtihani kabla ya kumaliza kulipa karo. Athari za kuanguka

mtihani ni kama vile aibu na hata kujiangamiza.

 

WAHUSIKA
SAMUELI

Ndiye mhusika mkuu

 

Mcheshi

1.Anaposema, “labda Mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda anapaswa kufanyiwa operesheni ya ubongo ama anahitaji maombi hasa atakuwa na akili razini tena.”

2.Samueli anasema kuwa mamake na babake wameumbwa kwa aina tofauti kabisa ya udongo.

3.Anamuarifu Muumba kuwa yumo njiani akienda mbinguni basi atengewe nafasi kwani ameamua kuruka foleni.

 

98.

Mwenye Matapo

Anaposema yeye hana moyo wa bua. Kile asomacho ndicho kijacho

kwenye mtihani. Anaelewa kuwa yeye si mwerevu sana laikini

anajua kupanga mikakati na pia anaamini ana bahati ya mtende

anaamini kuwa amepita mtihani wake vyema na kuwa motokeo

yake yangemshtua Mwalimu mkuu ambaye hakuwa na imani naye.

 

Mwongo

(uk 137) Samueli anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo

yake kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.

 

Mwoga

Uk 133: Anaogopa anapoingia katika osi ya Mwalimu mkuu.

Woga unajitokeza kutokana na anavyozungumza/anasitasita.

“Mwa…limu nimekuja kuchu…chukua matokeo…” “samaha…ni.

Waa…zazi wangu.” Samuel anatetemeka anapomwona babake

pale kwenye bwawa(uk 132)

Mwenye machoka

(uk 134)ni kutokana na tabia hiyo pale shuleni ndipo akapewa jina

‘Rasta’

 

Kufa moyo/kuvunjika moyo

Kuanguka mtihani kwa Samwueli si jambo alilokuwa akitarajia.

Alikuwa ana uhakika kuwa amepita mtihani wake.Jambo hili

ameliona kama la kumletea aibu mbele ya wazazi wake,

alivyopendekeza Samueli.

Anakata kauli kujitosa majini afe. Hakuna maana ya kuuendelea

kuishi. Anasema “Acha nijiondokee duniani niwaachie wafanisi

wafanikiwe anamwambia Mungu kuwa amekosa stahamala.”

 

MAMAKE
SAMUELI Mwenye utu

Mamake Samuel anaka kwenye bwawa la maji alipokuwa amejitosa Samuel, anamshika Samuel mkono na kumwomba waende nyumbani. Anamwambia Samuel maneno ya kumpa moyo, “huwezi kushindwa na mtihani wa shule na vilevile kushindwa na mtihani mwisho.

 

 

99.

Mwenye Matumaini

Hata kana kwamba Samuel ameanguka mtihani wa shule, mamake

Samuel anaamini kuwa kuna matumaini hata baada ya kuanguka

mtihani huo. Anaamini Samuel hajaanguka mtihani wa mwisho.

Anaamini pia kuwa Mungu hamkoseshi mja wake yote. (UK 139)

 

Mwenye Kuelewa Mambo

Samuel anasema kuwa kweli amemusaliti mamake kwa kuanguka

mtihani lakini mamake tofauti na babake, ataelewa.

 

Mpenda Amani

Samuel anapomdanganya babake kuwa hakupata matokeo ya

mtihani wake ati kwasababu hajamaliza kulipa karo, anakereka.

Mamake Samuel anaingilia kwa upole na kumshauri mume wake

amuone Mwalimu mkuu ili wasuluishe suitofahamu hiyo.

 

BABA
SAMUEL Katili

Samueli anamlinganisha babake na hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima.

Baada ya Samueli kuanguka mtihani alikuwa na kipindi kigumu na anaamua kujiangamiza. Babake hakuwa na huruma naye hajali kama atajitosa maji afe. Anasema “mnamzuia kwa nini? Mwachie ajitose majini kama anataka. Ana faida gani huyo? Sikuzaa mwana nilitoa tu maradhi tumboni.” Uk 139 Anampa Samueli kamba aitumie kujiangamiza.

 

Mwenye moyo mgumu

Babake Samueli ana moyo usiojua kusamehe. Anaamrisha watu

wamuache ajitose majini afe. Anampa Samueli kamba ajitie

kitanzi ikiwa anaogopa kujitosa majini. Samueli anasema kuwa

mamake ataelewa atakapojua kuwa Samueli amefeli mtihani.

Lakini babake aliyeumbwa na udongo tofauti hawezi.

 

Amewajibika

Aliweza kulipa karo yote ya shule.

 

 

 

100.

MWALIMU
MKUU Mwenye madharau

Samueli alipoingia katika osi yake,anachukuwa muda mrefu sana kuinua uso wake kumuangalia Samueli. Baada ya kuzichambua zile stakabadhi za matokeo, anatoa moja na kumtupia Samueli. Anamtupia kwa mtu anavyomtupia mbwa mfupa.

Amemakinika kazini

Hakuamini Samueli alipomwelezea kuwa amekamilisha kulipa karo, alitumia “daftari la karo” kuhakikisha. Anasema mali bila ya daftari hupotea bila ya habari. Ndio maana ameweka daftari la kuweka kumbukumbu ya wanaodaiwa karo na waliolipa karo.

 

 

MBINU
ZA
UANDISHI Tashbihi

Uk 131:waliokuwepo waliotoka wamenywea kama kuku walionoa maji ya mvua.

Uk 132:akitoka ndani atakuwa akitembea kama fahali.

Uk 131:amamtupia kama mbwa anavyomtupia mbwa mfupa. Uk 137:anamuona baba akilini kama hayawani.

Uk 135:imekwenda kama chendacho kwa mganga kisichokuwa na marejeo.

 

 

Tashhisi/uhaishaji/uhuishi(personication)

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai(sifa za kibinadamu).

Uk 134:Nzi wa kijani ya samawati waliokula wakashiba. Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unampokea kwa vigemo.

Uk 135: Safu sa ya D na E ilimkodolea macho bila kupesapesa. Uk 137:Ilimuradi mawazo yana mwadhibu sasa.

Uk 138:Alitupia jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na kuhangaika.

 

 

 

 

101.

Msemo

Uk 132:Uso wake wenye makunyanzi ulipiga mapeto.

Uk 133:Anakitazama kidole cha Mwalimu mkuu kupiga masafa.

Uk 135:Juhudi zake zimegonga ukuta.

Uk 137:Nina kuambulia patupu.

Uk 139:…huhu kila mtu akipigwa na kibuhuti.

 

Kichanganya ndimi

Kutumia zaidi ya lugha moja tofauti.

Uk 132:come on

:yes

 

 

Utohozi

Kuswahilisha maneno/kutamka maneno yasiyo ya Kiswahili kama

ya Kiswahili.

Uk 133: Bodi,operesheni.

 

 

Maswali balagha

Maswali yaliyoulizwa bila ya kutarajia majibu.

Uk 131: Mtu angesemaje ati? Wanafunzi na wakati huo huo

wanasononeka?

Uk 133: Nazo fedha ulitoa wapi mtoto pale ulipo.

Uk 135: Karo yote niliolipa iwe bure? Pesa aliyolipa baba tusome

imekwenda bure?

Uk 136: Ali umefeli mtihani ? sasa nitafanya nini?

 

 

Methali

uk 132:Mdharau biu hubiuka.

uk 132:Usione wembamba wa reli kwani gari moshi hupita juu

yake.

uk 135:Imekwenda kama kiendacho kwa mganga kisichokua na

marejeo.

uk 139: Mambo ni kuganga huenda yakaja.

 

 

 

 

 

102.

Uzungumzi nafsia

Mhusika hujizungumzia ama kwa kuongea au kuwaza bila kukusudia kusikika na yeyote.

Uk 132:mimi tangu hapo najijua bwana. Sina moyo wa bua. Mtihani haunibabaishi sana.

Uk 132:hajawai kuniamini huyo hambe. Lakini mimi mwenyewe najiamini. Lazima mtu ajiamini… au sio?

Uk 135: Hivyo ndivyo kusema lolote wala chochote . kwamba mimi si lolote wala chochote. Kwamba mimi si chochote wala lolote katika medani ya masomo?

 

Mdokezo/usemi usiokamilika

Uk 132:tena angaa sikukutana na paka mweusi njiani siku zote za mtihani…

Uk 133:…chukua matokeo…

Uk 135:si mjinga mimi. Najua vitu vingi tu… Uk 136: Mama ataelewa lakini baba…

 

Sadfa

Matukio mawili au zaidi yanayotokea kwa pamoja bila ya kupangwa.

Uk 135:Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitaka kujitosa majini ili afe, siku hiyo ilikua tofauti kwani wachunga wapitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni hawakuwepo. Ikawa rahisi kuweko kujitosa majini.

Uk 138: Inasadifu pia kuwa baada ya Samueli kujitosa majini na kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanamume mmoja akawa ameachwa na basin na akaamua kutumia njia karibu ya kamwokoa Samueli.

 

Taharuki

1.Kuna wanafunzi waliotoka osini mwa Mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka. Msomaji anabaki hata hamu ya kujua ikiwa walikuwa wamepita mtihani au la.

2.Msomaji pia angetaka kujua ikiwa Nina alimuacha Samueli kutokana na vituko vyake au la.

3.Msomaji anabaki na hamu ya kutaka kujua maisha ya Samueli yaliendelea vipi. Je alifaulu maishani. Baba alibadilika na kumsamehe .

4.Kuanguka mtihani wa elimu na kuanguka mtihani wa maisha?

 

 

103.

Maswali

1.Andika sifa za wahusika hawa kama zinavyojitokeza katika hadithi ya mtihani wa maisha.

i)Samueli ii)Babake Samueli iii)Mamake Samueli iv)Mwalimu Mkuu

Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Mtihani wa Maisha. Mwanamke amepuuzwa katika jamii. Hii inadhibitishwa na mtazamo wa baba kupitia elimu. Ingawa baba aliyaonea fahari mafanikio ya binti zake,aliwaona kama wanawake tu. Fahari yake ya dhati ilikua katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Samueli hakuamini vipi angeweza kushindwa katika mtihani na dada zake ilhali ni wanawake.

Mwanamke ni mpenda amani na mshauri mwema. Anamshauri mumewe aende shuleni wasuluhishe sintofahamu kuhusu karo

Pia ni mwenye utu.Anamshika Samueli mkono na kumwambia waende nyumbani. Anamwambia maneno ya kumpa tumaini.

 

13. MKUBWA

Na Ali Mwalimu Rashid

UFAAFU WA ANWANI MKUBWA

Neno mkubwa linatokana na kivumishi ‘–kubwa’ ambalo lina maana

ya kuzidi kwa umbo au kimo; -siyo ndogo. Pia neno hili lina maana ‘-

enye kwisha kukua’ au ‘kuwa juu’.

Anwani ‘Mkubwa’ inaaki kazi hii kwani yafuatayo ni mambo yaliyo

wazi zaidi;

 

F Msimulizi anatueleza kuhusu mhusika mkuu kazini aliyeitwa Mkubwa. Alikuwa anajihusisha na biashara ya kuuza pweza wa kukaanga. Hii ndiyo biashara iliyompa kipato na faraja.

 

F Mkubwa alipoingia uongozini alikuwa na madaraka makubwa.

Alikuwa na uwezo uliozidi. Viongozi walipapata pasipoti za kidiplomasia ziliwawezesha kutosachiwa bandarini wala kwenye uwanja wa ndege.

 

 

 

104.

F Uovu wa Mkubwa ulikuwa umezidi. Aliweza kumwingiza raki yake Mkumbukwa kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya. Mkumbukwa aliponaswa na kutiwa ndani kwa kupatikana na mkoba uliojaa dawa hizo alijuta mno. Majuto yake yalikuwa makubwa.

F Ushawishi wa Mkubwa ulikuwa umezidi. Aliweza kumtoa Mkumbukwa ndani baada ya siku tatu. Pia alipewa mzigo wake ukiwa katika hali ile ile.

F Baada ya Mkumbukwa kutolewa ndani , aliichukia sana biashara ya kuuza dawa. Aliapa na Mola kuwa hatofanya tena biashara hiyo tena.

F Mkubwa alipojilaza kwenye kochi na usingizi kumchukua anaota kuwa vijana wameongezeka mjini wanaosinzia ,wengine hali yao imedhooka sana na wizi umewazidi mitaani.

F Mshituko wa Mkubwa ulizidi alipoona kuwa watoto wake wa kiume walikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wameandikwa kwenye nyuso zao ‘mla unga’ jambo liliomfanya chizi.

 

DHAMIRA
YA
MWANDISHI

Mwandishi amelenga kupiga vita biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya au “kuuza unga”. Kupitia kwa Mhusika Mkubwa tunagundua kuwa viongozi ndio walanguzi wakuu wa dawa hizi. Viongozi wawa hawa huwatafuta vijana ambao huzipeleka dawa hizo kwa wateja. Wanaoumia zaidi ni vijana ambao wanaponaswa hutiwa ndani huku walanguzi halisi wakiufurahia uhuru wao nje.

 

WAHUSIKA

1. Mkubwa
– alikuwa muuzaji wa pweza wa kukaanga kabla

ya kuingia kwenye uongozi alikoingilia biashara haramu ya

kuuza dawa za kulevya. Ana sifa zifuatazo:

a) Mwenye bidii– alikuwa akishughulisha na kazi ya kuuza

pweza wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi

ili kuingia uongozini.

b) Mwenye utani– anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo

lililomfanya utingo kukimia kwa kuchekwa na abiria.

c) Ni mtambuzi- aliweza kuelewa maana ya unga japo

hakuwahi tu kuona vituko vyake.

 

 

 

105.

a) Mwenye utu– alimpigapiga kijana mbwia unga aliyekuwa ameinama kama kwamba anarukuu na kumuuliza iwapo anaumwa.

b) Mwenye tamaa ya mali– alipotanabahi namna viongozi wanavyotajirika kwa kuuza unga , maneno ‘unga na utajiri’ yalimkaa moyoni kiasi chake kukosa usingizi usiku huo.

c) Ni maskini– alikuwa akifanya biashara ya kuuza pweza iliyokuwa na kipato kidogo . vilevile kabla ya kupata uongozi, alikuwa na suruali na shati kipande papa

d) Ni sadi– baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya biashara ambayo huonekana kama ya kishetani. Vile vile alitoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea na ndipo akaupta ushindi.

e) Mwenye msimamo dhabiti– baada ya kuyatia moyoni maneno aliyopewa na kijana yule kuhusu utajiri na unga aliamua kutafuta kwa udi na uvumba na ndipo akamwendea rakiye kwa jina Mkumbukwa.

f) Ni msiri– mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake kuutafuta uongozi.

g) Mwenye wasiwasi- aliogopa kuwa huenda kisomo chake kingemzuia kupata uongozi.

 

 

2.
MKUMBUKWA

ni rakiye Mkubwa aliyejitwika jukumu la kuwarai watu ili wampigie Mkubwa kura.

a) Raki wa dhati– Mkumbwa alimwendea kwa mawaidha baada ya kuamua kuugombea uongozi na ndipo Mkumbukwa akamshauri Mkubwa augombee.

b) Mkakamavu – alimweleza Mkubwa bila kupepesa macho wala kugugumizi kuwa pesa na ukaragosi wa chama ndiyo mambo muhimu pale Mchafukoge yatayomwezesha

kuupata uongozi.

 

 

 

 

 

106.

c) Mwenye kutimiza ahadi– alimwambia Mkubwa kuwa akitafuta milioni kumi kisha ampe yeye ataupata uongozi na kuapa kuwa iwapo ataukosa amuue.

d) Ni mwenye bidii– baada ya Mkubwa kujaza fomu; alianza kazi ya kuingia /kupita nyumba baada ya nyumba kumtafutia kura mkubwa.

e) Mwenye busara– alifahamu ka kuwa ili kufanya kazi vyema ni lazima angemtafuta Bi Kibwebwe (Sada) na kumhusisha katika harakati za kumtafutia Mkubwa kura.

 

 

a) Mwenye majuto– aliponaswa na askari wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevya alijuta kimoyomoyo.

b) Mwenye kulalamika– alipotiwa ndani alikuwa akilalamika kupuuzwa kwa haki za mahabusu.

 

Zoezi

1. Fafanua sifa za wahusika hawa.

a) Sada

b) Vijana wabwia unga c) Askari

 

 

1) ATHARI
ZA
DAWA
ZA
KULEVYA

F Vijana wanaolangua dawa za kulevya(unga) huishi kwa

woga huishi kwa mfano yule kijana baada ya kumrushia

Mkubwa maneno aliogopa wenyewe wasije wakamwona.

F Vijana wabwia unga(wanaotumia dawa hizi) hugeuka

karakana za matusi. Km yule kijana mbwia unga alimuuliza Mkubwa kijeuri “kwani tunakula kwa babako? Vile vile kijana aliyekuwa kichochoroni alimwita Mkubwa juha.

 

 

MAUDHUI

Maudhui ni mengi yaliyomo katika kazi. Haya ni masuala

yanayoangaziwa na mwandishi wa kazi husika.

Mwandishi ameangazia maudhui yafuatayo;

 

 

 

107.

F Vijana wanaozitumia dawa hizi hugeuka na kuwa mazuzu- km kijana mwingine aliyekuwa kichochoroni alikuwa akitokwa na denda mdomoni huku amefumba macho.

F Vijana wabwia unga huota ndoto za kiajabu – kwa mfano kijana aliyekuwa kichochoroni alimkasirikia Mkubwa kwa kuwa aliikatiza ndoto yake na kumkatizia stimu. Analalamika kuwa Mkubwa aliiangusha ndege yake (katika ndoto) alipomshtua.

F Viongozi wanaojihusisha katika biashara hii haramu hugeuka matajiri na hatimaye kuliumiza taifa kama anavyorai kijana aliyeandamana na Mkubwa.

F Wabwia unga husinzia mchana. Hukauka midomo. Hujidunga mili yao ikawa kama jahazi la mtefu. Zaidi ya mno vijana hawa hujitoboa mishipa ya damu ikashabihiana na chungio.

F Vijana wanaojihusisha na biashara hii haramu huishia kwenye seli. Wanafungwa miaka mingi huku wakuu wao wakiyafurahia maisha yao nje.

 

1) UFISADI

Usadi ni uovu ambao umejitokeza katika hadithi kama

ifuatavyo;

F Pindi tu viongozi wanapopata pasipoti ya kidiplomasia wao

hujiingiza katika biashara haramu za kuuza dawa za

kulevya. Mkubwa aliweza kupita vizuizi vyote akiwa

ameubeba mkoba wenye dawa hizo na hakusachiwa.

F Mkubwa alipungiana mkono na wale askari ndani ya gari

pungiano hili lilikuwa na maana yake. Baadaye Mkubwa

alifanya mikakati na kumtoa Mkumbukwa ndani alikokuwa

amefungiwa. Bila shaka aliwahonga askari wamweke

Mkumbukwa huru.

F Vijana wanaopewa kazi ya kuviuza vidonge vile

wanapokamatwa hutiwa magerezani na kuwaacha viongozi

walanguzi wakiendeleza shughuli zao.

(mwanafunzi aongezee hoja ili kuonyesha namna usadi

unavyojitokeza)

 

 

 

108.

1) UONGOZI
MBAYA

Uongozi wa Mkubwa ulikuwa uingozi mbaya kwani;

FAlishiriki usadi- alitumia ushawishi wake kisiasa kumtoa

Mkumbukwa ndani na kuuokoa mzigo wake(dawa za kulevya)

FAlikuwa akiuza dawa za kulevya- sababu kuu ya Mkubwa

kujiingiza mamlakani ilikuwa ni utajiri na unga(dawa za kulevya). Alimwingiza Mkumbukwa kinaki kwenye biashara hii.

FViongozi hawasachiwi kwenye viwanja vya ndege na hivyo

basi kuwarahishia mipango ya kubeba dawa za kulevya. Idara yauchunguzi imefeli.

FIdara ya magereza haijukumiki kuwaweka ndani vigogo

wanaolangua dawa hizi. Wao huwaweka ndani vidagaa. (mwanafunzi aongezee hoja)

 

 

2) DHULUMA

Vijana mahabusu walio magerezani wanadhulumiwa kama

ifuatavyo:

F Wanalazwa chini kama magunia ya viazi mbatata.

F Wakiwa mle ndani kwenye vyumba vya mahabusu

wananyimwa chakula,hawakogi,hawafui nguo zao,

F Vijana hawa huhukumiwa kabla na kufungwa pasi

kupewa nafasi ya kujitetea

F Vijana hawa huteswa sana kwani hata chakula

wanachokileta jamaa zao huliwa na walinzi wa magereza.

F Viongozi huwauzia dawa vijana ambao huathirika si

haba. (tazama athari za dawa za kulevya)

ZOEZI

· Jadili maudhui yafuatayo kama yanavyojitokeza katika

hadithi ya Mkubwa. a) Ajira na kazi b) Tamaa

 

 

 

109.

FANI

Katika Fani tutashughulikia mbinu za uandishi pamoja na tamathali

za usemi.

 

1. Ndoto:

Mkubwa aliota alipojilaza kwenye kochi lake. Katika ndoto hii

mambo yafuatayo yalijitokeza;

F Vijana wanaotumia dawa wameathirika mno kwani

walikuwa wakisinzia tu.

F Baadhi ya vijana(wake kwa waume) wamekondeana

kana kwamba wanaugua ukimwi au kifua kikuu.

F Vijana hao walikuwa wac hafu na walikuwa

wakivitenda vitendo vichafu vya kihayawani.

F Watu wengi aliowaona hawakuwa na raha kwani wizi

ulikuwa umewazidi.

F Nyumba zote zilikuwa zimechanwa nyavu.

F Vijana aliowaona wote walikuwa wameandikwa

kwenye vipande vya nyuso zao “mla unga”

F Mkubwa aliwaona watoto wake wa kiume miongoni

mwa vijana hao.

 

2.
Tashbihi

Tashbihi zimetumiwa kwa mapana na mwandishi wa hadithi hii.

Mifano michache ya tashbihi ni kama

F Yule kijana alipita kama umweso…

F Majumba makubwa yamefumuka kamau yoga…

F … akipeleka pumzi juu kama mtu aliyepanda…

F …yalimkaa kama ngoma ya kimanga…

F Yalitembea kichwani kama damu itembeavyo mwilini…

F …alilidaka begi la Mkumbukwa kama mwewe anavyodaka

kuku…

F Alipita kama umeme…

F Mkubwa alikuwa amesimama kama mlingoti wa bendera…

F Lilikwama kooni kama mtu aliyekuwa anakula vigae…

 

 

 

110.

3.
Mbalagha

Maswali ambayo hayahitaji majibu moja kwa moja yametumiwa mara moja moja na mwandishi kama ifuatavyo;

F Kwani ulikuwa mwavuli?

F Wapi?

. Onomatopea
/tanakali

Mbinu hii imetumika kazini kama ifuatavyo.

FPopooooooo! Popooooooo! – kuashiria jinsi gari lilivyopiga

honi.

 

5. Utohozi

Mbinu ya kuyaswahilisha maneno ya lugha ya kigeni ili yatamkike na kuandikika kama yale ya Kiswahili.

FPasipoti – kutokana na ‘passport’ FKidiplomasia- kutokana na ‘diplomacy’ FHusachiwi- kutokana na ‘search’ FProfesa- kutokana na ‘professor’

FBegi- kutokana na ‘bag’ FKiboksi- kutokana na ‘box’ FPresha- kutokana na ‘pressure’

 

6.
Kuchanganya ndimi

Kuna mara kadha ambapo mwandishi amevichopeka vifungu vya lugha ya Kiingereza katika muktadha wa mazungumzo. Kwa mfano;

F Form four F Birthday F Brother

F Sober house

 

7.
Kinaya

Kinaya ni kinyume na matarajio. Mbinu hii imejitokeza kama ifuatavyo;

F Ni kinaya kuwa , ili kuwa kiongozi katika eneo la Mchafukoge huhitaji kuwa umesoma kwani cha muhimu ni pesa na kuwa mzalendo kwa chama chako(ukikatwa, damu yako inakuwa rangi ya chama)

 

 

111.

F Ni kinaya kuwawanafunzi wa Profesa walimpa kura

Mkubwa ambaye hakuwa na masomo.

F Ni kinaya kuwa walanguzi halisi wa dawa za kulevya huachwa huru( kama vile Mkubwa)na wanaofungwa ni vijana wanaowafanyia walanguzi hao kazi.

(mwanafunzi aongeze hoja)

 

8.
Takriri

Pia hujulikana ka uradidi. Lengo la kutumia mbinu hii huwa ni

kusisitiza ujumbe.

Mifano ya takriri ni kama ifuatayo;

F Halimezeki, halimezeki…uk 151

F Hapo hapo!…154

F Kifo,kifo,kifo…uk 150

F Unga!unga!…uk 142

 

 

9.
Istiara

Tofauti na tashbihi, istiara huwa haitumii maneno ya ulinganisho

kama ‘kama’. Mbinu hii imetumika kama ifuatavyo.

F Magereza kuna vitawi vitupu- vijana wanofungwa wameitwa vitawi

F …wao ni matela tu- vijana wanaowafanyia kazi vigogo

kama akina Mkumbukwa wanaitwa matela.

F …vichwa vya treni huachiwa…- viongozi (vichwa vya treni) huachwa nje wakiendelea na biashara zao haramu. (mwanafunzi aongezee hoja)

 

Zoezi

F Onyesha namna mbinu hizi zimejitokeza. a) Nidaa

b) Chuku

 

 

 

 

 

112.

Maswali
ya
kudurusu.

1. ” Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi,rudi

kwa Mola wako.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Fafanua sifa za msemewa.

c) Tambua tamathali ya usemi iliyotumika hapo juu.

d) Ni kwa nini msemewa anatakikana kurudi kwa Mola wake?

 

Majibu

a) Msemaji wa maneno hay ni Mkumbukwa. Anamweleza Mkubwa.

Walikuwa kwake Mkubwa.

b) Msemewa ni Mkubwa. Ana sifa hizi.

 

 

I. Mwenye bidii– alikuwa akishughulisha na kazi ya kuuza pweza wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi ili kuingia uongozini.

 

 

ii. Mwenye utani– anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo lililomfanya utingo kukimia kwa kuchekwa na abiria.

 

 

iii. Ni mtambuzi- aliweza kuelewa maana ya unga japo hakuwahi tu kuona vituko vyake.

 

 

iv. Mwenye utu– alimpigapiga kijana mbwia unga aliyekuwa ameinama kama kwamba anarukuu na kumuuliza iwapo anaumwa.

 

 

v. Mwenye tama ya mali– alipotanabahi namna viongozi wanavyotajirika kwa kuuza unga , maneno ‘unga na utajiri’ yalimkaa moyoni kiasi chake kukosa usingizi usiku huo.

 

 

I. Ni maskini– alikuwa akifanya biashara ya kuuza pweza iliyokuwa na kipato kidogo . vilevile kabla ya kupata uongozi, alikuwa na suruali na shati kipande papa

 

 

113.

ii. Ni sadi– baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya biashara ambayo huonekana kama ya kishetani. Vile vile alitoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea na ndipo akaupata ushindi.

 

 

iii. Mwenye msimamo dhabiti– baada ya kuyatia moyoni maneno aliyopewa na kijana Yule kuhusu utajiri na unga aliamua kutafuta kwa udi na uvumba na ndipo akamwendea rakiye kwa jina Mkumbukwa.

 

 

iv. Ni msiri– mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake kuutafuta uongozi.

 

 

v. Mwenye wasiwasi- aliogopa kuwa huenda kisomo chake kingemzuia kupata uongozi

c) Tashbihi– Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. d) Amevitenda vitendo vingi viovu kama vile

F kuuza dawa za kulevya.

F Kutoa hongo ili apate uongozi.

F Kumtapeli raki yake Mkumbukwa na kumuingiza katika uuzaji wa dawa za kulevya. Kutumia pasipoti ya kidiplomasia vibaya. nk

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

114.
Share this:


EcoleBooks | UCHAMBUZI/MWONGOZO WA RIWAYA YA TUMBO LISILOSHIBA (Maswali na majibu)

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*