Share this:

Maswali ya Ufupisho

 

1. Soma taarifa hii kisha ujibu maswali  

Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda walijaribu kusoma wakashindwa mapema kujipandisha kielimu. Ukosaji wa elimu huchangia sana katika kukuza ukata. Elimu huweza mtu kupata tonge kwa kujipatia kazi za kumwezesha kuyakidhi mahitaji ya maisha. Hali kadhalika, elimu humsaidia binadamu kupata maarifa mengi ya kutendea shughuli zake za kimaendeleo. Kwa mfano, kama ni wakulima wanaweza kutumia pembejeo zifaazo ili kuboresha uzalishaji wa mazao. Wakulima wenye elimu hawatapendelea njia duni za kuendeleza kilimo kama vile kutumia visagilima na mbinu nyingine za kijadi. Badala yake watatumia njia za kisasa za kuvunia mazao yao.

Umaskini mwingine huwa mwiba wa kujichoma. Baadhi ya watu ni mikunguni. Kulaza damu kwao kunawafanya kuwa wategemezi katika familia na jamii kwa jumla. Kwa vile hawajazoea kuinamia cha mvunguni, hata wakifunzwa kuchakura hawawezi. Ili kujaribu kuutibu uwele wao na ufukara baadhi yao hutafuta njia za mkato kama vile upwekuzi wa vitu vya wale waliojitahidi. Wakifanikiwa huweza kufurisha vibindo vyao. Hata hivyo mkono mrefu wa walinda usalama ukiwakumbatia wao hubakia kusagika kwa dhiki isiyomithilika ndani ya magereza.

Majanga ya kimaumbile kama vile mitetemeko ya ardhi, mikurupuko ya maradhi hatari, moto, ukame na mafuriko huchangia na kuzidisha umaskini. Matukio hayo yakiandama kidindia watu wengi huhasirika. Licha ya mali nyingi kupotea, manusura huachwa wakiwa maskini hohehahe. Matumizi yao hupotea kwani wengi huhitajika kuanza maisha upya.

Vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile. Endapo watajiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya, wataathirika wao wenyewe na jamii kwa jumla. Pamoja na kuwa vijana hawa hufuja pesa nyingi katika ununuzi wa dawa hizi, dawa zenyewe huwadhoofisha na kuwapoka nguvu za kushiriki katika uzalishaji mali. Kutokana na hali hii,umaskini hupaliliwa na kushamiri zaidi.

Umaskini huzua matatizo mbalimbali katika jamii. Ufukara huchachawiza juhudi za serikali za kuwapa raia wake mahitaji ya kimsingi kama vile huduma za afya. Pia umaskini husababisha maovu mbalimbali ya kijamii kama vile mauaji na ukahaba.

Baadhi ya wanajamii huona kwamba njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na hali ya ulitima ni kupitia kwa biashara haramu. Hali hii huchochea zaidi kudorora kwa maadili ya kijamii.

Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamezua mikakati mahsusi ya kukabiliana na umaskini. Baadhi ya mataifa yamebuni utaratibu maalum wa kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini. Mojawapo ya mipango hiyo ni kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mishahara minono na wafanyibiashara wenye pato kubwa. Aidha huduma za burudani hutozwa kodi ya kiwango cha juu. Kupitia kwa kodi hizo, na njia nyinginezo, serikali za nchi hizo hupata pesa za kuwahudumia maskini.

Mataifa yanayoendelea yanaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mifano ya miradi hiyo ni viwanda vya ‘Jua kali’, ususi wa vikapu na uchongaji wa vinyago. Hali kadhalika, serikali inaweza kuwatafutia masoko ya nje wafanyi biashara wadogo wadogo. Aidha, serikali inaweza  kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa na masoko ya nje wafanyibiashara wa aina hiyo. Mathalan, ushuru unaotozwa nguo kuukuu zinazoingizwa nchini ukipunguzwa, wauzaji wa nguo hizi watafaidika zaidi na hali ya umaskini itaendelea kupungua.

Sehemu za mashambani ni mhimili mkubwa wa uchumi. Ingawa kumekuwa na juhudi za kuzistawisha sehemu hizi kwa kusambaza huduma za umeme na maji kwa gharama nafuu, bado hali haijawa ya kuridhirisha. Ili kuimarisha sehemu hizi na kukabiliana vilivyo na tatizo la umaskini, hatuna budi kusambaza huduma hizi hasa katika sehemu kame. Sehemu hizi zikipata maji, kilimo chenye natija kitaendelezwa na umaskini utakuwa karibu kuzikwa katika kaburi la sahau. Ikiwa tutazitekeleza sehemu hizi, vijana wanaoweza kusistawisha watahamia mjini kutafuta maisha ‘bora’. Hali hii itazidisha msongomano wa watu mjini.

Umaskini ni nduli ambaye lazima aangamizwe ima fa ima. Vijana hawana budi kubadili mtazamo wao hasa kuhusu kazi za mashambani na kujitahidi kuimarisha kilimo. Fauka ya hayo, mifumo mwafaka ya elimu ibuniwe ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya taifa. Badala ya kuhimiza elimu ya kinadharia, elimu tekelezi isisitizwe zaidi ili wale wanaokosa kazi za kiafisi waweze kujiajiri katika kazi za kiufundi. Ukusanyaji wa ushuru uimarishwe zaidi. Hali ya usalama iendelee kustawishwa ili kuzidi kuwavutia wawekezaji, na hivyo kubuni nafasi zaidi za kazi.

 

Maswali

(a)Kulingana na kifungu ‘umasikini ni hali inayoletwa na udhaifu wa mtu binafsi’. Jadili

ecolebooks.com

 (maneno 30-40)

(b)Jamii ina uwezo wa kukabiliana na hali ya umaskini inayowakumba raia wake. Thibitisha

kwa mujibu wa kifungu (maneno 40-50)  

 

2.  MENO YA BINADAMU

Kila mara tunapokula, meno yetu huuma, kutafuna na kusaga chakula tunachokula. Meno yanatuwezesha kukivunja chakula ili kuwezesha mwili wetu kukitumia. Ili mwili uweze kukitumia chakula hicho, pana vitu fulani vinavyokifanyia chakula hicho kazi mpaka kikaweza kuingia kwenye mwili wenyewe. Hivi hujulikana kama vimeng’enya. Binadamu ana meno ya aina nne kuu. Kwanza, kuna meno ya mbele au makato ambayo kazi yake ni kuuma au kukata chakula. Haya yanasaidiana na mengine yanayojulikana kama michonge; yanakata pia lakini yako sehemu ya nyuma. Michonge hufuatwa na meno mengine yanayosaga chakula na ambayo hujulikana kama masagego. Masagego hufanya kazi na meno mengine yajulikanayo kama magego. Kazi ya aina hizi mbili za meno ni kutafuna na kusaga chakula kabisa kabla ya kukimeza. Idadi ya meno ya mtu mzima ni thelathini na mbili. Bila ya kuwa na meno mazuri, binadamu hukabiliwa na matatizo makubwa wakati wa kula. Meno huweza kuharibika kwa sababu ya kutopigwa mswaki vizuri mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa meno yetu ni mazuri, pana umuhimu wa kudumisha afya nzuri ya meno. Kila baada ya kulala, lazima tuhakikishe tumeyapiga mswaki vizuri bila ya papara ili kuondoa mabaki ya chakula yanayoweza kuwa chanzo cha viini vinavyoharibu meno. Pili, lazima tuhakikishe kuwa hatuharibu ufizi wa meno, yaani ile nyama inayoshikilia meno hasa kwa vijiti katikati ya meno baada ya kula. Afya ya meno ni muhimu ili kuhakikisha kuwa meno yetu yanadumu na kuendelea kutufaidi katika uhai wetu.

 

.  (a) Kwa nini ni muhimu kudumisha usafi wa meno?

  (Tumia maneno yasiyozidi 25)

(b) Fupisha taarifa uliyosoma. (Tumia maneno yasiyozidi 80).  

 

3. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanya kwa uagizaji ama uuzaji wa bidhaa za nchi nyingine.

Biashara ya kimataifa ina umuhimu mkubwa. Kwanza, inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi mbali na kusaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali. Uhusiano huu huiwezesha nchi kupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao, hasa ikiwa nchi inayohusika haina malighafi yanayohusika katika utengenezaji wa bidhaa hizo. Pia husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itaauniwa na nchi nyingine ingawa hali kama hii haihakikishwi, ushirikiano huu vile vile huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi.

Kwa sababu za kushughulikia utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma nyingine kutokana na uzoefu wa muda na kuwepo raslimali, nchi huwa na uzoefu fulani. Ni kwa sababu hii nchi inawezeshwa kupata pesa za kigeni na kuuza bidhaa za ziada.

Hata hivyo kuna matatizo yanayozikumba nchi za kiafrika katika biashara hii. Kwanza, biashara ya aina hii hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoendelea kwa ushindani usio sawa. Ajabu ni kwamba nchi zilizoendelea zimetumia bishara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini ama zenye athari kwa hali za kijamii.Urafiki haukosi. Ikiwa nchi inategemea uagizaji wa bidhaa, haitaweza kuikosea ama kuhitilifiana na nchi ambayo inategemea, hivyo kuathiri uhuru wa nchi kama hiyo.

Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeweka mikakati ya kulinda viwanda kutokana na athari ya biashara kama hii. Baadhi zimeweka ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa utoka nje kwa wasio washirika wa kibiashara. Licha ya hayo, baadhi ya bidhaa zinazonuiwa kwa nje kwa matumizi ya kielimu, utafiti wa kisayansi nabidhaa za maonyesho huagizwa bila ushuru huo. Wakati mwingine ni benki kuu ndiyo hutoa leseni kwa niaba ya serikali kama njia ya kudhibiti bidhaa kutoka nje. Njia nyingine ya kuvisaidia viwanda nchini ni kuuza bidhaa kwa njia ya kuvipunguzia ushuru, usafirishaji nafuu na kuvipa ushuru.

Serikali nyingine huhakikisha kuwa ni bidhaa kiasi fulani tu ambazo zinaweza kuagizwa kwa kipindi fulani. Kwa mfano, kuna idadi fulani ya magari kutoka nje yanayoweza kuagizwa kuja Kenya kwa mwaka mmoja. Hata hivyo, wakati mwingine, serikali husitisha uagizaji wa bidhaa kama vile dawa, sinema, maandishi ya kisiasa na vitabu kutoka nje; bidhaa ambazo zinachukuliwa kuwa hatari kwa nchi. Licha ya matatizo haya, biashara imekuwepo na inaendelea kujiimarisha.

 

Maswali

(a) Kwa mujibu wa mwandihsi wa makal haya, bishara ya kimataifa itaendelea kujiimarisha.

  Eleza (al. 6)  (maneno 40-50)

(b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (maneno 40-50)  

 

 

4.  Soma taarifa inayofuata kisha ujibu maswali yaliyoulizwa

Usafiri ni upelekezi wa watu na bidhaa au mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine. Tuseme kutoka kituo A na kuenda kituo B.

Katika ulimwengu wa leo, watu na bidhaa husafirishwa barabarani kwa mabasi au motokaa za kila aina au kwa kutumia magari moshi yanayopita juu ya reli, au meli zinazopita majini, kadhalika, usafiri unaweza kufanyiwa hewani.

Hivyo, hali haikuwa hivyo zamani. Usafiri uliojulikana sana kale ni usafiri kwa miguu. Watu waliposafiri kutoka eneo moja hadi jingine walilazimika kufanya hivyo kwa miguu. Kadhalika, watu waliposafirisha mizigo mizito kutoka eneo moja hadi nyingine, iliwabidi kuibeba mizigo hiyo wao wenyewe. Mpaka leo usafiri huu upo.

Wanyama vilevile walitumiwa kama njia moja ya usafirishaji. Huku Afrika ya mashariki kulitumika wanyama wengine kama vile punda. Punda ni mnyama anayependwa sana kwa sababu anaweza kuenda mwendo mrefu pasipo na kunywa maji. Mpaka leo, mnyama huyo hutumika sana na wamaasai, wagala, warendile na wengine.

Mnyama mwingine aliyetumika sana, na mpaka leo anaendelea kutumika ni ngamia. Ngamia anafaa sana katika usafiri wa jangwani. Kwato za ngamia huweza kusafiri kwa urahisi jangwani ama popote penye mchanga mwingi kwa sababu kwato zake hazizami kwenye mchanga. Isitoshe ngamia wanaweza kwenda mwendo mrefu bila maji au chakula huku wakitegemea mafuta yaliyohifadhiwa kwenye nundu zao.

Katika ulimwengu wa kisasa, binadamu amepiga hatua kubwa sana katika masuala ya usafiri. Baadhi ya maendeleo hayo ni ya kustaajabisha. Kwa mfano, binandamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu anaweza kuruka kwa kutumia vyombo vya angani kwenda kwenye anga za mbali. Katika karne iliyopita binadamu amefika mwezini kwa kutumia vyombo hivyo. Kuna tetesi kwamba sasa anajaribu kuzizuru sayari zilizoko mbali na ardhi.

Ama kwa hakika, usafiri bora in kipimo kimojawapo cha maendeleo ya nchi yoyote katika ulimwengu wa sasa. Bila njia ya kisasa za usafiri, baadhi ya mambo yanayofanyika katika nchi zetu hayangefanyika.

 

 (a) Katika habari hii, punda na ngamia wana sifa gani muhimu zinazowawezesha kutumiwa

kwa usafirishaji? (maneno 30-40)  (ala. 6, 1 mtiririko))

 (b) Kwa mujibu wa taarifa, usafiri wa zamani unatofautiana vipi na ule wa siku hizi?

(maneno 40-50)   (al. 7, 1 mtiririko)

 

5.  Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati ya mioyo yetu uweze kupata ufanisi na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa”. Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo chini mwetu yametuzonga. Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu.Tunahitaji taifa la watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wake. Wengi ni wale wenye mawazo kwamba lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wageni .

Mafunzo tunayopata nyumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya mwana Kenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu wazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, “Utengano ni uvundo”. Lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu ,wakati tunapokosea na kufanya masahihisho mara moja kwani, :Usipoziba ufa, utajenga ukuta. “Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi.

Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashtumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na nyumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo, amani na upendo; lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo. Tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo, basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kwa utajiri wake. Kwa hivyo basi, tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba au ya utajiri.

 

 a) Dokeza mambo muhimu yaliyomo katika aya ya kwanza. (Maneno 65 – 70)    

b) Fupisha aya ya mwisho kwa kuzingatia mambo muhimu yanayowapasa vijana kufanya

(Maneno (maneno 35 – 45)

 

6. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:

Usawa wa wanadamu upo kimaumbile – maumbile ya mtu kamwe hayatakosewa na yale ya mnyama wa mwituni. Lakini fikira, tabia, kimo, uwezo na mahitaji huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mintarafu hii yapasa wakufunzi na wazazi kuwapa watoto wao widhaa mapema ili wachague kwa wakati unaofaa kazi watakayoifanya maishani.

Watoto wanapopelekwa chuoni, wazazi wao huukilia kuwasomesha hadi kiwango fulani cha masomo kisha wajitafutie kazi ambayo itawapa masurufu na pesa za shughuli zingine maishani.

Katika nchi yetu tangu tupate uhuru mtindo wa kutoa kazi umekuwa ni ule wa kuchukua watu waliofaulu mitihani ya viwango fulani na kuwapa kazi moja kwa moja. Mwenendo huu wa kuajiri watu kazi umeendelea muda mrefu lakini sasa yamkinika utasitishwa na njia mpya kufuatwa. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa nafasi za kazi zimekuwa finyu sana. Kabla na punde baada ya uhuru nafasi hizo zilipatikana kila mahali. Nyingi ya hizo ziliachwa wazi na wageni walioihama nchi hii tulipojitawala. Siku hizi wanafunzi wanaokomea darasa la saba, kidato cha pili na hata cha nne huwa hawazioni ahadi za kupata kazi za madaraka fauka ya kazi yoyote. Wanaoiona tabasamu ya kazi mbele yao ni wale wanaotasawari masomoni wakifuata taaluma fulani.

Tatizo la kazi laeleweka vema kwa serikali na ni kwa ajili hii serikali imemtasulia kila mwananchi kuwa wakati wa kuania kazi za utanashati umetimiuka. Wakati uliopo ni wakati wa kujifunga vibwebwe kisaki na kuchapa kazi zile ambazo hadi sasa zafikiriwa kazi chafu na zisizofaa wasomi. Dhana kama hiyo ni ya kibwanyenye, na ubwanyenye hauji ila kwa sulubu. Usemapo kuna kazi nzuri na mbaya huwa unazusha maswali mengi. Utatakiwa ueleze kinaganaga kazi nzuri au mbaya kwa nini? Kazi huwa nzuri kwa upande wa tija au kwa upande wa wepesi wake? Kujibu maswali ya namna hii kutahitaji wekevu mwingi, waima mtesi ataonekana dufu.

Zipo kazi aina mbili. Ipo kazi ya kuajiriwa na ya kujiajiri. Kazi ya kujiajiri kwa kulinganishwa huonekana ngumu na yenye matatizo mengi mwanzoni. Lakini itakubalika pato lake ni kubwa zaidi ikishapata msingi imara. Msingi imara huwekwa kwa juhudi za mwanzoni zikiambatana na ujasiri. Mtu asiyejasiri kutenda tendo lolote maishani ni sawa na yule asiyejua atokako na kule aendako; yuaishi kungozwa. Ardhi ni thawabu, tena thawabu tunu. Ukiwa na kipande cha ardhi ifaayo kwa kilimo ufakiri ukikutawala ni wewe mwenyewe kupenda: la sivyo ufa umo ubongoni unaohitaji bwana mganga

 

 

 (a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza

na ya pili. maneno 60-70)  (b)  Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho. Eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na

mwandishi. (maneno (50-60)

 

 

7. Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata:-

Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, redio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki.

Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasilianao kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundisha. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Hali kadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.

Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.

Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.

Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.

Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa wanafamilia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.

Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalan, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.

Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaoutumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.

Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.

Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya waelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.

Maswali

(a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga

 (b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80

 

8. Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha

huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa

namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.

Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.

Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.

Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.

Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.

Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.

Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya

kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura

ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.

Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.

Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.

Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.

 

Maswali:

 1. Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa

kukumbuka.  

 b)  Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90  

 

9. Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

Faragha ni muhimu kwa binadamu kwani huwa ndio wakati ambapo mtu atakuwa akitulia pekee mahali na huku akijiuliza ni mema mangapi ameyatenda siku hiyo, maovu mangapi ameyafanya, na kama siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la.

Si binadamu wote ambalo wanapendelea kutumia wakati wao wa faragha kwa kupiga domo, nyumbani, kustawisha mabustani yao ya maua au mimea, au hata kuchukua kitabu au magazeti ya kusoma na kujifunza. Watu kama hawa huwa na fikira na mawazo mbalimbali juu ya umuhimu wa thamani ya wakati wa faragha. Watu kama hao utawakuta wakikusanyika katika makundi kwa matarajio ya kujinufaisha kwa mapato fulani au kujiingiza katika upigaji wa kamari. Wengine hunufaika wakasifu mafanikio yao ya siku ya mkusanyiko na baadhi yao ambapo hufanya mhanga wa michezo hii huibuka huku wakilaani na kuapiza bahati zao mbaya.

Kuna kundi jingine ambao hustahabu vilabu vya usiku kwa kujiliwaza au kujitumbuiza ili wapate kujituliza mawazo yao, wakayatafuta makali na kileo. Mwanzo wa ushirika kama huu huwa mzuri, watu huongea na kutoleana mawaidha yenye muafaka kiungwana kabisa. Lakini mara tu baada ya kuyakata makali haya kwa muda hivi, washiriki wake hupumbazwa na huanza kuyakata matindi mithili ya komba mpaka kiasi cha kubwata maneno ovyo ovyo na hatimaye kupoteza mbali fahamu. Ndipo kuruka kwa akili na kuanza zahama zenye kuonyesha utoto badala ya utu uzima. Kadiri makali hayo yanavyosiliwa kwa kuiva kwake, ndivyo wafuasi na mashabiki wake huyatumia kwa wingi na hata kuyaabudu, huyaabufu; huyabugia bila kujali uzito.

Na iwapo ndio kwanza wapokee mabunda yao, hakuna la kutia kikomo tafrija hizo ila uzito wa matendo ya ubadhirifu hujitokeza baada ya kurudi nyumbani, kulala fofofo na wazindukanapo siku ya pili yake ndipo wagundue walivyo taabani.

Mtindo wa matumizi ya faragha hutokea tangu mwanzo wa mazingira ya mtu; hivyo tangu utoto wake; tabia njema na zipasazo huhitajiwa kufunzwa. Sehemu kubwa ya mafunzo haya muhimu hutokana na malezi ya nyumbani chini ya uongozi wa mama na baba. Kama wasemavyo wahenga, mtoto akuavyo ndivyo alivyolelewa. Na mama mtu awe nyoka, hapana budi kuwa mwanawe naye atainuka kustahabu unyoke” wa mama yake. Hivyo ni wajibu wa wazazi kujenga mazingira yanayofaa kwa vizazi vya kesho kwa kuelekezwa namna yake. Ingewezekana himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha manufaa yake. Ingewezekana, himizo kubwa lingesisitizwa katika marekebisho ya tabia za wazazi kuwezesha watoto kuiga mtindo au mitindo ya maisha yanayofaa. Kielezo chema ni kuwa na mzazi mwenye tabia njema kwa mtoto wake, rafiki zake na kwa jamii yake.

 

 (a) Ni nini umuhimu wa faragha kwa binadamu kwa mujibu wa aya ya kwanza?(maneno 20)

  (b) Eleza jinsi watu wengine wanavyoharibu wakati wao wa faragha kwamambo ya upotovu

kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu    (maneno 30) (al. 5 al. 1ya utiriko)

 (c) Eleza mchango wa mzazi kwa mwanwe kuhusu matumizi bora ya wakati wa faragha.

Zingatia aya ya mwisho

 

10. Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kulingana na maagizo

Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa katika maeneo mbali mbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini.

Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo. Imesahaulika kuwa karibu asilimia sabini na tano ya wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia huletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao katika mataifa ya nje.

Wataalamu wa maswala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linalotokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja.

Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo. Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maeneo haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa.

Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia kilimo ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo kuhusu mihimili ya zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.

Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na lingine bali kukimbilia mataifa yaliyostawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa.

 

(a) Fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 50 -55)  b) Bila kubadili maana, fupisha aya mbili za mwisho (Maneno 55-60)

Utiririko ni alama 3

 

11.   Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Kwa hali nyingine , tunaweza kusema kuwa uchafuzi wa mazingira ni uharibifu wa vile

vitu vinavyowazunguka binadamu na wanyama maishani mwao. Kuna uchafuzi wa aina mbalimbali na kila uchafuzi humhusu binadamu kwa njia fulani.

Maendeleo ya viwanda duniani ni sababu mojawapo ya uchafuzi wa hewa. Mitambo katika karakana huwa inatoa moshi mwingi wakati bidhaa zinapotengenezwa. Moshi husambaa eneo kubwa na kuchanganyika na hewa inayovutwa na binadamu. Uchafu hutupwa ovyo ovyo na kuwa hatari kwa afya ya binadamu. Maji machafu huweza kutiririkia mtoni, maziwani na hata baharini. Yale yanayotiririka mitoni na maziwani huchafua maji ambayo hutumiwa na watu wa eneo hilo kwa kunywa, kupika na kunywesha mifugo wao. Yale yanayotiririka baharini huwa ni hatari kwa samaki wanaotegemewa na binadamu kuwa kitoweo muruwa.

Ongezeko la watu pia ni hali nyingine ya uchafuzi wa mazingira. Halaiki ya watu hufanya

uharibifu wa misitu ya asili. Hii ni kwa sababu ya kutaka kuongeza ekari za mashamba. Hili husababisha mmomonyoko wa udongo ; hivyo basi kuiacha ardhi bila rutuba yoyote. Katika hali hii, kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa nchi nyingi duniani huzoroteshwa. ”Maisha ya binadamu hutegemea kilimo kwa kila hali kwa hivyo kilimo kinapozoroteka hata uchumi nao huathirika. Kila uchao tunasikia kwamba nchi fulani imekabiliwa na njaa.

Ufugaji wa wanyama wengi bila mpango maalum pia huharibu mazingira ya asili kama nyasi na vichaka. Watu wengi hufuga ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kwa kuwa hawana mahali maalum pa kuwalisha, huzunguka nao huku na huko kutafuta nyasi na majani ya kuwalisha. Wanyama wanaotangishwatangishwa namna hiyo humaliza majani na nyasi zote na kuacha ardhi tupu ambayo hatimaye huyabisika kwa jua. Ardhi ya namna hii haishiki maji mvua inyeshapo. Nchi iliyoneemeka huweza kuwa jangwa lililo na chungu ya mchanga.

Watu wanapoongezeka huko mashambani huwabidi wakate misitu ili waanzishe maskani mapyapamoja na mashamba yao. Miti hukatwa bila hadhari na mabiwi ya matawi pamoja na majani huchomwa moto. Jambo la kusikitisha ni kwamba miti hiyo inapokatwa hakuna mingine inayopandwa kuchukua mahali pake.

Mahitaji ya binadamu ya kuendeleza njia za mawasiliano pia huzusha balaa nyingine. Barabara zinazidi kuongezeka na pia watu wanaozidi kuongezeka pamoja na mazao yao. Kwanza, barabara zinapotengenezwa misitu hukatwa mahali zinapopitia. Pili, wingi wa magari huzidi na baadhi ya hayo hutoa moshi unaoharibu hewa.

Njia kadha wa kadha za kuzuia uharibifu wa mazingira zimependekezwa. Ingawa suluhisho timamuhalijafikiwa, Serikali nyingi duniani zimo katika harakati za kutafuta suluhisho la uchafuzi huo.

Njia mojawapo ni kukomesha ujenzi wa viwanda katika miji mikuu na mahali palipo na watu wengi.Wenye viwanda pia wanahimizwa kufikiria jinsi ya kutupa takataka na maji machafu bila kudhuru afya ya binadamu.

Watu wakizingatia suala la upangaji wa uzazi na kuwa na familia ndogo ndogo, idadi ya watu haitaongezeka kwa kasi kwa hivyo itakuwa hakuna haja ya kuanzisha makao mapya mara kwa mara.

Serikali nyingi zimechukua jukumu la kuwaelimisha raia juu ya madhara yanayotokana na uharibifuwa mazingira. Raia wanahimizwa kupanda miti kwa wingi.

Jitihada zinazofanywa kuzuia uchafuzi wa mazingira hukumbana na matatizo. Tatizo kubwa ni fedha za kuendeleza miradi inayopendekezwa. Shida nyingine ni kwamba juhudi zingine huwa zinamwingilia binadamu na mali yake.

 


Maswali.

(a)  Fupisha aya za kwanza sita za taarifa uliyosoma (maneno 50-60)

(b)  Fupisha aya za mwisho tano kwa maneno 40-45

 

12. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Vijana wa siku hizi hujifikiria kuwa wao ni bora kuliko wazee wao. Wao hujifikiria kuwa wameelimika zaidi, wana busara zaidi, wanauelewa ulimwengu vizuri zaidi na wanaweza kujiamulia hatima yao bila uongozi wa wazazi wao. Wazee kwa upande wao, hawakubali kabisa madai ya aina hiyo. Kwao ni maasi tu. Wanachojua wazee kwa hakika ni kuwa vijana wa siku hizi hawaajibiki kwa lolote, wamedekezwa mno na wanapenda sana nafsi zao. Kwa sababu hiyo, vijana wanahitaji uongozi na ushauri wa wazeee.

Je, kuishi kwingi ni kuona mengi? Ingawa wazee wanafikiria wanajua mengi kwa sababu ya umri wao, vijana hupenda sana kukosoa fikira za wazee wao. Hawakubali imani na itikadi za wazee wao. Kwa mfano; vijana hupendelea mitindo ya mywele ambayo wazee wao hufikiria kuwa kichaa tu.

Wazee husifiwa sana enzi zao. Husifia jinsi walivyolelewa kwa kuchapwa na kufanyishwa kazi zinazohitaji uvumilivu mkubwa kama vile kuchanja kuni, kufyeka misitu, kutayarisha mashamba, kuwinda na kadhalika. Kwa sababu ya malezi hayo, wazee husema wao walirithi nidhamu nzuri na ushujaa. Vijabna kwa upande wao hawaoni chochote cha kujivunia katika zama za wazee wao; wao hufikiria kuwa wazee wao walilelewa kwa ukatili kwa sababu zama zao zilikuwa enzi za giza, kabla ya majilio ya uungwana na ustaarabu wa kisasa.

Wazee husifia kuwakumbusha vijana ule msemo mashuhuri wa wahenga usemao kuwa ‘mwacha mila ni mtumwa.’ Kwa maoni ya wazee, vijana wengi wamekuwa watumwa kwa sababu wao huonyesha kwa vitendo kuwa hawadhamini desturi za wazee wao. Ka mfano; vijana hawafuati miiko ya jadi, hawapendi kuhudhuria sherehe za kienyeji, kwa mfano sherehe za kutoa makafara. Vijana pia hawapendi ngoma za kitamaduni, na isitoshe vijana hawazionei fahari koo zao. Vijana hawakubali kuwa wao ni watumwa wa mtu yeyote. Mila wanazosifia wazeee wao si vitu vyenye umuhimu wowote kwa vijana. Kwa mfano; baadhi ya miiko ni kisayansi. Kuhusu ukoo, si vijana wengi wanaona umuhimu wake. Ukoo na kabila zilikuwa muhimu zamani wakati ambapo kulikuwa hakuna serikali, bima na hata kazi ya mtu binafsi. Mambo haya sasa ni kama masalia ya zamani ambayo yamepitwa na wakati.

Je, vijana hupenda sana burudani na anasa tu kama wanavyodai wazee! Wazee wengi hufikiria kuwa vijana hupoteza muda wao mwingi kujitafutia anasa na burudani kwa mfano vijana wengi hurandaranda barabarani au mitaani wakisingizia kupunga hewa. Wengine huenda sinema na kuhudhuria dansi na karamu zisizo na manufaa. Vijana kwa upande wao hawaoni kinachowawasha wazee wao; pilipili wasioila yawashia nini?

 

1. Katika makala haya wazee wana malalamiko yapi kuhusu vijana?  (maneno 50-60)

2. Msemo unaosema “Mwacha mila ni mtumwa” unathibitishwa vipi katika maoni ya wazee

katika makala haya?  (maneno 15- 25)

 

13. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na mpangilio wa jamii huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa, au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilia na udhibiti wa serikali.

Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mtaji kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfano wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu. Kwa mfano, inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu.

Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo adhibiti wa kiserikali ni lazima. Hii hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.

 

(a) Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii.  

  (maneno 25-30)  (al. 5, 1mtiririko)

 (b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu.

  (maneno 70-75) (al. 10,3 za mtiririko)

 

14. WAJIBU

Sisi vijana ni wa taifa. Hatuna budi kutumikia umma kwa moyo wetu wote.Hakuna haja ya kulaza damu ikiwa taifa linatuhitaji. Ni lazima tuwe shupavu kwa mambo yote. Tuwe wenye busara, adabu njema na ari ya kutenda kazi kwa moyo wa utu. Ni muhimu kabisa kulinda, kutumikia na kuendeleza taifa hili changa katika mbinu zake na mipango yake yote kuhusu zaraa, elimu, uchumi, ulinzi na mipango yote ya maendeleo ya ustawi wa nchi na jamii. Inatupasa tuelewe ujamaa wetu na jinsi ya kupambana na ubepari, ukabila, ukupe, unyonyaji na ukoloni mamboleo. Hii itaondoa kabisa jasho letu. Inatubidi sisi vijana tujifunze jinsi na namna ya kuwa watu bora.

Elimu tuipatayo kutoka nyumbani, shuleni na katika jamii, lazima igeuze fikira zetu. Elimu hiyo lazima tuitumie ili itupatie uwezo wa kuelewa mema na mabaya maishani mwetu. Ni bora tujue wajibu wetu katika kufikiri, kusema na hata kutenda kufuatana na wajibu huo kwa mioyo na dhamiri safi. Tuwe vielezo kwa wengine. Hasa tujitayarishe kuwa wazazi na viongozi bora wa kesho. Mno mno tuwe wazalendo na raia wema wa taifa hili changa. Tuhimize na kuendeleza utamaduni wetu wa lugha yetu ya taifa. Hatimaye tutambue usawa wa kila binadamu, popote alipo bila kujali taifa, kabila, rangi na hata dhehebu yake.

Tujifunze kujishutumu. Pia tukubali kusahihishwa makosa yetu na watu wengine. Hasa tuwe nguzo, kinga na ngao ya nchi yetu inapopigwa adharusi.

Acha nirudie kusema tena kuwa ni shabaha yetu sisi vijana kuwa na nidhamu njema. Nidhamu njema ni chanzo cha asili cha siha ya ujamaa na kujitegemea. Kwa hivyo, uongozi bora na bidii, ushirikiano mzuri na kujishughulisha. Uchaguzi bora wa viongozi na mifano mizuri ni kurunzi ya maendeleo ya ustawi wetu.

 

 (i) Ni nguzo zipi ambazo kifungu hiki kimezipa kipaombele kwamba zitasimamisha ustawi

na maendeleo ya nchi kutokana na vijana? Jadili kwa maneno thelathini

(ii) Vijana wameshauriwa wafanye mambo mengi mema. Jadili kinyume cha ushauri huu

ukitumia maneno yako mwenyewe

 

Majibu ya Ufupisho

1.   (a)  

 • Ukosefu wa elimu
 • Kulaza damu/ uzembe
 • Ufuaji
 • Umaskini pia huletwa na majanga ya kimaumbile  Kama vile:-
  • Mitetemeko ya ardhi
  • Maradhi hatari
  • Moto  
  • Ukame  
  • Mafuriko

b) – Kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini

 • Kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mshahara mnono na wafanya biashara

wenye pato kubwa

 • Huduma za burudani kutozwa kodi ya kiwango cha juu
 • Elimu tekelezi isisitizwe
 • Kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa
 • Kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo
 • Kusambaza huduma za umeme na maji sehemu za mashambani  

Utiririko

TAZAMA

 1. Kwa kila kosa la sarufi mtahiniwa huadhibiwa ½ alama hadi jumla ya makosa 10  
 2. Kwa kila kosa la tahajia mtahiniwa huadhibiwa ½ alama hadi jumla ya makosa 6  
 3. Kwa kila ziada ya maneno kumi, mtahiniwa huadhibiwa alama 1 na kwa kila mengine matano –huadhibiwa ½ alama

 

2.   a) – Kuzuia uharibifu

Kuhakikisha meno yetu ni mazuri

Kuhakikisha meno yetu yanadumu na kuendelea kutufaidi  

 • Kuondoa mabaki ya chakula ambayo ni chanzo cha viini   zozote 4×1=4 Mtiririko 1×1=1  

 

b)  Tunapokula meno yetu huvunja chakula

Vimegenye hukifanyia chakula kazi  

Meno ya binadamu ni ya meno nne  

Kazi ya meno ni kutafuna na kusaga chakula

Idadi ya meno ya mtu mzima ni 32  

Ni vyema kudumisha afya nzuri ya meno

Lazima tuyapige mswaki meno ili koundoa mabaki ya chakula

Tuhakikishe kuwa hatuaharibu ufizi wa meno

Afya ya meno ni muhimu ili kuhakikisha kuwa meno yetu yanadumu na kuendelea

kutufaidi katika uhai wetu  zozote 8×1=8 Mtiririko 2=2 Jumla =10

3.   Ufupisho

a) Inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi

 • Husaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali
 • Nchi hupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao
 • Husaidia wakati nchi imekumbwa na dharura au majanga kwani itasaidiwa na nchi nyingine
 • Huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi
 • Nchi inawezesha kupata pesa za kigeni na kuuza bigdhaa za ziada  (6×1=al.6)

 

b) Kuna matatizo yanayozikumbuka nchi za kiafrika katika biashara hii

 • Hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoedelea kwa ushindani usio sawa huku nchi zilizoendelea zikitumia biashara hii ‘kutupa’ bidhaa za hali ya chini
 • Nchi zinaweka mikakati ya kulinda viwanda vichanga
 • Kuwekwa kwa ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa
 • Kupunguzia viwango vyao ushuru
 • Kuvipa viwanda vyao mikopo
 • Kuhakikisha usafirishaji nafuu wa bidhaa kwa viwanda vyao
 • Kuweka viwango vya bidhaaa zinazoweza kuagizwa kutoka nje kwa kipindi Fulani (6×1=ala.6)

4.  (a) -Punda na ngamia wanaweza kwenda mwendo mrefu bila kunywa maji.

– Ngamia naye ana kwato nzuri zinazomwezesha kusafiri kwa urahisi jangwani

– Ngamia anaweza kwenda mwendo mrefu bila chakula

(b) –Zamani watu walisafiri kwa miguu, watu hao pia walitumia wanyama kusafiria.  

– Kinyume na ilivyokuwa zamani, usafiri kwa motokaa, gari la moshi na hata ndege.

– Biandamu leo amepiga hatua kubwa kwani anaweza kuruka kwa ndege na kwenda

anga za mbali  (3×2=al.6) (utiririko al.2)

5. a)

 • Inapasa vijana wa Kenya kufanya kazi kwa bidii ili kupata ufanisi na kuinua nchi yetu
 • Sharti tutilie maanani elimu ya vijana, watu wazima, kilimo uchumi na amani katika nchi yetu
 • Bila elimu itakuwa vigumu kutekeleza mipango ya maendeleo
 • Lazima tuzidishe mazao mashambani kwani idadi ya watu inaongezeka  
 • Pia tujishughulishe na biashara kwani wengi wana mawazo kuwa lazima kila mtu aajiriwe
 • Tujitahidi kuweka uchumi kwa mikono ya wananchi badala ya kuwaachia wageni

8X1 = 8 utiririko 2

b) Lazima vijana wayashughulikie na kutatua matatizo yanchi.

– Vijana wawe na nidhamu shuleni na nyumbani

Wawe na ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendelo  

– Wachague viongozi watakaoleta ufanisi , sio wale wanaotoka kwa nasaba kubwa au ya utajiri  4×1 = 4 utiririko 1

 1. 08
 2. 04

03  

6. A. Binadamu ni sawa kimaumbile ukilinganisha na wanyama

Binadamu hutofautiana kwa fikra, tabia kimo, uwezo na mahitaji.

Wakufunzi na wazazi wawape wanao widhaa mapema ili wachague kazi watakayoifanya

Wazazi huwasomesha watoto ili wajitafutie kazi itakayowapa pesa za shughuli

Tangu uhuru watu wa wakiajiriwa kulingna na viwango vya masomo

Kazi zilikuwepo wakati wa uhuru ziliwachwa na wageni walioacha nchini

Siku hizi wanafunzi wanaokomea viwango vya chini hadi kidato cha nne hawapati kazi au kupata za madarakawanaotawasiri masomoni wakifuata taaluma fulani ndiyo hupata kazi  

Hoja zozote 9×1=al. 9) Mtiriko (al. 2)

B.  

– Serikali imewatusilia wananchi kuwa wakati wa kuania kazi za utanashati

umekamilika

– Huu ni wakati wa kufanya kazi yoyote kwani uchaguzi wa kazi kimasomo ni dhana ya

  kibwanyenye ambayo haipo.

– Usemapo kuna kazi nzuri au mbaya unaanzisha maswali mengi  

– Kuna kazi ya kuajiriwa na ya kuajiri

– Ijapo kazi ya kujiajiri ni ngumu na ina matatizo mwanzoni, pato lake ni kubwa, ukishapata

msingi imara.  

– Ujasiri wahitajika ili kujenga msingi imara  

– Ardhi ni thawabu tunu kwani matumizi mazuri ya ardhi yataondoa umaskini

(Kila hoja alama 1×7 = al.7  Mtiririko ala. 2)

Namna ya kutuzwa

makosa ya sarufi (s)

Ondoa nusu alama (½) kwa kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza hadi makosa 10 yaani jumla alama 5

Makosa ya hijai (h)

Ondoa nusus alama (½) kwa kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza, hadi makosa 6 yaani alama 3

Idadi ya maneno Akiandika chiini ya idadi iliyopewa amejiadhibu mwenyewe kwa hoja chache

Akizidisha kwa maneno kumi (10) ya mwanzo uondolewe alama 1 (moja), kila matano yanayofuatana aondolewe alama moja moja (1).

Akiorodhesha tu hoja asipewe alamaza mtiririko

 

7.  (a)   – Ni nyenzo mwafaka ya kufundishia.

– Huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani kote

– Huauni katika kukuza stadi ya kujifundisha au kujielimisha

– Hutumbuiza na kuchangamsha

– Hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii

(b) – Hujumuisha ujumbe usio na maadili kama matumizi ya mabavu, ngono za kiholela, lugha chafu .

-Kuwafanya vijana kuingilia ulevi na afyuni na kuvaa vibaya

-Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano

bora miongoni mwa familia.

-Mawasiliano yakikosa, familia hutengana.

-Haichangii uhusiano bora

-Hukuza ubinafsi

-Huendeleza hulka ya kuhadaa na mengine mabaya

 

8.  a) Vyakula vyenye vitamini B, vyenye amino asidi na vile vyenye madini ya chuma kuimarisha

uwezo wa kukumbuka.

 • Vyakula vyenye glukosi husaidia kuendesha viungu vya mwili na ubongo. Lakini mtu anatakiwa kutahadhari asizidishe kiwango cha sukari mwilini, kwani kinaweza kuthiri uwezo huu.
 • Ni muhimi kutotumia vileo na vyakula vyenye nikotini kwani huzorotesha uwezo wa kukumbuka (Kila hoja na maelezo al. 2 na mbili za mtiririko).

b) Ni muhimu kuepuka woga na kuvurugika akili kulikozidi haya huathiri uwezo wa kukumbuka.

Halikadhalika, lazima mtu awe na ratiba kuonyesha viungo. Hili ni kwa kuwa unyooshaji wa viungo huimarisha ubongo pamoja na uwezo huu. Uimarishaji wa uweza huu ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na unahitaji mchango wa kila mmoja kila wakati.

 

9.  (a) – Ndio wakati mtu anaulia peke yake  

  -Anajisakaknakijiuliza mema mangapi amyatenda siku hiyo  

  – Maovu mangapi amayatenda

_ Iwapo siku hiyo ilikuwa ya manufaa au la(Hoja 4×1=al. 4) – (al. 1 ya utiririko)  

(b) – Hukusanyika katika makundi na kucheza kamari

– Hukusanyika kwa madhumuni ya kupiga gumzo

– Wengine huenda vilabuni kujiliwaza na kujiburudisha kwa vileso (hoja 3×2=al.6)  

c) – Wazazi watoe maongozi bora

– Wawe vielelezo bora kwa wana wao  (hoja 2 x 1= al. 2) (al. 1 aya utiririko)  

Image From EcoleBooks.com

 

 

 

 

10.   Mwongozo wa kusahihsisha muhtasari

(a)Ili kujiondoa kutoka umaskini ni lazima tuthamini kilimo/tukipe kilimo umuhimu

 • Mamilioni ya wakenya/zaidi ya wakenya milioni kumi wanaweza kufa njaa/kwa sababu ya njaa
 • Sababu ya njaa ni kupuuzwa kwa kilimo
 • Wakenya asilimia sabini na tano hutegemea kilimo kwa chakula na fedha
 • Kilimo hutoa nafasi za kazi
 • Huletea serikali robo ya mapato yake (kila hoja al. 1 x 6 = 6)

.   (b) Serikali za Afrika na wanaopanga masuala ya uchumi kujitahidi ili kumaliza njaa na umaskini

 • Wafunze wakulima wa mashamba madogo kukuza na kuzalisha matunda na mboga na kufuga wanyama na ndege
 • Kuanzisha nafasi za kazi
 • Serikali kufadhili kilimo
 • Kupunguza gharama za pembejeo
 • Kuweka sera zinazodhibiti kilimo
 • Kuongeza sehemu ya bajeti ya kilimo
 • Tusipofanya hivyo tatuzidi kuomba misaada kutoka mataifa  (al 6- kila hoja moja 1×6=al 6)

Image From EcoleBooks.com

 

 

 

Makosa ya sarufi; Kila kosa linapojitokeza, huadhibiwa kwa kuondoa ½ alama hadi makosa 6 x ½ = alama 3. Mtahiniwa akipata 0 makosa ya sarufi huondolewa.

 • Makosa ya hijai/tahajia huondolewa hadi makosa 6 x ½ = ala. 03
 • Mtahiniwa akizidisha kwa maneno 10 aondolewe alama 1, baadaye akizidisha kwa 5 ondoa ½
 • Mwanafunzi asipotiririsha kazi yake asituzwe alama za utiririko hasa akiorodhesha hoja au aandike vistari kabla ya hoja, atuzwe 0 katika sehemu ya utiririko.

 

11 .   (i)Viwanda hutoa moshi unaosambaa na kuchafuka hewa.  

(ii)Uchafu unaotupwa ovyo huhatarisha afya ya binadamu  

(iii)Maji machafu huchafua maji mitoni,maziwani na baharini

(iv)Wanyama wengi huharibu misitu,nyasi na vichaka

  (v)Barabara zaidi zinapojengwa miti hukatwa zinapopitia  

(vi)Magari hutoa moshi unaoharibuhewa

(vii) Ongezeko la watu huharibu misitu ya asili kwa kujiongezea ardhi ya makaazi

 

(b) (i) Kukomesha ujenzi wa viwanda mijini penye watu wengi  

  (ii) Takataka na maji taka kutupwa bila kudhuru afya ya binadamu

(iii)Upangaji wa uzazi usisitizwe kuzuia ongezeko la watu  

(iv) Raia waelimishwe kuhusu madhara ya uharibifu wa mazingira

(v)Wahimizwe kupanda miti mingi  utiririko alalma 3 jumla (alama 5)  

 

12.   (i) Hoja muhimu

– Vijana ni waasi na hawawajibiki vyovyote

– Vijana wamependekezwa na wana ubinafsi sana

– Vijana wamekataa uongozi wa wazee na wamepuuza imani na itikadi zao. Mfano; wanaoweka

nywele Kama za wendawazimu.

– Wanawaona vijana kama wavivu na wasio na nidhamu

– Vijana hupenda kuzurura ovyo ovyo.

– Vijana wanapenda anasa na raha za dunia

 

.- Hoja muhimu

– Huwafuati utamaduni wa kutii wazazi wao

– Hawafanyi kazi na kuonyesha nidhamu

– Vijana hawathamini sherehe za jadi kama kutoa kafara

– Hawajinasibishi na watu na koo au tamaduni zao wala ngoma zao badala yake wanapenda kuhudhuria

dansi na sinema za kileo pamoja na karamu.

 

13.  a) Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo shughuli zote za kiuchumi ghairi zile

za lazima kwa serikali huwa huria kwa watu binafsi

 b)

 1. Soko huru huwawezesha watu hatima yao
 2. Swala ibuka ni kule kuwekwa mipaka bainifu baina ya shughuli za kijekali na zile zinazoachwa huria kwa watu binafsi
 3. Haki za kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi haziwezi kuachiwa mtu binafsi
 4. Huduma za kimsingi za afya haziwezi kubinafsishwa
 5. Huduma hizo zikiachwa huru zitaishia kuwa istihaki ya watu wa kipato cha juu
 6. Udhibiti wa serikali hutokea kuyalinda mazingira dhidi ya uchafuzi
 7. Pia udhibiti huo hutokea kulinda haki za watu binafsi

 

14  1.- Kutumikia taifa kwa moyo wetu wote

– Tuwe shupavu, wenye busara, adabu njema na ari ya kutenda kazi

– Ni muhimu kulinda, kutumika na kuendeleza taifa

– Inatupasa tuelewe ujamaa wetu na jinsi ya kupambana na ukoloni mamboleo

– Tutumie elimu kuelewa meme na mabaya maishani mwetu

– Tutambue usawa wa kibinadamu

 

2.

 – Ni staha vijana wetu kukosa nidhamu

 – Wasitumikie taifa kwa mioyo yao yote

 – wasiwe shupavu na wenye busara na ari ya kutenda kazi

 – Pasiwepo ujamaa na jinsi ya kupambana na ukoloni mamboleo

 – Tusiweze kutambua usawa wa kibinadamu

 – Pawepo na uongozi nbaya, kutokuwa na bidii, ushirikiano na kutofuata sheria katika

uchaguzi wa viongozi (tazama makosa ya hijai/ sarufu. Adhibu ½ )


 
Share this:


EcoleBooks | Maswali ya Ufupisho na Majibu Yake

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*