Share this:

Maswali ya Hadithi Fupi : K. WAMITILA: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINEZO

1.  Ukirejelea mkusanyiko wa hadithi fupi: Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine,

 Onyesha msimamo wa mwandishi Rayya Timammy kuhusu kura na uongozi.

2.  K. Wamitila anatumlikia jamii iliyojaa uozo wa kila aina. Eleza kauli hii kwa kurejelea diwani

  ya Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine.

3.  “Euphrase Kezilahabi ni mwingi wa Jazanda na Ndoto katika uandishi wake.” Thibitisha

kauli hii kwa kurejelea hadithi ya Mayai waziri wa maradhi.  

4.  “Hii ni dunia ya dua la kuku halimpati mwewe!” Alijiambia. Baada ya muda aliongeza  “anayepanda juu kipungu hafikili mbinguni.”  

 (a) Eleza muktadha wa dondoo hili

 b) Ukirejelea hadithi ya Msamaria Mwema, onyesha vile hii dunia ni ya ‘Dua la kuku

5.  Soma makala haya kisha ujibu maswali

Angeko, Angeko ee

Angeko, Angeko ee

Ni kilio, Kilio ee

Ni kilio, kilio ee

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

ecolebooks.com

 (b) Eleza mbinu ya uandishi iliyotumiwa kwenye dondoo hili.  

 (c)Eleza matukio ya kweli ambayo mtunzi ameyaangazia katika hadithi. “Ndimi za mauti”.

6.  Kwa kurejelea hadithi ya Mkimbizi eleza madhara ya vita

7.  Sote tulisimama ghafla kama tumesimikwa ardhini”. Huu mwisho wetu sasa!”

 (a) Fafanua muktadha wa maneno haya  

 (b) Taja na ueleze mbinu ya lugha ambayo imetumiwa katika muktadha huu

 (c) “Nilikumbuka ile sura ya mama na ndugu zangu”. Ni kwa nini msemaji anawakumbuka

mama na ndugu zake?

 (d) Eleza matatizo yaliyowakumba wakimbizi kulingana na hadithi  

 (e) Eleza maudhui yanayoibuka katika muktadha

8.  Jadili wahusika wafuatao na dhima yao katika hadithi ya Fumbo la mwana :

i) Makulu

ii) Mwalimu

iii) Mzee Atanasi

9.  (a) Kwa kurejelea hadithi za Mkimbizi na Fumbo la Mwana, eleza jinsi ambavyo mchafuko

  wa kisiasa na matumizi ya dawa za kulevya zinavyoweza kuzorotesha ukuaji wa jamii  

 (b) Kwa kurejelea hadithi za Uteuzi wa Moyoni na Ngome ya Nafsi, eleza jinsi haki za

wanawake zilivyokiukwa

10.  “Unavyoona ni kama aligongwa…..basi mimi nikamkuta pale anagaragara chini. Unajua zamani

 nikienda kanisani.. nakumbuka kisa cha Msamaria ; kufupisha habari mimi ni Msamaria mwema

 niliyemwokota mzee huyu chini.”

 (a) Ni nini kilikuwa kimetendeka ili dereva ayatamke haya ?  

 (b) Ingawa Dereva alijiita msamaria mwema, ni yapi hakuwa tayari kufanya masamaria

mwema aliyoyatenda katika Bibilia ?  

 (c) Unafikiri ni ni kilichosababisha ajali ndiposa mzee huyu agongwe ?

 (d) Onyesha vitendo vya ‘Msamaria Mwema’ vinavyoelekea kuthibitisha kwamba ndiye

aliyemgonga mhasiriwa

 

11.  Mbinu ya majazi na mbinu rejeshi hutumiwa na waandishi wengi ili kuwasilisha ujumbe wao.

 Huku ukitoa mifano kutoka hadithi mbalimbali thibitisha ukweli wa kauli hii

 

12.  Utamaduni unaomkandamiza mwanamke umetamalaki katika jumuiya ya hadithi za Uteuzi

moyoni na ‘Ngome ya Nafsi’. Kwa kurejelea hadithi hizi, eleza jinsi utamaduni umetumiwa

kukandamiza wanawake

13.  Diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi imejikita katika masuala ibuka yanayofaa kushughulikiwa

 na jamii. Taja na uthibitishe.

14.  Fafanua dhamira ya Ken Walibora alipoandika kisa cha “Tuzo”  

15. “Mara nyingi vijana hushughulikia mambo ya kibinafsi. Mara nyingi mawazo yao

hufuata mkondo wa anasa za vijana tu.”

(a) Eleza muktadha wa usemi huu.  

(b) Onyesha ushahidi wowote katika tamthilia kudhihirisha ukweli wa kauli hii.

(c) Fafanua mambo waliyofanya vijana katika tamthilia kuonyesha kuwa walipigana kwa

niaba ya umma.  

 

Majibu ya Hadithi fupi K. WAMITILA: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINEZO

1.

 • Mwandishi namtunia mhusika wake mku Zena kuonyesha maonevu ya kijinsia yanayoendezwa katika maswla ya mpigaji kura na uongozi.
 • Anatuonyesha jamii ambayo mwanamke anachukuliwa kuwa hawezi kuongoza. Ndiyo sababu hata katika elimu watoto wengi wa kike wananyimwa.
 • Kutokana na mwandshi,uzindushi wa kielimu na uongozi aliopata zena kutoka kwa rafiye carol, ulimfanya Zena kuwa mkakamavu kiasi kwao. Hili ni jambo ambalo halijawahi kuonekana katkika jamii hii.
 • Anatuchorea jamii iliyojengeka katika tasubi za kiume. Ajabu ni kwammba hali imewaingia hata wanawake wenzake.
 • Anaonyesha namna jamii hii ilivyo mbali kuukubali uongozi wa mwanamke.
 • Uongozi hutawaliwa na kiasi cha fedha alichonacho mtu. Maskini Zena hangeweza kuwaleta wapiga kura kutoka mabli na kuwalionga wampigie kura.
 • Umma usiomjua wajibu wao katika kutena viongozi
 • Umma hauoni uwezo wa kwa wa kubadilisha maisha yao bali wako tayri kuuza kura zao.
 • Anaonyesha ilivyo vigumu kwa mwanamke kupata nafasi ya uongozi.
 • Mwandishi ana matumaini kuwa hali inawez kubadilika kutokana na majuto ya badhi ya wakaazi wanaoonekana kujiuma vidole wakijuta (zozote 10X2) ala. 20

 

2.

 • Zena kunyimwa haki ya kuendelea na masomo
 • Zena kuozwa mapema
 • Zena kupigwa na Ali.
 • Zena kutusiwa [ Iteuzi]

 

 • Kuumia wembe mmoja kuchanjia wateja wengi – ulaghai.
 • Uasherati [ siku ya Mganga]

 

 • Bintiye Mavitu kutungwa momba na jirani.
 • Mavitu kunya ng’unywa kijishamba na jirani.
 • (Kachukwa hatua Nyingine)
 • Ulagahi wa salim _ (pwagu)
 • Mawaziri kukojoa ndani yam to.
 • Hongo na mirungura. [ Mayai Waziri……..]

 

 • Tanbihi:
 • Lazima mtahiminwa ataje hoja kasha atambue hadithi. (zozote 10×2) ala. 20

 

3  Ni kweli kuwa kezilahabu ametumia jazanda nyingi na ndoto katika uandishi wake

 i) jazanda/ ndoto

 Watoto kumi waliodhoofika afya yao

 Wanadhihirisha umaskini na shida hata ya miaka ya uhuru

 Katika ile ajali, dereva na mama hawakufa ilhali ukombozi alikufa, dereva anasimamia kiongozi wa nchi na mama ni nchi yenyewe

 Kipofu anayepiga ngoma kumi inasimamia viongozi wasiokuwa na mwelekeo au maneno mema kwa taifa

  Ile lama ya “X” iliyoandikwa na ukombozi kwenye picha za viongozi wa baraza la mawaziri inaonyesha viongozi hawa ni wabaya, hawajahudumia nchi ipasavyo

 Kifo cha ukombozi ni jazanda inayoashiria kuwa wananchi hawakupata ukombozi waliotarajia baada ya uhuru. Waliendelea kuzama katika madhila umaskin na shida

 Katika ndoto moja, tunaonyeshwa watoto waliodhoofika na wanapewa chakula na ukombozi wanakula na kukimaliza; ishara ya njaa nchini

 Katika ndoto ya pili ukombozi anatumia vitabu vya wenzake kupandia juu ili kufikia picha za mawaziri na kuziwekea alama ya “X” kudhihirisha hawajafanya kazi ya ipasavyo zozote 4×5=20

 

4.  a) Anayesema maneno haya ni likono

Anajisema yeye mwenyewe (tashtiti)

Yuko katika hospitali ya Kenyatta alikopelekwa na mwuguzi Fulani baada ya kugongwa na gari kasha kupelekwa hospitali amabko hangeweza kugharamia malipo ya matibabu

Bwana aliyemgonga alipotelea mbali hakumshughulkia kwa vyovyote zozote 4×1=4

 

  b) Ni kweli hii ni dunia ya dua la kuku halimpati mwewe, maanake wanyonge wananyanyaswa

  na kudhulumiwa na matajiri kama ifuatavyo:

– Kizito hakutaka kumpleka likono hospitali licha ya kwamba yeye ndiye aliyekuwa na

makosa alipomgonga

Aidha kizito alidhihirisha madharau kwa kuwaita watu “wajinga wa pira”

Kizito alitoka garini polepole kwa tahadhari asikanyage maji ilhali Likoni alikuwa amelala mle majini.

Kizito hakufurahi Likono alipowekwa katika gari lake kwani aliona angelichafua.Haonyeshi huruma kwa Likoni.

Kizito alimpeleka Likono katika hospitali ya Gipfu na kumwacha huko bila kumlipia gharama ya matibabu.

Dhuluma vilevile inadhihirika pale ambapo daktari Gipfu anataka malipo kabla ya kumhudumia Likono.

Aidha daktari wa Gipfu alipendekeza upasuaji wa Likono ilhali mgonjwa hakuhitaji huduma za aina hiyo.

 Dhuluma vilevile inaendelezwa na mwajiri wa Likono anapomwachisha kazi ilhali alielewa

fika kuwa likono alikuwa mgonjwa. zozote (8×2=16 halimpati Mwewe’

 

5.  “Ndimi za mauti” na Arege

 (a) Muktadha  (al. 4)

  (i) Ni sauti akilini mwa Mbunda

 (ii) Yeye na wenzake Kamalina na Musesi walichoma bweni ili kumwadhibu mwalimu mkuu.

 (iii) Wanafunzi wenzao walichomeka ndani wakiwemo rafiki zao

 (iv) Watu walilaani waliotekeleza kitendo hicho

 (v) Mbunda aliamua kujisalimisha kwa askari  (zozote 4×1=al.4)

 

 (b) Mbinu za uandishi  (al. 2)

(i) Ushairi/wmbo

(ii) Takriri

(iii) Sauti  (zozote 2×1=al. 2)

 (h) Uhalisia katika ‘Ndimi za mauti’  (al. 4)

  (i) Malezi mabaya ya watoto

– Mbunda anasema ya kwamba hajawahi kugombezwa na hata kuadhibiwa na babake

 (ii) Adhabu ambazo zimepita mipaka/katili /zza kinyama

  – Mwalimu mkuu kuwaadhibu wanafunzi na kuwakasirisha hadi kuchukua hatua ya

kuchoma bweni

 (iii) Kanuni/sheria za shule ambazo zinawanyima wanafunzi uhuru ;kamaliza anadai kuwa

wao ni mahabusu wa mwalimu mkuu shuleni

 (iv) Mapuuza ya wale wenye mamlaka

Tume inaandaliwa kuchunguza uongozi wa mwalimu mkuu baada ya wanafunzi kuchoma bweni na wanafunzi wenzao

Viranja na walinzi kukosa kutambua njama ya wanafunzi kuchoma bweni na kuzuia kutokea kwa tendo hilo

Wazima moto kufika kama wamechelewa shule kukosa vifaa vya kushughulikia mikasa ya dharura kama vile moto shuleni

 

 (v) Majuto kama mjukuu

 – Kamaliza na Mbunda kujutia uchomaji shule na kujisalimisha kwa vyombo vya

usalama/ askari

 (vi) Uchomaji wa shule kama njia ya kuwaadhibu viongozi wa shule

 • Kamaliza anasema kuwa uchomaji wa bweni ni njia ya ‘kumshutua’ mwalimu mkuu kwa kuwaheshimu/kuwakazia.

 

 (vii) Uteuzi wa Tume za kuchunguza majanga na uhalifu baada ya tukio/hasara kutotendeka

 • Uchunguzi ulianzishwa kuchunguza uongozi wa mwalimu mkuuu wa shule baada ya bweni kuchomwa
 • Askari wanaanza kutafuta aliyehusika katika uchomaji wa bweni baada ya bweni kuchomwa

 

 (viii) Majengo yasiyozingatia viwango vya usalama

 •  Bweni la wanfunzi lilikuwa limekomelewa kwa nje

Madirisha yalikuwa yamewambwa kwa vyuma /nyaya kwa madai ya usalama wa wanafunzi

 

6.  (II) Umuhimu wa Gege

 (a)- Ametumiwa kuonyesha madhara ya tamaa. Tamaa huwafanya watu kutenda maovu.

(Gege anakubali kumuuwa nduguye ili apate mali)

 (b)- Ujinga ni kizingiti cha mabadidliko ya kweli katika jamii  

 (c) – Ukatili haulip chochote. Gege hakufurahia vitu alivyovikamia

 

II. MKIMBIZI – MWONGOZO

 • Vifo – watu wengi walikufa
 • Nyumba zilichomwa moto
 • Kutengana kifamilia  
 • Ukosefu wa chakula  
 • Ukimbizi
 • Kusafiri kwa mwendo mrefu- uchovu  
 • Tisho la kuuwawa  
 • Masomo kukatizwa  
 • Mazingira mabaya – kulala kwenye baridi  
 • ukosefu wa usalama  
 • Kuathiriwa kisaikolojia – baada ya kuona miili ya waliokufa  
 • Maradhi/magonjwa ya kuambukizwa  
 • Uharibifu wa mali  
 • Uhitaji wa habari kutokana na ukosefu wa vyombo vya mawasiliano

 

7.  a) Muktadha

 1. Anayezungumza ni (msimulizi) ambaye ni mhusika mkuu/ mkimbizi
 2. Wako njiani wakitorokea nchi jirani
 3. Alikuwa na wakimbizi wenzake wakitoroka vita walipotishwa na askari na kuwafanya wasimame ghafla kwa uoga na hofu
 4. Ni katika hofu hiyo iliyomtia kuyatamka maneno haya kuhusu askari waliokuwa mbele yao

b) Mbinu

 1. Taswira – jinsi walivyosimama …………….. ardhini
 2. ii) Tashbihi- kama tumesimikwa

c) Kwa nini akakumbuka mama na ndugu zake

Aliona miili ya wafu (maiti) iliokuwa imetapakaa kila mahali

d) Matatizo ya wakimbizi

 1. Maradhi k.v. kipindupindu na kifua kikuu
 2. Uhaba wa hakula
 3. Vifo njiani k.m. Jesse
 4. Ukosefu wa usalama wa wakimbizi
 5. Ukosefu wa maji safi ya matumizi
 6. Tatizo la kuvuka mto baluke ulipokuwa umefurika

e) Maudhui yanayoibuka:

 1. Vita – watu kupigana kusababisha ukimbizi
 2. Ukabila – kati ya walutu na watutsi
 3. Vifo – kutokana na vita pia magonjwa
 4. Utengano – familia zilitenhana
 5. Hofu/ woga – ilioletwa na vita, watu kuuawa

 

8.  (i) MAKULU

Mtu aliye na nafasi. Anampa Nanda kibarua na kumplipa. Ni muhimu kwa kuwa anawasaidia wakazi wa eneo lile pale wanapokuwa hawana hela.

Ni Mkarimu – kuwapa watu bidhaa ili kuwakopesha kama Nanda kuuza mihadarati.

 • Anawaajiri watoto wadogo. Mfano ni Nanda ambaye anaajiriwa na kupewa zawadi na pesa.
 • Ni mkosa maadili – kule kuwatumia watoto wadogo kulangua mihadarati
 • Ni msiri kwa kuwa anayafanya haya yote bila kumwambia yeyote
 • Ni mwenye bidii- Aendesha duka kwa bidii. Analima mashamba yake
 • Ni mnafiki kwa kuwa anajifanya rafiki mkubwa wa Mzee Atanasi huku akimharibu mwanaye.
 • Ni mwongo kwani Mzee Atanasi aliwahi kumweleza kuhusu mabadiliko ya Nanda na akasema yeye hana habari na mabadiliko hayo.

 Umuhimu wake:-

 • Anatusaidia kufahamu kuwa sio vyote ving’aavyo ni dhahabu
 • Ni kielelezo kuwa matajiri wengi hawakutajirika vivi hivi
 • Tunajifunza kutowaamini watu wengi hadi kuwapa watoto wetu kuwafanyia kazi

 (ii) MWALIMU

 • Anaielewa taaluma yake. Anafuatilia maendeleo ya mwanafunzi wake Nanda
 • Anawajibika . Ndio sababu amwita babake Nanda ili wajadiliane juu ya mabadiliko ya Nanda
 • Ni mshauri mwema. anamshauri Mzee Atanasi la kufanya ili kumwokoa mwanaye
 • Anajua kuweka miadi. Alimwalika Atanasi afike mapema naye amesubiri
 • Ni mtu makini sana. Ndio sababu ametambua mabadiliko ya Nanda miongoni mwa wanafunzi wengi

 Umuhimu wake

 • Kielelezo cha umuhimu wa kuwajibika kwa walezi wa kila nui
 • Ni kielelezo cha ulezi bora
 • Anatuonyesha umuhimu wa kuwa makini kazini

 

 (iii) MZEE ATANASI

 • Si makini- mwanaye anaonyesha mabadiliko naye hana habari.
 • Ana mapuuza. Yale mabadiliko anayoyaona katika maisha ya Nanda anayapuuza na kuchukulia tu kuwa mtoto anakua
 • Ni mshirikina . Akiambiwa kuwa mwanaye kabadilika anachukulia kuwa amerogwa na jirani yake Andanda.
 • Ni Mzembe. Amezembea jukumu la kumlea Nanda

 Umuhimu wake

 • Kielelezo cha wazazi wasiowajibika
 • Kielelezo cha hasara inayoweza kutokana na kuamini mambo ya ushirikina
 • Ni kielelezo cha urafiki wa chati
 • Ni kielelezo cha hasara inayotokana na ukwepaji wa majukumu

(Makulu – al. 7, Mwalimu al. 7 Atanasi – al. 6 = al. 20)

 

9. (a) (al. 5) – Mkimbizi

 •  Kukatizwa kwa masomo
 •  mauaji
 •  uharibifu wa ali
 •  uhasma miongoni mwa makabila
 •  magonjwa/maradhi
 •  kutamauka(kukata tamaa)
 •  kugura maeneo
 •  njaa na kukosa malezi
 •  kukabilia nahatari  (hoja zozote 5x 1= al. 5)

  – Fumbo la mwana

 Kuzorota kwa masomo

 kuzorota kwa afya

 kuzorota kwa usafi

 uvunjaji wa uhusiano

 kutowajibika  (zozote 5×1 = al. 5)

 

 (b) Uteuzi wa moyoni

 -Kukatizwa kwa masomo kwa wanawake

 – Udhalimu dhidi ya wanawake

 – Kunyimwa nafasi katika mambo ya siasa

 – Chombo cha mapenzi

 -Kutukanwa na kuteswa

 – Kutokuwa na suti  (zozote 5×1=al. 5)

 

 Ngome ya nafasi

 • Ndoa ya lazima
 • – Kukatizwa kwa masomo
 • – Hawana uamuzi
 • Hawana sauti
 • – Kudhulumiwa
 • udhalimu kutoka kw awanawake wengine
 • kukandamizwa na sheria (zozote 5×1= al. 5)

 

10.  a)

 • Dereva alimgonga Likono kwa gari lake
 • Alitaka kutoroka lakini alimlazimisha kumpeleka hospitalini
 • Alitaka kuficha ukweli kuwa hakuhusika katika ile ajali ila tu alijitokeza kama mwokozi

  b)

  • Msamaria mwema halisi (katika biblia) alimpa huduma ya kwanza mgonjwa wake jambo ambalo Dereva hakufanya
  • Alimbeba bila kumshurutisha na yeyote
  • Aligharamia mahitaji yote jambo ambalo Dereva hakufanya

  c) Dereva si mzingatifu

  Aliendesha gari huku akiongea katika rununu yake

  Barabara mbovu mfano Vidimbwi vya maji machafu

  Utovu wa utu na kuthamini sana gari lake – angeweza kumgonga binadamu kwani hana thamani yoyote ukilinganishwa na gari lake ‘Toyota Prado’

  Likono pengine alizama katika mawazo sana kuhusu masaibu yaliyomkumba, na ghafla kugongwa  Zozote 3×2=6

  d)

  • Anapoulizwa kilichotendeka, alisitasita dhihirisho la uongo- alipanga atakayosema mfano alijikohoza kikohozi cha bandia kabla ya kusema
  • Usamaria wema wake hungefika tu plae yaani kumleta hospitalini bali angemshughikia zaidi
  • Dereva na mwenye gari wanatoroka wakidai kwenda kutafuta pesa
  • Mwenye gari anafika mwanzo wanaenda chumba ‘Nzengwe’. Wanaongea huku wakitupa macho ya kuibaiba – Ishara ya kupanga watakayosema
  • Dereva na mwenye gari wanajaribu kumchanganya Likono kimawazo ati kagongwa na ile “Nissan Prado’ ilihali alijua visuri gari yake ni Toyota Prado Zozote 4×2=8

 

11.  A. Mbinu ya majazi

 i) kachukua hatua nyingine – mavitu – mwenye mali /mambo mengi

  – Shemeji – mke wa ndugu

 ii) Msamaria mwema – Kzito – uwezo/ tajiri

 iii) Pwaguzi – Shehe – kiongozi wa dini ya kiislamu

 iv) Tuzo – Kibwana – mtu anayejiona mkuu bila ukuu

 v) mayai waziri wa maradhi – Ukombozi

  – Mayai mtu ovyo

  – Dr. Pondamali  

 B. Mbinu rejeshi

 i) kachukua hatua nyingine

– Sakira kukumbu jinsi nduguye alivyomsaidia

– Sakira anakumbuka alivyoacha kazi na kujuta

 ii) Fumbo la mwana

 iii) Mkimbizi – Anakumbuka walivyouawa wazazi

 • Anakumbuka alivyokufa jesee n amzee savalanga

iv) Anakumbuka wosia wa mzee savalanga  

 

 

12.  (a) Uteuzi wa moyoni

 1. Wanawake wanapigwa na wanaume zao
 2. Ndoa za lazima
 3. Kufanyishwa kazi nyingi za nyumbani
 4. Kupewa elimu duni – darasa la nne, tano
 5. Kuitwa Malaya
 6. Kuadhibiwa na waume zao
 7. Lawama za kutopata watoto ziliwekewa wao
 8. Kutofaulu kwa ndoa walilaumiwa wao
 9. Mwanamke anajukumu la kumfurahisha mwanaume
 10. Kuozwa kwa mabinti mapema
 11. Mabinti kuachishwa masomo ili waolewe  (10×1=10)

 

(b) Ng’ombe ya nafsi

(i) Mabinti kuozwa mapema

(ii) Kuachishwa shule ili kuolewa

(iii) Kuozwa kwa lazima

(iv) Wanawake kupigwa

(v) Wanawake kuunga mkono utamaduni unaonyanyasa

(vi) Wanawake kutishiwa talaka

(vii) Utamaduni ulikubali ubakaji wa wanawake

(viii) Wanawake kulaumiwa kwa kutopata watoto

(ix) Msichana kutumiwa kuchumia mali

(x) Wanawake kutopewa nafasi ya kuchangia maswala ya ndoa   (10×1=10)

 

13.  Masuala Ibuka

 i) Ukimwi – siku ya mganga

– Mwaibale anausambaza kwa wembe

– wagonjwa/ wateja wamekondeana na kudhoofika kiafya

 ii) Haki za watoto i) Kuchukua hatua nyingine

– watoto kukosa sare, karo, chakula na kwenda shuleni

– Ajira ya watoto

– Mtoto kupachikwa mamba

ii) Fumbo la mwana

– dawa za kulevya

iii) Ngome ya nafsi

– Watoto kuozwa mapema

iv) Uteuzi wa moyoni

– Ndoa za mapema

– wasichana kukosa elimu

 iii) Ufisadi  – Mayai waziri, waziri fisadi, wizara ya mlungula

– Msamaria mwema – Bw. Kizito Kibambo

– Uteuzi wa moyoni – wapiga kura kuuza kadi zao

– Ngome ya nafasi – Chifu alihongwa, kuficha wahalifu

 iv)   – Matumizi ya dawa za kulevya/ mihadarati na madhara yake kwa vijana

Fumbo la mwana

Nanda anatumia dawa za kulevya

Anazorota kimasomo, mchafu n.k

v) Ndoa za mapema kwa wasichana

– Zena aliozwa mapea – uteuzi wa moyoni

– Ngome ya nafsi – Naseko anaozwa kwa mzee

vi) Migogoro shuleni

Ndimi za mauti – Wanafunzi kuchoma wenzao bwenini

Mayai waziri – Migomo ya walimu

vii) Vita vya kikabila na suala la wakimbizi

Mkimbizi

ix) Uongozi mbaya – Kuchukua hatua nyingine

Uhalifu wakati wa kura

Viongozi walikosa uwajibikaji

Chifu kuuza chakula kilichotolewa bure wakati wa ukame

Serikali ilifutilia mbali elimu ya bure na kusababisha maskini

Mayai waziri wa maradhi

Waziri mayai

Viongozi walafi

x) Uhalifu katika jamii

 – Pwaguzi

 – Salim ni tapeli na mizi mkuu

 – Kuchukua hatua nyuingine

 – Ngome ya nafsi

xi) Umaskini

kuchukua hatua nyingine

fumbo la mwana

msamaria mwema

mayai waziri wa maradhi

xii) Haki za wanawake katika jamii

Uteuzi wa moyoni

Ngome ya nafsi

Kuchukua hatua nyingine

Mayai waziri wa maradhi

Mayai haishi na mkewe

 

14.  Dhamira ni lengo/ nia ya mwandishi wa ‘Tuzo’

 i) . Anaashiria kauli kuwa yote yaweza yakatokea hata yasiyotarajiwa k.m. Salome na

kibwana hawana mkabala mzuri lakini Salome anakuja na kumletea habari. Mwandishi

aonyesha kuwa hafla ama matukio huleta wengi pamoja hata wasiosemezana wala

kuamkuana

ii) Anaonyesha kuwa mapeni ni msingi wa mengi. Nia ya kibwana unapokataliwa inakuwa

chanzo cha kutosemezana kwao tena

iii) Anaonyesha kuwa kunao, wakaao pamoja na kufanya kazi pamoja lakini hawana mkabal

mzuri, wao husemezana tu kwa sababu ya kikazi walakini wakitoka nje wanakuwa

mjamba miwili isiyoamba. Salome na kibwana wanasemezana wakati wa kazi

iv) Pia anatuonyesha kuwa kuna wenye vitendo vizuri vyenye sifa. Vitendo vyao vinajulikana

wazi wazi (kama saui zao)lakini wenyewe hawajui vitendo vinaweza kumtambulisha mtu.

v) Kuna haja ya kumtuza aliyefanya vizuri wanahabari wanatuzwa akiwemo Salome Dzoro

vi) Hamu ya kutuzwa huwa hasa katika sherehe ambayo mtuzwa hajatengezwa hadharani.

Tunaiona hamu aliyonayo kibwana

vii) Pia anasisitiza umuhimu wa kauli tahadhari kabla ya athari na kuwa mwangalifu

 Anaonyesha umuhimu wa kuwaza kabla ya kutenda

 Kibwana angalichunguza kwa makini hangeaibika machoni pake vile.

Tunaelewa alichanganyikiwa hadi katika choo cha wanawake

viii) Anathibitisha ukweli wa methali mzaha

 Mzaha hutubga usaha

 Mzaha wa Salome wa kumtania kibwana unamletea aibu na kuvurugika akili

ix) Anaonyesha jinsi kutaniana na kuchezeana shere kamwe hakufai. Hii huweza kuleta vita

namna kibwana alitaka walakini akajizuia

x) Anataka kuonyesha jinsi furaha huathiri akili. Kibwana alizidiwa na furaha na kusahau

kuwa anaweza kutaniwa. Mwandishi anaonyesha kuwa kuna kilio au aibu inayoweza

kutokana na futahi hiyo

xi) Anataka kuashiria kuwa vita sio suluhisho kwa kosa ulilotendewa. Kibwana alifumbata

konzi kutaka kuirusha walakini anajizuia. Hili ni funzo dhabiti kuwa haitupasi kusuluhisha

kwa vita

xii) Ni kawaida kuoa anayetuzwa akiringa ama akitembea kwa madaha. Tunaambiwa kuwa

Salome alitembea kwa ndweo kwenda kuitwa zawadi yake. Zozote 10×2=20

 

15.  a) Muktadha

 1. Msemaji ni Kaloo
 2. Anamwambia Mwelusi
 3. Kaloo alikuwa anaanda uwanja kwa mkutano wa kiongozi alipomwona Mwelusi
 4. Anapomwuliza anachofikiria anajibu kuwa anafikiria misha ya wananchi wote.(Al 4×1=4)

b) Ushahidi wa kudhihirisha kauli hii

 1. Gege nduguye Mwelusi anapenda kucheza ala ya muziki
 2. Yuko tayari kumsaliti nduguye kwa ahadi kuwa ataozwa binti wa Bokono Alida
 3. Muda wake anautumia kuzurura tu na kushiriki katika starehe na anasa
 4. Yeye hajali wala hashiriki katika shughuli za ukombozi wa Butangi (Zozote 3×2=6)

c) Mchango wa vijana

 1. Kuwaza kuhusu maisha ya umma
 2. Wanapigania ukweli na amani – Azena, Mwelusi, Andua
 3. Wanapinga mateso, Mwelusi
 4. Wanatetea uhuru, haki na heshima kwa kila mwanabutangi – Mwelusi
 5. Wanataka kutatua matatizo ya raia
 6. Wanawafahamisha wananchi kuhusu haja ya utawala wenye msingi wa haki – Mwelusi
 7. Wanahimiza maendeleo kwa wote
 8. Wanatumia maarifa kuondoa dhuluma k.m Atega kutumia mkate wa wishwa na tupa
 9. Wanaasi utawala usiofaa m.f Andua kuteka maji katika kisima cha mkomani

  (Alama zozote 10 x1 = 10)
Share this:


EcoleBooks | Maswali ya Hadithi Fupi : K. WAMITILA: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINEZO na Majibu Yake

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*