Maswali ya Matumizi ya lugha
1. (a) Badilisha sentensi ifuatayo iwe mazoea kwa kutumia kirejeshi “O“
Mtoto anayelia huchapwa
(b) Andika kinyume
Wavulana watatu wanaingia darasani kwa haraka.
(c) Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii:-
Kule ndimo alipoingia
(d) Taja aina za vitenzi vilivyopigiwa mstari katika sentensi iuatayo
Mama amewahi
kupika jikoni
(e) Eleza maana ya misemo ifuatayo :-
(i) Giza la ukata…
(ii) Meza mate machungu
(f) Unda vitenzi kutokana na :-
(i) Mkufunzi
(ii) Maeneo
(g) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, taja aina za sentensi za kiswahili
(h) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale
Mwalimu huyu mzuri anafundisha darasani.
(i) Eleza maana mbili za sentensi :-
Mama alimlimia mwanawe shamba
(j) Akifisha sentensi ifuatayo:-
ah huu ndio upuuzi aliotuitia mmoja wao akaropoka.
(k) Tunga sentensi itakayodhihirisha matumizi ya kielezi cha namna mfanano
(l) Andika sentensi ifuatayo katika msemo halisi :-
Mshtakiwa alidai kwamba alikuwa ameonewa kwa kuwa hakuwa ameshiriki ulevi kutoka
mwaka uliokuwa umetangulia.
(m) Pambanua viungo vya kisarufi katika kitenzi kifuatacho
Tuliwalimia
(n) Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo:
Mizizi ya mibaruti hii iliwaponya watu ambao walikuwa na shida kama hii yenu (kanusha
kwa umoja)
(o) Tunga sentensi ukitumia neno “Vile” kama:
(i) Kiwakilishi
(ii) Kivumishi
(iii) Kielezi
(p) Bainisha matumizi viambishi “ku” na “Ji” katika sentensi zifuatazo:-
(i) Mwanafunzi hukusoma kwa bidii
(ii) Atakupiga
(iii) Amejikata
(iv) Mchezaji huyu ni hodari
(q) Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa huku ukikanusha
Kijibwa changu ni kikali sana
2. (a) Jaza mapengo:-
Kutenda Kutendesha
(i) Chota
(ii) Lewa
(b) Taja sauti moja ya;
(i) King’ong’o
(ii) Kiyeyusho
(c) Tumia neno “shujaa” katika sentensi kama:-
(i) Kivumishi
(ii) Kielezi…
(d) Tambua vitenzi katika sentensi hii kwa kuvipigia mistari:-
Sisi tulikwisha kutambua alikuwa na nia mbaya. Yeye ndiye mwizi .
(e) Andika wingi wa sentensi hii katika hali ya ukubwa:-
Kichinjio hiki kilikarabatiwa kwa pesa nyingi
(f) Eleza maana zinazojitokeza katika vifungu vifuatavyo:-
(i) Jambazi kutoka dukani liliiba.
(ii) Liliiba jambazi kutoka dukani.
(iii) Kutoka dukani jambazi liliiba.
(iv) Jambazi liliiba kutoka dukani.
(g) Jaza neno ambalo ni kinyume cha lile lililopigwa mstari katika sentensi:-
(i) Vile vitu ulivyovichanganya itakubidi
(ii) Bomba hili limeziba mwite fundi aweze
(h) Unganisha sentensi hii kwa kutumia ‘O’ rejeshi :-
Wavu umekatika. Wavu ni wao
(i) Eleza matumizi mawili ya “ka” na utunge sentensi kwa kila mojawapo
(j) Yakinisha sentensi hii:
Sijafahamu kwa nini hawamkaribishi mpwa wao.
(k) Andika katika usemi halisi:-
Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo
(l) Akifisha sentensi ifuatayo:-
Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi, utaniazima siku ngapi bashiri
alimwuliza rita
(m) Changnanua kwa njia ya mishale
Mama anapika na baba akisoma gazeti
(n) Tunga sentensi moja na uonyeshe kwa mstari
(i) Shamirisho kipozi
(ii) Shamirisho kitondo
(iii) Shamirisho ala/kitumizi
(o) Tungia vitenzi vifuatavyo sentensi katika hali zilizobanwa:-
(i) Fa(mazoea)
(ii) La(kutendeka)
(iii) Pa (kutendea)
(p) Tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru
Wanafunzi walifoanya vyema walituzwa jana
(q) Pambanua viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo
Waliwapendezea
3. a) Onyesha viwakilishi katika sentensi zifuatazo kisha ueleze ni vya aina gani:-
i) Unamjua vyema kweli?
(ii) Hicho wanachokitaka hakipo
(b) Tumia viunganishi vifuatavyo katika sentensi:-
(i) Minghairi ya
(ii) Wala
(c) Yakinisha sentensi ifuatayo:-
Chakula hakipikiki vizuri
(d) Jibu kulingana na maagizo kwenye mabano:-
(i) Hatujui ambako alitorokea (tumia ‘O’ rejeshi)
(ii) Angekuwa na pete, angekupatia (ibadilishe katika wingi kisha uikanishe)
(e) Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi ifuatayo:-
Maksuudi alimjengea Tamima Kasri kwa matofali mazuri
(f) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale/mistari:-
Watoto wote wameamka mapema na wazazi wanatayarisha staftahi
(g) Unda nomino moja moja kwa kila kitenzi
Shuku
Vumilia
shona
lia
(h) Eleza maana ya ‘jinsi’ kama inavyojitokeza katika sentensi zifuatazo
(i) Naomba unionyeshe jinsi ya kuendesha gari
(ii) Wakenya hawapendezwi na jinsi viongozi wanavyoendeleza ufisadi
(i) Bainisha aina za nomino zilizopigiwa mistari katika sentensi hii:-
Uhodari wa wanariadha wa Kenya unahitajika kote duniani
(j) Tunga sentensi ukitumia mzizi – choyo kama :-
(i) nomino
(ii) Kivumishi
(iii) Kiwakilishi
(k) Eleza matumizi mawili ya kila mojawapo wa alama za uakifishaji zifuatazo:-
(i) msitari
(ii) Parandesi
(l) Geuza zentensi zifuatazo katika kauli kwenye mabano:-
(i) Fundi ameharibu saa (kutendea)
(ii) Umemwona mgeni? (kutendewa)
(m) Andika kwa udogo:-
Gari la Mzee Maritu limegonga ng’ombe wa jirani wake
4. (a) Andika sifa bainifu za sauti
(i) e:-
(ii) n:- .
(b) Eleza maana ya :-
(i) Kiimbo:.
(ii) Shadda…
(c) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha ngeli zifuatazo:-
(i) U-U
(ii) Pokomo /Pa-ku-mu
(d) Unda kitenzi kimoja kutokana na nomino ‘Mtubia”
(c) Eleza matumizi mawili ya kiambishi ‘ku‘
(f) Tunga sentensi ya maneno manne ambayo ina sehemu zifuatazo. Kielezi cha namna,
kivumishi,kitenzi na jina (g) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi:-
Ng’ombe aliyeletwa juzi ameuzwa leo jioni.
(h) Onyesha matumizi mawili mawili ya alama zifuatazo:-
(a) Alama ya mshangao
(b) Mshazari
(i) Tunga sentensi sahihi ukitumia –wa– katika kauli ya kutendeana
(j) Andika udogo wa sentensi:-
Ndama wa ng’ombe yule ameuzwa.
(k) Onyesha tofauti ya vitate vifuatavyo kwakuvitungia sentensi
(i) Dhamani
(ii) Thamani
(l) Kanusha sentensi ifuatayo katika wingi
Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari
(m) Ainisha shamirisho /yambwa katika sentensi ifuatayo:-
Mchezaji alimpigia mwenzake mpira kwa mguu wa kushoto.
(n) Huku ukitumia mifano mwafaka, eleza tofauti ya sentensi sahili na ambatano
(o) Onyesha aina za viambishi katika sentensi hii:
Nitajisomea
(p) Andika katika usemi wa taarifa:-
Tutaanza mashindano kesho, Mwalimu alimwambia mwanafunzi.
(q) Eleza maana mbili ya sentensi:-
Tumetengeneza barabara
(e) Tumia mifano mwafaka kueleza aina za mofimu
5. a) Unda nomino za/lm,k, dhahania kutokana na maneno yafuatayo :-
i) Kwea .
ii) Himarisha …
b) Huku ukitoa mifano eleza miundo mitatu ya silabi za Kiswahili
c) Tunga sentensi ukitumia kinyume cha kitenzi: ‘umba’
d) Andika katika
Meza ii hii ndiyo aliyotumia kulia
e) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendewa
i) cha …
ii) nywa
f) Ainisha viambishi katika neno lifuatalo:
atakuajiri
g) Sisi tunajua sheria ingawa tu wafisadi
Anza: Japo………….
h) Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo:-
i) Wanafunzi wote wameingia darasani ii) Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani
i) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia njia ya matawi :-
Amekuja kuwatembelea manusura waliopata ajali ya ndege
j) Taja sifa mbalimbali za sauti zifuatazo:
/Z/
/K/
k) Huku ukitumia mifano ya sentensi eleza matumizi mawili ya kiambishi, ‘ji’ l) Andika udogo wa:
Magari yote yaliyobakia yatauzwa na mzee yule mwembamba
m) Sahihisha:
i) Kila mwanafunzi alipewa ndazi na mayai moja
ii) Nipee huo mkoba nitoemo vitabu zangu
n) Tumia – ‘ako’ katika sentensi kama:
i) Kivumishi
ii) Kiwakilishi
iii) Kitenzi
o) Bainisha aina mbili za vishazi katika sentensi hii :-
Shamba lile kubwa litauzwa kesho
p) Andika katika usemi wa taarifa :
“Karibu Rahma, tafadhali kaa,” Musa akasema . Ahsante, je, habari za hapa?’ Rahma aliuliza
q) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi tofauti ya neno: ‘somo’
6. (a) Taja sauti mbili ambazo hutamkwa nyuma ya ulimi kati ya hizi
/h/,/o/,/y/,/u/,/kh/,/g/,
(b) Ng’oa kisiki hiki haraka askari akaamrisha mahabusu
(Andika kwa msemo halisi)
(c) Badili sentensi zifuatazo katika kauli iliyoonyeshwa kwenye mabano
(i) Si vizuri mwanafunzi kumwibia mwenzake pesa (Kutendeana)
(ii) Mpishi aliharibu mchuzi huu kwa kuongeza chumvi nyingi. (tendeka)
(d) Bainisha matumizi ya “po” katika sentensi ifuatayo:-
Alipowasili alionyeshwa walipo.
(e) Andika kwa usemi wa taarifa:-
“Wasichana wakielimishwa wataweza kuwa bora kuliko wavulana,” Naibu wa Chansela
wa chuo Kikuu aliwaambia mahafala.
(f) Tunga sentensi ambayo ina aina za maneno uliyopewa:-
N + V + V + T
(g) Tumia ”O”
rejeshi ya kati
Lisemwalo silo liwalo
(h) ‘Msipokuwa wenye bidii hamtayapata mafanikio maishani.’ Yakinisha katika umoja
(i) Changanua kwa kutumia mishale
‘Mimi sikumwona wala Mwenda hakumwona’
(j) Tunga sentensi ukitumia maneno haya katika kinyume.:-
(a) afikiana
(b) sifu
(k) Unda nomino mbili mbili kutokana na vitenzi vifuatavyo:-
(i) abudu
(ii) fisidi
(l) Andika katika hali ya ukubwa
Mwanamke huyu amezaa watoto wanne.
(m) Bainisha matumizi ya maneno yaliyopigwa mstari
(i) Mbio hizi hazitakufikisha mbali
(ii) Mwambie Abedi asifanye
mbio kuhusu hiyo kazi.
(n) Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi
Msichana aliyeitwa alikuwa mkorofi
(o) Eleza dhana zinazowakilishwa na viambishi awali katika sentensi zifuatazo: –
(i) Aliitwa
(ii) Hakupata
(p) Tunga sentensi mbili kubainisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:-
(i) Kuna
(ii) guna
(q) Taja mianzo mitatu tofauti ya ngeli ya U-ZI
(r) Eleza maana ya semi hizi :
(i) Kunja jamvi
(ii) Piga kambi
7. (a) Andika sentensi ifuatayo bila kutumia “amba“:-
(i) Jitu ambalo linatusumbua sharti liadhibiwe vikali
(ii) Weka sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea:-
Mmea ambao unapandwa katika msimu wa masika unamea
(b) Badilisha sentensi hizi hadi usemi wa taarifa:-
(i) “Nitarudi tu ikiwa mtakubali kuomba msamaha”. Juma alisema
(ii) “Elezeni vile mlivyokuja hapa na namna mtakavyokwenda.” Mwalimu mkuu alisema
(c) Fuata maagizo uliyopewa baada ya kila sentensi ili kujibu maswali haya :
(i) Aliogopa kumwangalia simba aliyekula mzoga. (Tumia neno ‘Ogofya’ bila ya
kubadililsha ya sentensi:-)
(ii) Mti wa zambarau ni rahisi kukatwa ukiwa unatumia msumeno. (Anza
Ni rahisi…)
(d) Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii :-
Alimlilia mwanawe
(e) (i) Kanusha sentensi hii:-
Tungewalaki kama tungejua watakuja
(ii) Sahihisha sentensi ifuatayo na uiweke katika wingi:-
Ningalifanya kazi ningekuwa tajiri
(f) Tunga sentensi nne kuonyesha matumizi na maana nne za kijineno ‘ki‘
(g) Tumia kivumishi kilichoko kwenye mabano kukamilisha sentensi:-
(i) Bibi yule alinunua gari ________________________(-pya)
(ii) Mti (-ingine) _______________________uliangushwa badala ya ule wa kwanza.
(h) Unda majina mawili mawili kutoka vitenzi hivi na utumie katika sentensi ili
kubainisha maana
(i) Safiri (ii) Zaa
(i) Akifisha kifungu hiki:-
Yohana na Emanueli walifunga safari wakielekea mashariki kusini na hatimaye magharibi
walifikia huko novemba mwaka jana walipokuwa wakirudi walimkuta mwalimu
mkuu njiani ambaye alishtuka kuwaona pale
(j) Geuza sentensi hii hadi udogo:-
Nyoka yule mrefu alifukuzwa na watu wengi
(k) Andika upya sentensi hii kwa kuandika kinyume cha kila neno lilipigwa mstari:-
Wifi alipovaa nguo na kusimama ajuza yule alikaa
(l) Sauti hizi ni za aina gani na hutamkwa wapi?
(i) gh
(ii) j
(m) Mahabusu walifyeka uwanja vizuri
Andika sentensi hiyo upya ukimaliza kwa neno mahabusu
8. (a) Onyesha maneno yaliyokopwa toka lugha za kigeni na kuswahilishwa kwa kuyaongezea
irabu
k.m. Bint (Kiarabu) – Binti
Toa mifano minne
(b) Andika sentensi ifuatayo kwa usemi halisi:
Mwalimu alipoingia darasani aliuliza kitabu chake kilipokuwa.
(c) Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi nafsi huru umoja
(d) Kanusha sentensi hizi kwa wingi:-
(i) Mtoto huenda shuleni kila siku
(ii) Mwalimu amemfunza mwanafunzi vizuri
(e) Eleza maana mbili ya sentensi ifuatayo
Wanafunzi waliandikiana barua
(f) Ziandike sentensi hizi bila maneno yaliyopigiwa mstari:-
(i) Mwanafunzi ambaye alituzwa ni wa shule yetu
(ii) Sikuziona nyuzi ambazo huzitengeneza ngoma ambayo huiona pale
(g) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vielelezo vya vishale:
Kiarie ni mwanafunzi mtiifu
(h) Bainisha ngeli za nomino hizi :-
(i) Kisu
(ii) Nyavu
(iii) Chai
(i) Ainisha viambishi katika neno lifuatalo :-
Kilichokikata
(j) Nyambua kitenzi ‘oa’ katika hali tatu zifuatazo: tendewa, tendwa, tendea
(k) Eleza matumizi manne ya nukta
(l) Onyesha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi ifuatayo:
Kamau alimlimia mamake shamba kwa trekta
(m) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi:-
(i) Chapa (ii) Goma
(n) Tambua kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi hii :-
Chakula ambacho ni muhimu, huweza kujenga au kobomoa mwili wako.
(o) Sahihisha sentensi ifuatayo:
Ukienda mle pao atakuweko
(p) Andika sentensi ifuatayo katika udogo:
Mbwa mdogo amekanyagwa na gari.
9. (a) Andika katika usemi halisi
Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo
(b) Andika kwa umoja
Uovu waliotuonyesha hautasahaulika
(c) Tunga sentensi moja moja kuonyesha tofauti kati ya vitate vifuatavyo:
(i) Pamba
(ii) Bamba
(d) Sauti zifuatazo hutamkiwa wapi?
(i) /f/
(ii) /v/
(e) Onyesha matumizi manne ya kistari kifupi
(f) Tunga sentensi ya neno moja yenye mofimu zifuatazo
(i) Nafsi ya tatu umoja
(ii) Wakati uliopita
(iii) ‘O’ rejeshi
(iv) kitendwa
(v) mzizi
(vi) kiishio
(g) Tambulisha aina za vitenzi vilivyotumika katika asentensi hizi
(i) Kazi hii ni nzuri.
(ii) Mazingira yamekuwa yakihifadhiwa.
(h) Pigia mistari chini ya viwakilishi katika sentensi zifuatazo
(i) Ambaye ni mjinga hatafaa kwa shughuli hizi
(ii) Nani anaye huzunisha?
(i) Ngeli ya LI-YA hujumulisha nomino za vitu vya aina mbalimbali. Toa mifano minne
ambayo ni tofauti na uelezee
(j) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo na ueleze ni shamirisho ya aina gani?
Wazazi wanalipia watoto karo kwa hundi;
(k) Neno ‘tikiti’ hupatikana katika ngeli mbili tofauti. Taja ngeli hizo na utunge sentensi
(l) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale.
Hakimu alimwadhibu kinyama.
(m) Nyambua vitenzi hivi kulingna na kauli ya kutendua na kutenda
Kutenda | Kutendua | Kutendama |
Ficha | ||
Tanda |
(n) Ni nini maana ya neno kirai ?
10 . (a) Kati ya nomino za Kiswahili taja ngeli mbili ambazo nomino zake hazibadiliki katika umoja
na katika wingi. Kisha utoe mfano mmoja kwa kila ngeli (b) Yakinisha: Waumini wale hawaimbi wala hawaombi
c) Andika kwa umoja
Nguo zile uzionazo zilinunuliwa Ulaya
(d) Taja na kutolea mifano aina nne za silabi za Kiswahili (e) Unda nomino moja kutokana na nomino hizi
(i) Mtu. (ii) Mhasibu..
(f) Andika kwa ukubwa
Kipaka hiki hakitosheki kwa maziwa haya kimezoea kipanya
(g) Onyesha shamirisho kipozi na shamirisho kidondo katika sentensi hii:-
Mama amempikia moto chakula kizuri
(h) Tunga sentensi ya neno moja inayoonyesha sehemu zifuatazo:-
(i) Kiambishi kikanushi nafsi
(ii) Kiambishi kiwakilishi cha hali timilifu
(iii) Kiambishi kiwakilishi cha kitendwa (nafsi)
(iv) Kauli
(v) Kiishio
(i) Sahihisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti
Mtoto mwenye alicheza ameteguka
(j) Andika visawe vya maneno haya


(i) Rabsha….. (ii) Damu..
(k) Jaza mchoro ufuatao kwa irabu inayofaa


(l) Tunga sentensi ukitumia ‘ni’ kama
(i) kitenzi (ii) kielezi
(m) Andika katika msemo halisi
Johana alisema kuwa angepata alama zote katika majaribu ya wiki iliyotangulia
(n) Tumia ‘O’ Rejeshi ya mazoea katika sentensi ifuatayo;
Jembe ambalo lilinunuliwa limepotea (o) Changanua ukitumia mtindo wa mishale
Mtoto anayelia sana ameadhibiwa leo asubuhi (p) Onyesha matumizi mawili katika sentensi ya alama (‘) (q) Wafuatao wana ulemavu upi?
(i) Toinyo . (ii) Huntha ..
11. (a) Andika vinyume vya vitensi vilivyopigwa mistari
(i) Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya
(ii) Kuimba kulifurahisha hadhira
(b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi
(i) Abiria waliojeruhiwa sana walipelekwa hospitali haraka
(c)Eleza maana mbilimbili za sentensi zifuatazo
(i) Bibi yake amefika
(ii) Alimpigia mpira
(d) Kwa kutoa mifano, onyesha namna mbili vile kiambishi –j- hutumiwa
(e) irabu a, i, na u hutamkwa wapi kwenye ulimi?
(f) Kamilisha na kueleza maana ya methali hii
(i) Mfinyanzi -…………………………………
(g) Andika usemi huu kwa usemi wa taarifa
“Kefule! Mtoto huyu ni kaidi kama kirongwe. Hamheshimu babake!” alisema mzee Kamau.
(h) Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentenzi ifuatayo
(i) Darasa lililojengwa limefunguliwa rasmi
(ii) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo;
(j) Kanusha sentensi ifuatayo kwa udogo
(i)Mbuzi wake ana manyoya mengi na harufu kali
(k) Onyesha maana mbili ya neno taka (ala. 2)
(l) Andika kwa umoja (ala. 2)
(i) Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru
(m) Eleza maana ya misemo:- (ala. 2)
(i) Fuga mtu –
(ii) Kuwa na faragha –
(n) Panga nomino hizi katika ngeli mwafaka (ala 2)
(i) Kipofu- .
(ii) Uyoga- .
(o) Bainisha viwakilishi katika sentenzi kisha useme ni vya aina gain. (alama
i) Mimi nitaondoka kesho
(ii) Huyo alichaguliwa na wengi
12. (a) Tumia kiulizi kifaacho kukamilisha maswali yafuatayo:
(i) Waashi wale wanaishi kwa
(ii) Mtoto alitaka majina…
(iii) Wanitania hivyo
(b) Tambua mzizi katika neno:
Tuliwalimia :
(c) Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii
Pale ndiko alimoingia
(d) (i) Nini maana ya yambwa (shamirisho)
(ii) Taja aina ya yambua iliyoipigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:
Mama amempikia baba wali kwa sufuria
(e) Neno “mlango” lina maana ya “uwazi wa kuingilia nyumba.” Tunga sentensi mbili
kubainisha matumizi mawili ya neno hili
(f) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya “ndivyo”
(g) Chai hiyo iliwavutia watahi (Anza : Watahi…………..) (al. 2)
(h) Tumia neno “haraka” katika sentensi kama: (al. 2)
(i) Nomino (ii) Kielezi
(i) Andika maana mbili za sentensi:
(i) Nenda ukamwone mwenyewe, usiogope.
(j) Onyesha maana za ‘ni‘ zilizopigiwa mstari
Nihamrishe “Tokeni darasani”
(k) Atakapokuja atamletea mlinzi uta na upote
(l) Maneno hayo yako katika ngeli gani?
(i) Ridhaa (ii) Nanasi
(m)Andika mifano ya sauti zenye sifa zifuatazo:
(i) Kipasuo cha kaakaa laini (ii) Nazali ya ufizi
(n) Tumia neno “ngali” kutunga sentensi kuonyesha
(i) Kitenzi kisaidizi (ii) Kitenzi kishirikishi
(o) Tumia kirejeshi kuonyesha mazoea katika sentensi ifuatayo:
(i) Mtoto anayelia ni huyu (ii) Neno maana ya kiwakilishi?
(q) Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo na ueleze ni vya aina gani?
1.Nani alikukasirisha?… 2. Huyu huwashinda wote
(r) Tunga sentensi moja itakayodhihirisha matumizi ya kielezi cha namna mfanano
13. (a) Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi
(i) Kishirikishi kipungufu
(ii) Kikuu
(b) Akifisha
je, unaipenda hali ilivyo mwenzake alitaka kujua
(c) Eleza matumizi ya ‘ka‘ na ‘hu’ katika sentensi zifuatazo.
(i) Nilienda kanisani nikamkuta, nikamwamkua, nikamwomba msamaha.
(ii) Baba hufika nyumbani usiku wa manane
(d) Yakinisha sentensi ifuatayo :
Mama hakutuchapa, hakutupa chakula wala maji
(e) Tofautisha kati ya sauti ghuna na sauti si ghuna huku ukitolea mifano miwili kwa kila aina
(f) Tunga sentensi mbili kutofautisha matumizi ya vitate hivi: Dua na tua
(g) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo wingi
Njia nyembamba ni hatari kwa usafiri wa gari
(h) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia matawi
Mzee ambaye hukuza pamba amefaidika sana
(i) Ainisha mofimu zinazojitokeza katika kitenzi hiki
Waliochekeshwa
(j) Andika sentensi zifuatazo kulingana na kauli ulizopewa katika mabano
(i) Ugonjwa wa saratani hufanya watu wafe polepole. (kauli ya kutendesha)
(ii) Mkulima alisuka kamba ndefu. (Kauli ya kutendata)
(k) Tunga sentensi moja inayojumulisha sehemu hizi, Ala, kipozi, kitondo na chagizo
(l) Neno kijana linaweza kutumiwa kama kivumishi au nomino, tunga sentensi kudhihirisha*U
(i) Kivumishi
(ii) Nomino
(m) Sahihisha sentensi zifuatazo
(i) Mtoto ambaye aliyekuwa anacheza ameanguka.
(ii) Vitabu hizi ambazo zimesahihishwa ni za wanafunzi.
(n) Tunga sentensi mbili ukitumia vielezi vya namna mfanano na viigizi.
(o) Bainisha maneno yafuatayo yapo katika ngeli gani kisha tunga sentensi mwafaka:
(i) Manukato (ii) Uwati
(p) Eleza maana ya methali ifuatayo:
“Avunjaye nazi ni lazima aafaidi tui.
14. A) Eleza maana mbili za:
Mwanaida alikwenda sokoni peke yake.
B) Akifisha sentensi hizi.
i) Hodi hapana wenyewe nini Juma alimwaka nitarudi kesho.
C) Andika maana ya methali ifuatayo.
Achanikaye kwenye mpini hafi na njaa.
D) Tumia “O” rejeshi katika sentensi hii.
Mwanafunzi ambaye hudurusu ndiye hupita mtihani.
E) Andika sentensi ifuatayo kwa kunyambua maneno yaliyo kwenye mabano kwa usahihi.
Dhambi za mwanadamu zilim____________ (fa) Bwana Yesu.
F) Eleza maana ya misemo ifuatayo.
i) Teka bakunja.
G) Taja maana ya maneno yaliyopigwa mistari.
Tulipogawa mkate kila mtu alipata sehemu moja kwa nane tu kwani tulikuwa wanane
- Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maelezo.
i) Sikusoma kwa bidii ndiposa sikufaulu katika mtihani ule.
(Anza: Ningalisoma …………………………………………)
ii) Anakuja (andika katika wakati ujao hali timilifu)
I) Eleza maana ya neno chungu kama lilivyotumiwa katika sentensi zifuatazo.
i) Chungu yule ni mkubwa.
ii) Chungu kile ni kikubwa.
J) Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo kama vivumishi.
i) Sote. i) Zote.
K) Andika nomino mbili kutokana na kitenzi safari.
- Tumia viunganishi mwafaka kuunganisha sentensi hizi ziwe sentensi moja.
Alikimbia kwa nguvu zake zote. Alishindwa, kulikuwa na mtu mwenye mbio kumliko.
- Eleza maana ya matumizi ya “ka” katika sentensi ifuatayo.
Aliingia ndani, akaoga, akala kisha akalala.
N) Taja sauti mbili za ving’ong’o
O) Andika kinyume cha sentensi ifuatayo.
Juma ameinjika chungu mekoni.
P) Andika sentensi ifuatayo katika wingi wa udogo.
Mtu/ mchoyo hamfai mwingine kwa vyovyote vile.
Q) Kanusha sentensi hii;-
Ukionana naye mwambie aje anione.
R) Eleza na udhibitishe kwa mfano, matumizi mawili ya tu.
S) Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu.
Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa
T) Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo
Soroveya atapima wanunuzi viwanja.
U) Nomino zifuatazo ni za ngeli gani? i) Insi … ii) Soksi
Majibu ya Matumizi ya lugha
1.
- Mtoto aliaye huchapwa
- Wavulana watatu wanatoka darasani pole pole (hakuna kinyume cha nomino)
- i)Kule ndiko alikoingia
ii) Pale ndipo alipoingia
iii) mle ndimo alimoingia
- amewahi- kitenzi kisaidizi
Kupika
e) i) hali ya umaskini mkubwa
ii) Vumilia shida/ taabu
f) i) Funza
ii) Enea
g) i)Sentensi sahihi- mfano; mama anapika jikoni (kitenzi kimoja)
ii)Sentensi ambatano- mfano mama anapika jikoni na baba anasoma gazeti
iii) Sentensi changamano – mfano mwanafunzi aliyechelewa aliadhibiwa
(vishazi viwili) tegemezi na huru)
h) S____ KN+KT
KN_____N+ V+V
V_________Huyu
V_________ Mzuri
KT________ T+E
T_________ Anafundisha
E__________ Darasani
i) i Mama alifanya kwa niaba ya mwanawe
ii) Mama alilima shamba ili mwana afaidike
j) “Ah huu ndio upuzi aliotuitia?” mmoja akaropoka
k) Anakula kifisi
Kitausi
Kinyama nk
l) “Mimi nimeonewa kwa kuwa sijashiriki ulevi kutoka mwaka jana”.
Mshtakiwa alijitetea
m) TU- Nafsi ya kwanza uwingi (watendaji)
LI- Wakati uliopita
WA- Nafsi ya tatu uwingi (Watendewa)
LIM- Mzizi wa kitenzi
I- kauli ya kutendewa
a-Kiishio/ kimalizio
n) Mzizi wa mbaruti huu haukumponya mtu ambaye alikuwa na shida kama hii yako
o) i) vile vitauzwa
ii) Vitu vile vitauzwa
iii) Viti huuzwa vile meza huuzwa
p)
- KU- kiambishi kanushi cha wakati uliopita
- KU- kurejesha nafsi ya pili umoja
- JI- binafsi yenye mwenyewe
- JI – uzoefu wa kutenda jambo
q) jibwa langu si kali sana
2. (a) (i) Chota – chovya (al.1)
(ii) Lewa – levya (al. 1)
(b) (i) King’ong’o – m, n, ny, ng’ (yoyore 1×1 =al.1)
(ii) Kiyeyusho – y,w (yoyote 1×1=al.1)
(c) Kwa mfano:-
Kivumishi : Askari shujaa ametuzwa (1×1= al. 1)
Kielezi: Askari yule alipigana kishujaa (1×1=al. 1)
(Hakiki jibu la mwanafunzi)
(d) Vitenzi – tulkwisha, kutambua, alikuwa ndiye (hoja 4 x ½ = al. 2)
(e) Ma(ji) chinjio haya ualikarabatiwa kwa ma(ji) pesa mengi (al. 2)
(f) (i) Jambazi lililoiba linaishi dukkani (al. 1)
(ii) Jambazi linaloishi dukani ndilo liliiba (al.1)
(iii) Jambazi liliiba punde tu baada ya kutoka dukani (al.1)
(iv) Jambazi liliiba vitu kutoka kwenye duka (al. 1)
(g) (i) Uvichanganue (al. 1)
(ii) Kulizibua (al. 1)
(h) Wavu uliookatika ni wao (al. 1)
(i) –(i) Lengo /nia k.m. Nipe pesa nikanunue kitabu
– (ii) Kitendo cha pili (matokeo ya kitendo cha kwana k.m. Alianguka akaumia.
(k) “Harakisheni mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo” mama alisema
Mama alisema “Harakisheni mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo”.
(l) “Sijaona kitabu kizuri kama “Mayai waziri wa Maradhi,” Utaniazima siku ngapi?” Bashiri
alimwuliza Rita.
(m) Mama anapika na baba akisoma gazeti. (al. 4)
S S1 + U + S2 S1 KN + KT KN N N Mama KT T T anapika U na | S2 KN + KT KN N N baba KT T+N T akisoma N gazeti |
(n) Hakiki jibu la mwanafunzi.
k.m. Ziada alimfagilia mama nyumba kwa ufagio
Nyumba – kipozi, mama-kitondo- ufagio – ala/kitumizi
(o) (i) Fa (mazoea) k.m. watu hufa kwa maradhi mbalimbali
(ii) La(kutendeka) k.m. Chakula hiki hulika upesi.
(iii) Pa(kutendea ) k.m Alinipea mtoto maziwa nilipochelewa kazini (kwa niaba yangu )
(p) – Wanafunzi waliofanya vyema – kishazi tegemezi
– Walituzwa jana- kishazi huru(al. 2)
(q) wa – nafsi
li – wakati
wa – nafsi (mtendewa)
pend – mzizi .shina
eze- kauli/kinyambuzi
a – kiishio 6x ½ = 3)
3. a) i) U- nafsi tegemezi
ii) hicho- Kiwakilishi kionyeshi
kutaja alama ½ maelezo alama ½
b) i) Sentensi iwe na maana bila ya, pasipo, ghairi ya n.k Mfano wanafunzi walisafiri
mighairi ya shida
ii) Wala – sentensi ileta maana ya kulinganisha na kupinga. Mfano sitaenda kazini wala
kuhudhuria mkutano
c) Chakula kinapikika vizuri
d) i) Hatujui alikotorokea
ii) Wangekuwa na pete, wangewapatia
Wasingekuwa na pete wasingewapatia
e) Tamina- Shamirisho kitondo
Kasri- Shamirisho kipozi
Kwa matofali- shamirisho ala/ kitunzi
f) S______S1+U+S2
S1_____KN1=KT1
KN1____ N1+V
N1_____Watoto
V______Wote
KT1____T+E
T_______Wameamka
E_______Mapema
U_______na
S2______KN2+KT2
KN2____N2
N2_____Wazazi
KT2_____T2
T2______Wanatayarisha
KN3____N3
N3_____Staftahi
g) Shuku- mshukukiwa/ kushuku/ ushukiwa
vumilia- uvumilivy/ mvumilivu/ kuvumilia
Shona- Mshono/ mshoni/ mshonaji/ ushonaji/ kushona
Lia- mlio/ kilio/ kulia
h) i) jinsi- Imetumika kuonyesha jinsi ya kutekeleza jambo
ii) Jinsi- Imetumiwa kuonyesha mwenendo
i) Uhodari- nomino dhaharia
Wanariadha- nomino ya kawaida
Kenya- nomino ya pekee
j) i) Choyo kama nomino
Mfano Uchoyo wa kocho ni wa kupita kiasi
ii) kama kivumishi
Mfano Mtoto mchoyo hapendwi na wenzake
iii) Kama kiwakilishi
Mfano Mchoyo aliyeninyima chakula ameshikwa na polisi
k) i) Mstari ________
Hutumika a) kutilia neon au fungu la maneno msisitizo
Mfano Ukienda dukani uninunulie daftari la hesabu
b) Kuonyesha anwani ya vitabu, vichwa vya habari au majina ya machapisho
kama Mjarida
Mfano Tamthilia ya kifo kisimani imesifika
ii) Parandesi [ ]
a) Kufungia maneno yatoayo maelezo zaidi kuhusu maneno yanayotangulia
Mfano Alipoenda katika maabara [chumba cha sayansi] hakufuata maagizo ya
mwalimu
b) kubainisha nambari au herufi katika orodha
Mfano [a] [b] [c]
c) kutoa maelezo na maelekezo kwa waigizaji katika mchezo wa kuigiza
Mfano Bokono: [Akiashiria kwa kidole] tukutane pale kwa haraka!
l) i) Fundi ameharibu saa
ii) umeonewa mgeni?
m) Kigari cha mzee Maritu kimekigonga kigombe cha jirani wake
4. Matumizi ya lugha
a) i) e – Irabu ya mbele – hutamkwa kutumia sehemu ya mbele ya ulimi
– Irabu ya midomo – hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa
ii) n – sauti ya ufizi
– Nazali
b) i) Kiimbo – Ni upandaji na ushukaji wa sauti unaofanyika wakati mtu anapozungumza
Shadda – Ni mkazo katika nenoau maneno
c) i) U – U – Nomino za dhaharia zitumiwe
ii) Pokomo/ Pakumu k.m Mahali humu ndimo alimoingia
d) Tubu
e) – Kudhihirisha vitenzi vya silabi moja – kula, kuja n.k
- Mwanzo wa vitenzi
- Wakati wa ukanusho k.m haku, hatuku……
- Kuonyesha mahali k.m kuliko na miti
- Kiwakilishi cha nafsi k.m anakuita
f) Mfano: Msichana yule anasoma barabara
g) Ng’ombe aliyeletwa juzi ameuzwa leo jioni
h) a) Mshangao
- Kuonyesha hisia
- Kuamrisha
- Kutahadharisha/ kuonya
b) Mshazari
- Katika uandishi wa kumbu 2
- Kuonyesha maneno Fulani yana maana sawa
- Kuonyesha ‘au’
i) Mfano: majirani waliwiana radhi baada ya utesi wa siku nyingi
j) Kijdama cha kijigombe kile kimeuzwa
k) i) Dhamani – mwezi wa mwisho wa kusi (demani)
ii) Thamani – Gharama / ubora wa kitu/ bei
l) Tusingalikuwa na pesa tuingalinunua magari
m) Mchezaji – kipozi
mwenzake – kitondo
kwa mguu- ala
n) Sahihi – sentensi ya wazo moja/ kitenzi kimoja
Ambatani – sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa
o) Ni- e- tamati
ta- awali a – ji-
p) Mwalimu alimwambia mwanafunzi kuwa wangeaza masshindano kesho yake/ siku
itakayofuata
q) – Njia
– Vizuri/ mwafaka/ sawasawa
r) Mofimu huru
Mofimu tegemezi
5. a) (i) Mkwezi, ukweaji, mkweaji
(ii) Uhimarishaji, kuimarisha
b) (i) Muundo wa irabu pekee; mfano, a, e, i , o, u
(ii) Muundo wa konsonanti na irabu, mfano; pa, ma, to
(iii) Muundo wa konsonanti, konsonanti na irabu, mfano; kwa, cho, twa
(c) Mungu ndiye aliye na uwezo wa kuumba na kuumbua
(d) Meza zizi hizi ndizo zilizotumiwa kulia
(e) (i) chiwa
(ii) nywewa
(f) a nafsi ½
Ta wakati ½
Ku mtendwa ½
– Ajiri kiini/mzizi ½
(g Japo tu wafisaidi tunajua sheria.
h) (i) darasani – kielezi cha mahali
(ii) kisabuni – namna mfanano
j) /z/ hutamkiwa kwa ufizi
– ni sauti ghuna
/k/ – hutamkiwa kwa kaakaa gumu
– ni sauti hafifu
(k) – kuonyesha ukubwa
– Jia la kuingia ikulu limefungwa
– Kiambishi cha kurejelea mtenda
– Rehema anajitahidi sana.
(l) Vigaari vyote vilivyobakia vitauzwa na kizee kile chembamba (vitahiniwa 7-2;vitahiniwa
m) (i) Kila mwanafunzi alipewa andazi a yai moja.
(ii) Nipe huo mkoba nitoe ndani vitabu vyangu.
(n) (i) Darasa lako ni safi.
(ii) Chako kinapendeza sana.
(iii) Watoto wako uwanjani
(o) Shamba lile kubwa – kishazi tegemezi
– Litauzwa kesho – kishazi huru.
(p) Musa alimkaribisha Rahma na kumsihi akae.
– Rahma alishukuru na kumuuliza habari za pale
q) Somo la kiswahili lilikamilika vizuri
– Rita ni somo yangu kwa sababu tunaitwa jina moja.
6. (A) O na U
(B) Ngoa kisiki hiki haraka!”Askari akaamrisha mahabusu.
(C) (i)Si vizuri wanafunzi kuibiana pesa.
(ii)Mchuzi huu uliharibika kwa kuongezwa chumvi vyingi.
PO-ya pili-mahali
(E) Naibu wa Chansela chuo kikuu aliwaambia mahafala kuwa wasichana wakichumishwa
wangeweza kuiwa zaidi masomoni kuliko wavulana.
(F) Mtoto wetu mdogo amepotea. (Mwalimu akadirie) .
(G) Linalosemwa silo linalokuwa.
(H) Ukiwa mwenye bidii utayapata mafanikio maishani
(I) S S1+U+S 2 S2 KN+K
S1KN+KT KNN
KNW N Mwenda
WMIMI KTT
KTT THakumwona
T sikumwona
U wala
(J) (i)Hitilafiana /kosana/pigana
(ii)Kashifu (Mwalimu akadirie
(K) Ibaada
Maabadi
Ufisadi
Mfisadi
(L) Janajike hili limezaa matoto manne.
(M) (i)Mbio –Nomino
(ii)Mbio-Kielezi
(N) Msichana aliyeitwa – tegemezi
alikuwa mkorofi-huru
(O) A-nafsi
(i)Aliitwa (ii)Ha-Kikanushi
A-nafasi Ku-Nafsi ya tatu
Li-Wakati Wakati uliopita kikanushi
(P)(i)Kuna- kukwaruza kutumia kitu chenye meno mf-Kukuna nazi. Dhana ya-Kuwa na kitu
Guna-Kukataa
mf-Mwanafunzi aliguna alipotaka kuchapwa
(Q) Huanza na U halafu hudondoa u
mf Uzi-Nyuzi
U-Mb
Wa-Nya nk (alama 3)
(R) (i) Kuhama
(ii)Kukaa mahali
7. (a) (i) Jitu linalotusumbua sharti liadhiwe vikali
(ii) Mmea upendwao/ambao hupandwa katika msimu wa masika humea
(b) (i) Juma alisema ya kuwa /kuwa/ ya kwamba / kwamba angerudi tu ikiwa/ kama
wangekubali kuomba msamaha
(ii) Mwalimu Mkuu aliwataka /aliwaambia waeleze vile Walivyoenda hapo na
namna wangeenda watakavyoenda
(c) (i) Simba aliyekula mzoga alimuogofya kwa hivyo hakumwangalia
(ii) Ni rahisi kukata mti wa zambarau ikiwa unatumia musumeno
(d) (i) Alilia kwa sababu ya mwanawe
(ii) Alimnyenyekea mwanawe ili ampe msaada
(e) (i) Hatungewalaki kama hatungejua hawaji
(ii) Tungalifanya kazi tungalikuwa matajiri au Tungefanya kazi tungekuwa tajiri
(f) – ki ya masharti
– ki ya udogo
– ki ya lugha kwa mfano kikamba
– ki ya ngeli ya ki-vi
– ki ya jinsi / namna kwa mfano tembea kijeshi n.k
(g) (i) Jipya
(ii) Mwingine
(h) (i) Safari/msafara/usafiri
(ii) Mzazi/mzaliwa/uzazi
(i) Yohana na Emanueli walifunga safari wakielekea Mashariki, kusini na hatimaye
MagharibiWalifika huko Novemba mwaka jana . Walipokuwa wakirudi, walimkuta
Mwalimu mkuu njiani ambaye alishtuka kuwaona pale.
(j) Kijoka kile kirefu kilifukuzwa na vijitu vingi
(k) (i) Alipovua
(ii) Alisimama
(l) (i) gh – Kikwamizo /kaakaa laini
(ii) j – kikwamuzo /kaakaa gumu
(m) Uwanja ulifyekwa vizuri na mahabusu
8. (a) (i) Kiosk (Kiingereza) – Kioski
(ii) Hundir (Kihindi) – hundi
(iii) Lakh (Kihindi) – Laki
(iv) Shukran (Kiarabu) – Shukurani
(v) Shirt (Kiingereza) – Shati
(vi) Rushn (Kiajemi) – roshani
(vii) Kod (Kiajemi) – Kodi
(viii) Duvin (Kifaransa) – divai
(ix) Court (Kiingereza ) – Korti zozote 4 x ½ = al. 2)
(b) “Kitabu changu kipo wapi?”Mwaimu laiuliza alipoingia darasani ( ½X 4 (vitahiniwa)
(c) (i) Mimi
(ii) Wewe
(iii) Yeye
Mtahini ahakiki sentensi za watahiniwa sentensi (tuza al. 1)
Viwakilishi tuza al. 1)
(d) (i) Watoto hawaendi shuleni kila siku
(ii) Walimu hawajafunza wanafunzi vizuri (2×1=al. 2)
(e) (i) Kila mmoja aliandika kwa niaba ya mwenzake
(ii) Kila mwanafunzi alimpelekea mwenzake barua (2×1=al.2)
(f) (i) Mwanfunzi aliyetuzwa ni wa shule yetu
(ii) Sikuziona nyuzi zitengenezwazo ngoma tuzionazo pale (2×1=al.2 )
(g) Sentensi sahili
S – KN +KT
KN – N
N – Kiarie
KT – t + KN
t – ni
KN – N + V
N – mwanfunzi
V – Mtiifu
(h) (i) Kisu – Ki-Vi
(ii) nyavu – U-Zi
(iii) Chai –I-I
(i) KI – Kiambishii awali kiwakilishi nomino (nafsi)
LI – Kiambishi awali – wakati
CHO – Kiambishi awali kirejeshi
KI – Kiambishi awali –kitendwa
KAT – Mzizi
A – Kiishio
(j) (i) Olewa
(ii) Ozwa
(iii) Olea
(k) – Kukamilisha sentensi
– Kuandika vifupi
– Kuonyesha tarehe
– Kuonyesha desmali
(l) (i) Shamirisho kipozi – Shamba
(ii) Shamirisho ktiondo – mamake
(iii) Shamirisho ala – kwa trakta
(m) (i) Cahapa – uchapishajiii, machapishi, mchapishaji, kichapo, kuchapa
(ii) Goma – mgomo, migomo, mgomaji, ugomaji, kugoma
(n) (i) Kishazi huru – Chakula huweza kujenga au kubomoa
(ii) Kishazi tegemezi – ambacho ni muhimu
(o) (i) Ukienda mle mwao atakuwemo
(ii) Ukienda pale pao atakuwepo
(iii) Ukienda kule kwao atakuweko
(p) Kijibwa kidogo kimekanyagwa na kigari
9. a) “Mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo,” mama alihimiza
b) Uovu aliotuonyesha hautasahaulika
c) i) Mkulima alipanda Pamba shambani ( Mmea)
Au
Msichana yule alijipamba vizuri (kujipodoa)
ii) Jambazi yule alimbamba askari (Kamata kwa nguvu)
Au
Gari lake liliharibiwa bamba (Sehemu ya gari)
d) – Mdomo/ meno
– Mdomo/ meno
e) i) Kuonyesha neno linaendelea katika mstari wa pili k.m tulikwenda uwanjani
kuji – onea mchezo wa kandanda
ii) Kuonyesha silabi za maneno k.m ba – ba
iii) Kutenganisha maneno ambatano k.m elimu – viumbe, isimu – jamii
iv ) Kuonyesha kipindi cha muda Fulani 1950 – 1960, 1970 – 1983
v) kuonyesha aina za maneno yaliyoandikwa kwa vitengo; kwa mfano:-
– Nyanya amepanda ndizi za aina ya mkono – wa – tembo!
vi) Kudumisha sauti k.m masala – a – a – le!
f) Aliyepiga
g) i) ni – kitenzi kishirikishi kikamilifu 1
ii) yamekuwa – kitenzi kisaidizi 1
– yakihifadhiwa – kitenzi kikuu 1
h) Ambaye – kiwakilishi kirejeshi 1
nani- kiwakilishi kiulizi 1
i) Kuonyesha ukubwa wa nomino
Jitu limekufa
Majitu yamekufa
ii) Kuonyesha nomino ambazo hazina umoja na wingu
Tikiti lililonunuliwa
Tikiti yaliyonununliwa
iii) Kuonyesha vitu visivyo na uhai
Jiko lilivunjika
Meko yalivunjika
iv) Kuonyesha vitu dhahaima
Shetani lilifukuzwa
Mashetani yalofukuzwa
j) – Karo – SH kipozi
– Watoto – SH kitondo
– Kwa hundi – SH Ala/ kitumizi
k) I – ZI – Tikiti ienunuliwa
Tikiti zimenunuliwa
Li – ya – Tikiti lilinunuliwa
Tikiti yalinunuliwa
l)
S KN + KT 1
KN N 1
N Hakimu 1
KT T + E 1
T alimwadhibu 1
E kinyama 1 (al 4)
m)
Kutenda Ficha Tanda | Kutendua Fichua 1 Tandua 1 | Kutendama Fichama 1 Tandama 1 |
n) Kivai – Ni tungo ambalo huundwa kwa maneno aghalabu mawili na huwekwa pamoja
kuwasilisha kitu kimoja (al 1)
10. (j) Rabsha – fujo, ghasia
Damu- ngeu
(k)
(l) Kijani ni mrefu
Nendeni shambani
(m) Johana alisema; Nitapata alama zote katika majaribu wa jana
(n) Jembe linunuliwalo hupotea
(o)
S | ||||
KN | KJ | |||
N | J | T | E | E |
Mtoto | anayelia sana | ameadhibiwa | leo | asubuhi |
(p) Kibainishi (‘)
Fupisha neno ‘taondoka
Ving’ong’o ng’ombe
Kuonyesha tarakimu iliyodondolewa ’95
Hakikisha majibu ya mwanafunzi
(q) Toinyo- mtu aliyekatwa sikio moja
Huntha – mtu aliye na sehemu mbili za siri
11. (a) (i) Alisifiwa
(ii) Kuliridhi
(b) Abiria waliojeruhiwa sana walipelekwa hospitali haraka
(c) (i) – Nyanya yake amewasili
– Mke wake amewasili
(ii) – Alimrudi kwa sababu ya mpira
– Alimpiga kwa kutumia mpira
(d) – Kuonyesha hali ya ukubwa, mfano; jitu, jisu, jiji n.k.
– Ikiwa mwishoni mwa kitensi jina ili kuunda nomino yenye maana ya kazi ya mazoea.
Kwa mfano; msemaji, mwimbaji, mchoraji n.k.
– Kama kiambishi cha kuonyesha dharau au kudumisha mfano jivulana, jisichana, n.k.
– Kiambishi rejeshi kinachotambulisha kama mtendaji amejifanyia kitendo yeye mwenyewe au
anajionyesha kuwa mtu wa tabia au matendo fulani .
mfano; – Mavitu alijitia kitanzi
– Amejiwekea akiba ya kutosha n.k
(e) a – Karibu na kati, chini ya ulimi
i – Juu mbele ya ulimi
u – Juu nyuma ya ulimi
f) (i) – Mfinyanzi hulia gaeni
Kigae- Kipande cha kitu
Mfinyanzi – Mtu anayetengeneza vyungu
-Ina maana kuwa mtu anaweza kutengeneza kitu kama chungu na badala ya kufaidika na maarifa yake kwa kutumia kile chungu hubakia kutumia kitu cha hali duni (kigae). Ni wengine ndio wanafaidika na maarifa yake
(g) Mzee Kamau alishangaaa na kusema kuwa mtoto huyo alikuwa mkaidi kama kirongwe hasa kwa
kutoheshimu babake.
(h) – Kishazi huru – Limefunguliwa rasmi
– Kishazi tegemezi darasa lililojengwa
(i) – Shamirisho kitondo – watoto
– Shamirisho kipozi – karo
– Shamirisho ala – kua hundi
(j) Kibuzi/kijibuzi chake hakina vijinyoya/vinyoya vingi wala kiharufu/kijiharufu kikali
(k) – Kuhitaji
– Uchafu
– Kuwa na nia ya kufanya jambo fulani
(l) Nimekuondolea tatizo lako yafaa unishukuru
m. (i) Nyima mtu uhuru unaohitajika
(ii) Kuwa na siri
n) (i) A – WA
(ii) U – U
(O) (i) Mimi – cha nafsi
(ii) Huyo – kiwakilishi kiashiria
12. a) i) nani?
ii) Yapi?
iii) Mbona?
b) LIM 1
c) i) Pale ndipo alipoingia1
ii) Kule ndiko alikoingia 1
iii) Mle ndimo alimoingia 1
d) i) Ni nomino inayopokea athari ya kitenzi 2
ii) Wali – shamirisho kipozi 1
Baba – shamirisho kitondo 1
Kwa sufuria – shamirisho ala 1
e) i) Ukoo/ nasaha – hawa ni watu wa mlango/ wa samba
ii) Kifungu katika Biblia – Kitabu cha Yohana mlango wa 3 mstari wa 4
f) i) Hivi ndivyo alivyofanya kazi (kielelezi cha namna) 1
ii) Viatu hivyo ndivyo tulivyonunua (kisisitizi) 1
g) Watalii walivutiwa na chai hiyo
h) i) Haraka zake zilimwumiza 1
- Tembea haraka ili usichelewe 1
i) (i) Yeye mwenyewe aende asitumie mtu mwingine 1
(ii) Mtu anayemiliki ktu atembelewe
j) NI – nafsi ya kwanza umoja1
– uwingi wa wahusika1
– undani wa mahala 1
k) Watakapokuja watawaletea walinzi nyuta na pole
l) (i) I – ZI 1
(ii) LI – YA
m)- k/g 1
-N 1
n) (i) Mama angali anapika jikoni (kitenzi kisaidizi)
(ii) Mama angali ji koni (kitenzi kishirikishi)
o) Mtoto aliaye ni huyu
p)- Nani- kiwakilishi kiulizi 1
– Huyu – kiwakilishi kionyeshi 1
13. a) (i) Sisi tu wanafunzi
(ni, ki, u, zi, li, yu, ndisi, ndimi)
(ii) Mwalimu alikuwa anafundisha .
(Tathmini jibu ya mwanafunzi)
(b) “Je, unaipenda hali ilivyo ?’ Mwenzake alitaka kujua . alama za mtajo ½
Kuanza kwa herufi kubwa ½ (Je)
kama ½
Alama ya kiulizi ½
Mwenzake kuanza kwa herufi kubwa ½
Kituo mwishoni mwa sentensi (.) ½
(c) Ka – Inaonyesha mfululizo/mfuatano wa matukio/vitendo
hu – Kuonyesha hali ya mazoea
(d) Mama alituchapa, akatupa chakula na maji.
(e) – Ghuna – zinasababisha mtetemeko wa nyuzi za sauti;
/b,/d/,/v/, /z/, /g/, /gh/ /l/,/r/, /m/, /n/, /ng/, /ny/, /w/, /dh/.
– Si ghuna – Hazisababishi mtetemeko wa nyuzi za sauti; /h/, /th/, /ch/, /tag/, /p/, /f/, /s/, /k/, /sh/
maana
mifano miwili kila aina
(f) Dua – maombi – Marehemu aliombewa dua na kasisi
Tua-shusha – Ndege ilitua kiwanjani abiria wakashuka
(g) Vijia vyembamba ni hatari kwa usafiri wa vigari
(h)
(i) Wa – Mofimu ya nafsi (tatu wingi) /ngeli (A-WA)
Li – Mofimu ya wakati (uliopita)
O- Mofimu ya ‘O’ rejeshi
Chek- mofimu ya mzizi/shina la kitenzi
eshw – mofimu ya kauli /mnyambuliko
a = kiishio (mofimu)
(j) – Ugonjwa wa saratani hufisha watu polepole
– Mkulima alisokota kamba ndefu
(k) Ongancha alimjengea babake nyumba kwa matofali mazuri sana
babake – kitondo
nyumba – kipozi
kwa matofali – ala
sana – chagizo
Kitondo- mtendewa/kitendewa
Kipozi – kilichotendwa
Ala – kilichotumika kitenda
Chagizo – Kielezi, jinsi kilivyotendwa
(l) Mchezaji kijana alifunga bao- kivumishi
Kijana yule alifunga bao – Nomino
(Tathimini majibu ya mwanafunzi)
(m) – Mtoto ambaye alikuwa anacheza ameanguka au
– Mtoto aliyekuwa anacheza ameanguka
– Vitabu hivi ambavyo vimesahihishwa ni vya wanafunzi
(n) – Msichana yule alitembea kitausi – kielezi namna mfanano
– Mbwa alibweka bwe! – kilezi nmana kiigizi (1×1=al.1)
(Tathmini majibu ya mwanafunzi)
(o) Manukato – YA-YA: Manukato – manukato
– Manukato yananukia
– Manukato yananukia
uwati – U-Zi: Uwati – mbati
- Uwati uliotumiwa kujenga nyumba umevunjika
- – Mbati zilizotumiwa kujenga nyumba zimevunjika
(p) Tui ni maji meupe yanayopatikana katika nazi iliyokunwa
– Mtu anayevunja nazi lazima afaidi tui lake
– Yeyote anayeifanya kazi ngumu lazima afaidi matunda ya kazi yake.
– Anayehusika na shughuki yoyote yenye tija atafaidika (jibu lolote moja al. 1)
14. A) Mwandishi hakuwa na mtu mwingine yeyote alipoenda sokoni. (al. 2)
Mwandishi hakwenda mahali pengine ila sokoni.
B) “Hodi! Hapana wenyewe nini?” Jinani alimaka. Nitarudi kesho. (al. 4)
D) Mwanafunzi adurusuye ndiye apitaye mtihani. (al. 1)
E) Dhambi za mwandamu zilifisha Bwana Yesu. (al.1)
F) Kumchukulia kuwa mjinga (kumdhalilisha/dudisha mtu) (al. 1)
G) Thumni. (al. 1)
H) i) Ningalisoma kwa bidii ningalifaulu katika mtihani ule .
ii) Atakuwa amekuja.
I) i) Chungu – Mdudu
ii) Chungu – Chombo cha kupikia.
J) i) Sisi sote tuna soma (Nafsi ya kwanza wingi)
ii) Kuni zote zimewaka moto ya ‘U-zi’ wingi.
K) Msafiri – safari
Kwafiri – msafara usafiri.
L) Alikimbia kwa nguvu zake zote lakini (ijapokuwa, ingawa) alishindwa kwa
vile/madhali/ kwa sababu kulikuwa na mwenye mbio kumliko.
M) Kutokesakwa vitendo mtawalia (Kimoja mara tu baada ya kingine)
N) M n ny ng’
O) Ameepua/ Amedeua/Ametegua chungu mekoni.
P) Vijitu vichoyo havifai kwa vyovyote vile. (al. 2)
Q) Ukionana naye mwambie asije kuniona. (al. 2)
R) i) Kama kiambishi kiwakilishi cha nafsi yakwanza wingi (sisi). (al. 1)
Tutasafiri kesho kutwa)
ii) Kuonyesha kuwa hakuna ziada ya kilichotajwa. (Mkutano ulihudhuriwa na wanachama
watano tu). (al. 1)
S)
KN | KJ | ||
N | S | T | E (CH) |
Mwanafunzi | Aliyeleta kitabu | amepongezwa | sana |
T) Wanunuzi viwanja (al.2)
SH Kitondo SH Kipozi
U) i) a-wa
ii) i-zi

