Form 4 Kiswahili
Maana na Umuhimu wa Lugha
Maana
Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua maana ya katiba na sheria.
- Kutaja baadhi ya sheria zinazotumika katika nchi ya Kenya.
- Kutaja taasisi zinazohusika na kuunda na kutekeleza sheria.
Utangulizi
Katiba ni sheria au kanuni zilizooanisha namna ambavyo nchi, chama au shirika inavyoendesha shughuli zake. Katiba ya nchi ni sheria inayooanisha misingi ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba hubainisha haki za wananchi. Kidemokrasia, katiba inafaa kubatilishwa baada ya kufanyiwa marekebisho yanayokubalika na wananchi kwa jumla. Nchini Kenya tangu kupata uhuru tumekuwa tukitumia katiba iliyoundwa zama za wakoloni.
Mwaka wa 2010, wananchi walipata fursa ya kubadilisha katiba hiyo na kuchagua iliyobatilishwa ili kuwafaa kupitia kura ya maoni.
Katiba mpya nchini Kenya inafafanua haki za kimsingi za wananchi kama vile: haki ya kuishi, usawa na uhuru, usalama wa wananchi, uhuru wa dhamiri na imani ya dini na maoni. Katiba mpya inawapa Wakenya uhuru wa kujieleza. Pia katiba mpya inalinda wanahabari kwa kuwapa uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari. Katiba mpya inaendeleza utamaduni na lugha za kiasili. Haki za wafungwa zinazingatiwa kwa mujibu wa kanuni za kibinadamu; kwa mfano, masilahi ya wafungwa yanazingatiwa na pia wamepewa haki ya kuchagua wawakilishi wa eneo bunge lao.
Raia kwa jumla wanalindwa na katiba katika maswala ya ndoa, jinsia, urithi, ajira na dini ambapo wanawake na wanaume wana haki sawa katika nyanja tatu za maisha, mfano kiuchumi, kijamii na kisiasa. Wanasheria hutunga na kujadili sheria za nchi.
Sheria ya katiba huhusisha sheria za umma na zile za kibinafsi za wananchi, ilhali sheria za kimataifa hutawala shughuli za kibiashara, vikwazo vya kimazingira na mipaka, ulinzi na kadhalika baina ya nchi na nchi. Katika demokrasia halisi, sheria hutafsiriwa na matawi matatu makuu: mahakama, bunge na serikali ya kuwajibika. Matawi haya ndiyo huunda vyombo vya dola vinavyohakikisha uzingativu wa sheria nchini. Kamati na idara tofauti za bunge na serikali huhakikisha sheria zinazoundwa zinatekelezwa vilivyo.
Katiba mpya inasisitiza haki za watoto kwa kuhakikisha kuwa mtoto anapata kuelimika, kutunzwa vyema na hadhulumiwi. Mtoto haruhusiwi kutengwa na wazazi wake kwa njia yoyote.
Aidha, sheria hutilia mkazo matumizi ya lugha nchini. Katiba mpya inatambua aina tatu za lugha nchini: lugha rasmi, lugha ya taifa na lugha nyingine kama vile za kiasili, ishara na Braille. Ni dhahiri kuwa bunge linajukumu la kujumuisha maoni ya vikundi tofauti vya jamii katika kuimarisha sheria zilizoundwa katika katiba.
Memo
SHULE YA UPILI YA MADIVINI
S.L.P 1234 009
KIKWAO
SIMU: +254 056 5101600
BARUAMEME: [email protected]
MEMO
KWA: WANAFUNZI
KUTOKA: MWALIMU MKUU
TAREHE: MACHI 12, 2011
KUH: MATOKEO YA MTIHANI WA KCSE 2010
Kutokana na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, ningependa kuwaarifu kuwa shule yetu imeweka rekodi ya ushindi kuibuka nambari tano kati ya shule ishirini bora nchini. Kwa niaba ya Halmashauri ya shule, ningependa kuwapongeza walimu na wanafunzi kwa kazi nzuri iliyotuletea ufanisi wa kiwango hiki. Ili kuhakikisha tunadumisha matokeo bora shuleni, kila mmoja wetu anapaswa kuzingatia nidhamu, kutumia vyema mema ya wakati, maktaba na vifaa vyote vilivyomo na kuzidisha juhudi zetu katika utendaji kazi ili kufikia malengo yetu.
Elekezi Robai
Mwalimu mkuu.
Umeona na kusikia nini? Bila shaka umeona maandishi na kusikia ujumbe maalum wa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu anawaandikia wanafunzi wake. Barua hii imepachikwa ukutani. Barua hii huitwa memo au arifa. Memo ni taarifa fupi ya kiofisi ambayo hutoka kwa mtu mmoja hadi kwa wengine.
Sifa za Memo
- Hutangulizwa kwa anwani.
- Huwa na ujumbe maalum.
- Huwa na umbo la kipekee.
- Walengwa wa habari hubainishwa.
- Mwandishi hubainishwa.
- Mwandishi wa memo hutia sahihi.
- Huwa na sehemu tano kuu: anwani, utangulizi, Mintarafu, ujumbe, mwandishi.
- Huwaandikwa kwa karatasi maalum.
- Neno “memo” huandikwa kwa wino uliokolezwa.
- Huwa salamu hazitolewi.
Umuhimu wa memo
Memo huwa na dhima kubwa sana hasa katika kujuza ujumbe. Hii ndiyo sababu zimepachikwa nyingi labda. Memo ni njia rahisi ya kuwasiliana katika shirika lolote lile. Memo zinakumbusha walengwa wajibu wao kazini, kuweka kumbukumbu ya mambo yaliyojadiliwa na kufahamisha sera za shirika au taasisi kama hii yetu.
Muundo wa Memo
Memo huwa na hatua tano muhimu ambazo lazima zijitokeze:
- Anwani ya shirika hutangulia na huandikwa sehemu ya juu ya karatasi.
- Neno “MEMO” hufuata kwa herufi kubwa na kukolezwa wino.
- Upande wa kushoto chini ya mstari huandikwa utangulizi ufuatao:
- Kwa: sehemu hii huelezea ujumbe unalenga akina nani.
- Kutoka: sehemu hii huonyesha ujumbe umetoka kwa nani.
- Tarehe: sehemu hii huonyesha tarehe memo ilipoandikwa.
- Mintarafu: hapa shabaha ya barua hudokezwa kwa herufi kubwa zilizokolezwa wino.
- Mwili wa memo au maelezo ya mada inayoshughulikiwa huendelezwa.
- Hitimisho la memo hubeba sahihi, jina na cheo cha mwandishi.
Tazama mfano huu:
KIWANDA CHA CHAI CHA MAEMBENI
S.L.P. 998646 00300
MAEMBENI
SIMU: +452 7220 707404 474
BARUAE: [email protected]
MEMO
KWA: WAFANYIKAZI WOTE
KUTOKA: MENEJA MKUU
TAREHE: MACHI 23, 2011
Mintarafu: Nyongeza ya Mishahara
Kiwanda chetu kimepata faida kubwa msimu uliopita. Mapato ya kifedha yameongezeka maradufu miaka miwili iliyopita. Hii inatokana na juhudi za kila mmoja wetu. Kwa niaba ya Halmashauri ya Wakurugenzi, nawapongeza sana kwa bidii yenu. Kwa shukrani na pia kuwahimiza kujibidiisha zaidi, halmashauri ya wakurugenzi wa kiwanda hiki wamependekeza nyongeza ya mishahara yenu. Wafanyakazi wa kiwango cha F na G watapata nyongeza ya asilimia 52. Wale wa kiwango cha H-J watapata nyongeza ya asili mia 21. Wafanyakazi wa kiwango cha K-P watapata asilimia 8. Ni matumaini yangu kuwa nyongeza hizi zitawapa motisha wa kufanya kazi hata zaidi. Kila hali ya uchumi wa kiwanda unavyoimarika ndivyo wasimamizi watazidi kuchunguza na kuimarisha mishahara ya wafanyakazi wake.
Abdulmajid Rajab.
(Mkurugenzi Mkuu)
Shughuli
Katika sehemu hii, utapata maelezo zaidi juu ya somo husika. Bonyeza mada yoyote kati ya zilizoorodheshwa ili ufaidi!
Katika sehemu hii, unatakiwa kubonyeza mazoezi yaliyoorodheshwa ili uweze kujipima iwapo umeyapata yaliyofunzwa katika somo. Vilevile, unaweza kuupima uelewaji wako wa mada hata kabla hujashughulikia mafunzo ili uweze kujua unayopaswa kutilia mkazo zaidi.
Sajili ya Viwandani
Haya ni mazungumzo yanayohusisha matumizi ya lugha katika maeneo ya viwandani. Huhusisha mazungumzo kati ya wafanyakazi mbalimbali na wasimamizi wao.
Sikiliza na kutazama mazungumzo haya.
Je, kufikia hapo, unafikiri mazungumzo haya yanahusu watu wa aina gani? Bila shaka nataraji umegundua watu hawa wako kazini. Hawa wanafanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza sukari. Kiwanda ni mahali ambapo mafundi au watu wenye ujuzi katika kazi maalum hufanya kazi ya kutayarisha bidhaa au vifaa fulani. Kuna aina nyingi za viwanda namna kulivyo na bidhaa mbalimbali. Sajili inayotumika katika viwanda hutegemea shughuli za kiwanda husika, wafanyakazi hao na hata vyeo vyao. Ni sifa gani za sajili hii zinazojitokeza katika mazungumzo haya?
Tazama video hii na kusikiliza mazungumzo. Unadhani mazungumzo haya ni kati ya akina nani? Ndiyo, natumai umeona hawa ni wafanyakazi wa ngazi ya juu katika kiwanda. Meneja mkuu ndiye kiongozi na wasaidizi wake ni meneja. Lugha ya meneja inatofautianaje na ile ya Mkurugenzi mkuu? Sajili ya viwandani ina sifa gani kutokana na mazungumzo haya?
Hitimisho
Bila shaka umeweza kutambua sajili ya viwandani na sifa za sajili hii. Ni vyema ukifanya utafiti zaidi ili kujua sifa za sajili ya viwandani kwa vile itakurahisishia mawasiliano endapo utakumbana na hali hii. Waweza kutalii viwanda mbalimbali na kuchunguza kwa makini wafanyakazi wa daraja mbalimbali wanavyowasiliana.
Bunge
Zoezi
Mazungumzo Bungeni
Bonyeza na kusikiliza mazungumzo.
Hitimisho
Imedhihirika kwamba sajili ya bunge ina sifa za kutumia istilahi maalum. Aidha lugha huwa ya kisheria na huzingatia nidhamu. Ili kuelewa zaidi sajili hii inakubidi kufuatilia mazungumzo hayo katika vyombo vya habari.
Vivumishi ni maneno yanayotoa maelezo zaidi kuhusu nomino katika sentensi. Ni lazima kupatanisha vivumishi na nomino katika ngeli mbalimbali ili kuwa na sentensi sahihi kisarufi. Upatanisho wa kisarufi ni hali ya nomino kukubaliana na kiambishi kiwakilishi cha nomino husika katika maneno ambayo huandamana na nomino hiyo katika sentensi kama vile vivumishi.
Hivi ni vivumishi vinavyoeleza nomino kwa njia za kipekee kila moja. Vivumishi hivi ni vya aina sita kama ifuatavyo: -ote, -o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo. Tazama mifano ya sentensi:
- Wanafunzi wote wanastahili kuwa na nidhamu.
- Tunda lolote linaboresha afya.
- Mwalimu mwenyewe anawapenda watoto wake.
- Bilauri nyinginezo zinahitajika.
Sasa tazama jedwali lifuatalo:
| Ngeli nomino | -ote | -o-ote | -enye | -enyewe | -ingine | -ingineo |
|---|---|---|---|---|---|---|
| A | samaki wote | wote yoyote | wenye | wenyewe | mwingine | wengineo |
| U | miswaki wote | yote wowote | yenye | yenyewe | mwingine | mingineo |
| LI | meno lote | yote lolote | lenye | lenyewe | jingine | menginyo |
| KI | vifurushi chote | vyote chochote | chenye | chenyewe | kingine | kinginecho |
Hivi ni vivumishi vinavyoonyesha au kuashiria ilipo nomino. Vivumishi vionyeshi pia huitwa viashiria. Vivumishi hivi ni vya aina tatu: vya karibu, vya mbali kidogo na vya mbali sana. Kwa mfano:
- mtu huyu, mtu huyo, mtu yule
- kiti hiki, kiti hicho, kiti kile
- jumba hili, jumba hilo, jumba lile
Hebu tazama jedwali lifuatalo:
| Ngeli Nomino | Vya karibu | Vya mbali kidogo | Vya mbali sana |
|---|---|---|---|
| U | miko huu | hii huo | hiyo ule |
| LI | majani hili | haya hilo | hayo lile |
| U | maasi huu | haya huo | hayo ule |
| I | darubini hii | hizi hiyo | hizo ile |
| KU | kushinda huku | huko kule |
Zoezi
Sasa tazama jedwali lifuatalo:
Upatanisho wa kisarufi kati ya nomino na vivumishi hutokea kupitia viambishi vya ngeli au viambishi vya upatanisho wa kisarufi kama ulivyoona katika jedwali.
Zoezi
Vivumishi vimilikishi
Hivi ni vivumishi ambavyo huonyesha umiliki wa au kuwa na kitu. Viambishi awali hubadilika kulingana na nomino inayomilikiwa na nafsi inayomiliki. Tazama mifano katika jedwali lifuatalo:
- Kalamu yangu ina wino mwekundu.
- Kalamu yako ina wino wa rangi ya samawati.
- Kalamu yake ina wino mweusi.
Zoezi
Vivumishi viulizi
Hivi ni vivumishi vinavyouliza maswali kuhusu nomino. Vivumishi hivi vinapotumiwa katika sentensi ni sharti sentensi hiyo ikamilishwe kwa alama ya kiulizi. Vivumishi viulizi huwa ni vitatu: -pi?, -ngapi? na gani (ambacho hakiambishwi). Mifano ya vivumishi viulizi ni kama ifuatayo:
- Mtoto yupi anapenda kusoma?
- Mishipi gani inatumika kama sare ya shule yetu?
- Vyumba vingapi vimesafishwa?
- Uhalisia upi wa maisha unawafaa wanafunzi?
Mifano zaidi:
- Jengo lipi ni kubwa?
- Ni mwanafunzi yupi hajavaa sare?
- Viatu gani ni vya watoto?
- Unga upi ni wa mahindi?
Sasa tazama mifano zaidi katika sentensi:
- Kitabu kipi ni kizuri zaidi? Vitabu vipi ni vizuri zaidi?
- Papai lipi limeiva? Mapapai yapi yameiva?
- Uteo gani umenunuliwa na nyanya? Teo gani zilinunuliwa na nyanya?
- Maziwa gani yalinywewa na paka?
- Wasichana wangapi walikuja?
- Maradhi mangapi yalitibiwa?
Zoezi
Vivumishi vya idadi
Hivi ni vivumishi vinavyotaja idadi ya nomino. Kuna vinavyotaja idadi maalum na vyenye kutaja idadi kwa jumla. Tazama mifano ifuatayo:
Vya kutaja idadi maalum:
- Tembe mbili za dawa zilimezwa.
- Viti vitatu vimetengenezwa.
Vya kutaja idadi jumla:
- Chakula kingi kimebaki.
- Maji mengi yamehifadhiwa.
Tazama jedwali lifuatalo;
Kutokana na jedwali imebainika kuwa viambishi vya upatanisho katika vivumishi vya idadi hutegemea aina ya kivumishi cha idadi na nomino inayohusika.
Zoezi
Vivumishi vya A-unganifu
Hivi ni vivumishi vinavyohusisha nomino moja na nyingine. Vivumishi hivi huishia kwa herufi ‘a’. Kwa mfano:
- Mtu wa watu.
- Chama cha wananchi.
- Mizizi ya mimea.
- Nyumba za wazee.
- Gari la mwalimu.
Zoezi
Vivumishi visisitizi. Hivi ni vivumishi ambavyo husisitiza nomino fulani. Vivumishi hivi huundwa kwa kurudiarudia vivumishi vionyeshi. Visisitizi hujitokeza katika viwango vitatu: Nomino ikiwa karibu; nomino ikiwa mbali kidogo; nomino ikiwa mbali. Kwa mfano:
- Jiwe lili hili ndilo lililowafaa waashi.
- Taarifa iyo hiyo ndiyo ilinipa matumaini.
- Machungwa yale yale yaliwaburudisha watu.
- Papa yuyo huyo ndiye aliyepikwa.
Zoezi
Hivi ni vivumishi vinavyohusisha nomino moja na nyingine. Vivumishi hivi huishia kwa herufi ‘a’. Kwa mfano:
- Mtu wa watu
- Chama cha wananchi
- Mizizi ya mimea
- Nyumba ya wazee
- Shule ya watu wote
Vivumishi vya Pekee
Hivi ni vivumishi vinavyoeleza nomino kwa njia za kipekee kwa kuwa kila kimojawapo huwa na maana mahsusi. Vivumishi hivi ni vya aina sita kama ifuatavyo: -ote, -o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo. Tazama mifano ya sentensi:
- Wanafunzi wote wanastahili kuwa na nidhamu.
- Tunda lolote huboresha afya.
- Mwalimu mwenyewe anawapenda watoto wake.
- Bilauri nyinginezo zinahitajika.
- Kitabu chenye manufaa kimenunuliwa.
- Maji mengine yanahitajika.
Sasa tazama mifano zaidi katika jedwali lifuatalo.
| Ngeli nomino | karibu | mbali kidogo | mbali |
|---|---|---|---|
| a) Mtoto | yuyu huyu | yuyo huyo | yule yule |
| b) Gari | lili hili | lilo hilo | lile lile |
| c) Nyumba | zizi hizi | zizo hizo | zile zile |
Vivumishi Vionyeshi
Hivi ni vivumishi vinavyoonyesha au kuashiria ilipo nomino. Vivumishi vionyeshi pia huitwa viashiria. Vivumishi hivi ni vya aina tatu: vya karibu, vya mbali kidogo na vya mbali sana. Kwa mfano:
- Mama yule anaenda sokoni.
- Kiti hiki ni cha mtoto.
- Magoti yangu haya yanauma.
- Ukuta huo una rangi gani?
- Chai hii haina sukari.
Hitimisho
Hivi ni vivumishi vinavyoeleza nomino kwa namna ya kipekee kwa sababu kila kimoja wapo kina maana yake mahususi. Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuweza:
- Kueleza maana ya viunganishi.
- Kutambua aina za viunganishi.
- Kutumia aina mbalimbali za viunganishi katika sentensi.
Viunganishi viongezi au vya kuongeza huleta dhana ya “zaidi ya”. Mifano zaidi ya viunganishi hivi ni: na, tena, pia, aidha, pamoja na, zaidi ya.
Tazama mifano ya sentensi zifuatazo:
- Utulivu wake na bidii yake ilimfanya atuzwe katika hafla hiyo.
- Wanafunzi pamoja na walimu wao waliingia maabara.
- Fatma aliruhusiwa kwenda Mombasa na wewe pia utaandamana naye.
Viunganishi visababishi/vya sababu hutoa sababu ya kutendeka kwa jambo. Huweza kutumiwa mwanzoni au katikati ya sentensi. Mifano ni kwa sababu, kwa vile, na kutokana na.
- Wanafunzi walisherehekea kwa sababu ya matokeo yao bora.
- Kwa vile hakuwa na nauli hakuendelea na safari yake.
Kiunganishi cha asili ya kibantu ni “na”. Kwa mfano:
- Mtoto na mzazi wametoka shambani.
- Waziri mkuu na naibu wake wanaelekea bungeni.
Viunganishi vya Asili ya Kigeni
Kuna viunganishi vya asili ya kigeni. Mifano ni: fauka ya, ilhali, sembuse/seuze.
- Zuleka anawasaidia majirani wake sembuse aila yake.
- Nchi zinazoendelea zina uwezo wa kuyaboresha maisha ya raia wake seuze nchi zilizoendelea!
- Aliniagiza kwenda kwake ilhali hakunipa nauli.
Aina za Vitenzi
Vitenzi hugawanyika katika makundi yafuatayo: vitenzi halisi, vikuu, visaidizi, vishirikishi na sambamba.
Vitenzi Halisi
Hivi ni vile vinavyoarifu tendo linalotendwa na kitu chochote kile chenye uwezo wa kutenda. Kwa mfano:
- Mkulima analima shamba.
- Watalii walizuru nchi yetu.
- Abdul atatembelea Afrika Kusini.
- Mutua anasakura kwenye mtandao.
- Faiza amempigia mama simu.
Vitenzi Vikuu (T)
Kitenzi kikuu huelezea tendo kuu katika sentensi. Huhusisha ujumbe kwa usaidizi wa kitenzi kingine ambacho huitwa kitenzi kisaidizi. Mifano:
- Marangi anapenda sana kupaka rangi.
- Wanafunzi wamekuwa wakisoma tangu asubuhi.
Kitenzi Kisaidizi
Hiki ni kitenzi ambacho huandamana na kitenzi kikuu. Kitenzi kisaidizi huwa na kazi ya kukisaidia kitenzi kikuu ili sentensi ilete maana kamilifu. Mifano:
- Mwalimu alikuwa anawafunza wanafunzi.
- Umewahi kumwona fisi.
- Amina alijitahidi kumbebea mzee huyo mzigo.
- Hataenda kuogelea mtoni.
Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi vishirikishi ni vile ambavyo vinashirikisha kiima cha sentensi na kijalizo. Kwa mfano, “Kisu hiki ni kikali”. Katika sentensi hii kisu ni kiima na kikali ni kijalizo. Kijalizo husaidia kukamilisha maelezo kuhusu kiima. Kwa mfano:
- Huyu ni mwalimu.
- Huyu ni kiima.
- Ni ni kitenzi kishirikishi.
- Mwalimu ni kijalizo.
Mifano mingine ni kama:
- Hayo yalikuwa maneno mazito. Hayo ni kiima. Yalikuwa ni kitenzi kishirikishi. Maneno mazito ni kijalizo.
Kuna aina mbili ya vitenzi vishirikishi:
- Vitenzi vishirikishi vipungufu
- Vitenzi vishirikishi vikamilifu
Vitenzi vishirikishi vipungufu huchukua viambishi nafsi/vya ngeli. Vitenzi hivi havichukui viambishi vya njeo (wakati) na hali. Kwa mfano:
- Otieno ni daktari.
- Mwanafunzi yu darasani.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu huchukua viambishi vya njeo/wakati/hali/nafsi/ngeli, kwa mfano:
- Wanafunzi wanastahili kuwa darasani.
- Wabunge walikuwa wangali bungeni.
- Wanakijiji watakuwa wakihudhuria arusi.
Vitenzi Sambamba
Vitenzi sambamba ni vitenzi ambavyo hutokea katika mfululizo. Mfululizo wa aina hii unaweza kuleta pamoja kitenzi kisaidizi au kishirikishi na kitenzi halisi. Uweza pia kuhusisha vitenzi visaidizi kadha na kitenzi kikuu. Kwa mfano:
- Wanafunzi wanakimbia wakiimba uwanjani.
Wanakimbia ni kitenzi kikuu.
Wakiimba ni kitenzi kisaidizi. - Watahiniwa walikuwa wanataka kujiandaa kupita mtihani.
Walikuwa ni vitenzi visaidizi.
Wanataka ni kitenzi kisaidizi.
Kujiandaa kitenzi kisaidizi.
Kupita kitenzi kikuu. - Wakulima wangali wanalima.
Wangali ni kitenzi kisaidizi.
Wanalima ni kitenzi kikuu.
Kufikia mwisho wa kipindi unapaswa:
- Kufafanua maana ya vitenzi.
- Kubainisha aina za vitenzi.
- Kutumia vitenzi katika sentensi (zoezi).
Vitenzi Kisaidizi
Kikundi Kitenzi
Hii ni sehemu ambayo huwa na kitenzi na pengine maneno mengine kama vile kielezi, shamirisho, kishazi tegemezi na kadhalika. Kitenzi chaweza kuwa kikuu, halisi, kishirikishi, au hata kisaidizi. Kwa mfano:
- Juma anaimba vizuri;
- Mombasa ni mji safi;
- Mwanafunzi anasoma kitabu chake.
Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi sambamba ni vitenzi ambavyo hutokea katika mfululizo. Mfululizo wa aina hii unaweza kuleta pamoja kitenzi kisaidizi au kishirikishi na kitenzi halisi. Uweza pia kuhusisha vitenzi visaidizi kadha na kitenzi kikuu. Kwa mfano:
- Wanafunzi wanakimbia wakiimba uwanjani.
Wanakimbia ni kitenzi kikuu.
Wakiimba ni kitenzi kisaidizi. - Watahiniwa walikuwa wanataka kujiandaa kupita mtihani.
Walikuwa ni vitenzi visaidizi.
Wanataka ni kitenzi kisaidizi.
Kujiandaa kitenzi kisaidizi.
Kupita kitenzi kikuu. - Wakulima wangali wanalima.
Wangali ni kitenzi kisaidizi.
Wanalima ni kitenzi kikuu.
Zoezi
Yambwa kitondo ni nomino ambayo hutendewa jambo. Huathiriwa na jambo kwa njia isiyo moja kwa moja. Kitondo hunufaika au kupata hasara kutokana na vitendo vya mtenda. Kwa mfano:
- Watoto wametambiwa hadithi na babu.
- Mwashi amemjengea Farida nyumba nzuri.
- Kasisi alinipa mawaidha bora.
- Mpishi amekupikia chai tamu.
Kutokana na mifano hii utaona kuwa viambishi viwakilishi nomino huweza pia kuchukua nafasi ya kitondo.
Yambwa Ala/Kitumizi
Yambwa ala au kitumizi hurejelea kifaa ambacho hutumika katika kufanikisha tendo. Kile kifaa kinahusika katika kutekeleza kitendo kile. Kwa mfano:
- Wanafunzi wanaandika kwa kalamu ya wino. (ala/ kitumizi)
- Tulisafiri kwa gari la moshi. (ala/ kitumizi)
- Waimbaji wanaimba kwa tarumbeta. (ala/ kitumizi)
- Wanafunzi wanasoma kwa miwani. (ala/ kitumizi)
Chagizo (CH)
Chagizo ni sehemu ya sentensi ambayo aghalabu huja baada ya kitenzi au yambwa/shamirisho. Chagizo huwa kielezi au kirai kielezi. Chagizo hutofautishwa na kielezi kwa kuzingatia uamilifu wake katika sentensi. Kwa mfano:
- Mkulima anapanda miti sasa. (chagizo)
- Mwanafunzi anasoma kitabu kwa makini. (chagizo)
- Mtoto anacheza mpira uwanjani. (chagizo)
- Mara kwa mara mimi huandikiwa barua kwa kalamu nzuri. (chagizo)
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua maana ya yambwa/shamirisho.
- Kubainisha aina za shamirisho.
- Kutumia shamirisho ipasavyo katika sentensi.
Aina za Yambwa
Virai Nomino
Katika aina hii ya kirai neno kuu huwa ni nomino au kiwakilishi chake. Nomino huandamana na maneno mengine. Kwa mfano, kivumishi, kiunganishi, kielezi na kadhalika. Hata hivyo, kundi hilo lote huwa lina uamilifu wa nomino. Tazama mifano hii:
- Mama mpole amefika.
- Moshi ambao hutoka viwandani ni hatari.
- Mwanafunzi bora ametuzwa.
- Baba na mama wamefika.
Kirai Kivumishi
Katika kirai kivumishi neno lake kuu huwa ni kivumishi. Kirai kivumishi hufafanua sifa za nomino au kiwakilishi chake. Kundi la maneno huweza kuwa na kivumishi na maneno mengine kama vile, kielezi, kiunganishi, kihusishi na kadhalika. Kwa mfano:
- Mwashi amejenga jumba kubwa sana.
- Kasisi yule mwanasiasa amewapotosha wananchi.
- Nguo yangu mpya imepotea.
- Gari kubwa jeusi la mwalimu limepakwa rangi upya.
Chagizo (CH) Kirai Kielezi
Katika kirai kielezi, neno lake kuu ni kielezi. Kirai kielezi huwa mwandamano wa vielezi. Kwa mfano:
- Panya ameingia shimoni haraka mno.
- Tutaenda kuchezea uwanjani kasarani kesho alasiri.
- Utandawazi umeenea vururu kote dunia.
Kirahi Kihusishi
Kirai kihusishi ni kundi la maneno ambalo hufanya kazi ya kihusishi na neno lake kuu ni kihusishi. Mifano ya sentensi zenye kutumia kirai husishi ni kama vile:
- Ndege ametua juu ya mti.
- Uongozi wa nchi hii umeimarika sana.
- Shule yetu iko karibu na bwawa la sulu.
- Kijiti cha mti huo kimevunjika.
Vishazi
Kishazi ni kundi la maneno lenye muundo wa kiima na kiarifa. Kishazi hutokea katika muktadha wa sentensi kuu. Baadhi ya vishazi hujisimamia kimaana hata vikiondolewa kwenye sentensi kuu. Hivi ni vishazi huru. Vile haviiwezi kuleta maana vikiondolewa katika sentensi kuu huitwa vishazi tegemezi.
Aina za Vishazi
Kuna aina mbili za vishazi:
- Vishazi huru.
- Vishazi tegemezi.
Vishazi Huru
Hivi ni vishazi ambavyo vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu vitaweza kujisimamia kimaana. Kwa mfano:
- Kengele imelia na wanafunzi na wanafunzi wameingia darasani. Kengele imelia ni kishazi huru. Wanafunzi wameingia darasani pia ni kishazi huru.
- Ukuta uliojengwa umebomoka. Umebomoka ni kishazi huru.
- Mvua imenyesha kwa wingi hivyo wakulima wamevuna mazao mengi. Wakulima wamevuna mazao mengi ni kishazi huru.
- Ijapokuwa hakunialika, nilitamani sana kuhudhuria arusi yake. Nilitamani sana kuhudhuria arusi yake ni kishazi huru.
- Katiba iliyopitishwa itaimarisha maisha ya wananchi. Kishazi huru.
Vishazi Tegemezi
Hivi ni vishazi ambavyo haviwezi kujisimamia kimaana vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu. Vishazi tegemezi huhitaji vishazi vingine ili kuleta maana.
- Ungesikia ushauri wa mwalimu ungepita mtihani.
- Akimlipia nauli atamletea vitabu hivyo.
- Maadam umeniomba msamaha, nimekusamehe na kusahau.
- Wananchi wakibadilisha mienendo yao maenezi ya ugonjwa wa ukimwi yatapungua.
- Mwajiri aliyekiuka haki za watoto ameshtakiwa.
Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua umbo la sentensi sahili, ambatano na changamano.
- Kuchanganua aina tofauti za sentensi kwa:
- Mtindo wa mchoro wa matawi
- Mtindo wa mistari
- Mtindo wa visanduku
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua maana ya virai na vishazi.
- Kubainisha kirai na kishazi katika sentensi.
- Kutaja na kufafanua aina tofauti za virai na vishazi.
Uchanganuzi wa Sentensi
Kuchanganua sentensi huhusu kutenga sentensi katika sehemu mbalimbali za kisarufi. Sentensi yaweza kuchanganuliwa kwa:
- Mtindo wa mchoro wa matawi
- Mtindo wa mistari
- Mtindo wa visanduku
Katika aina hii ya kirai neno kuu huwa ni nomino au kiwakilishi chake. Nomino huandamana na maneno mengine kama kivumishi, kiunganishi, kielezi n.k. Hata hivyo, kundi hilo lote huwa lina uamilifu wa nomino. Tazama mifano hii.
Uchanganuzi wa Sentensi Sahili
Sentensi sahili huwa na muundo ufuatao: S-KN+KT
Katika uchanganuzi sehemu ya kikundi nomino na kikundi kitenzi huweza kuchanganuliwa ili kuonyesha vijenzi vya kila kijisehemu.
a) Uchanganuzi wa Sentensi Sahili kwa Mchoro wa Matawi
Utandawazi umeenea duniani
Mwanafunzi mwerevu amepita mtihani
Gari lililoharibika limekarabatiwa
Atakupikia wali mtamu.
b) Mtindo wa Mstari
Ufisadi hurudisha nyuma maendeleo.
Uendeshaji wa magari vibaya husababisha ajali.
Mazingira ni uhai.
c) Mtindo wa Visanduku
Mwandishi huyu ameandika riwaya.
Ali amenitumia arafa.
Mwanariadha hodari ameshinda nishani.
Katika kirai kivumishi neno lake kuu huwa ni kivumishi. Kirai kivumishi hufafanua sifa za nomino au kiwakilishi chake. Kundi la maneno huweza kuwa na kivumishi na maneno mengine kama vile, kielezi, kiunganishi, kihusishi na kadhalika. Kwa mfano:
Uchanganuzi wa Sentensi Ambatano
Sentensi ambatano huwa na muundo ufuatao: S
Uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa michoro ya matawi
Mwalimu: Karani unaweza kutukumbusha kirai kihusishi ni nini?
Karani: Kirai kihusishi ni kundi la maneno ambalo hufanya kazi ya kihusishi na neno lake kuu ni kihusishi.
Mwalimu: Hongera Karani. Nitakupa mifano ya sentensi zenye kutumia kirai husishi.
Aina za Vishazi
Kuna aina mbili za vishazi.
Vishazi Huru
Hivi ni vishazi ambavyo haviwezi kujisimamia kimaana vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu. Vishazi tegemezi huhitaji vishazi vingine ili kuleta maana. Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua umbo la sentensi sahili, ambatano na ambatano.
- Kuchanganua aina tofauti za sentensi kwa:
- Mtindo wa mchoro wa matawi
- Mtindo wa mistari
- Mtindo wa visanduku
Sentensi Sahili Huwa na Muundo Ufuatao: Vitenzi vya Asili ya Kibantu
Hivi ni vitenzi ambavyo kwa kawaida huishia kwa irabu ‘a’. Kwa mfano:
- soma
- cheza
- enda
- imba
- lima
Jedwali hili linaonyesha mifano ya mnyambuliko wa vitenzi vya asili ya kibantu.
Mnyambuliko wa Vitenzi vya Asili ya Kibantu
Mnyambuliko wa kitenzi ni hali ya kukiongezea kitenzi silabi ili kukipa maana zaidi. Vitenzi hunyambuliwa katika kauli au jinsi mbali mbali.
Vitenzi vya Asili ya Kigeni
Hivi ni vitenzi ambavyo kwa kawaida huishia irabu ‘e’, ‘i’, na ‘u’. Vitenzi hivi hutokana na lugha za kigeni kama vile kiarabu. Mifano ya vitenzi vya kigeni ni:
- sahau
- samehe
- thamini
- fuzu
- fariji
- salimu
- safiri
- durusu
- zuru
- hukumu
Mfano wa Mnyambuliko wa Vitenzi vya Asili ya Kigeni
Mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja
Hivi ni vitenzi ambavyo huwa na tamko moja au silabi moja. Mara nyingi huongezewa kiambishi ku- ili viweze kutamkika ipasavyo. Mfano:
-la huongezewa ku ikawa ‘kula’. Mifano zaidi ya vitenzi vya silabi moja:
- -ja
- -pwa
- -la
- -pa
- -wa
- -chwa
- -nywa
- -nya
- -pwa
- -fa
Tazama jedwali lifuatalo ili kuona mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja.
Hitimisho
Ni matumaini yangu kuwa unaweza sasa kubainisha vitenzi vya asili ya kibantu, vitenzi vya asili ya kigeni na vile vya silabi moja na kuweza kuvinyambua. Sasa jaribu kuvitungia sentensi na kueleza maana ya sentensi hizo. Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kubainisha vitenzi vya asili ya kibantu.
- Kutambua vitenzi vya asili ya kigeni.
- Kubainisha vitenzi vya silabi moja.
- Kutambua mzizi na shina la kitenzi.
- Kunyambua vitenzi hivi katika kauli mbalimbali.
Imedhihirika kuwa vitenzi hivi vinaishia irabu ‘a’. Isitoshe, vitenzi vilivyoorodheshwa viko katika kauli mbalimbali. Aghalabu, irabu ‘a’ huambikwa katika mzizi wa kitenzi ili kuunda shina la kitenzi. Ninafikiri unaweza kutofautisha kati ya mzizi na shina.
Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya kitenzi inayobakia baada ya kuondolewa kwa viambishi awali na tamati katika kitenzi hicho. Mizizi ya vitenzi vya asili ya kibantu huwa mizizi funge au ambata.
Uundaji wa Nomino
Nomino huweza kuundwa kwa njia tatu, nazo ni:
- Nomino kutokana na nomino.
- Nomino kutokana na vivumishi.
- Nomino kutokana na vitenzi.
Uundaji wa Nomino Kutokana na Mzizi wa Nomino
Tazama jedwali lifuatalo;
Sasa tazama mifano katika sentensi zifuatazo:
- Mtu ni utu.
- Mdeni amenilipa deni langu.
- Kiwango cha umaskini kinapozidi, idadi ya maskini huongezeka maradufu.
- Daktari alirudi chuoni kupigia msasa ujuzi wake wa udaktari.
Uundaji wa Nomino Kutokana na Mzizi wa Kitenzi
Tazama jedwali lifuatalo.
Tazama mifano ya sentensi zifuatazo:
- Nilikula chakula kitamu sana jana.
- Baada ya kuomba, ombi langu lilijibiwa.
- Msafiri huyo alisafiri kwa muda wa siku arobaini.
- Rudisha aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wanariadha wengine wote.
Uundaji wa Nomino Kutokana na Mzizi wa Kivumishi
Tazama jedwali lifuatalo.
Sasa tazama mifano katika sentensi:
- Umoja wao uliwafanya kuwa kitu kimoja hasa.
- Jumba hilo likuwa chafu sana, lilijaa uchafu wa kila aina.
- Yeye ni mwerevu kwelikweli, aliweza kutudhibitishia werevu wake kupitia mtihani huo.
- Bidhaa bora hutegemea ubora wa malighafi.
Uundaji wa Vitenzi
Vitenzi huweza kuundwa kutokana na aina nyingine za maneno kama vile nomino na vivumishi.
Uundaji wa Vitenzi Kutokana na Mizizi ya Nomino
Tazama jedwali lifuatalo.
Sasa soma sentensi zifuatazo ili kuelewa zaidi:
- Maana ilieleweka alipoeleza vyema alichomaanisha kutumia msemo huo.
- Wanasayansi wanaendelea kutafuta tiba ili waweze kutibu ugonjwa wa ukimwi.
- Ni muhimu kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa elimu.
- Alisababisha maafa, sababu zake zikiwa kujinufaisha mwenyewe.
- Mali aliyoibia taifa letu, ilitaifishwa.
Uundaji wa Vitenzi Kutokana na Mizizi ya Vivumishi
Tazama jedwali lifuatalo.
| Kivumishi | Mzizi | Kitenzi Kilichoundwa |
|---|---|---|
| Fupi | fupi- | fupisha |
| Bora | bor- | boresha |
| Sanifu | sanif- | sanifisha |
| Chafu | chafu- | chafua |
| Kamili | kamili- | kamilisha |
Sasa soma sentensi zifuatazo ili upate kuelewa zaidi.
- Meza fupi ilifupishwa zaidi na seremala.
- Chakula bora huboresha afya.
- Lugha sanifu ya Kiswahili ilitokana na kusanifishwa kwa lahaja ya kiunguja.
- Watu wengi huchafua mazingira kwa kutupa vitu vichafu ovyo ovyo.
- Mwalimu alimuamuru mwanafunzi kukamilisha insha yake alipowasilisha insha isiyokuwa kamili.
Uundaji wa Vivumishi
Vivumishi huweza kuundwa kwa kutumia maneno mengine kama vile nomino na vitenzi.
Uundaji wa Vivumishi Kutokana na Mizizi ya Nomino
Tazama jedwali hili.
Sasa tazama mifano ifuatayo ya sentensi:
- Mtu huyo mwerevu alijitajirisha kwa kutumia werevu wake.
- Wahusika wajinga hutumiwa katika fasihi ili kuonyesha ujinga miongoni mwa watu.
- Wembamba wake ulimwezesha kuivaa nguo hiyo nyembamba.
Uundaji wa Vivumishi Kutokana na Mizizi ya Vitenzi
Sasa angalia mifano ifuatayo ya sentensi:
- Ingawa mzee yule mlemavu amelemaa miguu yote, anajitahidi kutembea kwa mkongojo.
- Nilikutana na mtu mtulivu sana, alikuwa ametulia kama maji ya mtungi.
- Usipopoa hutaweza kuwa mpole kwa watu wengine.
- Msichana huyu mnyamavu alinyamaza tu kimya bila kujitetea.
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuweza:
- Kutambua aina tofauti tofauti za maneno.
- Kuunda aina mbalimbali za maneno kutokana na maneno mengine.
- Kuyatumia maneno hayo katika sentensi.
Lugha huwezesha uundaji wa maneno mapya kwa njia mbalimbali. Njia mojawapo ni uundaji wa maneno kutokana na yale yaliyopo. Kwa mfano: nomino kutokana na nomino, vitenzi kutokana na nomino na nomino kutokana na vivumishi. Nomino huweza kuundwa kwa njia tatu, nazo ni:
- Nomino kutokana na nomino
- Nomino kutokana na vivumishi
- Nomino kutokana na vitenzi
Uundaji wa Nomino Kutokana na Mzizi wa Nomino
Hutumiwa kama kiwakilishi cha nafsi ya pili umoja (wewe). Mifano katika sentensi:
- Nitakusomea riwaya ya Utengano.
- Mwalimu anakuita.
- Watakutumbuiza ukiwaruhusu.
Hutumiwa kama kiwakilishi cha mahali. Kwa mfano:
- Kuliko na fujo kuna wasiwasi.
- Kwenye miti kuna wajenzi.
- Wanafunzi wataimbia huku.
Kiambishi NDI- ndi- Hutumiwa kwa Namna Mbili
a) Pamoja na kitenzi kishirikishi kipungufu kwa mtindo wa kufupisha.
b) Hutumiwa kuonyesha msisitizo. Msisitizo huu hurejelea kiima yaani kinachozungumziwa. Ili kuonyesha kurejelea huku lazima pawepo na upatanisho wa kisarufi. Kwa mfano:
- Ndisi (ni sisi)
- Ndiwe (ni wewe)
- Ndiye (ni yeye)
- Ndio (ndio wao)
Kiambishi-JI- hutumiwa kwa namna zifuatazo:
- Kama kiambishi cha ngeli ya li-. Kwa mfano:
- jino
- jiko
- jipu
Mfano: Jino linalouma litang’olewa.
Jiko hilo lilichukuliwa na mwenyewe. - Kuonyesha ukubwa wa nomino. Kwa mfano:
- Jitu hilo liliwahangaisha wanakijiji.
- Jitu hili latisha mno.
- Kuonyesha dharau. Kwa mfano:
- jiatu
- jivulana
- jizee
Mfano:
- Jivulana lile ni jisumbufu sana.
- Jizee hilo linashikilia utamaduni uliopitwa na wakati.
- Kama kiambishi cha urejeshi katika vitenzi katika nafsi zote tatu. Kwa mfano:
- Nilijikata
- Ulijikosea
- Alijitia hatarini
Mfano:
- Nilijitia matatani kwa kutofika mapema.
- Alijikosea kwa kutofuata maagizo aliyopewa.
- Huambishwa mwishoni mwa kitenzi kuunda nomino ili kuonyesha mtu anayetenda kitendo fulani. Mifano katika sentensi:
- Mlimaji huyo alipata mavuno mengi.
- Msemaji yule alielewa kwa urahisi.
Vitenzi huweza kuundwa kutokana na aina nyingine za maneno kama vile nomino na vivumishi.
Kwa
- Neno kwa hutumiwa kuonyesha mahali.
- Nitakula chamcha kwa Ahmed.
- Mkutano utakuwa kwa Nyaga.
- Walipofika kwa nyanya walishangazwa na jinsi walivyopokelewa kwa mikono miwili.
- Neno kwa hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima.
- Wanafunzi ishirini kwa hamsini wanajizatiti.
- Atieno alipata themanini kwa mia katika somo la Kiswahili.
- Huonyesha jinsi kitendo kilivyofanyika.
- Walisherehekea arusi hiyo kwa furaha.
- Uchaguzi huo ulimalizika kwa amani.
- Hutumiwa pamoja na vivumishi vimilikishi kuonyesha umilikaji.
- Kule kwao kunaogofya.
- Kuimba kwake kuliwafurahisha.
- Huonyesha dhana ya “pamoja na”.
- Napenda kula wali kwa mchuzi wa samaki.
- Mkutano huo ulihudhuriwa na wazee kwa vijana.
- Huonyesha kitu fulani kilitumiwa kufanya jambo fulani.
- Aliambua mhogo kwa kisu.
- Alichanja kuni kwa shoka.
- Huonyesha kusudi, nia au sababu.
- Waliadhibiwa kwa uovu walioutenda.
- Alimwendea nyanya kwa kutaka kumjulia hali.
Ila
Neno ila ni kiunganishi kinacholeta dhana ya kinyume. Pia hutumika kuleta maana ya isipokuwa. Kwa mfano:
- Alipopatwa na msiba jamaa zake walimtoroka ila rafikize.
- Alijaribu kumshawishi katika swala hilo ila hakukubali.
- Anab alitarajiwa mkutanoni ila hakufika.
Labda
Huonyesha shaka au kutokua na uhakika nao.
- Labda sitampata kwake nyumbani.
- Najihisi kichefuchefu labda nina malaria.
- Sijui viliko vijiko labda tumwulize mama.
Na
Hutumiwa kama kiambishi cha wakati uliopo hali ya kuendelea. Kwa mfano:
- Fatuma anasoma riwaya ya utengano.
- Wabunge wanajadili bungeni.
- Daktari anatibu mgonjwa.
Hutumiwa kama mzizi wa kitenzi cha kuonyesha hali ya kumiliki au kuwa na. Kwa mfano:
- Mzee Juma ana wajukuu wane.
- Shamba hili lina magugu mengi.
- Nguo hii ina madoadoa mengi.
Hutumiwa kama kihusishi kuonyesha mtenda/kitenda. Kwa mfano:
- Unaitwa na mwalimu.
- Mtoto alinyweshwa maziwa na Yaya.
- Katiba hiyo ilipendekezwa na wananchi.
Hutumiwa kama kiunganishi kuleta maana ya “pamoja na”.
- Mwimbaji yule alivaa tai na kofia.
- Mama alinunua mafuta, sabuni na rangi ya viatu.
Maelezo
Utandawazi au kuunganishwa kwa jamii kumechukua mitazamo miwili ya kinadharia. Kwanza, kuna kuunganishwa kwa ushirikiano wa kisiasa ambao ni wa nchi kuu kadhaa na mashirika makubwa ya kimataifa. Hali hii ndiyo huitwa uunganishwaji wa juu. Mtazamo wa pili ni ule wa uunganishwaji wa mashirika ya kiuchumi na nchi moja moja kuelekeza mitaji na fedha zake kwingineko. Uunganishwaji huu hufanyika kama hatua ya kupanua shughuli zake. Uunganishwaji huu ndio hutambulika kama wa chini.
Utandawazi
Manufaa na matatizo ya utandawazi
Teknolojia ya habari na mawasiliano hushughulika na kuzalisha, kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha na kusambaza habari. Utandawazi una manufaa na matatizo yake. Faida kubwa ni kwamba utandawazi umeimarisha maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa. Hali ya mawasiliano imeboreshwa zaidi miongoni mwa watu wanaokaa mbalimbali. Jamii katika ulimwengu wote zimepata kuunganishwa kiasi cha kufanya dunia kuwa kama kijiji.
Baadhi ya matatizo yanayotokana na utandawazi ni kupanuka na kusuasua kwa uchumi katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Nchi za Asia Kusini na Mashariki na Marekani Kusini ndizo zilizoathirika. Tatizo jingine ni kupanuka zaidi kwa utabaka kunakoletwa na uwezo wa kiuchumi na kisiasa. Nchi zilizoendelea, na matabaka ya juu katika ulimwengu wa tatu ndizo hufaidika kwa utandawazi. Baadhi ya viongozi wa serikali na wasomi katika maeneo ya kiuchumi ambayo hayajaunganishwa katika utandawazi hujiona kama wamewekwa pembezoni – wametengwa.
Kumezuka makundi mawili, kundi linalopinga utandawazi na ambalo hudai kuwa utandawazi ni kama ukoloni mamboleo. Kundi hili huamini kuwa mataifa ya juu yana njama ya kuendeleza ukoloni kupitia kwa utandawazi. Kwa upande wa kundi linalounga mkono hutaka kumiliki na kudhibiti rasilmali za dunia kupitia kwa utandawazi. Hali hii imeliudhi kundi la kwanza na kusababisha pingamizi yao kwa utandawazi.
Utandawazi umefanya dunia kuanza kuendeshwa kwa masharti mapya. Kwa mfano, sasa kuna mabadiliko katika utoaji wa huduma. Hivi kwamba imewalazimu watu kuchangia kugharamia maisha. Masoko pia yamefanywa kuwa huria. Kila eneo limejipa uwezo wa kujiamulia bei ya kuuza na kununua bidhaa.
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kueleza maana ya utandawazi.
- Kueleza dhana kuhusu asili ya utandawazi.
- Kujadili upeo na ufanisi wa utandawazi.
- Kufafanua matatizo yanayotokana na utandawazi.
- Kufurahia na kushiriki katika matumizi ya utandawazi.
Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kufafanua maana ya teknolojia.
- Kubainisha aina mbalimbali za teknolojia.
- Kueleza umuhimu wa teknolojia.
- Kufurahia kutumia teknolojia.
Simu
Maendeleo ya kiteknolojia ni mengi na yameenea katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu kama vile elimu, mawasiliano, uchukuzi, biashara, zaraa, utabibu, usalama, ofisi n.k. Tazama mifano ifuatayo kasha baada ya kila sehemu ya mifano hiyo, utajibu maswali yanayofuatia.
Aina za Maendeleo
Maendeleo ya kiteknolojia ni mengi na yameenea katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu kama vile elimu, mawasiliano, uchukuzi, biashara, zaraa, utabibu, usalama, ofisi na kadhalika. Tazama mifano ifuatayo.
Uchukuzi na Mawasiliano
Tazama picha zifuatazo.
Biashara
Kuna mitambo mingine mingi na vifaa vya kiteknolojia vinavyotumiwa katika sekta ya biashara. Taja mifano zaidi mbali na hii iliyotolewa.
Zaraa
Zaraa au sekta ya kilimo imesheheni matumizi ya kiteknolojia. Kila kukicha ndivyo uvumbuzi mpya unajitokeza. Utafiti unazidi. Umewahi kusikia kuhusu kutumbishwa kwa mifugo? Jaribu kutafuta makala zaidi ujisomee.
Mafunzo Meme
Tazama picha hizi. Hawa wanafunzi wanafanya nini?
Matibabu
Sikiliza na kutazama mazungumzo haya. Nyumbani
Tazama picha hizi
Teknolojia ya nyumbani imerahisisha sana kazi za nyumbani. Tafuta makala zaidi kuhusu teknolojia hii ili upate maarifa zaidi.
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuweza:
- Kueleza maana ya mazingira.
- Kuangazia aina mbalimbali za mazingira.
- Kufafanua umuhimu wa mazingira.
- Kueleza njia mbalimbali za kuhifadhi mazingira.
Mazingira ni hali au mambo yaliyomzunguka kiumbe pale anapoishi kama vile hali ya anga, ardhi, majumba, miti, mito na bahari. Hebu tuone aina mbalimbali za mazingira ambayo huwa yanatuzunguka. Mazingira huwa na manufaa mengi kwetu. Kwa mfano: Maji: Maji ambayo tunapata kutoka kwa mito na maziwa hutumiwa kwa njia nyingi kama vile, kunywa, kufulia nguo, kupikia, kunyunyizia mimea.
Milima na mabonde huweza kuwa vivutio vya watalii na kutupa fedha za kigeni. Vile vile, hutupa mandhari ya kupendeza. Milima pia huvuta mvua. Licha kuwa mazingira yana faida chungu nzima, huharibiwa kwa njia mbalimbali kama vile:
- Moshi kutoka viwandani huchafua hewa.
- Ukataji ovyo wa miti husababisha kuwe jangwa hivyo kukauka kwa mito na maziwa.
- Utupaji ovyo wa taka hufanya mandhari kuwa chafu na kuleta maradhi.
- Kumwaga taka katika mito, maziwa na bahari.
Mazingira yanaweza kuhifadhiwa kwa njia tofauti. Njia hizo ni kama zifuatazo:
- Kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa mazingira ili waweze kuyahifadhi.
- Kupanda miti zaidi.
- Kunadhifisha mazingira.
- Kuwa na sera au sheria ambazo zinatetea uhifadhi wa mazingira.
Umuhimu wa Mazingira
Mazingira huwa na manufaa mengi kwetu. Kwa mfano:
- Maji: Maji ambayo tunapata kutoka kwa mito na maziwa hutumiwa kwa njia nyingi kama vile, kunywa, kufulia nguo, kupikia, kunyunyizia mimea.
- Miti: Miti hutumiwa kwa njia mbalimbali. Miti hutupa chakula, mandhari ya kupendeza, hutupa mvua, hutumiwa kutengenezea dawa na vitu vingine vya matumizi ya nyumbani.
- Milima na mabonde: Milima na mabonde huweza kuwa vivutio vya watalii na kutupa fedha za kigeni. Vile vile, hutupa mandhari ya kupendeza. Milima pia huvuta mvua.
Uharibifu wa Mazingira
Licha kuwa mazingira yana faida chungu nzima, huharibiwa kwa njia mbalimbali kama vile:
- Moshi kutoka viwandani huchafua hewa.
- Ukataji ovyo wa miti husababisha kuwe jangwa hivyo kukauka kwa mito na maziwa.
- Utupaji ovyo wa taka hufanya mandhari kuwa chafu na kuleta maradhi.
- Kumwaga taka katika mito, maziwa na bahari.
Njia za Kuhifadhi Mazingira
Mazingira yanaweza kuhifadhiwa kwa njia tofauti. Njia hizo ni kama zifuatazo:
- Kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa mazingira ili waweze kuyahifadhi.
- Kupanda miti zaidi.
- Kunadhifisha mazingira.
- Kuwa na sera au sheria ambazo zinatetea uhifadhi wa mazingira.
Katiba
Katiba ni sheria au kanuni zilizooanisha namna ambavyo nchi, chama au shirika inavyoendesha shughuli zake. Katiba ya nchi ni sheria inayooanisha misingi ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba hubainisha haki za wananchi. Kidemokrasia, katiba inafaa kubatilishwa baada ya kufanyiwa marekebisho yanayokubalika na wananchi kwa jumla. Nchini Kenya tangu kupata uhuru, tumekuwa tukitumia katiba iliyoundwa zama za wakoloni. Mwaka wa 2010, wananchi walipata fursa ya kubadilisha katiba hiyo na kuchagua iliyobatilishwa ili kuwafaa kupitia kura ya maoni.
Tazama video hii: (Kwa hisani ya KBC channel 1) Katiba mpya nchini Kenya inafafanua haki za kimsingi za wananchi kama vile: haki ya kuishi, usawa na uhuru, usalama wa wananchi, uhuru wa dhamiri na imani ya dini na maoni. Katiba mpya inawapa Wakenya uhuru wa kujieleza. Pia katiba mpya inalinda wanahabari kwa kuwapa uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari. Katiba mpya inaendeleza utamaduni na lugha za kiasili. Haki za wafungwa zinazingatiwa kwa mujibu wa kanuni za kibinadamu, kwa mfano, masilahi ya wafungwa yanazingatiwa na pia wamepewa haki ya kuchagua wawakilishi wa eneo bunge lao.
Raia kwa jumla wanalindwa na katiba katika maswala ya ndoa, jinsia, urithi, ajira na dini ambapo wanawake na wanaume wana haki sawa katika nyanja tatu za maisha, mfano kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Wanasheria hutunga na kujadili sheria za nchi. Sheria ya katiba huhusisha sheria za umma na zile za kibinafsi za wananchi, ilhali sheria za kimataifa hutawala shughuli za kibiashara, vikwazo vya kimazingira na mipaka, ulinzi na kadhalika baina ya nchi na nchi. Katika demokrasia halisi, sheria hutafsiriwa na matawi matatu makuu: mahakama, bunge na serikali ya kuwajibika. Matawi haya ndiyo huunda vyombo vya dola vinavyohakikisha uzingativu wa sheria nchini. Kamati na idara tofauti za bunge na serikali huhakikisha sheria zinazoundwa zinatekelezwa vilivyo.
Katiba mpya inasisitiza haki za watoto kwa kuhakikisha kuwa mtoto anapata kuelimika, kutunzwa vyema na hadhulumiwi. Mtoto haruhusiwi kutengwa na wazazi wake kwa njia yoyote.
Aidha, sheria hutilia mkazo matumizi ya lugha nchini. Katiba mpya inatambua aina tatu za lugha nchini: lugha rasmi, lugha ya taifa na lugha nyingine kama vile za kiasili, ishara na Braille. Ni dhahiri kuwa bunge linajukumu la kujumuisha maoni ya vikundi tofauti vya jamii katika kuimarisha sheria zilizoundwa katika katiba.
Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi, unapaswa kuwa na uwezo wa:
- Kueleza maana ya memo.
- Kufafanua umuhimu wa memo.
- Kupambanua sifa za memo.
- Kuandika memo.
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
- Kueleza maana ya insha ya maelekezo au maagizo.
- Kutaja umuhimu wa insha za maelekezo.
- Kufafanua sifa za insha ya maelekezo.
- Kubainisha aina za maelekezo.
- Kuandika insha ya maelekezo.
Memo
Umeona na kusikia nini? Bila shaka umeona maandishi na kusikia ujumbe maalum wa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu anawaandikia wanafunzi wake. Barua hii imepachikwa ukutani. Barua hii huitwa memo au arifa. Memo ni taarifa fupi ya kiofisi ambayo hutoka kwa mtu mmoja hadi kwa wengine.
Muundo wa Memo
Memo huwa na hatua tano muhimu ambazo lazima zijitokeze:
- Anwani ya shirika hutangulia na huandikwa sehemu ya juu ya karatasi.
- Neno ‘MEMO’ hufuata kwa herufi kubwa na kukolezwa wino.
- Upande wa kushoto chini ya mstari huandikwa utangulizi ufuatao:
- Kwa: sehemu hii huelezea ujumbe unalenga akina nani.
- Kutoka: sehemu hii huonyesha ujumbe umetoka kwa nani.
- Tarehe: sehemu hii huonyesha tarehe memo ilipoandikwa.
- Mintarafu: hapa shabaha ya barua hudokezwa kwa herufi kubwa zilizokolezwa wino.
- Mwili wa memo au maelezo ya mada inayoshughulikiwa huendelezwa.
- Hitimisho la memo hubeba sahihi, jina na cheo cha mwandishi.
Tazama mfano huu:
- Kueleza maana ya barua kwa mhariri.
- Kufafanua ujumbe katika barua kwa mhariri.
- Kueleza sifa za barua kwa mhariri.
- Kutaja umuhimu wa barua kwa mhariri.
Barua kwa mhariri huwa na sifa zaidi ya zile za kimuundo. Baadhi ya sifa hizi ni:
- Huonyesha hisia au mtazamo wa mwandishi.
- Huwa na msimamo mmoja madhubuti.
- Urefu wake hutegemea jambo ambalo linazungumziwa.
- Lugha rasmi hutumiwa.
- Lugha nyepesi ya moja kwa moja isiyohusisha tamathali wala mafumbo.
Barua kwa mhariri zina umuhimu kwa jamii kwa jumla. Huwapa wananchi kujieleza waziwazi. Huangazia mambo muhimu yanayofaa kutekelezwa. Hutumiwa kuwakilisha maoni ya watu kwa viongozi mbalimbali ili kuimarisha au kurekebisha hali ya maisha nchini.
Umuhimu wa Maagizo
- Maagizo huongoza anayefanya jambo kulitekeleza ipasavyo.
- Maagizo hutahadharisha, yanapofuatwa huepushia mtu madhara ambayo yangempata.
- Maagizo hudumisha nidhamu na utendakazi wa jambo fulani.
- Maagizo husaidia kuelewa jinsi kifaa kinavyofanya kazi.
- Maagizo husaidia kulenga na kuhakikisha ubora.
Bila shaka umesikia jinsi maagizo yalivyo muhimu. Je, unaweza kutaja dhima zaidi za maagizo? Sifa za Maagizo
Uandishi wa maagizo
Tazama na kusoma mfano huu wa maagizo.
Maagizo
- Hakikisha simu hii ina vifaa vyote.
- Fungua uchopeke kadi ya simu.
- Chopeka seliumeme pahali pake.
- Weka simu hii kwa stima ipate chaji tosha.
- Betri ikishajaa chaji izibue kutoka kwa umeme.
- Ianzishe kufanya kazi.
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuweza:
- Kueleza maana ya ratiba.
- Kufafanua muundo wa ratiba.
- Kuandika ratiba kwa kufuata muundo sahihi.
Ratiba ni mpangilio wa matukio ya shughuli au hafla fulani kutegemea jinsi yanavyofuatana kiwakati. Kunazo aina kadha za ratiba kulingana na shughuli. Mifano:
Barua kwa Mhariri
Barua kwa mhariri huwa na sifa za kimuundo kama ifuatavyo:
- Anwani mbili ya mwandishi na mwandikiwa ambaye ni mhariri.
- Mtajo, mfano Bw, Mhariri.
- Mada au Kuhusu – sehemu huonyesha kiini cha barua.
- Yaliyomo (mwili) – huhusu ujumbe husika maoni au msimamo wa mwandishi.
- Hitimisho – kimalizio cha heshima. Sehemu hii huonyesha jina la mwandishi na sahihi yake. Pia inaweza kutaja mahali.
Ratiba
Ratiba ni mpangilio wa matukio ya shughuli au hafla fulani kutegemea jinsi yanavyofuatana kiwakati. Kunazo aina kadha za ratiba kulingana na shughuli. Mifano:
- Ratiba ya masomo
- Ratiba ya mashindano
- Ratiba ya sanaa na maonyesho
- Ratiba ya arusi
- Ratiba ya mazishi
Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuweza:
- Kueleza maana ya matangazo.
- Kutaja na kufafanua sifa za aina mbalimbali za matangazo.
- Kufafanua dhima za matangazo.
- Kuandika aina mbalimbali za matangazo ukizingatia kanuni za utungaji.
Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuweza:
- Kueleza maana ya ratiba.
- Kufafanua muundo wa ratiba.
- Kuandika ratiba kwa kufuata muundo sahihi.
- Matangazo ya matukio maalum
- Tangazo la zabuni
- Matangazo ya mikutano
- Matangazo ya matokeo ya mitihani
Mfano wa pili. Ratiba ya vipindi vya mwalimu wa Hesabati na Kemia.
Kufikia mwisho wa kipindi, unatakiwa kuweza:
- Kueleza maana ya juu na ya ndani ya methali yoyote.
- Kuandika kisa kinachoafiki methali uliyopewa.
- Kuandika kwa ufasaha ukizingatia mtiririko ufaao wa hadithi.
Matangazo ya Kazi
Tangazo la Kifo
Tangazo la Biashara
(Kwa hisani ya Safaricom) Baada ya kuangalia au kutazama tangazo hili, umetambua kuwa hili ni tangazo la biashara. Sifa:
- Kuna viambata vya lugha, kwa mfano, picha na nyimbo.
- Lugha ya ushawishi, kwa mfano katika tangazo la Safaricom – nafurahia.
- Majina ya bidhaa na kampuni hutajwa.
- Lugha ya chuku hutumiwa.
- Kuna kusifu bidhaa.
- Kuna matumizi ya sentensi fupi.
Methali
Methali ni fungu la maneno lenye maana maalum. Fungu hili huwa na maana ya juu na ya ndani. Vilevile huwa na sehemu mbili. Insha ya methali hufafanua methali kwa kutumia kisa au hadithi. Kisa hiki hueleza kikamilifu maana ya ndani ya methali.
Maelezo
Hebu sikiliza maelezo zaidi kuhusu uandishi wa insha hii. Kabla ya kuanza kuandika insha ya methali, ni lazima uyazingatie mambo yafuatayo:
- Uelewe maana ya juu na ya ndani ya methali. Kwa mfano, “Jifya moja haliinjiki chungu.” Maana ya ndani ni kuwa mtu pweke hawezi kufanya jambo likamilifu. Watu wakiungana wanaweza kufanya mengi, tena vyema.
- Fikiria kisa kinachoafiki kikamilifu maana ya ndani ya methali.
- Panga utaratibu wa kisa kuanzia mwanzo hadi mwisho.
- Simulia kisa ukitumia msamiati ufaao na mapambo ya lugha ya kuvutia kama vile misemo na methali. Vilevile, zingatia sheria za kisarufi kama uakifishaji na aya.
Sifa za Insha ya Mawazo
Insha ya mawazo hutumia lugha ya mvuto. Huhitaji ubunifu wa hali ya juu na huhusisha wahusika wa kufikirika kuendeleza ujumbe wa mwandishi. Kisa huwa na mawazo ya kuaminika yaliyona uhalisia wa maisha. Insha ya mawazo huzingatia kanuni za sarufi na uwakifishaji wa makala. Msamiati hujikita katika mada husika. Insha hii huonyesha msimamo wa mwandishi na hujikita katika matukio ya kuwazia.

