Share this:


UANDISHI WA MATANGAZO

Matangazo ni habari za kijamii katika vyombo vya habari kwa lengo la kushawishi au kutoa taarifa kwa jamii ili kununua, kuuza au kupata taarifa iliyokusudiwa kwa muhtasari. Matangazo hulenga watu mahsusi kwa jamii
Dhima za matangazo katika jamii
 • Kutangaza bidhaa mbalimbali
 • Kutoa tahadhari kabla ya tukio linalokusudiwa kutekelezwa siku za usoni
 • Kuelimisha jamii – hutumika kama kutoa ujuzi, stadi, maarifa mbalimbali: mfano; kuhusu UKIMWI, Malaria, Kipindupindu n.k
 • Kusaidia kuboresha shughuli za kiuchumi
Mambo muhimu katika uandishi wa matangazo
 • Kichwa cha habari (kuandikwa kwa herufi kubwa)
 • Kufanya aina ya biashara (kama matangazo ya biashara)/ aina za bidhaa
 • Mahali inapopatikana hiyo bidhaa au huduma
 • Kufanya njia ya mawasiliano
UANDISHI WA MATANGAZO MAGAZETINI
Vitu vya kuzingatia
 • Kutilia mkazo dhumuni la tangazo hilo
 • Kutumia lugha rahisi yenye sentensi fupi zenye tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa
 • Kutumia vivumishi vyenye kuvutia na kushawishi walengwa
 • Kutumia lugha ya kibunifu
Mfano wa matangazo
EcoleBooks | KISWAHILI KIDATO CHA 3 - UANDISHI WA MATANGAZO

UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA
INSHA- Ni kifungu cha habari chenye aya moja au zaidi. Insha hizo zinaweza kuwa za kisanaa au zisizo za kisanaa.

Insha za kisanaa-Hizi ni Insha ambazo hutumia vipengele mbalimbali vya fasihi katika kuwasilisha ujumbe. Mfano nahau, methali, misemo au tamathali za semi huweza kutumika

Mfano wa Insha za kisanaa

Mzee toboa mpenda haki

-Mzee toboa ni dereva wa teksi kwa miaka mingi jijini Dar es Salaam kutokana na uzoefu wa kazi yake, Uaminifu, Uzungumzaji na Ucheshi kwa wateja wake aliweza kujipatia chumo nono la kila siku. Wenzanke walimwonea gere mzee huyo, maana hata anapokuwa katulia katika kundi la madereva akisubiri abiria wa kukodi teksi wengi humtaka yeye. Alikuwa na Umri wa miaka arobaini au hamsini hivi, mwenye Umbo la wastani si mnene wala si mwembamba aidha si mrefu wala mfupi kichwa chake hakikuwa kikubwa lakini kilijaa busara. hulka njema na hekima yake kubwa vilimfanya aheshimiwe na watu.

Japokuwa hakusoma sana, mzee Toboa alijaliwa kuijua siasa ya nchi yake barabara. Alikuwa na tabia ya kuongea na kila mtu, watoto, vijana,wazee, viongozi matajiri na makabwela, kwa maneno mengine mzee Toboa alikuwa mcheshi na mwema. Kwa tabia yake hiyo aliweza kujua matukio mbalimbali mitaani kwa urahisi zaidi. Yeye hakupenda Uovu wala dhuluma. Alisubiri kwa hamu siku ambapo maovu yangetoweka kabisa .

Mzee Toboa aliweza kukemea watoto wenye tabia mbaya kwani aliweza kuwaambia Asiyesikia la Mkuu huvunjika guu, kwa maana kwamba Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Mzee Toboa aliweza kufanikiwa kujua kila Ovu lililokuwa likitokea kwani aliweza kuchukua hatua harakaharaka.
Share this:

EcoleBooks | KISWAHILI KIDATO CHA 3 - UANDISHI WA MATANGAZO

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*