Maswali ya Fasihi Simulizi
1. Soma kisha ujibu maswali
Lala mtoto lala x2
Mama atakuja lala
Alienda sokoni lala
Aje na ndizi lala
Ndizi ya mtoto lala
Na maziwa ya mtoto lala
Andazi lako akirudi
Pia nyama ya kifupa
Kifupa, kwangu, wewe kinofu
Kipenzi mwana lala x2
Titi laja x2
Basi kipenzi lala
Baba atakuja lala
Aje na mkate lala
Mkate wa mtoto lala
Tanona ja ndovu lala
Maswali
(a) Huku ukithibitisha jibu lako eleza huu ni wimbo wa aina gani?
(b) Eleza sifa za wimbo wa aina hii
(c) Onyesha umuhimu wa wimbo huu
(d) Eleza amali kuhusu jamii zinazojitokeza katika wimbo huu
(e) Tambua mbinu zozote mbili za utunzi zilizotumika katika wimbo huu
(f) Taja vitendo viwili vinavyoambatana na uimbaji wa aina hii ya wimbo
(g) Wimbo huu una wahusika wangapi? Wataje
2. Soma hadithi hii halafu ujibu maswali ulivyoulizwa
Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.
Maswali
(a) (i) Hadithi hii huitwaje?
(ii) Toa sababu zako
(b) Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii
(c) Kinyonga ni mhusika wa aina gani?
(d) Hadithi hii ina umuhimu gani?
(e) Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi
(f) Tambulisha vipera hivi:-
(i) Kula hepi
(ii) Sema yako ni ya kuazima
(iii) Baba wa Taifa
3. (a) Fafanua sifa tatu za ushairi simulizi
(b) Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake
(c) Ainisha mambo yanayobainisha muundo wa nyimbo
(d) Jadili muundo wa kitendawili
(e) Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:-
(i) Ujana ni moshi ukienda haurudi
(ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta
(f) Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho
kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii
4. Soma wimbo/shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata
MUITALIA ANAZWE
Saa kumi alfajiri
Sote tuliamshwa
Safari tuliianza
Lazima tuimalize
Maji ukiyavulia nguo
Lazima uyaoge
Wazee kwa vijana waliimba
Muitalia lazima anazwe
Mashamba yao walilia
Uui! Jikaze wavulana
Hawataki rangi hii
Wengi wanauliza
Mwitalia alikuja lini? Na ataondoka lini?
Mnaze huyu mlowezi
Hatuchoki
Hatuchoki
Lazima yeye anazwe
Vifaranga na mbuzi
Mbavu zao zahesabika
Meee! Sauti zilihinikiza kote
Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia
Nguvu kweli tunayo
Simama mbele tunayo
Simama mbele uone !
Muitalia ondoka !
Au nikuondoe kwa nguvu
Maswali
(a) Taja madhila yaliyosababishwa na Muitalia katika makala haya.
(b) Thibitisha kuwa utungo huu ni wimbo.
(c) Eleza maana inayojitokeza katika mistari ifuatayo:-
(i) Mbavu zao zahesabika.
(ii) Haya yote hakika, ni madhilia ya Muitalia.
(d) Huu ni wimbo wa aina gain? Eleza ukitoa ushahidi
(e) Eleza kwa sentensi mbili au tatu shughuli muhimu za kiuchumi za watu wanaimba
wimbo huu
(f) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika wimbo huu. Toa ushahidi
(g) Taja mafunzo mawili yanayotokana na wimbo huu
5. (a) Eleza maana ya miviga kisha uonyeshe inakotumika
(b) Eleza sifa za miviga
(c) Onyesha umuhimu wa miviga
6. Ni nini maana ya wimbo ?
Ni nini maana ya nyimbo zifuatazo.
Tenzi
Kongozi
Sifo
Wawe
Tendi
(a) Eleza umuhimu wa nyimbo
(b) Eleza sifa za wimbo wa aina ya Bembelezi
7. (a) Nini maana ya khurafa/kharafa?
(b) Fafanua sifa tano za kharafa
(c) Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi
8. (a) (i) Ngomezi ni nini katika fasihi simulizi?
(ii) Eleza sifa zozote mbili za ngomezi
(b) Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi:
(i) Hekaya
Hurafa
(ii) Visakale
Visasili
(iii) Ngano za mtanziko
Ngano za mazimwi
(c) (i) Vitendawili ni nini?
(ii) Fafanua kwa mifano, mbinu zozote nne za lugha zinazopatikana katika vitendawili
(d) Soma kifungu hiki cha wimbo kisha ujibu maswali yafuatayo :
Kuumeni : (Waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake. Chikicha x2
Kukeni : (Wimbo wao kwa sauti tofauti)
Tausi waendaa x2
Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda
Kuumeni : (Wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba
Kukeni : Mama ataota nini x2
Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni
Kuumeni : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi, wa magunzi.
Twamchukua , kisura wetu, kisura wetu, kisura wetu.
Tausi ni wetu, sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.
Maswali
(i) Wimbo huu ni wa aina gani na unastahili katika hafla gani ?
(ii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu
9. Soma kifungu kifuatacho kisah ujibu maswali yafuatayo :
(vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3)
Kuumeni : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2
Kukeni : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2
Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda.
Kuumeni : (wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba.
Kukeni : Mama ataota nini x2.
Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni.
Kuumeni : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi wa magunzi. Twamchukua, kisura wetu,
kisura wetu, kisura wetu.
Tausi ni wetu sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.
(a) (i) Wimbo huu ni wa aina gani, na unastahili katika hafla gani ?
(ii) Bainisha wahusika Kuumeni na Kukeni
(iii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu
(iv) Wimgo huu una umuhim;u gain hafia ulioimbiwa?
(v) Tambua mtindo uliotumika katika utungo huu
(b) Taja na ujadili aina nyingine sita za nyimbo
10. a) Taja sifa za tanzu zifuatazo za fasihi simulizi
i) Hurafa
ii) Mighairi
iii) Miviga
b) Eleza umuhimu wa ngomezi katika jamii
c) Eleza umuhimu wa mafumbo
d) Eleza tofauti kati ya malumbano ya utani na mawaidha
11. (a) Huku ukizingatia sifa za kimuundo za methali, jadili matumizi ya tamathali za usemi
sifuatazo:-
(i) Istiari/sitiari
(ii) Tashihisi
(iii) tashbihi
(b) Vitanza ndimi vina dhima gani katika jamii?
(c) Taja majukumu matatu ya nyimbo katika fasihi simulizi
(d) Eleza sifa tatu za ngano za mtanziko
(f) Eleza sifa tatu za Nyiso
(e) Fasihi simulizi ina sifa ya kuhifadhiwa akilini. Eleza udhaifu wa uhifadhi wa akilini (al. 4)
12. (i) Eleza maana ya vitanza ndimi.
(ii) Taja na ufafanue umuhimu wa vitanza ndimi katika jamii .
Majibu ya Fasihi simulizi
1. Uongozi wa kusahihisha 102/3 (Fasihi)
a) Bembelezi (lal mtoto). Wimbo unambembeleza motto alalye alama 2
b) Sifa za wimbo
- Huimbwa na walezi wa motto
- Huimbiwa watoto wachanga
- Huimbwa kwa sauti nyororo
- Huonyesha hisia za mlezi
- Maneno hurudiwa rudiwa
- Mdundo na taratibu
- Vifungu vifupi vifupi hutumiwa
- Huambatana na kumpapasa papasa motto kwa upole
- Huhusisha watoto wazazi
- Humpatia motto matumaini ya kumwona motto
c) Umuhimu wa wimbo huu
- Hufunza utamaduni
- Hufunza lugha ya ulezi/ mama
- Huliwaza motto mama akiwa mbali
- Hubembeleza motto alale
- Hufunza kuhusu amali ya jamii k.m chakula n.k.
- Mlezi hutoa malalamiko yake
- Hufunza motto mahusiano ya watu
d) Amali za jamii zinazojitokeza
- Vyakula k.v nyama, mkate, ndizi n.k
- Biashara, sokoni
- Ukulima wa ngano (mkate), mgomba (ndizi) Zozote 2×1=2
e) Mbinu zilizotumika
- Kiashiri
- Takriri
- ufafanuzi-1
f) Vitendo ambatano
- Kupapasa motto
- Mlezi hutembea tembea
- Tikisa motto
- Beba motto mgongoni/ begani/ kifuani
g) Wahusika
- Wawili
- Mtoto wa mlezi
2. . a) i)Kisasili
ii) Inaeleza jinsi kifo kilivyoingia duniani
– Asili ya kifo alama 2
b) Sifa za ngano
- Mwanzo maalum (fomula) hapo zamani za……..
- Wahusika wanyama mfano mjusi na kinyonga
- Wanyama kuwasilisha tabia na hisia za binadamu mfano kuongea, kujibizana n.k.
- Tanakali za sauti m.f pu! Zozote 3×1=3
c) Kinyonga ni
- Mvivu/ mzembe/mlegevu
- Si mzingativu- anachelewesha ujunmbe
- Mtiifu- mwishowe alifikisha ujumbe zozote 3×1=3
d) Umuhimu wa hadithi
- Kuelezea asili ya binadamu
- Asili ya kifo
- Huipa jamii melekeo
- Hukumbusha jamii
- Huburudisha/ huliwaza
- Ni historian a utamaduni wa jamii
- Huonya/ huadhibu zozote 4×1=4
e) Njia za kusanya fasihi simulizi
- Mahojiano yaliyopangwa na mtafuti na wahojiwa wake
- Kutumia vinasa sauti
- Kutumia video
- Kwa kuandika data au kazi husika zozote 4×1=4
f) Tambulisha vipera
- Kula hepi- msimu(kuwa na haraka)
- Sema yako ni ya kuazima- msemo (mtu asiringe)
- Baba wa taifa – lajabu (kiongozi wan chi)
3 a) – Huiwasilishwa kwa njia ya mdomo.
- Huhitahi uwepo hadhira
- Huweza kubadilishwa kulingana na hadhira/mahitaji
- Huandama na matendo
- Unaweza kuamba tanishwa na (3X1) ala. 3
b) – Wawe: nyimbo za kilimo (ala. 1)
Kimai: Nyimbo zinazohusiana na shughuli za uvuvi (ala. 1)
Faida:
Kuhimiza bidii.
Shukura kwa mavuno.
Beza uzembe.
Kuchapua utendakazi. ( zozote 2×1 ala. 2)
c) – Huwa na Mdundo| Mahadhi.
-Hupangwa kibeti.
-Hutumia lugha ya mkato.
-Matumizi mengi ya istiari. (zozote 3×1 ala 3.)
d) – Huwa ni fumbo|swali
-Humuia lugha iliyojaa sitiari.
-Ina fomula ya uwasilishaji.
-Huhusisha makundi mawili| watu wawili. (zozote 3×1 ala 3.)
e) i) Istiari
i) Jazanda |Nasiha (ala.1)
f) Matatizo
Watu wanaendelea kuhamia mijini
Dini zinakashifu baadhi ya tamaduni.
Wazee waliohifadhi kumbukumbu hizi wanaendelea knadimika.
Mapendekezo (3×1) ala.3
- Kuborehs zaidi mashidnano katika tamasha za muziki za shule.
- Kuhifadhi kwenye kanda
- Tuwe na makazazi inayoshughul;ikia tamaduni ( 3X1) ala. 3
4. (a)Madhila ya Muitalia (al. 4) “.
– Yeye aliwanyang’anya mashamba wenyeji”.
– Walikuwa wabaguzi wa rangi
– Mwafrika alidunishwa
– Mlowezi alikuja mika mingi na amekataa kuondoka katika nchi ya mwafrika”.
– Mifugo ya wenyeji inateseka kwa njaa na imekonda mno. Vifaranga, mbuzi n.k”.
(b) Sifa za wimbo “.
– Urari katika vina haupo
– Mizani katika mishororo haina urari
– Mishororo katika kila ubeti haijagawanywa kwa ukwapi na utao
– Katika ubeti wa pili wanasema wazee kwa vijana waliimba
(c) Maana ya vifungu (al.4)
(i) Mbavu zao zahesabika
– Mifugo wamekonda mno
– Wamekosa malisho (al. 2)
(ii) – Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia.
– Haya ni mateso/masaibu/matatizo yanayotokana na mlowezi Muitalai “.
(d) – Aina ya wimbo (al.2)
– Wimbo wa ukombozi/uzalendo
– Wenyeji wanaimba na kuonyesha cheche za kutaka kujikomboa kutokana na dhuluma
madhila ya walowezi (Waitalia) (kutaja al.1, maelezo al. 1= al.2
(e) Shughuli za kiuchumi (al.2)
(i) Ni wakulima wa mifugo
- Hufuga kuku na mbuzi
(ii) Ni wakulima wa mimea
– Mashamba ambayo wako nayo wanayatumia kwa kilimo cha mimea mbalimbal 2×1=al.2)
(f) Mbinu za lugha (al.2)
(i) Methali- Maji ukiyavulia nguo, ni lazima uyaoge
(ii) Tanakali ya sauti/uidaa/siyahi
Meee !
uui !
Maswali ya balagha /mubalagha
Muitalia alikuja lini ?
Na ataondoka lini ?
- Takriri – Hatuchoki
(g) Mafunzo katika wimbo
-Mkoloni/ mlowezi, muitalia alipokuja vbarani Afrika aliwakandamiza waafrika kwa mengi
– Umoja wa mwafrika ndio uilioweza kumwondolea dhuluma dhidi ya wanyanyasaji
– Dhuluma in mwanzo na mwisho wake
(viii) Majengo yasiyozingatia viwango vya usalama;
- Bweni la wanafunzi lilikuwa limekomelewa kwa nje
- Madirisha ya bweni yalikuwa yamewambwa kwa vyuma/nyaya kwa madai ya usalama wa wanafunzi
- Shule na hasa bweni kukosa vifaa vya kupambana na moto”.
5. a) Maana ya mivigo na inakotumika
Mivigo ni sherehe au/ bada zinazofuata utaratibu Fulani wa kisanaa za maonyesho ya fasihi simulizi Al. 1
Inakotumiwa
- Katika matanga miviga hutumiwa kuliwaza waliofiwa
- Katika jando na unyago, makunguni, maghariba na manyakanga hutumia miviga kufunza wavi, nasaha na mazingira yao
- Katika mavuno miviga hutumiwa kutoa shukrani
- Baada ya vita – hutumiwa kuongoa na kuwatolea shukrani mashujaa waliotoka vitani
- Motto anapozaliwa au kupewa jina, miviga ya kumkaribisha ilifanywa
- Wakati wa arusi
- Matambiko ya kutakasa n.k. k.m. aliyemuua mtu
- Kutawaza kwa viongozi
b) Sifa za Miviga
Hulenga kundi maalum katika jamii
Hutoa mawaidha
Hukusanya wanaotoa mawaidha na wanaotolewa hayo mawaidha
Hutokea kwa misimu
Kila tukio (jambo) huwa na mivigo yake
Hutumia pesa katika
c) Onyesha umuhimu wa Miviga
Hudumisha mila na utamaduni wa jamii
Huwawezesha vijana kuwa na kumbukumbu za kila sherehe ilivyofanywa, wakati na maana yake
Huelimisha vijana
Hutahadharisha kuhusu maovu
Huwezesha vijana kuelewa au kufahamu desturi zake
Huleta umoja na ushirikiano katika jamii
Huburudisha
Hufundisha unyumba na malezi
Uhimiza bidii ya kufanya kazi na kujitegemea
Huleta maendeleo
6. (a) Ni tungo zilizoundwa kwa mpangilio wa maneno au sauti zilizoteuliwa na msani na zenye
utaratibu za kimuziki zinazopanda na kushuka (al. 2)
(b) (i)Tenzi – nyimbo za kutoa mawaidha
(ii) Kongozi – ziliimbwa wakati wa kuaga mwaka
(iii) Sifu – zinaotoa sifa kwa wahusika kutokana na umaarufu
(iv) Wawe – zinazoimbwa na wakulima wakiwa shambani
(v) Tendi – Za masimulizi ya mashujkaa (al.5)
(c)- Huhifadhi matukio muhimu ya kihistoria
– Chombo cha kupitisha utamaduni
– Ni burudani inayotumbuiza waimbaji / hadhira
– Huliwaza na kufariji wenye majonzi
-Huhamasisha watu kushiriki katika kutenda mambo fulani
– Ni njia ya kujipatia kipato
– Hudumisha/huwasilisha usanii wa tamaduni za jamii mbalimbali
– Huelimisha, huonya, husimanga (zozote 5)
(d) BEMBELEZI
- Ziliimbiwa watoto ili watulie/wanyamaze
- Ziliimbwa na walezi /wazazi hasa mama
- Sauti ni ya kubembeleza
- Hutoa ahadi mbalimbali kwa mtoto
- Huwa fupi / hurudiwa –rudiwa
- Ziliburudisha watoto (zozote 5 =al. 5)
7. (a) – Hizi ni hadithi zinazotumia wanyama kama wahusika (mnyama anaweza kusemezana na
binadamu)
(b) – Huwezesha fanani na hadhira yake kusema mambo ambayo kwa kawaida ingekuwa
mahali/aibu kuyatamka hadharani (kusema kitasifida)
– Ni njia ya pekee ya kufunzia maadili na amali za jamii (kuyapigia mambo chuku)
– Kutahadharisha hadhira dhidi ya watu waovu katika jamii (Sungura na Fisi ujanja wao ni
sawa na matapeli)
– Hufurahisha . Hii ni kwa sababu, nyingi ya hadithi hizi huchekesha na kuleta huruma kwa
wengine (Sungura kupigana na Ndovu na kumshinda ni kichekesho)
(c) – Watu wazima kuwasimulia watoto
– Watoto kusimuliana hadithi wenyewe kwa wenyewe
– Watu wazima kusimulia mseto wa watu wazima na watoto
– Watoto kusimulia hadhira ya mseto wa watu wazima na watoto
8. (a)(i) Fasihi ya ngoma
(ii) Matumizi ya ala
Hakuna sauti ya binadamu
Mdundo hotoa ujumbe fulani
Hutumiwa kw anjia ya mawasilinao
Saiuti ni ya kupasha ujumbe (zozote 2×1=al. 2)
Wapigaji ngoma na ala zingine
ni watu teule katika jamii
(b) (i) Hurafa- Wahusika ni wanyama
Hekaya- ujanja, ucheshi , werevu an ushindi hujitokeza al.2)
(ii) Visasili /ngano za zuli – hutoa maelezo kuhusu asili ya hali fulani
- Hujibu swali kwa nin kitu fulani kiko jinsi kilivyo
- Visakale – visa vya kale vya mashujaa /majagina (migani)
(iii) Mtanziko – Ngano zinazomwacha msomaji/ mhusika katika hali ya kutojua achague lipi.
– Ni msimulizi huuliza swali
Mazimwi – Hadithi za majitu za kuogofya
– Kiumbe cha kufikirika akilini
(c) (i) Vitendawili – tungo fupi inayotoa maelezo yanayoishia kwenye swali
(ii) Mbinu – Takriri
– Istiara\- Ukinzani
_ Tanakali ya sauti (zozote 4×1= al. 4)
9. a) i)
- Tumbuizo – wimbo wa kuburudisha katika hafla ya arusi
- Wimbo wa kitamaduni
ii) Kuumeni – wanaume
Kukeni – wanawake
Wanaume wanawakilisha wakwe na Tausi (anayeolewa) na wanawake wanawakilisha wazazi wa Tausi
iii) – Watu wa kukeni wana moyo wa kisebusebu na roho kipapo. Walipenda mtoto
wao aolewe lakini awaondokeapo na kwenda kwa mumewe waliona
uchungu, kwani walijua huduma alizokuwa akiwapa tausi, zingekoma mara moja
– Upande wa kuumeni walifurahi kwani walijua Tausi angeongezea huduma
upande wao
iv) – Unaburudisha waliofika kwenye sherehe ya arusi
– Unaleta ushirikiano baina ya pande mbili
– Unatoa ujumbe kuwa kuondoka kwa mtu mliyezoena huwa ni wakati mgumu sana
v) takriri – Kurudia maneno kwa madhumuni ya kusisistiza mfano kisura wetu,
b)
- Mbolezi – nyimbo za matanga
- Bembelezi – kunarai watoto walale
- Hodiya/ kazi – wakati wa kazi
- Nyimbo za kitaifa – kuonyesha uzalendo kwa taifa
- Nyimbo za kisiasa – kumsifu au kumkejeli kiongozi wa kisiasa
- Nyimbo za kidini – katika ibada
- Vichapuzi – nyimbo zinazoandamana na usimulizi
10. a) i) Sifa za Hurafa
– Ni hadithi
– Wahusika aghalabu huwa wanyama
– Hupewa sifa na matendo ya binadamu
– Huwa na mafumbo Zozote 2×1=2
ii) Sifa za Mighani
- Ni hadithi za mashujaa
- Ni hadithi za kihistoria
- Wahusika huwa mashujaa
- Hupigania haki za wanyonge Zozote 2×1=2
iii) Sifa za Miviga
- Hujumuisha vitendo maalum k.v. kuimba, kuruka, kucheza ngoma
- Huhusisha maombi
- Aghalabu wahusika hutoa sadaka
- Wahusika huweka ahadi (kiapo)
- Kuna matumizi ya vifaa, mavazi na mapambo maalum Zozote 2×1=2
b) Umuhimu wa Ngomezi
– Hutoa taarifa kwa njia nyepesi na kuwafahamisha wanajamii kuhusu matukio Fulani k.v. sherehe, mkutano
– Hutumika kutahadharisha watu
– Hutumika kutoa matangazo rasmi
– Ni njia ya kudumisha utamaduni
– Ni njia ya kudhihirisha ufundi wa jamii 5×1=5
Umuhimu wa mafumbo
- Huburudisha
- Huonya na kutoa mawaidha
- Huimarisha uwezo wa kiakili
- Hufikirisha
- Huimarisha usikivu na uwezo wa kukumbuka
- Hukuza lugha Zozote 5×1=5
Tofauti kati ya malumbano ya utani na mawaidha
Mawaidha
| Malumbano ya utani
|
12. i) Maana ya vitanza ndimi
Ni maneno ambayo hutatanisha wakati wa kutamka kwa sauti ambazo zinafanana
ii) Kumzoesha anayetamka ufasaha wa kuyatamka maneno
Kueneza maarifa kuihusu lugha Fulani
Kufikirisha hasa kuielewa maana ya kitanza ulimi kinachohusika
Kuujenga uwezo wa kuongea au kuzungumza bila ya shida
Kuendeleza utamaduni kwa kurithishana maarifa ya sanaa folklore
Kuwanoa wanajamii ambao baadaye watakuwa na ugwiji wa ulumbi alama 8


1 Comment