Share this:

Maswali ya Insha za kawaida

1.  Andika insha itakayotamatika na ….kweli dunia ni mwendo wa ngisi, ina masalata wengi.

2.  Elimu bila malipo nchini Kenya ina changamoto zake. Jadili

3.  Eleza namna katiba mpya inavyofaa kutetea nafasi na hadhi ya jinsia ya kike.

4.  Ajira ya watoto ina madhara mengi. Fafanua.

5.   Zigo la kuliwa halilemei.

6.  Andika insha itakayomalizikia kwa :

….mkuu wa askari aliwaeleza kuwa ikiwa njia hizo zingetumika, uhalifu ungezikwa

kwenye kaburi la sahau

7.  Mwenye kovu sidhani kapoa.

8.  Elimu ya bure inayotolewa na serikali katika shule za msingi za umma humu nchini,

imekuwa na athari mbalimbali. Jadili.  

9.  Andika insha itakayomalizikia maneno yafuatayo:-

….aliyakumbuka mashauri ya mamake ambayo aliyakaidi. Machozi yalimbubujika

alipojiona kadhoofika kiafya jinsi ile; mguu mmoja duniani, mwingine kaburini.

10.  Uhaba wa kazi ni tatizo sugu katika nchi zinazoendelea. Jadili.  

ecolebooks.com

11.  Andika kisa kinachodhihirisha ukweli wa methali: “subira huvuta heri

12.  Andika insha itakayoishia kwa maneno haya:- ………..nilipiga magoti chini na kumshukuru Maulana kwa kuyanusuru maisha yangu.  

13.  Kumekuwa na kilio kila uchao. Pendekeza njia mbalimbali za kutokomezea mbali umaskini

 katika jamii yako. Fahali wawili wapiganapo, nyasi huumia.  

14.  Andika insha itakayoishia kwa maneno yafuatayo:-

15.  ….hapo ndipo nilipoapa kwamba sitawahi kumfungulia mtu yeyote yule mlango usiku.

16.  Asifuye mvua imemnyea.Thibitisha ukweli wa methali hii kwa kisa.

17.  Utovu wa nidhamu shuleni umesababishwa na mabadiliko katika sekta ya Elimu. Jadili.

18.   Andika insha itakayomalizikia kwa maneno …ama kweli dunia ni mti mkavu; ukiuegemea

utaanguka. Nilikuja kutambua kwamba ni heri uwe maskini wa mali na tajiri wa fadhili

kuliko tajiri wa mali na fukara wa utu.  

19.  Licha ya kufaulu kiasi, utoaji wa elimu ya bure katika shule za msingi na upili umekumbana

 na matatizo si haba. Jadili

20.  Mchuma janga, hula na wa kwao.

21.  Andika insha itakayoishia kwa maneno haya………… moyo ulinidunda nilipoona gari letu

 likibingiria kuelekea ufuo wa bahari, machozi yakanitoka kwa wingi nikakumbuka yote  

 niliyokuwa nimetenda ulimwenguni, nikayafunga macho yangu.

22.  Udongo uwahi/upatilize ungali maji.

23.  Kuavya mimba ni uovu usioweza kuvumiliwa , jadili.

24.  Andika insha itakayomalizikia kwa maneno haya:

……………..ndipo nilipogundua kuwa mtu ambaye siku yake imefika hana budi kufa hata

akafanyiwa dawa za aina gani.

25.  Wewe kama Mwalimu ambaye amehitimu katika chuo kikuu cha Kenyatta, kuna nafasi ya kufundisha katika shule ya upili ya Angeko. Andika wasifu-kazi utakaoandamana na barua yako.

26.  Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.  

27.  Vizingiti \Vikwazo vya kuundwa na kupatikana kwa katiba mpya nchini Kenya sio wanasiasa

 pekee.Fafanua.  

28.  Andika insha itakayomalizikia kwa: . . . Na katika uchaguzi wa marudio uliofanywa baada ya kisa hicho, Hidaya akapata ushindi mkubwa na kuwa mbunge wa eneo bunge la Kubali.

29.  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo  

30  Uavyaji wa mimba ni suala sugu hapa nchini Kenya. Jadili  

31.  Ilikuwa mara ya kwanza kufikishwa mahakamani…………….. endeleza

31.  Kisa cha mwanafunzi kilingane na chanzo hiki na aonyeshe ubunifu na matumizi mazuri

ya lugha

32.   Eleza jinsi haki za watoto zinavyokiukwa katika jamii huku ukipendekeza suluhu.  

33.  Cha Mchama huchama, cha Mgura hugura.

34.  Rais Julius Kabarage Nyerere ni mtu anayejulikana katika taifa la Afrika kusini na

 Mataifa mengine. Alipozaliwa………………………………………………………………….

35.  Shughuli ya kuavya mimba iharamishwe. Jadili

36.  Ganga ganga ya mganga humlaza mgonjwa na matumaini.

37.  Andika insha itakayomalizikia kwa: Baadaye niligundua kuwa kutotii wazazi kunaweza kuwa na

madhara ya muda mrefu sana.

38.  Bandu bandu huisha gogo.

39.  Suluhu kwa matatizo yanayoikabili nchi yetu ni katiba mpya. Jadili,

40.  Kamilisha mtungo wako kwa kifungu kifuatacho.

 ………………………………………………. Ni uso wa nani usiotahayuri kwa kisa kama hiki?  

41  Mchumia juani hulia kivulini.

42.  Uhalifu umekithiri sana humu nchini. Jadili sababu zinazochangia hali hii na upendekeze

njia za kukabiliana nao.

43.  Andika insha itakayomalizikia maneno haya———————–niliketi nikishika tama.

Iliyokuwa nyumba yangu ikawa jivu tu! Sikuyazuia machozi yalionibubujika.

44.  Andika Mtungo unaothibitisha ukweli wa methali: Jitihada haiondoi kudura.

45.   Simu za rununu zina madhara mengi kuliko manufaa . Jadili.  

46.  Andika insha itakayoisha kwa maneno yafuatayo: …………..nilipogutuka niliangaza macho huku

na kule. Aah! kumbe nilikuwa nikiota!  

47.  Fafanua njia mbalimbali za kukabiliana na umaskini nchini mwetu.  

48.  Samaki mkunje angali mbichi.

49.  Hauchi hauchi unakucha. Naam, siku njema niliyosubiri kwa hamu na ghamu iliwadia.

Nilifurahi ghaya ya kufurahi……. (endeleza insha hii).

 

 

Majibu ya Insha za kawaida (KA)

1.  Sharti mwanafunzi amalizie kwa maneno aliyopewa

 • Kisa kieleze hali ya maisha ambapo inaenda kando na matarajio ya wengi
 • Insha iwe na awani iliyopigiwa msitari
 • Azingatie msamiati mwafaka
 • Ashughulikie kisa kinachoonyesha namna watu (marafiki) hugeuka na kusaliti walioamini.

 

2.  Changa moto za elimu bila malipo

 • Kichwa k.m chanagmoto zinazokumba elimu bila malipo
 • Kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigwe mstari
 • Ataje changamoto

 – wanafunzi wengi shuleni

 – Ukosefu wa walimu wa kutosha

 – Ukosefu wa vifaa vya kutosha

 – Matokeo kudidimia

 – Ukosefu wa vitabu

 – Dhana potofu miongoni mwa wazazi na wafadhili kutegemea serikali

 – Ufisadi miongoni mwa maafisa, walimu wakuu na wafanya biashara, wanakandarasi n.k.

 – Wizara na idara mingine kukosa ufadhili

 – Shule za kibinafsi kuongeza karo kwa sababu ya matokeo mema

 – Mbinu zisizofaa kutumika kuimarisha matokeo k.m. wizi wa mitihani, kuzuia watahiniwa

dhaifu kufanya mtihani

3.  Usawa masomoni

 – usawa kazini

 – Kupiga marufuku ukeketaji wa wasichana

 – Kupinga ndoa za mapema

 – Kupinga ndoa za lazima

 – Kuweka idadi maalum ya wabunge wa kike

4.  Hili ni swali la maelezo

Mtahiniwa aeleze madhara ya ajira ya watoto kwa kina

Madhara ni kama vile:

 1. Ukosefu wa elimu
 2. Kudhulumiwa kimapenzi
 3. Magonjwa  
 4. Utovu wa nidhamu
 5. Malipo duni  
 6. Ulemavu  
 7. Vifo
 8. Mapigo  
 9. Lishe duni  
 10. Kukosa mavazi
 11. Huchangia uhusiano mbaya katika jamii
 12. Kulemaza ukuaji wa motto

5.  Hii ni insha ya methali

Maana ya nje: Mzigo uliobeba chakula hata ukiwa mzito haumchoshi

Anayeubeba

Maana ya ndani: jambo lililo na manufaa halimchoshi mtu  

Matumizi: Hutumiwa kumhimiza mtu anayefanya jambo lililo na manufaa kwake kwamba aendelee kujikaza licha ya ugumu anaokabiliana nao. Mtahiniwa atunge kisa au visa vinavyoonyesha ukweli wa methali hii.  

Ikiwa na visa na muumano. Arejelee pande zote mbili za methali kikamilifu

Aonyeshe jinsi jambo husika lilivyo zigo la kuliwa na namna lisivyolemaa

 

 • UTAHINI  

  Kisa kisipotoa maana ya methali, takuwa amejitungia swali. Atuzwe Bakshishi (BK 01 –

 • Asiyeshughulikia pande zote mbili hajajibu swali. Atuzwe (BK 01 – 02 )

 

6.

 • Hii ni insha ya mdokezo
 • Lazima mtahiniwa atamatishe insha yake kwa maneno haya
 • Atakayekosa maneno yote, au baadhi ya maneno swali. Atuzwe BK 01 02
 • Atakayeongeza maneno mengine, vile vile atakuwa amejitungia swali. Atuzwe KB 01 – 02
 • Kisa kionyeshe njia za kuzuia uhalifu ambazo zitapendekezwa na mkuu wa askari au wananchi

 

 

MBINU ZA KUZUIA UHALIFU

 1. Kuelimisha watu kuhusu madhara ya uhalifu  
 2. Wahalifu kuchukuliwa hatua kali
 3. Wahusika doria wawepo kuzuia uhalifu
 4. Ajira kuwepo ili watu wapate riziki
 5. Sheria ziimarishwe
 6. Wavyele wapewe mafunzo ya malezi
 7. Maadili ya kidini yahimizwe  
 8. Miradi ya mapato ianzishwe  
 9. Kuwe na njia za kuwatambua wahalifu
 10. Kuwe na njia za kuwatuza/ kuwapongeza walioadilika  

UTAHINI

 1. Anayetunga kisa kisichorejelea mambo haya amejitungia swali
 2. Azingatie angalau mambo matano

 

7.  Mwenye kovu sidhani kapoa

Hii ni insha ya methali

Mtahiniwa anaweza kufahamu methali kimaana na kimatumizi (si lazima) . Kilicho

muhimu ni kisa au visa kilichoandikwa kuonyesha ukweli wa methali hii.

Mwenye kovu- Mtu aliyewahi kukumbwa na jambo Fulani baya/ lenye kuumiza/ lenye kusababisha uchungu Fulani

 

Sidhani kapoa- Usihukulie kuwa amesahau jambo lile na kutulia

Maana: Mtu aliyewahi kukumbwa na jamboo lenye kutia uchungu au kuumiza atabaki

akilikumbuka hasa kwa hasira. Atakuwa akitafuta nafasi ya kulipiza kisasi hasa

ikiwa jambo lile lilisababishwa na mtu anayemjua

Kisa kitasawiri hali ya kulipiza kisasi kwa uovu aliotendewa mtu  

Anayekosa kutunga kisa atakuwa jajalijibu swali

 

8.  Elimu/ masomo ya bure

 Athari- matokeo; yaweza kuwa mazuri au mabaya

  Aonyeshe pande zote mbili kwa kutoa hoja mwafaka

Mfano: Athari mbaya  

 • Uhaba wa vifaa
 • Ushuru kuongezeka kulipia
 • Miradi mengine ya serikali kuathiriwa
 • Kiwango cha masomo kimezorota  
 • Uhaba wa walimu

 

Faida

 • Nchi imeimarisha uwezo wa kusoma na kuandika
 • Watoto kutoka jamaa maskini kuendelea na masomo
 • Wazazi wamepunguziwa mzigo wa malipo ya karo n.k.
 • Hakiki na utambue hoja zozote zaidi zinazoafikiana na mada

 

9.  Hii ni insha ya madokezo

 Mtahiniwa abuni kisa kitakachoafikiana na kimalizio kilichotolewa

Kisa kionyeshe majuto; mhusika kuonywa dhidi ya tabia Fulani, ayakaidi mashauri na

hatimaye kukumbwa na balaa; kudhoofika kiafya kutokana na tabia yake

Kisababishi chaweza kuwa

 Ugonjwa wa ukimwi  

 Kuathirika na dawa za kulevya n.k.

Anayekosa kumalizia kimalizio hiki achukuliwe kuwa hajajibu swali, na kuwekwa katika

kiwango cha D 03  

 

10.  Uhaba wa kazi

– Mwanafunzi ajadili pande zote mbili

kuunga mkono

uhaba wa kazi umesababisha :-

 • umaskini  
 • ukosefu ya usalama
 • matumizi ya dawa za kulevya  
 • Uvunjaji wa sheria
 • uhasama kati ya walio na kazi na wasio na kazi  
 • wizi wa mabavu

Kupinga

 • Mtu anaweza kujiajiri
 • walio na kazi huchangia katika visa vya uvunjaji wa sheria k.v. ufisadi  
 • Mwishoni mwa mjdala mwanafunzi atoe msimamo wake/aonyeshe msimamo wake
 • Taz- ashughulikie hoja tano au zaidi

 

11.  Maana : Subira ni sawa na kungojea ili jambo fulani likutokee au utendewe jambo

fulani la haja.

 • Heri i sawa na matokeo mazuri/mema yanayopatikana baada ya mtu kuwa mvumilivu kwa kusubiri labda kw amuda mrefu hata ingawa kuna mambo mengine sawa sawa na yale anayoyasubiri. Lakini yanayopatikana baada ya subira huwa yenye manufaa ziaidi kuliko yanayopatikaka kwa haraka.
 • Mtahiniwa aeleze kisa au visa vinavyoafiki maana ya methali
 • Insha izingatie pande zote mbili za methali
 • Asiyeshughulikia pande zote mbili atakuwa amepungukiwa kimtindo.  
 • Insha isipoafiki maana ya methali alikuea anajitungia swali. Kwa hivyo atuzwe

 

 

12.  Insha iakisi hali ya kunusirika, kuponea chupuchupu, kuokoa  

– Mtahiniwa akamilishe kisa kwa kifungu cha maneno aliyopewa  

– Asiyehitimisha kwa hilodondoo atakuwa amejitungia swali – atuzwe D-02

– Atakayeongezea maneno yasiyozidi matano ataondolewa maki 02m (maneno) kazi nzuri !

 

13.  Namna ya kumaliza umaskini katika jami  i

 1. Kuendeleza kilimo cha kisasa
 2. Kuhamasisha watu dhidi ya ufisadi  
 3. Kushirikisha wafadhili katika shughuli za kielimu na kilimo  
 4. Kukuza/ kuipa kipa umbele sekta ya juakali na kuongeza nafasi za kazi
 5. Serikali kuwapa mkopo wafanya biashara ndogo ndogo  
 6. Kupuuza mila na desturi zilizopitwa na wakati- idadi kubwa ya mifugo wa kienyeji  
 7. Ulipaji wa ushuru kuimarishwa
 8. Ugavi sawa wa raslimali za nchi
 9. Kumaliza mizozo ya kisiasa
 10. Uzembe/ ulazaji damu kumalizwa kwa kuwapa kiinua mgongo wanaofanya bidii  
 11. Matumizi ya mihadharati na pombe haramu kukomeshwa  
 12. Elimu ya msingi kuimarishwa ili kuondoa ujinga nchini  
 13. Serikali kuwapa wakulima pembejeo kama vile mbolea, mbegu n.k

 

14.  Mwanafunzi atunge kisa/ visa vinavyooana na maana ya methali  

– Watu wenye uwezo wanapozozozana/ kupigana/ wanaoteseka/ kuumia ni wale walio chini yao

 

15.  Mwanafunzi atunge kisa kitakachomalizika kwa mdokezo, aliopewa na kukipa kisa hicho

mada inayooana na mdokezo

 

16.  Hii ni methali. Kisa kirejelee sehemu zote mbili. Atoe kisa/visa kinacholenga maana ya methali na matumizi yake. Mtu akizungumzia jambo Fulani huwa amelipitia na anaielewa tosha. Hasemi tu kwa kulisikia au kulisoma vitabuni kwa mfano aliyewahi kuporwa mali, kunajisiwa au hata kupata msaada kutoka kwa mtu Fulani atampa sifa kutokana na ule usaidizi alioupata

Kutuza

Asiyelenga methali/ anayepotoka asipate zaidi ya D 03

Atakayerejelea sehemu moja ya methali asipate zaidi ya C 08  

Hii ni insha ya kukadiria

 

17.  Maudhui

Mabadiliko katika sekta ya elimu ni kama vile:  

 1. Kuondolewa kwa adhabu ya kiboko
 2. Kutoajiriwa kwa walimu na tume ya kuwaajiri walimu. Wanafunzi ni wengi na walimu

  Wachache

 3. Elimu ya bure imesababisha msongamano wa wanafunzi wakiwemo walio na utovu wa nidhamu
 4. Masuala ya haki za watoto
 5. Mtaala ulio mwema unaotokana na mfumo wa elimu wa 8-4-4 unaowalemea wanafunzi
 6. Msisitizo uliotiliwa suala la kupita mtihani

Katika kupiga

Kuna masuala mengine kamam vile:  

i) Uozo katika jamii kwa jumla  

ii) wazazi kuwapa majukumu yao ya malezi

iii) athari za kigeni

iv) Kudorora kwa mila na desturi za kiafrika  

18.  Hii ni insha ya mdokezo

Mwanafunzi aandike mtungo (insha ya kubuni) utakaomalizikia kwa maneno aliyopewa

Akikosa kuyatumia atakuwa amejitungia swali lake la binafsi. Atapewa bakshishi 01

Akiongeza maneno yake ataadhibiwa kwa kuondolewa 2 (kimalizio)

Kisa chake kionyeshe mja aliye tajiri lakini asiye na utu na anavyoangamia kutokanan na uroho/ ukatili wake. Aidha aonyeshe maskini anayepata ufanisi kutokana na matendo yake mema (maadili)

 

19  MAFANIKIO YA ELIMU YA BURE  

 • Watoto wengi kupata elimu
 • Njia ya watoto kupunguka – kiasi kikubwa
 • Idadi ya watoto wanaorandaranda  
 • Wazazi wengi wasiojiweza wamenufaika na mpango huu n.k.
 • Matatizo
 • Msongamano wa wanafunzi
 • Ukosefu wa vifaa – vitabu vya kutosha n.k.
 • Upungufu wa walimu
 • Kiwango cha elimu kuathirika
 • Majengo kutoweza kutosheleza mahitaji yanahitaji upanuzi  
 • Walimu kulazimika kuwafunza watu wazima (Umri mkubwa)  
 • Uhaba wa pesa za kutosha kutosheleza mahitaji shuleni n.k.  

 

20. Hii ni methali

 Chuma – kufanya kazi na kupata faida  

 Janga – Balaa; shida; hatari; tabu; matatizo

 Maana: Yeyote asababishaye shida, huwatia hasara watu wa nasaba yake.

 Hili lina maana kuwa watu wa jamii moja hushirikiana kwa kila hali, iwe ni mbaya

au nzuri

 Matumizi: Huambiwa mtu aliyetia ukoo wake hasara

 • Mtahiniwa ashughulikie pande zote mbili za methali yaani : kuchuma na kula
 • Atakayechagua kisa aonyeshe kazi iliyofanywa na ile faida au matokeo kwa wa kwao
 • Anaweza kuonyesha methali nyingine zinazoweza kuchukua maana yah ii methali
 • Wakati wa kutuza, ambaye hatashughulikia pande zote mbili, awekwe katika

kiwango chake kisha aondolewe alama 4 (maudhui)  

Anaweza kutumia visa zaidi ya kimoja ila tu inabidi vionane  

 

21.  Mtahiniwa aandike kisa

 • Kisa kinachomhusisha yeye akitenda makosa
 • Pawe na majuto  
 • Ziada
 • Asiyejihusisha amepotoka awekwe kiwango cha D – (alama 2)
 • Akikosa sehemu ya makosa au majuto aondolewe alama 2 (maudhui)
 • Asipomalizia maneno ya dondoo amepotoka apewe D – alama 2
 • Asipomalizia maneno matano (5) ya mwisho aondolewe alama 2 (Kimalizio)  

Akizidisha baada ya dondoo maneno yake, hajajibu swali  

 

22.  Insha ya methali  

 • Udongo uwahi/upatilize ungali maji
 • Udongo hauwezi kusarifiwa kama umekauka lakini mtu huweza kuusarifu na

kuufinyanga vizuri kama maji. Methali hii hutumiwa kutufunza kwamba tunaponuia

kulifanya jambo fulani tusingojee hadi wakati uakapita, tunapaswa kuliwahi mapema.

Watu wngine husema upatilize udongo uli maji au udongo ukande uli maji. Udongo

uuwahi ungali maji.  

 • Lazima mwanafunzi alenge swali/methali kionyeshe kuwa jambo liliwahiwa

kabla halijaharibika.  

 • Kisa kilenge methali hiyo.

Mfano: Matumizi ya dawa za kulevya, uhifadhi wa mazingira, kujiingiza katika ukahaba

 

23.  Ubaya wa kuavya mimba

– Ni uhalifue

– Huzorotesha afya ya mhusika

– Husababisha kifo  

– Inaweza kusababisha utasa

– kiwango cha laana/dhambi/imani

– Hushusha heshimana hadhi ya mhusika  

Uzuri wa kuavya  

– Huokoa maisha ya wale walioathirika.  

– Mimba ambazo hazihitajiki mfano ubakaji, watoto wadogo, undugu

Msimamo

 • Mwanafunzi atoe msimamo wake

 

24.  Hii ni insha ya mdokezo. Kisa cha mwanafunzi kiafiki maneno hayo na asiongeze wala

kubadili mpangilio wa maneno hayo.  

Mwanafunzi abuni kisa cha kusisimua kinacholenga maneno hayo.

DOSARI

 • Uozo katika jamii
 • Ukosefu wa kazi
 • Magonjwa  
 • Uchafuzi wa mazingira
 • kuvuruga maisha ya binadamu  

Mtahiniwa aonyeshe kwamba hiyo teknolojia imemwathiri  

Asipojihusisha aondolewe alama (2w) za wahusika  

 

25.   Wasifu – Kazi iwe na mpangilio au vipengele vifuatavyo:-  

Maudhui

(i) Maelezo ya kibinafsi  

 1. Jina
 2. Tarehe ya kuzaliwa
 3. Mahali pa kuzaliwa
 4. Ndoa/Hadhi  
 5. Lugha
 6. Anwani
 7. Nambari Ya simu  
 8. Barua pepe  

Vipengele hivi vitengwe kwenye mstari mmoja

(ii) Kiwango/viwango vya elimu

– Mwanafunzi aanze na kiwango cha juu cha elimu.

– Mwaka wa kusoma – Kiwango na cheti alichopata baada ya kuhitimu/kufuzu

mfano :- 1999 – 2004 – Chuo kikuu cha Kenyatta Shahada ya kwanza ya ualimu.  

(iii) Tajriba ya kitaaluma  

Aanze kwa kazi anayoifanya kwa sasa  

(iv) Uteuzi (ikiwa upo) majukumu au nyadhIfa ulizowahi kupewa.

(v) Semina ulizo hudhuria (ikiwa zipo)

(vi) Kazi za ziada/ tuzo/ machapisho

(vii) uraibu

(viii) Wadhamini/ warejelewa ataje wawili au watatu lakini wasizidi hapo.

26.  Methali

  Mwongozo

MTAHINIWA ATOE MAANA YA NJE NA NDANI YA METHALI

 • Pande zote mbili ya methali zishugulikiwe
 • Anaweza kutumia visa au kisa kufafanua methali
 • Anawaza kuonyesha maana ya ndani /yenye/kuanzia kisa au visa moja kwa moja
 • Kisa/visa vionyeshe mali akisifwa kwa jambo zuri huauza kuregea ua kuharibu mambo

27.

 • Insha itamatishwe kwa mdokezo uliotolewa
 • Mtahiniwa asimilie kisa kinacholenga uchaguzi katika uwanja wa kisisa kisa chenyewe
 • Uchaguuzi kufanyua baada ya kifo cha mbunge wa eneo bunge hilo
 • Mbunge wa awali kuhusika katika wizi wa kura
 • Mtahiniwa asipomaliza kwa maneno aliye atakuwa amepotoka hivyo kupewa Al:2(bakshishi)

 

28 – sha itamatishewe kwa mdokezo ulitolewa  

 • Mtahiniwa asimilie kisa kinacholenga uchaguzi katika uwanja wa kisisa kisa chenyewe
 • Uchaguuzi kufanyua baada ya kifo cha mbunge wa eneo bunge hilo
 • Mbunge wa awali kuhusika katika wizi wa kura
 • Mtahiniwa asipomaliza kwa maneno aliye atakuwa amepotoka hivyo kupewa Al:2(bakshishi)  

  29.  Kisa cha mwanafunzi kionyeshe ukweli wa methali hii. Anayehama kambini au pahala Fulani hawezi kunya au kuchafua pale eti kwa kuwa anatoka, la. Huenda ikatokea haja, ikabidi arudi

  pahali hapo. Tusidharau cha zamani kwa kuona kipya (Usiache mbachao kwa msala upitao)

30.  Mwanafunzi aonyeshe

 – Maana ya uavyaji wa mamba

 – Madhara ya uavyaji mamba

 – Kusababisha vifo vya wahusika

 – Kutozaa baadaye  

 – Mauaji ya vilenge/ vijusi

 – madhara ya kiafya kwa mama mfano maradhi ya chupa ya motto n.k

 – Waweza kushtakiwa / kufungwa

 – Dhambi kwa mola – kuua

 

 Manufaa ya uavyaji  

 – Kuokoa maisha ya mama aliye hatarini  

 – Mimba ya ukooni mwa mama- mivigo, kuondoa aibu

 – Mwanafunzi arudi shuleni (mama)

 

N.B  – Katika aya ya mwiso, atoe uamuzi au maoni yake

 – Aeleze upande mmoja mfano apinge kisha aunge mkono mjadala kisha atoe uamuzi  

Au

 • Atoe uamuzi wake, kisha atoe maoni

32.  Mtahiniwa kwanza aeleze hiyo halafu atolee suluhu

Maudhui

 1. Ubakaji wa watoto wadogo

Suluhu:- Watoto wachungwe na wazazi au walezi wahusika waadhibiwe vikali

 1. Watoto kuteswa na wazazi k.v. kuchapwa hadi kulemazwa au kuchomwa.

Suluhu : Wazazi waadhibiwe mahakamani

 1. Ajira ya watoto

Suluhu:-Serikali ihakikishe kila mtoto yu shuleni kwani masomo ni ya bure na wasiopeleka hao wachukuliwe

hatua kali

 1. Kuavya mimba-

Suluhu – wahusika wafungwe kifungo cha mda mrefu

 1. Watoto wachanga kutupwa pipani

Suluhu: Serikali ijengee watoto kama hao makao wahusika wachukuliwe hatua

 1. Watoto kuadhibiwa na walimu kupita kiasi

Suluhu: Walimu kama hao wafutwe kazi

 1. Ukosefu wa chakula

Suluhu Wazazi washurutishwe kuwalea watoto wao vyema; serikali itoe misaada ya chakula

(Hoja tano na zaidi zifafanuliwe vyema huku masuluhu yakitolewa )

UMUHIMU

Sura

 • Insha iwe na kichwa kilichoandikwa kwa herufi kubwa na kupigwa mstari
 • Au aanze tu kuandika insha muradi ameonyesha ni swali nambari gani.
 • Urefu wa kunasa mbili au zaidi uzingatiwe ili kutimiza idadi ya maneno
 • Asiyetimiza idadi ya maneno aondolewe alama 2u baada ya kukadiriwa katika kiwango chake

 

33.  – Mtahiniwa atunge kisa kifaacho

Maana : Kitu cha anayeondoka pamoja naye.

_ Huweza kutumiwa kuipigia mfano hali ambayo imebadilikka na kuwa mbaya zaidi au

kubadilika na kuwabora zaidi

– Si lazima mtahiniwa aeleze maana mwanzoni

– Si lazima aandike anwani/kichwa cha insha yake

– Anaweza kuanza moja kwa moja kisa chake

– Mtahiniwa azingatie maana kikamilifu

 

34.  – Mwanafunzi ajaribu kuelezea wasifu wa ‘Rais Julius Nyerere

– Si lazima mwanafunzi azungumzie ukweli na kihistoria

– Mwanafunzi amekubaliwa kubuni na kumpatia Rais Nyere sifa ziada zisizo halisi

MAUDHUI

 • Mwanafunzi aeleze jinsi mhusika huyu anavyojulikana kitaifa na kimataifa
 • Kiwangochake cha elimu
 • Umaarufu wake kisiasa
 • Familia yake  
 • Alivyoendelea kuichumi
 • Duri
 • Marafiki zake  
 • Jinsi alivyopata umaarufu wake
 • Maudhui yasipungue matano

Sura

 • Maandishi ya mfululizo.
 • Mwanafunzi atimize urefu unaohiajika .
 • Aisyetosheleza urefu aondolewe al. 2u.  

35. (i) Anaweza kuunga mkono, kupinga au kujadili pande zote mbili

  (ii) Akishughulikia pande mbili atoe uamuzi katika hitimisho

Kuunga mkono

 • Kuavya mimba ni kinyume cha amri ya Mungu isemayo usiue. (Maadili ya Kidini)
 • Mtoto anayeaviwa ni kiumbe ambaye ana haki ya kuishi
 • Ni kwenda kinyume cha utu wa mwanadamu
 • Kuavya kukiruhusiwa ni kuchochea kuporomoka kwa maadili
 • Ni sawa na kuhalalisha mauaji
 • Huhatarisha maisha ya mama
 • Ni hatari kwa afya ya mama (magonjwa)
 • itachangia utasa katika jamii
 • huweza kusababisha kuwepo kwa mayatima
 • Ni hasata katika uchumi wa taifa kwani mama akifa mchango wake utakosekana

Kupinga

 • Kuavya kuruhusiwe ikiwa afya ya mama iko hatarini
 • Kuavya kuruhusiwe ikiwa mimba ilitokana na ubakaji
 • Wanaosaidia kuavya mimba watakuwa ni madaktari waliohitimu na hivyo hamna wasiwasi wa kutokea maafa.
 • Kutazuia vifo vingi kwa sababu kuharamisha kutawazwa wasichana na wanawake kuavya kwa siri na madaktari bandia/hasi/matapeli.
 • Kuruhusiwe kwa sababu maisha huanza baada ya mtoto kuzaliwa.
 • Kuruhusiwe ikiwa wahusika wote ni wachanga na hawajawajibiki
 • Kutusaidia kupanga uzazi
 • Ili kupunguza mayatima kwa sababu mama aweza kufa anapokuwa akizaa
 • Yaweza kuwapa wahusika muda wa kujiandaa katika ndoa halali
 • Ili kuepusha wanaharamu katika jamii

 

36.   (i) Mtahiniwa aeleze maana na matumizi ya methali

(ii) Atoe kisa kinahcoafikiana na methali

Maana :- Mtu awapo na tatizo lolote halafu mtatuzi au masaidizi akionyesha nia ya kumsaidia, kumwacha mwenye tatizo na matumaini/matarajio.

Matumizi : Hutumiwa kuwahimiza watu kuwa wanapoendewa ili kuombwa msaada au ushauri, wasioneshe nia ya kutojali kwani kufanya hivyo huwakatiza wahasiriwa tamaa.

37.  (i) Lazima amalizie maneno ya mdokezo

(ii) Asipomalizia maneno hayo atakuwa amepotoka

(iii) Akiongezea zaidi maneno matatu (3) atolewe alama mbili

(iv) Yakizidi kwa maneno matano, amepotoka.

38.   Bandu Bandu Huishia Gogo

Mwanfunzi atunge kisa kinacho dhihirisha ukweli wa hiyo methali (juhudi za kidogo kidogo hatimaye huleta ufanisi katika shughuli).  

– Si lazima mwanafunzi kufafanua maana. Mwanafunzi aweza kuanza kwa masimulizi

yake moja kwa moja. Hata hivyo aliyefafanua methali vilivyo asiadhibiwe.

– Kisa kimoja kirefu au visa vidogo vidogo vinavyioafikia methali vitafaa.

– Kisa cha mwanafunzi kisiishilie kupinga methali.

39.  MATATIZO

 1. Ukosefu wa ajira kwa vijana.
 2. Ufisadi uliokithiri.
 3. Raslimali kuliandikiwa wachache.  
 4. Uongozi mbaya – Taasisi za serikali kuingiliwa na serikali kuu.
 5. Ukosefu wa usalama.
 6. Ukabila.

KUUNGA

SULUHU

Katiba iweze kuweka mikakati ya

KUPINGA  

40.  – Mwanafunzi atunge kisa kinachoaibisha.  

  – Asiongeze maneno yake katika kile kifungu cha kuishilia.

  – Utaratibu wa kuhakiki insha uzingatiwe katika utuzaji na utozaji wa alama.

41.   Hii ni insha ya methali

Mchumia – chuma – tafuta riziki

Juani – kustahimili ugumu/ kwa shida

Mtu anayeshughulikia jambo fulani kwa dhati na kwa kuvumilia ugumu wowote hatimaye hufanikiwa na kustareheka.

Mtahiniwa aweza kutoa ufafanuzi wa maana na matumizi ya methali

Atoe kisa/visa vinavyooana na maana ya methali

Asiyetoa kisa achukuliwe kuwa hajajibu swali na kuingizwa katika kiwango cha D.

42.  Sababu zinazochangia uhalifu

(i) Umaskini

 1. Kuimarika kwa teknolojia k.m. rununu
 2. Ukosefu wa ajira
 3. Uhasama baina ya makabila
 4. Siasa duni – k.m viongozi kuchochea uhasama baina ya makabila  
 5. Ulanguzi wa silaha hatari  
 6. Ulegevu wa maafisa walinda usalama
 7. Ufisadi
 8. Matumizi ya dawa za kulevya

Njia za kukomesha

(i) Walinda usalama walegevu waachishwe kazi  

 • Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya walanguzi na watumizi wa dawa za kulevya
 • Ajira zibuniwe
 • Vijana kusaidiwa kuanzisha miradi ya maendelo k.m. mikopo.
 • Vituo vingi vya polisi kujengwa
 • Vituo vya urekebishaji tabia vijengwe
 • Hatua kali zichukuliwe dhidi ya wavunjaji wa sheria

43.  Hii ni insha ya mdokezo

 • Ni insha iliyo na kimalizio  
 • Mhusika ajipate katika hali ya huzuni. Mkasa k.m. wa moto kuzuka na kuichoma nyumba yake – likaonekana jivu tu palipokuwa nyumba yake
 • Lazima mtahiniwa amalizie maneno ya kimalizio
 • Anayepunguza au kupunguza maneno hadi manne ya kimalizio aondolewe

maki 2m baada ya kutuzwa.

 • Anayekosa sehemu ya kimalizio aondolewe maki 4mk baada ya kutuzwa.  

44.  Jitihada haiondoi kuduru

  Maana: Bidii za mja haziwezi kubadilisha majaliwa au mpango wa Mungu.

Matumizi: Hutumiwa kuwatia moyo na kuwahimiza watu ambao huenda bidii wanazotia

katika shughuli zao zisifanikiwe kuwapa wanachotarajia. Wanachopata ni kile

Mungu aliwapangaia.

 • Mwanafunzi atunge kisa/visa kadhaa vinavyolenga mada ya methali
 • Insha ionyoshe ukomavu wa mtiririko kilugha na kimsamiati
 • Mtahiniwa ashughulikie sehemu zote mbili za methali.  
 • Tanbihi: Anayeshughulikia sehemu moja atakuwa amepotoka

 

45.  
MADHARA YA RUNUNU  

(i) Kuchangia kuongezeka kwa visa vya ajali barabarani  

(ii) Kuchangia katika kuzoroteka kwa maadili ya jamii/zina filamu potofu.

(iii) Visa vingi vya uhalifu vimefanikiwa kupitia rununu

(iv) Familia/ndoa zimevunjika – kukosana kutokana na rununu.  

(v) Wanafunzi wameshindwa kujimudu kilugha kwa sababu ya rununu – wamezoea lugha ya

mkato na isiyo sahihi kisarufi na msamiati.

(vi) Zinaathiri mbegu za uzazi iwapo zinawekwa kwenye mfuko wa nguo kwa muda mrefu.

(vii) Ni ghali kutumia kwa vile huhitaji kununua kadi ili kuwasiliana

FAIDA YA RUNUNU

 1. Kuwezesha kufanikiwa kwa mawasiliano wakati wowote.
 2. Husaidia katika kuweka ujumbe (siri muhimu)  
 3. Ni nyepesi / hubebeka kwa urahisi

 

46.   – Ni insha ya kubuni

– Mwanafunzi azingatie sehemu zote k.m. utangulizi, mwili na hitimisho

– Mtahiniwa atunge kisa kinachomalizia kifungu kilichotolewa  

Tanbihi :- Mwanafunzi ambaye atashindwa kumaliza insha na kimalizio hiki achukuliwe

amejitungia swali na atuzwe D- (01-02)

 

47.  Hili ni swali la kutoa hoja na kuzifafanua  

 Baadhi ya hoja:  

 • Masomo kuimarishwa
 • Kubuni nafasi nyingi za ajira
 • Serikali iimarishe sera k.v kazi kwa vijana  
 • Riba ya mikopo ipunguzwe
 • Mashauri kupitia kwa mikutano ya hadhara na mabaraza kuhusu kukinga ugonjwa wa ukimwi – ukimwi husababisha utegemezi mkubwa na hivyo umaskini
 • Watu kuhimizwa kushiriki kazi, wasizembee
 • Usambazaji wa nguvu za umeme katika sehemu za mashambani
 • Kilimo kipewe kipaumbele

 

48.  Samaki mkunje angali mbichi

 Hili ni swali la methali

 Mtahiniwa aweza kufafanua maana na matumizi (si lazima)  

 Maana: Jambo linapoharibika lirekebishwe mapema kabla halijakuwa gumu

kulirekebisha. Rekebisha jambo likiwa bado laweza kurekebika. Likiachwa likitiri

hufikia kiwango kisichoweza kurekebishwa

Mtahiniwa atunge kisa/ visa vinavyoonyesha ukweli wa methali hii

 Aweza kuchukua mtazamo wa:

 1. Hali iliyoharibika na hatua za haraka kuchukuliwa na hivyo hali nzuri kurejeshwa
 2. Hali Fulani kuonyeshwa kuharibika na kuachwa hadi ikawa vigumu kuirekebisha

 

Kisa kinachobuniwa kiweze kuoana na moja kwa moja na methali.

Kisa kikikosa kuhusiana na methali mtahiniwa achukuliwe kuwa amepotoka na kuingizwa katika kiwango cha D (03)

Ikiwa mtahini hatatunga kisa achukuliwe kuwa hajajibu swali na kuwekwa katika kiwango cha D (02)

 

49.  Hili ni swali la mdokezo Mtahiniwa amepewa kianzio cha insha  

Lazima ayatumie maneno yale yote mwanzo wa insha   Kisa kionyeshe kwanini siku hiyo ilisubiriwa kwa hamu; ilikuwa na umuhimu na gani?  

  Mtahiniwa adhihirishe bayana tukio/ shughuli/ jambo muhimu ambalo lingetokea siku hiyo

Atumie nafsi ya kwanza katika masimulizi yale.  

 


 
Share this:


EcoleBooks | Maswali ya Insha za kawaida na Majibu Yake

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*