Share this:

Maswali ya TAMTHILIA: KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA

1.  Kwa kurejelea tamthilia ya “Kifo Kisimani”, eleza jinsi utawala mbaya unavyoathiri jamii

 

2.  Kwa kurejelea diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine, tetea kauli kwamba

 “Hadithi katika Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi Nyingine inamulika jamiii iliyojaa uozo

 wa kila aina  

3.  . . . hatuwezi kuendelea kuwa na mwiba katika mguu wa Butangi . . .Butangi imo

  safarini . . . imo mbioni . . . Inasonga mbele.

  (a) Eleza muktadha wa dondoo hili  

 (b) Ni mbinu zipi za sanaa zilizotumika katika dondoo hili? Taja na utoe mifano

 (c) Taja na ufafanue sifa zozote tano za anayezungumza.

 (d) Taja na ueleze mfano mmoja wa maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili

4.  Linganisha hulka za wahusika wafuatao. Gege na Mwelusi kisha ueleze umuhimu wa Gege

katika tamthilia hii

5.  (a) Eleza mchango wa wahusika wafuatao katika harakati za ukombozi katika tamthilia

ya Kifo Kisimani.  (al.14)

ecolebooks.com

(i) Mwelusi

(ii) Raia

(iii) Nyalwe

(iv) Askari I na Kame

 (b) Mbali na haki ya kuchota maji kisimani, taja mambo mengine sita ambayo Mwelusi

  angependa yazingatiwe katika Butangi mpya.

6.  “…Njiwa na kozi ni ndege wenye maisha tofauti; Tungalikuwa sote njiwa au sote Kozi …”

 (a) Eleza muktadha wa mazungumzo haya.  

 (b) Eleza mbinu ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili.

 (c) Kando na mbinu uliyoitaja katika swali la (b), taja na kueleza mbinu nyingine za

  lugha tano zilizotumiwa katika tamthilia ya Kifo Kisimani.  

 (d) Ni vipi mzungumzaji ni kielezo cha wanyonge katika tamthilia ya kifo kisimani?  

7.  Linganisha wasifu wa wahusika wafuatao na uonyeshe umuhimu wao katika tamthilia ya

 Kifo Kisimani.    (i) Mtemi Bokono

 (ii) Mwelusi

8.  “Kazi ya mikono yangu yenyewe nimeuchomoa mwiba tayari, kisu kilimpata sana tumboni.

  Pengine kwenye ini au wengu”.

 (a) Eleza muktadha wa dondoo hili  

 (b) Ni yapi yaliiyomfanya msemaji kuuchomoa mwiba  

 (c) Fafanua yaliyofuata kauli hii na hatima ya wazungumzaji

9.  Huku ukirejelea tamthilia ya Kifo Kisimani fafanua vile uongozi mbaya unaweza kuwa kikwazo

 cha maendeleo katika jamii

10.  Eleza jinsi vijana walivyosawiriwa katika tamthilia ya ‘Kifo Kisiamani.”

11.  “Nimeshakwambia tulale hapa langoni! Tulale umati unaokuja kumtoa mfungwa gerezani utukute

 hapa. Watu wanatupenda sana kwa kazi nzuri ya kumzuia mfungwa gerezani. Kwa hivyo

tuwasubiri waje watupake mafuta.”

 (a) Eleza muktadha wa dondoo hili

  (b) Taja na kueleza mbinu ilivyotumika katika dondoo hili

 (c) Eleza kwa kutolea mifano maovu matano yaliyotekelezwa na wahusika katika dondoo hili

12. A : Mtemi ataingia hivi punde. Na anatarajia kusikia habari nzuri …

B : Mtemi nataka kumsamehe kwa masharti gani ?

(a) Eleza muktadha wa maneno haya  

(b) Taja masharti ambayo yanarejelewa hapa

(c) Jumuiya ya Butangi ililemewa na ufisadi. Eleza

13.  Tamthilia Kifo Kisimani imedhihirishaje ukweli wa methali ‘Kikulacho ki nguoni mwako ?

14.  Butangi ni kielezo cha mojawapo wa nchi za kiafrika zianzua. Thibitisha.

15.  a) Taja jazanda zilizotumika katika tamthilia ya kifo kisimani na ueleze maana yake  

 b) Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika

i) Methali  

ii) Tashhisi  

iii) Kinaya  

16.   “Msimamo wangu hautokani na uoga, unatokana na kuthamini maisha ya binadamu”

 a) Eleza muktadha wa maneno haya

 b) Eleza sifa za anayeambiwa maneno haya  

 c) Taja wahusika wanne wanaoendeleza maudhui ya uzalendo katika kifo kisimani  

 d) Eleza msimamo wa mwandishi wa tamthilia ya Kifo Kisimani kuhusu uongozi mbaya

 

17.  “Ha-li Haa-ih! Nyoka ameniuma! Sumu ya nyoka!

 (i) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili  

(b) Maneno haya yanaashiria nini kuhusu hali ya mnenaji?  

(c) Taja mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili

(ii) Jadili mbinu alizotumia Mtemi Bokono kuudhiti utawala wake  

18.  Diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi imejikita katika masuala ibuka yanayofaa kushughulikiwa

 na jamii. Taja na uthibitishe.

19.  Fafanua dhamira ya Ken Walibora alipoandika kisa cha “Tuzo”  

 

Majibu ya TAMTHILIA: KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA

1.  Athari za utawala mbaya kwa jamii

 • Dhuluma- unyanyasaji- usaliti
 • Wanajamii kutiwa kizuizini kwa kuchongwa makosa- Mwelusi
 • Wanajamii kulazimishwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa
 • Makabila kuchochewa/ kushambuliwaili kueneza hofu- Wanabatuitui na Wabausi
 • Wanajamii kuteswa kwa kuuawabila sababu maalum- Askari wa pili na mshukiwa- Mwelusi
 • Mwelusi kuteswa na baadaye kuuwawa
 • Ukosefu wa chakula kusababisha njaa
 • Uharibifu wa mazingira na viongozi kunyakua misitu kujifaidi
 • Unyakuzi wa ardhi ya umma- uwanja wa kuchezea watoto
 • Wananchi kunyimwa haki za kutumia raslimali za jamii- maji ya kisima
 • Jamii kugawika katika matabaka mbalimbali viongozi na vibaraka wao kisha wananchi
 • Mauaji ya wazalendo wanaopinga utawala mbaya
 • Mizozoz katika familia- Nyalwe anazozana na mumewe Bokono kwa kuupinga utawala mbaya
 • Gege anazozana na mamake kwa kuwa kikaragosi wa kutumikia utawala mbaya
 • Gege anazozana na hatimaye kumuua nduguye Mwelusi kwa kudanganywa
 • Ufisadi- Watu kuajiriwa bila kuzingatia uwezo/ elimu au tajriba- motto wa Kaloo
 • Unyanyasaji wa kijinsia- Andua kupapaswa

 

2.  Jamii ilivyojaa uozo katika mayai Waziri wa maradhi na hadithi nyingine

 UTEZI WA MOYONI

 • Wanawake kutopewa elimu ya kuwawezesha kujikimu
 • Wanawake wanaozwa wangali wachanga wala hawana hiari ya kujichagulia waume
 • Taasubi za kiume k.m Ali alivyomdhibiti Zena na wanawake kulaumiwa kwa kukosa kuzaa
 • Wanawake kuchukuliwa kama vyombo vya wanaume na kupigwapigwa bila sababu
 • Wananchi kuuza kura zao badala ya kushiriki katika kujagua wabunge watakaotetea haki zao

SIKU ZA MGANGA

 • Watu kumwendea mganga mganga ili kupata cheo
 • Mganga kumpatia Asteria mume wa mke mwingine kwa kutumia uganga
 • Mganga Mwaibale kuwaibia wateja kwa kudai alinunua jembe kila wakati
 • Uzinifu- Asteria na mazungumzo yake na rafikiye kuhusu kiruka njia

 

  KACHUKUA HATUA NYINGINE

 • Uongozi mbaya unaokubali mauaji ya wapinzani k.m. Kala nduguye Sakina
 • Chifu kuuza chakula cha bure kilichotolewa kwa watu maskini
 • Jirani kumtunga motto wa Mavitu mamba
 • Mavitu kunyang’anywa kipande cha ardhi na jirani na deni lake kuongezwa

 

  PWAGUZI

 • Shehe kijuba kujihusisha na upigaji ramli
 • Salimu kuwaibia watoto 2500/= na Shehe 10,000/=
 • Tamaa ya shehe kumfanya amkaribishe Salimu kwake akamfungie vijana ili aendelee kupiga bao
 • Shehe Kijuba alikuwa mnafiki aliyejifanya kuelewa mambo ya dini lakini wapi

 

 TUZO

 • Ufisadi unamfanya profesa Dzoro umtangaza Salome Dzoro kama mshindi kwa kuwa alikuwa amu yake
 • Unafiki- Salome kumdanganya Kibwani kuwa alikuwa mshindi akijua vizuri kuwa ilikuwa uongo
 • Ubaguzi- Profesa Dzoro kuwabagua washindani wengine na kuchagua aliyekuwa naye na uhusiano wa kidamu

Hakiki majibu ya wanafunzi na kuutuza hoja yoyote nyingine iliyo sahihi

Zozote 10×2 alama 20

3.  (i) Anayezungumza ni Bokono

  (ii) Anazungmza na washauri wake Batuzigu na Kame

 (iii) Wako katika ukumbi wa utawala wa Mtemi Bokono

 (iv) Washauri walikuwa wakingoja Bokono aliyetaka kujua hatua watakazochukua

kua(washauri) kumkomesha Mwelusi  (1×4=al.4)

 

 (c) Sifa za msemaji

 (i) Mkatili

 – Anashiriki katika kuwatesa wansnchi anaowatawala, pia anaamrisha aksari kuwa wale wote  wanaokosoa viongozi wateswe kwa kupwa gerezani

 (ii) Ni mwenye kiburi

 • Anaonyesha kiburi kwa mkewe anapomkosoa
 • Hamsikilizi mama Agoro anayekuja kulalamika kwa kwake kuhusu kunyakuliwa kwa kiwanja

 (iii) Mfisadi

– Yeye pamoja na viongozi wengine wanashirikiana kupoa mali ya wanachi kama vile ardhi,

kisima cha Mkomani n.k

 (iv) Ni Mkware

 • Ana tamaa ya wanawake
 • Anafanya mapenzi haramu na hawara Fulani aliyepigwa na mkewe. Anamnyemelea Kaloo

 (v) Mbinafsi

– Utawala wake unalengo la kumnufaisha yeye kwani anautumia kukilimbukizia mali

 (vi) Mnafiki – Amejua hapendwi lakini anajifanya anapendwa

 (vii) Mwenye majivuno – Nadai kuwa uongozi wake ni bora kuliko wa watu wote

 (viii) Ni mwoga – Alihofu sana pale alipohisi kuwa angeweza kung’atuliwa  (zozote 5×2=al.10)

 (c). Mbinu za Sanaa

 • Jazanda/Istiari – Mwiba –kumnyelea mweluso
 • Uhuishi / Tashhisi – Butangi iko safarini – Butangi imo mbioni (2×2=al.4)

 (d). Maudhu

Udhalimu/Unyanyasaji – Vitendo vya kutoa mwiba mguuni ili Butangi kendelee (kumuua Mwelusi)

AU

4.  (I) Gege na Mwelusi

 1. Mwelusi ni mjasiri – anaamua kukabiliana na utawala wa Mtemi Bokono. Haogopi kuteswa na askari. Gege ni mwoga anaogopa kuwakasirisha viongozi, anapitwa an aMweke anatetemeka,
 2. Mwelusi ni mwerevu- anauelimisha umma wa Butangi kuhusu uovu wa utawala wa Butangi na namana wangewa kujikwamua kutokana na uongozi huo-mbaya. Anatumiwa kumuua nduguye
 3. Mwelusi ni mwadilifu – Anashiriki na wanawake katika vita vya ukombozi lakini mapenzi nao (Atega). Gege ni mnafiki /mwongo. Anadanganya mamake
 4. Mwelusis ni mzalendo- anapenda nchi yake ndiposa anajitolea mhanga kupigania mabadiliko. Gege ni mbinafsi – hataki kushughulikia mambo yaw engine
 5. Mwelusi ni mvumilivu – anavumilia mateso ya askari huko gerezani. Gege ni mbishi anabishana na Mwelusi kuhusu utawala wa Butangi, Anabishana hata na mamake

Mwelusi anamsimamo thabiti- anashikilia msimamo ule ule wa kupigania haki za

wanabutangi hadi mwishoni. Anakataa vishawishi vya Bokono. Gege ni msaliti , anamsaliti ndugu yake pale anapotumiwa na utawala wa Bokono.  (zozote 4×4=al.16)

 

5.  Mchango wa wahusika

  Mwelusi

 1. Alitambua chanzo cha matatizo/shida za wanabutangi
 2. Mwelusi na wenzake wajiitao « Nuru ya Butangi » waliwazindua raia kupitia elimu kuhusu haki zao. Gege anathibitisha hayo.
 3. Mwelusi aliwaongoza raia kupigania haki zao kwa kuvunja kanuni/sheria potovu na basi kuleta mabadiliko.
 4. Alijitolea kuteseka na hata kuuwawa kwa ajili ya mabadiliko  (Zozote 4×1=4)

 

 (b) Raia (Tanya, Atega, Andua) au umma.

  (i) Raia walisusia mkutano ambao ulifaa kuhutubiwa na mtemi Bokono

  (ii) Raia kama vile Andua waliandamana na kutetea haki zao kama kuchota maji kisimani – mkomani.

Andua alimkabili zigu kijasiri akidai haki ya kutumia maji ya kisimani.

 (iii) Raia kama vile Tanya walianza kupinga washauri wa Mtemi Bokono. Tanya alimpinga

Batu na kufichua uovu wa serikali ambayo kupitia kwa Batu inatumia askari wa kukodi

kuwashambulia raia ili kulazimisha uzalendo.

 (iv) Raia walisaidia mfungwa (Mwelusi) kutoroka kutoka gerezani. Atega alimpelekea Mwelusi

tupa aliyoitumia kukata minyoro huku askari wakiwa walevi.

(v) Raia walifanya mapinduzi na kuwatega nyara viongozi chini ya Atega  (zozote 5×1=al.5)

 

(c) NYALWE

(i) Aliwasilisha malalamishi ya mama Agoro kwa Mtemi Bokono kuhusu unyakuzi wa ardhi-kiwanja

cha watoto kuchezea.

(ii) Alifichue unafiki wa washauri wakuu wa Mtemi

Bokono kuwa raia hawampendi Mtemi Bokono na utawala wake.

(iii) Alimshutumu/kumkashifu mumewe kwa vitendo vya kuwadhulumu raia.

(iv) Alimshauri mumewe abadilishe uongozi wake ambao ulikuwa unawaumiza raia  (zozote

 

(d) Askari I na Kame

Askari I

 1. Alipinga kanuni za kidhalimu za gerezani za kumtenga mfungwa na jamaa yake
 2. Alipigania haki za watuhumiwa dhidi ya madai kuwa ni waharibifu na pia kupata chakula mfano Mwelusi
 3. Alishirikiana na raia (wapinzani) katika kuung’oa utawala dhalimu wa Mtemi Bokono)
 4. Alikusanya ushahidi wa mauaji ya mtuhumiwa ‘jiwe’ kutoka kwa askari II (zozote 2×1=2)

Kame

 1. Alipinga kumtenganisha mfungwwa (Mwelusi) na uhai/maisha
 2. Alishirikianana na raia katika kuung’oa utawala dhalimu wa Mtemi Bokono
 3. Anaunga mkono kutoroka kwa Mwelusi na kuwaondolea lawama askari jela kuhusu kutoroka kwa mwelusi  (yoyote 1×1=1)

(b) Mabadiliko ayatakayo Mwelusi.

(i) Butangi iliyo na uslama kwa wananchi wote

(ii) Butangi yenye shibe/isiyo na njaa.

(iii) Butangi itakayochukulia sawa watu wote bila kujali kijiji au ukoo.

(iv) Butangi inayozingatia haki na heshima kwa watu wote

(v) Butangi ambayo haibagui mtoto wala wazee/mwanamke na mwanamume

(vi) Butangi iliyo na usawa, haki na maendeleo (zozote 6×1=6

 

6.  (a) Muktadha

(i) Msemaji ni Tanya

(ii) Anamweleza Batu

(iii) Wako uani kwa Tanya

(iv) Batu yuko hapa katika harakati za kumsaka ili amtie kufika kwake kwa Batu

ambaye anamlinganisha na kozi naye njiwa  (zozote 4×1=al.4)

.  (b) Mbinu ya lugha

– Sitiari

– Batu mwenye nguvu na katili ni kozi

– Tanya mnyonge na mnyanyaswa ni njiwa  (ala.2)  (kutaja mbinu 1, maelezo 1= al. 2)

 

 (c) Mbinu za uandishi katika tamthilia ya kifo kisimani  (ala. 10)

 Jazanda

 • Pembe na nyati au kifaru – njia za mauti
 • Mwiba katika mguu wa Butangi- Mwelusi kuwa kikwazo kwa utawala dhalimu wa Mtemi Bokono
 • Njiwa, kazi na vifaranga – tofauti za kitabaka k.v. Tanya ni njiwa, Batu ni kozi, na watoto wa Tanya (Mwelusi, Andua) ni vifaranga.
 • Minyororo – hali ya watu kufungwa
 • Kisima – Chanzo cha uhai wa watu n.k

Tashihisi

 • Mawazo yakanishika miguu – hakuendelea kutembea kwa sababu alikuwa akifikiri.
 • Usipoondoka, utatembelewa na kofi – askari alitisha kumpiga Andua
 • Ulimi wako utakufisha umeme – onyo la askari III kwa askari I kwani alikuwa anatisha madai yake kuwa Mwelusi ni mharibifu.
 • Dunia haipendi wenye kukata tamaa-Azena anamweleza Tanya kuwa duniani hakuna nafasi kwa wanaokufa moyo/kata tamaa

Semi Misemo/nahau)

 • Hunikoroga nyongo – hunikasirisha sana.
 • Kukata tamaa- kupoteza matumaini
 • Nikupe nikupe – hongo/hakuna cha bure
 • kilichomtoa kanga manyoya – kumta adabu

Tashbihi

 • Viuno vitatingishwa mpaka viyeyuke kama mafuta karibu na moto- maelezo jinsi wanawake watakavyomkatikia Bokono
 • Ni wazalendo thabiti kama majabali
 • Ukweli huuma kama nge
 • Bahati kama mtende
 • Mara nyingi uhalisi huonekana kama ndoto
 • Utakuwa kama ndege anayeishi juu ya mbuyu
 • Moyo wangu wangalikuwa mzito kama jiwe

Taswira

 • Pale ambapo Mwelusi yuko uwanjani, mahali pa mkutano kupitia kwa mawazo yake tanaiona picha ya pale – mapambo
 • Kipigo na kuingizwa kizuizini kwa Mwelusi
 • Vifo vya wale waliopigania ukombozi – Askari wa II alieleza jinsi walivyomuua mtu waliyekuwa wakimhoji.
 • Vita vya kikabila – Mashambulizi ya askari wa kukodi waliwaacha wengi wakiwa wamefariki, wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa.

Istiari

 • Alikuwa jiwe – hakukubali mashtaka yake
 • Ni gogo la mti – Tanya anaeleza hisia za Gege aliyekuwa amekataa kumtembelea kakaake
 • Wana mawe vifuani – hawana utu
 • Askari ni wanyama – hawana utu- wamejaa ukatili

Methali

 • Sikio la kufa, halisikii dawa- Bokono alikuwa anapotoshwa na hakutaka kurekebishwa
 • Hasira hasara – askari wa II anawaeleza aksari I na wa III wanapotaka kupigana  

(zozote 5×2=al.10))(kutaja =1, kueleza/mfano =1 = 02×5=ala. 10)

 

(d) Umuhimu wa mzungumzaji – Tanya (ala.4)

 • Ananyimwa nafasi ya kumwona mwanawe gerezani ambaye ni Mwelusi.
 • Anaandaa chakula kwa lengo la kumfikia mwanawe Mwelusi gerezani lakini kinaliwa na askari II na III.
 • Anakosewa heshima na askari II na III anaposisitiza kumwona mwanawe gerezani.
 • Askari III anamwangusha Tanya kule kwake uani/nyumbani katika harakati za kumsaka kutoka kizuizini na Mtemi kuamrisha akamatwe.
 • Ni mmoja wao wanaonyimwa haki mfano kuchota maji kisimani.  (zozote 4×1=al.4)

 

7.  (i)  MTEMI BOKONO – WASIFU

 1. Mwenye tama ya uongozi- anasema ataongoza Butangi kwa miaka mia moja
 2. Kiongozi dhalimu – anatesa wake k.m. Mwelusi
 3. Mwepesi wa kushawishika – anaamini vile Batu anamdanganya kuwa watu wa Butangi wanampenda
 4. Mtawala wa kiimla/ kidikteta/ mabavu – anawatisha washauri wake kuwa angetafuna mifupa yao wasipofaulu kumkamata Mwelusi kwa siku nne
 5. Hataki upinzani wowote kwa utawala wake
 6. Mwenye hasira – anapandwa na hasira wakati watu wanasusia mkutano wake pia anakasirika anapopashwa habari kuwa Mwelusi ametoroka kizuizini
 7. Ni mwoga mwenye wasiwasi mwingi, ana wasiwasi kuhusu kunyang’anywa uongozi.Anaota akizikwa akiwa hai
 8. Katili – anaunga mkono utesaji na mauaji kwa wapinzani wake k.v Mwelusi na mtoto wa Chendeke
 9. Mwenye mapuuza – anapuuza Nyalwe na mama Agoro kuhusiana na uongozi wake mbaya na pia kuhusu unyakuzi wa kiwanja cha watoto kuchezea
 10. Ni fisadi- Anawapa ardhi watu kama askari mkuu kupitia kwa mgawa ardhi. Pia motto wa Kaloo kupewa kazi, kukataza matumizi ya kisima na bonde la ilangi kwa manufaa yake na marafiki zake

 (ii)  UMUHIMU WA BOKONO

 1. Ni kielelezo cha viongozi ambao huongozwa na tama baada ya kuingia mamlakani
 2. Anawakilisha viongozi wanaodhulumu wapinzani wao k.m Mwelusi
 3. Anaendeleza ujinga wa viongozi wanaoshauriwa na wapambe wao laghai
 4. Ni kielelezo cha viongozi wanaowasaidia marafiki zao wanaounga mkono tawala – zao ili kuimarisha kudumisha utawala potovu – k.m. mgawa ardhi kumpa askari mkuu ardhi
 5. Ni kielelezo cha viongozi ambo hupuuza maoni ya wananchi- anakataa kusikiza maoni ya Nyalwe na Agoro eti kwa sababu ni wanawake
 6. Anawakilisha viongozi waliokosa kuadilika katika jamii k.m. kukosa heshima katika asasi ya ndoa yake
 7. Ametumika kuonyesha jinsi viongozi wengine hutumia utesaji na mauaji kama nyenzo za kuimarisha na kudumisha uongozi wao
 8. Anawakilisha viongozi ambao wanatafuta kila mbinu kama vile mauaji ili kuyalinda mamlaka yao wanayohofia kunyang’anywa
 9. Ni kielelezo cha uongozi ambao huhasirika na huhasiri nchi zao baada ya kutawaliwa na hasira
 10. Ametumiwa kuonyesha jinsi udikteta unavyoweza kutenga maendeleo kwa kuwakandamiza na kuwanyamazisha wanaojaribu kupinga uongozi mbaya

 

(iii) MWELUSI – WASIFU

 1. Ni mzalendo wa kweli- anaongoza harakati za kukomboa Butangi kutokana na uongozi mbaya
 2. Jasiri- anakashifu uongozi wa Butangi bila uoga – anajasiri kutoroka gerezani na hata kuongoza watu kukivamia kisima
 3. Mwanaharakati- anatak kuleta mabadiliko ya uongozi
 4. Mwenye msimamo thabiti- licha ya kuteswa gerezani habadilishi msimamo wake
 5. Mwenye busara- anajaribu kuwazindua wanabutangi (amezinduka kimawazo)
 6. Mwenye maarifa – anatumia maarifa kutoroka kizuizini kwa kukereza minyororo kwa tupa
 7. Ni mwerevu- akiwa kisimani, baada ya kutoroka kizuizini, anamkuta Zigu na kumweleza kuwa Mwelusi hajatoroka bali kajificha momo humo gerezani
 8. Ni mbishi- anabishana na Zigu pale kisimani kuhusu matumizi ya kisima

(iv)  UMUHIMU WA MWELUSI

 1. Ni mhusika kielelezo cha wazalendo wanaodhihirisha apenzi ya dhati kwa nchi yake
 2. Anawakilisha vijana wanaopenda nchi yao na hata kuyatoa maisha yao kwa manufaa ya jamii
 3. Anasaidia kubainisha ujinga wa viongozi wasiowajua raia wanaowaongoza- Zigu
 4. Anaonyesha kuwa juhudi za ukombozi zinahitaji uvumilivu na subira
 5. Anatumiwa kuonyesha malezi mema ya Tanya
 6. Ndiye mhusika muhimu zaidi anayeendeleza na kuthibitisha anwani ya kifo kisimani anapouawa karibu na kisima cha mkomani
 7. Ni kielelezo cha jinsi wanaharakati wanavyofaa kutetea haki na kupima bila kukubali yote waambiwayo
 8. Ni kielelezo cha jinsi wanaharakati wanavyoweza kutumia maarifa yao kujikomboa na kukomboa jamii kutokana na uongozi dhalimu
 9. Ametumiwa kuelimisha wanabutangi kuhusu uovu unaotokana na utawala mbaya. Anawaonyesha jinsi ya kujikomboa kutokana na uongozi huo
 10. Ametumiwa kuhimiza wanaharakati kutokata tama licha ya kupitia mateso au changamoto mbalimbali hadi wafikie lengo lao
 11. Anatumiwa kuonyesha matatizo yanayowasibu viongozi na wanaharakati (wanamapinduzi) katika jamii ambao aghalabu huteswa hata kupoteza maisha yao

  Kutuza: wasifu, zozote Bokono tano, Mwelusi tano Jumla 10

Umuhimu zozote Bokono tano, Mwelusi tano , jumla 10  Jumla 20

 

8.  “Kazi ya mikono yangu yenyewe”

 a)  i) Msemaji ni Gege

ii) Wakiwa kwenye majengo (ukumbi) ya utawala ya Butangi

iii) Anazungumza na Bokono akiwepo Batu na Mweke

iv) Anaripoti jinsi alivyomuua nduguye Mwelusi plae kisimani kwenye chemba  4×1=4

 b) Yaliyomfanya msemaji kuuchomea mwiba

 1. Alikuwa ameahidiwa Alida bintiye Bokono
 2. Aliahidiwa ardhi kubwa yenye rotuba
 3. Aliahidiwa mitumbwi ya kuvulia samaki
 4. Angepata mashamba ya minazi na miembe
 5. Aliahidiwa mashamba yam tama na migomba
 6. Atavua samaki kwa majahazi makubwa na
 7. Kuwa tajiri mwenye mali nyingi na jina kubwa

c) Yaliyofuata kauli hii na hatima ya mzungumzaji

 1. Alipewa jina la mkuki wa Almasi – baada ya kuuchomoa mwiba. Yaani kumuua Mwelusi
 2. Kulikuwa na mapinduzi – waliokuwa namakani waling’olewa k.m. Bokono na kundi lake la washauri
 3. Gege alitiwa mbaroni baada ya kupigwa na wanamapinduzi
 4. Bokono, Batu, Mweke, Zigu na Tahu walifungwa na kutupwa gerezani wakingojea kufunguliwa mashtaka
 5. Baraza la hukumu liliundwa upya ili kutoa hukumu kwa Mtemi, Bokono na washauri wake
 6. Gege alipigwa kofi kali na kufurushwa nje na Mweke baada ya Gege kudinda kuondoka ukumbini akidai zawadi yake kuu – Alida
 7. Gege hakupata ardhi kubwa alioahidiwa kwa sababu mapinduzi yalitokea kabla hajaonyeshwa pamoja na zawadi zingine mali
 8. Utawala wa kiimla wa Bokono ulifikia mwisho
 9. Nyalwe alibahatika kukwepa hasira kali za wanabutalangi kwasababu alikuwa akisaidia kumshauri Bokono japo alitia masikioni
 10. Mitumbwi ya kuvulia samaki, mashamba makubwa ya migomba na miembe aliyokuwa ameahidiwa Gege hakuipata

 

9.  UONGOZI MBAYA

 • Mauaji ya Mweluzi yameipokonya jamii kiongozi mwenye maendeleo.
 • Kukata miti ovyo ovyo kumesababisha ukame/jangwa na njaa.
 • Kuendeleza ufisadi ni chanzo cha umaskini.
 • maandamano na misukosuko husababisha uhasama na ukosefu wa amani/utulivu.
 • Husababisha vibaraka/vikaragosi ambao ni wasaliti waletao madhila kwa wananchi.
 • Vijana kukoasa ajira.
 • Uozo wa kijamii k.m. Kaloo.
 • Hukuza matabaka.
 • Hukuza unyanyasaji (Mbutwe kunyimwa haki yake (malipo).
 • Uhasama wa kikabila.
 • Kusetiri uhalifu, k.m. mfungwa kuuawa kisiri. (10 x 2 = al. 20

 

10.  – Vijana wamesawiriwa katika makundi mawili:

 (i) Wazalendo

 • Mwelusi
 • Askari
 • Andua
 • Atega
 • Kame
 • Mgezi

 (ii) Wasaliti

 Gege

 •  Askari II
 •  Askari III
 •  Makacheto (Mweke, Talui)

  Kila mhusika (al. 1) , maelzo ya aliyesawiriwa (al. 1)

  Wazalendo – (Wahusika watano – (al. 5)

 ( Maelezo matano – (al. 5)

Wasaliti – (wahusika watano – (al. 5) (Maelezo matano – al

 

11  (a)  -Msemaji ni askari wa pili

 -Anamsemesha askari wa tatu

 -Wako nje ya gereza

  -Askari wa pili aligundua kuwa Mwelusi alikuwa amekata pingu na umati wa watu

wenye hasira ulikuwa unawajia

 

b)   i) Kinaya- maneno yaliyo kinyume cha ukweli

ii)Askari alisema watu waliwapenda ilhali waliwachukia

 • Alidai walifanya kazi vizuri ya kumzuia mfungwa gerezani ilhali walimtesa na kula chake
 • Mfungwa alitoroka
 • Askari hawangepakwa mafuta bali wangepigwa  

c) -Waliwaua watu k.m mtu jiwe

 • Walikula chakula cha wafungwa k.v askari II na III walikula chakula cha Mwelusi
 • Walikosa heshima na adabu kwa watu wote wa rika zote k.m Tanya aliambiwa asitoe hotuba ya uzazi, kumgusa adua kifuani
 • Askari waiwatesa washukiwa kwa njia mbali mbali ili wawape habari walizotaka k.m kung’oa kucha n.k
 • Kuwapiga wanabutangi k.m majeraha ya andua, motto wa chendeke aling’olewa meno

 

12.  a)Batu 1 anazungumza na washauri1 wengine wa Bokono1 wakiwa wakiwa katiak

ukumbi1 wa

  utawala wa Butangi.  

b) Masharti yalikuwa ikiwa amekata msamaha basi ashirikiane na Batu Kwa:

 • Mwelusi awataje vijana wanochochea chuki dhidi ya utawala wa Bokono.
 • Apelekwe vijini awatangazie watu kwamba ameacha uchochezi
 • Aseme umuhimu wa kuungana pamoja chini ya uongozi wa hekima wa Bokono
 • Aseme uchochezi katika Butangi umepangwa na majirani ambao wanaonea wivu amani na maendeleo ya Butangi.

c) Ufisadi:

 • Kisima cha Mkomani: kinabina fsishwa – watu wanakatazwa kutummia maji eti yanahifadhiwa kwa siku zijazo.
 • Wananchi wasikanyage Bonde la Ilangi,kumbe limetengewa Bokono na marafiki zake.
 • Ardhi kunyakuliwa
 • Wasaliti kuahidiwa ardhi.
 • Mali ya Butangi ilikuwa ya wachache.
 • Batu hakuwa tayari kumlipa Mbutwe pesa za viti.
 • Botono alibinafsisha bahari/ziwa – alikuwa na sehemu yake ya kuuna samaki.
 • Bokono alikuwa na mali nje ya Butangi – Macheleni.
 • Mtoto wa Kaloo kupewa kazi kwa ‘mapendeleo.
 • Watu kupata vyeo kwa sababu ya uhusiano wa kifamilia na Bokono.
 • Uharibifu wa Kufichwa.
 • Motto wa mteni ku chafua maji ya bwawa.  (hoja 12X1 ) ala 12

 

13.   Maana – kinachokuathiri ama kitakachokuangamiza daima kimekundama; u nacho

kila wakati

 • Kame – ana uhusiano wa kiukoo na Bokono, lakini anawatetea wachochezi na kuungana nao katika harakati za kumpindua Bokono
 • Mgezi – anahudumu nyumbani mwa Bokono na huwapelekea wanabutangi habari kuhusu yanayoendelea katika nyumba ya utawala
 • Askari I – mwana mapinduzi ingawa yuko serikalini. Huenda alishiriki katika njama ya kuingia tupa gerezani
 • Gege – anamsaliti nduguye na kummua kwa kisu
 • Wanabutangi – wametangana wao kwa wao kutokana na ubinafsi na woga wao

  Kutaja mhusika – al 1

  Maelezo – ala 3

  Hoja 5×4

14.  

 • Hakuna maendeleo yoyote k.v. askari kutumia mapanga na mikuki kulinda usalama na nchi
 • Hakuna utumizi maalumwa pesa bidhaa hubadilishwa mfano Mbutwe kudai malipo ya mbuzi wawili
 • Wanachi hawajakua kiakili kuhusu siasa, waijue haki yao. Gege haoni uovu unaoendelezwa na utawala wa Bokono
 • Hakuna mfumo wa kuajiri na kufuta kazi. Bokono anatoa amri k/v. mtoto wa Kaloo. Ujira pia huendelezwa kwa misingi ya kiakbila
 • Serikali ya Butangi haijajitajirisha kwa majanga yanayoweza kutokea wakati wowote k.v. askari kukosa mikuki ya kutosha hinvyo basi hawawezi kukabiliana na umati uliokwenda gerezani kumnasua Mwelusi
 • Butangi haina mfumo maalum na sheria – Mtemi ndiye bunge – anatunga sheria za kiubinafsi k.v. utumiaji wa kisima
 • Hakuna demokrasia – wananchi hawachangii katika ujenzi wa taifa lao
 • Kiongozi yuko juu ya sheria – anatenda lolote alitakalo bila hoja wakati wowote
 • Hakuna vikundi vya kutetea haki ya mwananchi. Vilivyoko vimeundwa na serikali sio kuwatetea bali kuwaonyesha kuwa malalamiko yao yanashughulikiwa
 • Kuna utawala wa nyumba kuu- inayohusiana na Mtemi kama dadke ameolewa na kakake Mtemi. Wana wa Mtemi ndio wanaosimamia kandarasi n.k. familia ya Mtemi ina mamlaka zaidi- kawaida katika nchi zinazokua

 

15.  a)Jazanda

 1. Bafe – wapinzani wanaomshambulia Bokono
 2. Mamba – Bokono na uwezo wake unaowadhuru watu
 3. Nyati/ kifaru- matumizi ya silaha kuwaua wapinzani
 4. Fisi – ulafi wa askari II na III
 5. Chui – Bokono na ukali wake, mkewe Bokono na ukali wake
 6. Zimwi – Bokono na washauri wake
 7. Njiwa – watawala wanaonyanyaswa
 8. Kozi – Ndege mwenye uwezo – Bokono anatumia uwezo wake kuwaangamiza watawala
 9. Mwiba katika mguu – Mwelusi – kikwazo kikuu katika utawala wa Bokono Zozote 5×2=10

 

b)  i) Tashhisi

 – Mawazo yakashika miguu – Mwelusi hakuendelea kutembea kwasababu alikuwa

anafikiria

 – Usipoondoka utatembelewa na kofi – vitisho

 – Ndoto zimekifanya kichwa changu kuwa uwanja wa kuchezea . Tanya anaota kila wakati

Zozote 2×2= 4

 • Dunia haipendi wenye kukata tama- Azena anamshauri tanga
 • Pombe haipendi tumbotupu
 • Huzuni imejenga nyumba moyoni mwangu – Tanya anahuzunika daima mtoto wake kizuizini, mume wake alikufa
 • Jua lilimchekelea akiwa papo hapo kwa muda mrefu Zozote 3×1=3

ii) Methali

 • Sikio l aa kufa halisikii dawa
 • Bandu bandu huisha gogo
 • Udongo uwahi ungali maji
 • Dawa ya moto ni moto
 • Maziwa yakimwagika hayazoleki
 • Uerevu mwingi huondoa maarifa Zozote 3×1=3

iii) Kinaya

 • Bokono anasema kwamba nia yake ni kuongoza Butangi kwa busara ilihali wananchi wa Butangi wanateseka
 • Batu anasema kwamba ataongoza Butangi kwa manufaa ya wanabutangi wote wote ukweli ni kwamba ni wachache wanaonufaika

 

16.  a) Msemaji ni kame alimwambia Batu katika ukumbi wa utawala wa Bulangi batu

alipendekeza Mwlusi auwawe kama anapinga 4×1=4

 b) – mwongo

 • Katili
 • Mnafiki
 • Mchochezi
 • Kigeugeu
 • Kibaraka
 • Mbinafsi 5×1=5

c)- Mwelusi

– Andua

– Atege

– Askari 1

– Tanya

– Nyalwe

– kame

Kutaja mhusika 1

Kutoa mifano 1

 

17.  (a) Maneno haya yalisemwa na Mtemi Bokono

– Anajisemesha mwenyewe

– Alikuwa katika makao ya utawala

-Alikuwa na wasiwasi

(b) (i) Mwenye wasiwasi na uwoga

(ii) Anahofia huenda uongozi wake ukaanguka

(iii) Hadhibiti tena uongozi wa Butangi

(iv) Kuumwa na nyoka ni ishara ya kufa/kushindwa na adui hivyo uongozi wake

waelekea kwisha.

(c) Nidaa- hai

(ii) Jazanda – Sumu ya nyoka ni nguvu za upinzani

(iii) Taashira – Nyoka kumuona ni ishara ya kuanguka kwa uongozi wake.

(iv) Mchezo ndani ya mchezo  (2×1= 2)

 1. (i) Tenga utawale – aliwatenganisha watu ili kuvunja umoja wao na aweze kutawala kwa urahisi mfano; Gege na Mwelusi.

(ii) kuwatia jela na kuwatesa wapinzani wake mf. Mwelusi

(iii) Kuwaua wapinzani wake mf. Mwelusi

(iv) Kuwatenga wapinzani wake na jamaa, marafiki mf. Hakuna anayeruhusiwa kumwona

mwelusi kizuizini.

(v) Kuwatumia askari kushambulia wapinzani wake kisha kusingizia majirani. M.f. wabalusi

kushambulia batuitui

(vi) Kuwatunza wazalendo na wafanyikazi watiifu kwa mfano Gege, Kaloo na askari mkuu

(vii) Kuunda tume za uchunguzi kuuliza raia kila kulipozuka swala nyeti (malalamiko)

(viii) Kueneza propaganda kuwa Bokono amepewa utawala na Mungu ili watu waache kumpinga

na wamtii

(ix) Vitisho – anawatisha washauri wake kuwa angekula mifupa yao kwa siku tatu kama

hawangemsaka na kumrejesha

(x) Kuzorotesha uchumi ili raia wasiweze kujitegemea na ili atawale kwa urahisi- kuwanyima

maji, kuwanyima ardhi

(xi) Kuwanunua/kuwahadaa wapinzani wake. Mwelusi anahadaiwa kuwa akiacha uchochezi

angefanywa

kuwa kiongozi wa vijana angepewa ardhi na ng’ombe.

(xii) Kutumia washauri kutawala na kupata habari kwa mfano Batu na Kame.

(xiii) Kuunda Baraza la hukumu kwa lengo la kunyamazisha wapinzani wake  (10×1=al. 1))

 

18.  Masuala Ibuka

 i) Ukimwi – siku ya mganga

– Mwaibale anausambaza kwa wembe

– wagonjwa/ wateja wamekondeana na kudhoofika kiafya

 ii) Haki za watoto i) Kuchukua hatua nyingine

– watoto kukosa sare, karo, chakula na kwenda shuleni

– Ajira ya watoto

– Mtoto kupachikwa mamba

ii) Fumbo la mwana

– dawa za kulevya

iii) Ngome ya nafsi

– Watoto kuozwa mapema

iv) Uteuzi wa moyoni

– Ndoa za mapema

– wasichana kukosa elimu

 iii) Ufisadi  – Mayai waziri, waziri fisadi, wizara ya mlungula

– Msamaria mwema – Bw. Kizito Kibambo

– Uteuzi wa moyoni – wapiga kura kuuza kadi zao

– Ngome ya nafasi – Chifu alihongwa, kuficha wahalifu

 iv)   – Matumizi ya dawa za kulevya/ mihadarati na madhara yake kwa vijana

 • Fumbo la mwana
 • Nanda anatumia dawa za kulevya
 • Anazorota kimasomo, mchafu n.k

v) Ndoa za mapema kwa wasichana

– Zena aliozwa mapea – uteuzi wa moyoni

– Ngome ya nafsi – Naseko anaozwa kwa mzee

vi) Migogoro shuleni

 • Ndimi za mauti – Wanafunzi kuchoma wenzao bwenini
 • Mayai waziri – Migomo ya walimu

vii) Vita vya kikabila na suala la wakimbizi

 • Mkimbizi

ix) Uongozi mbaya – Kuchukua hatua nyingine

 • Uhalifu wakati wa kura
 • Viongozi walikosa uwajibikaji
 • Chifu kuuza chakula kilichotolewa bure wakati wa ukame
 • Serikali ilifutilia mbali elimu ya bure na kusababisha maskini
 • Mayai waziri wa maradhi
 • Waziri mayai
 • Viongozi walafi

x) Uhalifu katika jamii

 – Pwaguzi

 – Salim ni tapeli na mizi mkuu

 – Kuchukua hatua nyuingine

 – Ngome ya nafsi

xi) Umaskini

 • kuchukua hatua nyingine
 • fumbo la mwana
 • msamaria mwema
 • mayai waziri wa maradhi

xii) Haki za wanawake katika jamii

 • Uteuzi wa moyoni
 • Ngome ya nafsi
 • Kuchukua hatua nyingine
 • Mayai waziri wa maradhi
 • Mayai haishi na mkewe

 

19.  Dhamira ni lengo/ nia ya mwandishi wa ‘Tuzo’

 i) . Anaashiria kauli kuwa yote yaweza yakatokea hata yasiyotarajiwa k.m. Salome na

kibwana hawana mkabala mzuri lakini Salome anakuja na kumletea habari. Mwandishi

aonyesha kuwa hafla ama matukio huleta wengi pamoja hata wasiosemezana wala

kuamkuana

ii) Anaonyesha kuwa mapeni ni msingi wa mengi. Nia ya kibwana unapokataliwa inakuwa

chanzo cha kutosemezana kwao tena

iii) Anaonyesha kuwa kunao, wakaao pamoja na kufanya kazi pamoja lakini hawana mkabal

mzuri, wao husemezana tu kwa sababu ya kikazi walakini wakitoka nje wanakuwa

mjamba miwili isiyoamba. Salome na kibwana wanasemezana wakati wa kazi

iv) Pia anatuonyesha kuwa kuna wenye vitendo vizuri vyenye sifa. Vitendo vyao vinajulikana

wazi wazi (kama saui zao)lakini wenyewe hawajui vitendo vinaweza kumtambulisha mtu.

v) Kuna haja ya kumtuza aliyefanya vizuri wanahabari wanatuzwa akiwemo Salome Dzoro

vi) Hamu ya kutuzwa huwa hasa katika sherehe ambayo mtuzwa hajatengezwa hadharani.

Tunaiona hamu aliyonayo kibwana

vii) Pia anasisitiza umuhimu wa kauli tahadhari kabla ya athari na kuwa mwangalifu

 Anaonyesha umuhimu wa kuwaza kabla ya kutenda

 Kibwana angalichunguza kwa makini hangeaibika machoni pake vile.

Tunaelewa alichanganyikiwa hadi katika choo cha wanawake

viii) Anathibitisha ukweli wa methali mzaha

 Mzaha hutubga usaha

 Mzaha wa Salome wa kumtania kibwana unamletea aibu na kuvurugika akili

ix) Anaonyesha jinsi kutaniana na kuchezeana shere kamwe hakufai. Hii huweza kuleta vita

namna kibwana alitaka walakini akajizuia

x) Anataka kuonyesha jinsi furaha huathiri akili. Kibwana alizidiwa na furaha na kusahau

kuwa anaweza kutaniwa. Mwandishi anaonyesha kuwa kuna kilio au aibu inayoweza

kutokana na futahi hiyo

xi) Anataka kuashiria kuwa vita sio suluhisho kwa kosa ulilotendewa. Kibwana alifumbata

konzi kutaka kuirusha walakini anajizuia. Hili ni funzo dhabiti kuwa haitupasi kusuluhisha

kwa vita

xii) Ni kawaida kuoa anayetuzwa akiringa ama akitembea kwa madaha. Tunaambiwa kuwa

Salome alitembea kwa ndweo kwenda kuitwa zawadi yake.  Zozote 10×2=20


 
Share this:


EcoleBooks | Maswali ya TAMTHILIA: KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA na Majibu Yake

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*