Share this:

Maswali ya RIWAYA: UTENGANO: S.A. MOHAMMED

1. ‘Pesa iweke mbele, Pesa mwanzo. Sisi tuna msemo wetu. Watose. Ndio, watose, maana sisi

tumeshatoswa

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili

(b) Eleza mawaidha mawili ambayo msemaji alimpa katika muktadha huu

(c) Eleza maana ya ‘Sisi tumeshatoswa” kwa kurejelea riwaya ya Utengano

 

2.  “Maisha ya Maimuna yalitawaliwa na Majaaliwa kwa kiasi kikubwa.” Thibitisha kauli

 hii kwa kurejelea matukio kumi katika riwaya ya Utengano.  

3.   “Mkinipa mimi kura zenu nitajenga njia, nitawapa watu kazi, nitajenga skuli zaidi na maisha

 yenu yatakuwa katika raha.”

 (a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake

  (b) Msemaji ana ila gani zinazomfanya atoe ahadi hizi?

  (c) Onyesha jinsi wanasiasa walivyosawiriwa katika riwaya  

4.  Said .A. Mohammed ameangazia migogoro na misukosuko inayosambaratisha jumuiya ya

 Utengano na Jamii kwa jumla. Jadili.

ecolebooks.com

5.  “Mama usifanye ivyo.” :Ikiwa kuogopa kuvunja miiko ya nyumba hii, tusiogope. Naivunja

leo hiyo miiko. Hujui utazaa vipi mama. Tutangojea idhini ya mtu asiyekuwepo, wala

tusiyemtarajia kurudi saa hizi?”

 (i) Eleza muktadha wa dondoo hili

 (ii) Fafanua miiko inayorejelewa katika dondoo hili

 (iii) Eleza sifa za mhusika ‘asiyetarajiwa kurudi saa hizi’

6.  Ndoto na nyimbo za Maimuna ni ufundi wa kisimulizi unaojikita katika misingi ya taswira.

Onyesha jinsi mwandishi anavyotumia taswira kufanikisha malengo yake ya usimulizi  

7.  Mkamia maji hayanywi, na akiyanywa humsakama. Kwa kurejelea wahusika wowote watano

 katika riwaya ya Utengano thibitisha ukweli wa kauli hii

8. “…mkubwa kabisa ni mwananchi. Umma ndio mkubwa kabisa, na umma umeshautenda

vya kutosha……………

 (a) Eleza muktadha wa mazungumzo haya  

 (b) Eleza mambo aliyoutendea umma mhusika anayezungumziwa katika muktadha huu  

 (c) Eleza mafunzo ambayo umma unajifunza kutokana na kisa kinachoibua mazungumza haya

9.  Hapo ndipo ninapokuona mjinga wewe nani hasa wakukataa ?

(a) Eleza muktadha wa dondoo

 (b) Taja mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili

 (c) Eleza sifa nne za mzungumzaji

 (d) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo

10.  Fafanua kwa mifano mwafaka aina tano za uozo wa kijamii katika riwaya hii

11.   “Akakumbuka ubeti wa shairi alilolitunga karibuni katika jumla ya mashairi aliyoyakusanya

katika kitabu alichokiita Kilio cha Wanyonge”.

 (a) Eleza muktadha wa maneno haya

 (b) Fafanua ujumbe mkuuu katika shairi linalorejelewa hapa.

 (c) Onyesha Inspekta Fadhili anavyotofautinana na kakake Maksuudi.,

12.  “Mwanamke ni kikwazo na adui kwa maendeleo na ukombozi wake”. Kwa kutoa mfano mwafaka

 kutoka kwenye riwaya ya Utengano, ifafanue kauli hii  

13.  “Mwanamke Mtumwa. Nani kasema utumwa umeondoka. Viumbe vya kupika na kupakua,

 kufua na kupiga pasi…”

 (a) Eleza muktadha wa dondoo hili

 (b) Jadili maudhui yanayoonyesha maonevu ya wanawake katika riwaya

  (c) Je, wanawake wamejitokeza vipi katika kupigania mabadiliko katika maisha yao

kwenye riwaya hii

14.  “Majuto ni mjukuu” Onyesha ukweli wa uneni huu kwa kurejelea wahusika: Maksuudi

na Maimuna

15.  Mwandishi wa riwaya ya Utengano amefaulu kuichora picha ya mwanamke katika uhalisi wake

 katika jamii nyingi za kiafrika. Thibitisha  

16.  Mimi nilidhani umepata mtoto mwenye sura na tabia zake, mtoto mwenye kwao….nimesafiri kwa

 mwendo wa meli mia mbili na hamsini kujaniletea kwa mtu asiye na asili wala fasili ? ”

  (a) Fafanua muktadha wa maneno haya :  

 (b) Kwa nini mzungumziwa anachukuliwa kuwa hana asili wala fasili ?

 (c) Fafanua mbinu zozote tatu za lugha katika muktadha huu  

 (d) Mzungumzaji amekuja nini ?

 (e) Fafanua kwa ufupi yaliyotendeka baada ya usemi huu

17   “Leo amekomolewa na bado ataumwa na nge kwa mdomoni na mkiani.”

(a) Fafanua muktadha wa maneno hayo  

(b) Eleza kwa kutoa hoja nane jinsi anayerejelewa alivyoumwa na nge

(c) Eleza sifa nne za mnenaji

18. Eleza jinsi kinaya kimetumiwa katika riwaya ya Utengano  

19.  Kuna mengi ambayo Kazija anayachukia. Ndiyo, anachukia……kwanza, anamchukia

mwanamme.  Ni sababu zipi zinazosababisha wanawake kama kazija kuwachukia wanaume?  

20.  Anwani “Utengano” inafaa katika jumuiya ya utengano. Fafanua.  21.  Mshiba Mungu staghafiru, naye mwepesi wa kusamehe waja wake

 1. Eleza muktadha wa Dondoo hili

(ii) Eleza yaliyomsukuma anayezungumziwa kufikia kiwango hiki  

(iii) Taja alama alizo nazo anayezungumziwa  

(iv) Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili

(v) Eleza jinsi maudhui ya Dini yanavyojitokeza katika riwaya ya utengano

22.  Mwandishi wa riwaya ya Utengano anakashifu mambo kadhaa katika jamii . Taja na ueleze

kwa kutoa mifano  

23.  Haloo, nani ? Aha Mr. Smith….ni wewe. Nilikutarajia . Nilikuwa nakusubiri kwa hamu.

 Ndiyo…Nitafanya kama ulivyoagiza.

 (a) Eleza muktadha wa dondoo hili  (b) Kabla ya mazungumzo haya kujiri, kulikuwa na ushairi wa “kilio cha mnyonge”. Taja

ujumbe unaojitokeza katika ushairi huu  

(c) Mzungumzaji katika muktadha huu alikuwa mwovu. Thibitisha  

24.  “Nataka nikueleze hivi darling….”

Unajua watu wakikaa pamoja kama vilivyo visahani hugongana”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili

(b) Eleza sifa za aliyeelekezwa maneno haya  

(c) Baadhi ya mabailiko yametokea katika riwaya ya ‘Utengano”  

 

 

Tamthilia

 

Majibu ya RIWAYA: UTENGANO: S.A. MOHAMMED

1.  a) – Msemaji ni mama Jeni.

 • Msemewa ni maimuna.
 • Mahali – mkahawa wa Café Afrique.
 • Trikio – Baada ya ziara ya kumnunulia maimuna mavazi katika duka la baniani Mama Jeni alitaka kumpa Maimuna kuzozana na James, baharia aliyetaka kufanya mapenzi na maimuna. ( 4×1) ala.4

b) i) Watu wanapoishi pamoja hawana bud kuzozana hivyo basi ilibidi pawe na sheria au

makabiliano ya kuongoza maingiliano yao.

ii) Ingebidi Maimuna Kumgawia mama Jeni sehemu ya pesa alizopata kutoka kwa wateja wake.

iii) Alimhakikishia kwamba angeyazoea maisha yale baada ya muda. ( zozote 2×2) ala. 4

c) i) Wasichana hakupewa elimu kama vile Maimuna ilhali waume walipata elimu (Mussa).

ii) Maksuudi alimtawisha mkewe Tamima na bintiye.

iii)Wanaume walikuwa wazinifu ku maksuudi na shoka bila kujali wake zao.

iv) Maksuudi alihini Mwanasuru mali yake na kusababisha kifo chake.

 • Wanawake walipigwa bila sababu muhimu.
 • Wanawake walipewa talaka na wanaume bila sababu muhimu
 • Pesa za mkewe Japu ziliwa na Mksundi alipofika amwekee sahihi.
 • Nchi zilizostawi zuilinyanyasa nchi maskini  (zozote 6X2) ala. 12

2. Majaaliwa ni mambo yatokanayo na rehema za Mungu, Kindura, mambo amabyo binandamu

hana mamlaka nayo.

 • Maimuna alipata fursa ya kutoroka kwao siku ambayo mamake alijifungua.
 • Ni majaliwa kuwa siku ambayo Maimuna alitoroka nyumbani Bw. Maksuudi hakuwa nyumbani, alikuwa kwa kazija.
 • Mkutano wa Maimuna na Maulidi ni ya kimajaaliwa. Alikuwa akiimab huku akiosha vyombo ndiposa akapata kazi ya kuimba huko Kumbalola Hoteli.
 • Maimun a aliposingiziwa kwamba ameiba kwa mama Jeni alisaidiwa na Dora kwenda kwa Biti surur.
 • Ndoa yake kwa kabi ilimbadili nia na akajisameha na pia kusamehe babake.
 • Uchechefu wa chakula ulimleka kuzuru upwa alipokutana na Kabi – wakawa wachumba.
 • Matatizo yaliyomkumba maishani hatimaye yalimzindua akawa msomaji wa magazeti na mwanaharakati wa ukombozi wa wanawake.
 • Alipata shida nyingi kujikimu huko Futoni. Hili lilimfanya awe alghaina kusababisha kupata mali kwa Bwana Ashuru.
 • Anapotoroha kwa Biti suru ndipo anapopata fursa ya kwenda Futoni na kuanza maisha mapya.

(zozote 10X2) ala. 20

3.  a) Muktadhaa wa dondoo

 • Haya ni maneno ya Zanga, mmojawapo wa wagombeaji kiti cha ubunge
 • Alikuwa akihutubia umati wakati wa kampeini
 • Alikuwa katika uwanja wa Uhuru
 • Alitaka maswali yaulizwe na umma lakini watu wakanyamaza kama ishara ya kutoridhika
 •    (Zozote 4×1=4)
 • b) Ila za msemaji (Zanga)
  • Zanga hawajibiki katika kutumikia umma
  • Anawadharau na kupuuza waliomchagua
  • Anajilimbikizia mali bila kuwajali waliomchagua k.m. magari matatu na nyumba tatu
  • Hapatikani kazini
  • Anabagua watu maskini na kupendelea matajiri
  • Ana kiburi na majivuno mengi
  • Hakutimiza ahadi za awali alizoahidi kabla ya kuwa mbunge (zozote 3×2=6)

 

  c) Jinsi wanasiasa walivyosawiriwa

 • Wanasiasa ni pamoja na waasi wa chama, Zanga, Maksudi, Siwa na wakoloni wakongwe waliotawala nchi
 • Maksudi ni kiongozi asiyetimiza ahadi yake
 • Wanajilimbikizia mali k.m. Maksudi ana kasri na amejiwekea akaunti huko nje naye Zanga ana nyumba tatu na magari matatu
 • Wanadhulumu umma kwa mfano Maksudi anatwaa ardhi ya umma
 • Wafisadi k.m Maksudi anajaribu kumhonga inspekta Fadhili
 • Wanajihusisha na magendo k.m Maksudi
 • Wakoloni wakongwe walijipenda na kumiliki majumba makubwa makubwa
 • Wakoloni wakongwe walikuwa wabaguzi, waliwabagua watu wa tabaka la chini na kuita mtaa wao mtaa wa ‘walatope’
 • Waliwadhaulumu wapigania uhuru
 • Siwa ni mwaminifu, anatoa hotuba fupi bila kutia chumvi kama Zanga na Maksudi katika uwanja wa Uhuru
 • Siwa ana mienendo mizuri na anakabiliwa na umma

Kutaja wanasiasa alama 2 Hoja zozote 8×1=alama 8; Jumla (c) alama 10

 

4. Migogoro/ misuko suko – (haya mawili yajadiliwe sambamba)

(i) Ufafanuzi- migogoro- hali ya kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi- fujo- kusiko

na utulivu, ugomvi/ sokomoko. Misukosuko- hali ya kutowepo na utulivu au Amani ghasia ,

machafuko/ migogoro

(ii) Familia ya Bwana Maksudi Kambe. Anawatisha/ anafungia binti na mkwewe Tamima wana

Huzuni, wana sosononeka kwa kufungiwa kama watumwa. Maimuna anaamua kutoroka,

naye Tamina baada ya kuzalishwa apewa talaka. Familia ya Maksudi inapitia misukosuko

na migogoro unayosababisha isambaratike kabisa. alama 3

(iii)Bwana Maksudi, Mussa na Kazija. Hawa wanapita migogoro wanapokutana kwa karija.

Wote wawili wamevutiwa na urembo wake wanataka penzi. Wanapokutana, kuna vita,

fujo- nusura kuuana. Vita hivi vinasabibisha uhusiano kati ya baba na mwanawe

kusambaratika- hawaonani tena Mussa atokomea kwenye giza.  alama 2

(iv) Bi. Farashuu- Ana kisasi na Bwana Maksudi kwasababu huyu wa pili alimwoa

bintiye akamtesa, akamnyan’ganya urithi/ mali kisha akamtaliki na kusababisha kifo

chake.

Farashuu anadhamiria kusambaratisha uhusiano kati ya baba na mwanawe kusambaratisha

familia ya Maksudi. Anafaulu vilivyo kwa kutumia binti Kocho, Bi. Kazija na hata yeye

mwenyewe kuingia nyumbani mwa hasimu wake na kusababisha talaka.  alama 3

(v)(Umma na Maksudi- Katika mkutano wa kisiasa, Maksudi anapoomba kura,

anakumbushwa

uovu wake, kama kiongozi mfano kujilimbikizia mali, kunyanyasa maskini, kusahau

alikotoka.

Bi kazija kkwa niaba ya umma anampasulia mbarika. Maksudi anaaibika umma wataka kumwangamiza mabo yanasambaratika- anakamtwa na kufungwa jela. alama 3

(vi) Zanga na umma- Katika mkutano wa kisiasa- Anapojitetea mbele ya umati unapuuza, Kazija

tena anakumbusha umma, kuwa Zanga amejilimbikizia mali, ana maringo- hajali raia wa kawaida.

Ni mjeuri. Mambo yanamharibikia. Raia wako tayari kulipiza kisasi. Naye pia awekwe pingu na

kupelekwa na askari alama 3

(v) Migogoro ya Danguriko kwa mama Jeni- Fujo kati ya Maimuna na James, fujo ya Maimuna na

wasichana wengine waliomwonea gere/ uwivu hadi kumsingizia wizi. Mambo yanasambaratika

Maimuna ahamia Bobea. alama 3

(vi) Danguroni kwa inti Sururu- fujo ya ulevi, uasherati, ugomvi kati ya Maimuna na kijakazi.

Ulevi wa Shoka na uasherati unasambaratisha familia yake. Mkewe alalama. Ugomvi waleta

vita, majeraha, kovu kwa Maimuna. Ni picha kamili ya jamii iliyosambaratika.  alama 3

(vii) Hotelini Rumbalola- Maksudi ajaribu kumfikia Maimuna lakini anamkosa, anapigwa

vibaya na mashabiki- anaishia kwenye hospitali nusu maiti. Maimuna anatoweka bila

ilani-afutwa kazi na mwenye hoteli- Balaa na fujo tupu- mambo yamesambaratika.  alama 3

(viii) Bobea kwa Binti Sururu- Maksudi kwa mara ya pili aandamana na Mussa na Rashid

kumtafuta Maimuna, wanampata Maimuna katika hali ya kutisha wanajaribu kumpata

lakini awaonya “Tokeni mbele nyie——— nirejee kwao———– sahau uk 145” mambo

yanasambaratika. alama 3

(ix) Kuna matumaini- Maimuna abadilisha maisha- aolewa na Kahi na kujenga jamii mpya.

Maksuudi aaga dunia, Mussa na Tamina wanaungana tena katika ujenzi za jamii mpya

Isiyosambaratika. alama 1 Kutuza   Alama

Maelezo:Alama 1

Matumaini: Alama 1

Hoja- Kutaja aina ya migogoro (Alama 1)

Maelezo alama 2=2

Jumla 3×6=18+2= Jumla 20

5.  (i) – Hapa ni nyumbani mwa Bw. Maksuudi

 • Anayezungumza ni maimuna bintiye Maksuudi na anamzungumzia Tamina mamake
 • Bi Tamina alikuwa mja mzito na siku hiyo alianza kupiga kite kwa kuhisi kujifungua
 • Maksuudi alikuwa nyumbani na hiyo ilimaanisha kuwa hangeeza kupelekwa hospitali na mtu mwingine ila Maksuudi. Wala hangeweza kuagiza mkunga wa kienyeji kuja kumzalisha pale nyumbani
 • Maimuna alimwonea mamake huruma na ulimwelekeza kumsihi mamake wavunje miiko/ sheria ya Bw. Maksudi. Hapa ilikuwa baada ya kuzungumza na kushawishiwa na Binti Kocho mmja wa watumishi wa Bw. Maksudi  

  (ii) – Bi Tamina na Bintiye Maimuna walikuwa wakitawishiwa na Bw. Maksudi

 • Hawakuwa na ruhusa ya kutoka nje bila idhini yake
 • Maimuna na mamake hawakuwa na uhuru wa kujiamulia lolote walilotaka hata kama maisha yao yalikuwa hatarini Zozote 3×2=6

 

  iii)  SIFA ZA MAKSUUDI

 • Ni katili- k.m kumchapa mkewe Bi tamina
 • Ni fisadi- k.m alipata utajiri wake kwa kujilimbikizia mali kwa njia isiyofaa
 • Mnafiki- Husema aneanda kwa kaburi la shehe kumbe huenda kwa kazija
 • Mzinifu- Ana mpenzi nje ya ndoa –Kazija
 • Mbinafsi- Hajali maslahi ya watu wengine
 • Maksudi ni mwongo na ni mwenye kutoa ahadi za uongo- wakati wa kufanya kampeini zozote

6.

 • Ndoto ni mbinu anayoitumia mwandishi
 • Mbinu hii kwa kiasi kikubwa hutegemea hisia za msomaji ili kumchochea hisia za uoni, usikizi, ugusaji na uonaji
 • Mwandishi ametumia ndoto na nyimbo za Maimuna kujenga picha kadha wa kadha akilini mwa msomaji
 • Maimuna anaota ndoto mbili, ndoto ambazo ni ruya na jinamizi kwa sababu zinatisha na kuogofya
 • Ndoto ya kwanza ni juu ya nyama kubwa, ndumakuwili labda linalommeza Maimuna
 • Mwandishi ametumia ndoto zote mbili kama utangulizi pale Maksuudi anapotoka kwenda kumtafuta bintiye Maimuna
 • Ndoto hizi zinatumika kuashiria maandaizi ya mikosi na maafa yatakayomsibu Maksudi
 • Maksudi katika ndoto zote anawasilishwa na kuthibitishwa kwa mifano ya kutisha. Kwanza kam nyama la kutisha lisilotambulikana
 • Ndoto ya pili imechukua taswirahiyo hiyo ya nyama la kutisha isipokuwa mara hii ni chatu, joka la kutisha
 • Jambo hili la Maaksudi kujitokeza katika mifano ya wanyama wa kutisha na ambao wajibu wao ni kuua
 • Maimuna aliwahi kushuhudia unyama aliotendewa, kutawishwa na kunyimwa uhuru
 • Si ajabu basi kwamba kila Maksudi alipojitokeza katika ndoto za Maimuna alijitokeza kama nyama mla mtu
 • Nyimbo za Maimuna nazo zina umuhimu unaokaribiana na ule wa ndoto, nyimbo hizi pia zinatanguliapale Maksudi anapojitokeza kumtafuta bintiye
 • Wimbo anaotumia Maimuna una simango na sumbulio inayochora picha nzima ya maovu ambayo jamii imemtendea
 • Maneno ya Maimuna katika nyimbo yanamsimanga na kumsuta Maksuudi kwasababu alimtia Maimuna kovu na dosari inayomkosesha na kumwondolea ukamilifu wa utu
 • Dosari alizonazo, madhila aliyo nayo na kovu alilo nalo ni matokeo ya tabia ya maingiliano na babake
 • Ndoto na nyimbo hizi zinaonyesha ukwasi wa kiumbuji wa mwandishi
 • Anazitumia ndoto hizi na nyimbo kifani na kiufundi , kama utangulizi na ubanishaji dhahiri wa mambo Fulani muhimu katika kazi
 • Ndoto na nyimbo zinazomwandaa msomaji na kumtangulizia na mikasa ielekeayo kutokea
 • Zinatumika pia kama mbinu rejeshi
 • Ndoto na nyimbo hizi pia zinatekeleza jukumu na kuwa kama vituo vya mapumziko katika mtiririko wa muumano wa masimulizi
 • Ndoto na nyimbo hizi ni mbinu ambayo mwandishi anaitumia kuivisha hadithi na masimulizi kwa jumla kutoka daraja moja hadi nyingine, kutoka hatua moja hadi nyingine  zozote 21×1=20

 

7.   Mkamia maji hayanywi, na akiyanywa humsakama  (al. 2)

 Ithibati – Maana – Akusudiaye kwa hamu kubwa kupata kitu fulani hukumbwa na pingamizi kiasi

 cha kukosa na hata kupata hasara.

  mifano

 (a) Bwana Maksundi

  Kukamia

 1. Kutaka mali
 • Alimfilisi mwanasururu
 • Alikuwa akiitisha pesa kutia sahihi stakabadhi kwa mfano kutoka kwa mzee Japu
 • Alipora mali ya umma
 • Alishiriki biashara haramu/magendo
 • Alitwaa ardhi ya via sera isivyo halali
 • Alitaka kuwa mbunge

 

 

(ii)  Kutaka anasa na starehe

 • Kwenda kwa kazija Juma la mwisho wa kila mwezi
 • Pamba kasri lake kwa fenicha za thamani kuu
 • Kushiriki ulevi

Sakama

 1. Kisasi na chuki kutoka kwa Bi. Farashuu,Biti Kocho na Kazija
 2. Ndoa yake kuvurugika na kuvunjika.
 3. Kutoroshwa kwa mwanawe Maimuna.
 4. Kufumanishwa na mwanawe Mussa
 5. Alimtaliki mwanasururu na Bi. Tamima
 6. Kesi ya jinai na kifungo jela cha miaka miwili
 7. Siri zake kufichuliwa hadharani na kazija
 8. Upweke na ukiwa baada ya kutorokwa na jamaa.
 9. Ugonjwa
 10. Kifo  (kukamia 3, sakama -3 = al.6)

 

 (b)  Maimuna (al. 4)

Kukamia

 1. Kutafuta uhuru/kuvunja utawa
 2. Kukubali kutoroshwa nyumbani na Biti kocho na Bi. Farashuu

 

Sakama

 1. Kutumiwa na wanaume na kutupwa
 2. Kusingiziwa kuwa mwizi kwa mama Jeni kuchukiwa na kufukuzwa
 3. Kupigania mwanamume (shoka) na kijakazi na kujeruhiwa vibaya.
 4. Kuzoroteka ki-afya na wanaume kwa mfano kushiriki ukahaba na James, na shoke (kamia al.2 , sakama al. 2= 04)

 

 (c) Bwana Zanga (al. 04)

Kamia

 1. Mali na utajiri – magari matatu, nyumba tatu
 2. (ii) Alitaka uongozi – ubunge

 

 sakama

 1. Wananchi wanamsuta kwa kutojali maslahi yao
 2. Anashikwa na askari na kushtakiwa kwa kosa la jinai
 3. Anakataliwa na wananchi katika uwanja wa uhuru
 4. Siri zake kufichuliwa hadharani na Kazija  (kamia al.2 , sakama al. 2= al 4)
 1. Mussa  (al.2)’

  Kamia

 1. Starehe na Anasa kwa Kazija

 Sakama

 1. Fumanizwa na babaake Bwana Maksundi kwa Kazija na kuaibika
 2. Kabwa koo, kunyongwa nusura afe
 3. Kutoroka nyumbani na kutengana na familia yake  (kamia al. 1, sakama al 1=al.2)

 

(e) Bi Farashuu  (al. 4)

Kamia

 • Kulipiza kisasi dhidi ya Bw. Maksundi
 • Kumtorosha Maimuna hadi kwa waendesha madanguro – Mama Jeni – pumziko
 • Tenganisha Bi Tamima na Bw. Maksundi
 • Tnganisha Bw. Maksundi na Bi Maimuna
 • Fumanisha Bi. Maksundi na Maimuna
 • Kujaribu kuvunja ndoa kati ya Maimuna na Kabi

 

Sakama

 1. Maimuna alimharibu kuolewa na mjukuu wake –Kabi
 2. Familia ya Bw. maksundi aliyeichukia kuungana na yake kupitia ndoa kati ya Kabi (mjukuye) na Maimuna bintiye Bw. Maksundi
 3. Alisikitika kwa kumsababishia Bwana Maksundi kifo chake

(Kamia al.2, Sakama al. 2= al. 4

 

8.  (a) Muktadha

 (i) Msemaji ni Inspekta Fadhili

 (ii) Alikuwa anaelezea Bw. Maksundi

 (iii) Wamo katika “kasri la watawa”  nyumba ya Bwana Maksundi

 (iv) Inspekta Fadhili alikuwa amekataa kuhongwa ili kuficha ushahidi wa kesi ya magendo

dhidi ya Bw. Maksuudi.

 (v) Bw. Maksundi alimweleza kuwa Inspekata Fadhili ana wakubwa wake (zozote 4 x1=ala.4)

 

 (b) Maovu ya Bw. Maksundi

(i) Unyang’anyi – alihalifu via Sera kutoka kwa Rembani kijana wa kihadharami.

– Alihalifu shamba, ng’ombe, pesa, na vyombo vya dhahabu kutoka kwa Mwanasururu

(ii) Ukatili:- Alizoea kupiga Mwanasururu na hata Bi. Tamima

 •  -Alimfukuza Bi. Tamima kando ya mapigo bila kujali hali yake. Alikuwa ndio

amejifungua mtoto

 •  Bi Tamima alifukuzwa bila mtoto wa siku moja tu

(iii) Hongo- alichukuwa shilingi 200/= kutoka kwa mzee Japu

 • Anakubaliana na wafidiwa nusu bin nusu ili kuwapa fidia licha ya kutokuwa halali

 (iv) Unafiki

 • Alidai kutetea haki za akina mama nawatoto wasichana dhidi ya kutawishwa. alitawisha Mwanasururu, Bi Tamima na Maimuna.
 • Ni muumini wa dini ya Kiislamu/shehe, lakini anamwendea mkewe/Bi. Tamima kinyume. ana vipusa nje/kazija.
 • Aliendeleza biashara za magendo na kuficha pesa nje ya nchi licha ya kudai kuwa mzalendo.

(v) Amejaa ubinafsi  

 • Alijitenga na wananchi na kujali wenye pesa pekee- Smith
 • Hakuruhusu mtu kuingia au kutoka kwake bila idhini yake
 • Alimfukuza nduguye Fadhii alipokataa kushirikiana naye kwa manufaa yake-ubunge
 • Alidhalisha wanawake kwa kuwaita paka, mbwa, maskini, viumbe vya kuliwa n.k

 (zozote 5×2 = al.10) (kutaja -1, maelezo/mfano -1 = ala. 2)

(c) Mafunzo ambayo Umma unajifunza kutokana na kisa kinachoza mazungumzo haya ni  (alama6)

(i) Mabadidliko yanahitaji ujasisir. Inspekta Fadhili anakataa kushiriki katika uhalifu na nduguye

Bw. maksundi

– Alikataa kuhongwa kuficha ushahidi wa uhalifu/kesi ya jinai dhidi ya Bw. Maksundi

(ii) Uwajibikaji kazini – Inspekta Fadhili alimkataza ndeugye Bw. Maksundi dhidi ya kujilimbikia

mali ambazo si za halali.

– Alihoji chanzo utajiri wa Maksundi akitilia Maanani mshahara wake

– Alikataa kuchukua hongo kama wafanyavyo wakubwa wake katika madai ya Maksundi

(c) – Utiifu na mazingatio ya sheria na kanuni za kazi

– Alimtia mbaroni Bw. Maksundi (nduguye) na Zanga

(d) Kuwa na msimamo thabiti

– Inspekta Fadhili alidumisha msimamo wake wa siasa za ujamaa kutetea wanyonge kutoka wakati wa ukoloni hadi sasa licha ya vishawishi vya pesa.

– Bw. Maksundi na Zanga walibadilika na kuwa mabepari makabaila  

 

9 .  (a) Anayesema ni Bw. Maksundi

  Akimwambia Inspekta kadhili

  Wakiwa nyumbani kwa Bw. Maksundi.

 Fadhili alikuwa amepata mwaliko kutoka kwa kakake

 

 (b) Mbinu

  Balagha – wewe nani hasa wakukutaa ?

  Mdokezo – Hapo ndipo ninapokuona mjinga …  (2×1=2)

 

 (c) Sifa nne za mzungumzaji – maksundi

  (i) Mkatili

– Anampokonya Mwanasururu mali na kumtaliki

    Kumtawisha mkewe na bintiye

-Kumchapa mkewe na kumetenganisha na kitoto chake

 (ii) Mwepesi wa hasira

  Hasira zinampanda kwa haraka pale anapokuta kwake bado kwawaka taa usiku wa manane

 (iii) Mzinifu/mkware

 • Yeye ni mteja wa Kazija ambaye ni kahaba

 

 (iv) Mfisadi

 • Anakabiliwa na shtaka la ufisadi na kufungwa jela
 • Mazungumzo yake na Mr. Smith yanalenga ufisadi
 • Ametajirika kwa haraka

 (v) mbinafsi

 (vi) Mnafiki- Anapoenda kwa kazija ingawa anajulisha kwake kwamba anaenda kufanya

maombi kwa kaburi la shehe wake

 (vii) Mpenda anasa – Kila mwezi anajipa wiki nzima ya kwenda kujistarehesha kwa kazija

 (d) Maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo

  (i) ufisadi – Maksuudi alitaka kumhonga Inspekta Fadhili afiche habari kuhusu kesi ya

ufisadi iliyokuwa ikimkabili

  (ii) Uongozi mbaya – Maksundi alitrajia kugombea kiti cha ubunge, kwa hivyo alitaka

kesi ya ufisadi iliyomkabili isijulikane na wananchi. Kwani huenda

ikamharibia nafasi ya kuibuka mshindi

(iii)Kutoajibika – Maksuudi alitaka kutumia mamlaka na uwezo wake kuficha uozo alio nao

 

10.  UOZO

 Ukahaba

–  Kazija alishiriki ukahaba pale kwake

 • Aliwakaribisha wanaume na hata kuwalewesha k.m. Musa, Maksuudi
 • Mama Jeni na Biti Sururu wanashiriki na kukuza madanguro. Wanatumia wasichana wadogo kama vitega uchumi vyao
 • Wanawanasa wanaume kama James na Shoka ili kuwapoka pesa na wakati huo huo kuwaharibu wasichana na kuwakosesha maadili
 • Biti Sururu ameendeleza ukahaba, anampokea Maimuna, anawazungusha wanaume walevi kana kwamba anamnadi Shoka anaendeleza ukahaba kwa kuwa na macho ya nje

 

 (ii) ULEVI

 • Musa ni kijana mdogo, anajizamisha kwenye anasa ya ulevi. Katika hali hiyo anafoka kijinga na kumtusi Kazija
 • -Shoka alishiriki ulevi na kumaliza pesa zake na kuisahau jamaa yake
 • Maimuna anazidi kujidhuru afya yake kwa ulevi wa pombe kali. Ilimfanya akapoteza urembo wake
 • Mamake Kabi (Mwanasururu) katika hali ya ulevi wake anajaribu kumshurutisha mwanawe kutenda ‘maovu’
 • Walevi ni kama Manda walioshiriki kwa Biti Surru. Badala ya kuwakanya na kuwatenganisha kijakazi na Maimuna waliwachochea wapigane zaidi

 

 (iii) KISASI

 • Hali ya kulipiza ubaya uliofanyiwa mtu mwingine. Wanaoshiriki ni Kazija, Maksundi – kutenganisha familia yake
 • – Kazija amepanga njama ya kumfumanisha Bwana Maksundi na manaye Musa wote wakija kwa shughuli za ukahaba
 • Bi Farashuu na Biti Kocho wanafaulu kutenganisha familia ya Bwana Maksundi zaidi kwa kumtorosha Maimuna nyumbani kwao
 • Bi Kazija kumwangusha Maksundi kisiasa pale uwanjani wa Uhuru. Anapopata kusema, anamchambua Bw. Maksundi kama mtu ovyo aliyeshindwa kuendesha nyumba yake, mnyang’anyi, na aliyesababisha kifo cha mke wake wa kwanza.
 • Katka uwanja wa Uhuru, umati unataka kulipiza kisasi dhidi ya Bwana Maksundi ingawa mpango huu unatibuliwa na Inspekta Fadhili anapowaka moto na kupelekwa kortini

 

(iv) UFISADI

 • Ni kitendo cha kupokea hongo ili kumtendea mtu jambo fulani
 • Baada ya uhuru, Bwana Maksuudi alipata cheo cha mkuu wa wilaya alitumia kujitajirisha .
 • Pia alipokuwa mkurugenzi wa shirika la bima la Taifa
 • Bw. Maksuudi alimtaliki, Mwanasururu ili apate fursa ya kupora mali yake aliyoachiwa kama urithi na babake
 • Mazungumzo ya Bw. Maksuundi na Mr.smith inaonyesha dhahiri kuwa wanazungumzia swala la ufisadi ambako wangawana pesa nusu bin nusu
 • – Ushawishi wa Bw. Maksuudi kwa Inspekta Fadhili ili afiche vitendo vyake vya kifisadi

 

 (vi) UNYANYASAJI WA WANAWAKE (UKATILI)

– Bi Tamima na Maimuna wanatawishwa nyumbani na Bw. Maksuudi

Bi Tamima anachapwa akiwa angali na tumbo bichi/bado tu ya kujifungua

Biti Kocho na Bi Farashuu wanamtorosha Maimuna nyumbani kwao wakifahamu tosha kuwa nia yao ni kumkaribia maisha

Mwanasururu kwa kuteswa na kuchapwa, na kunyang’anywa urithi alioachiwa na babake na Bw. Maksuudi

Bi. Selume anadhulumiwa na mumewe Shoka kwa kuachiwa aikimu familia yao pekee. – Mumewe pia anatembea na wanawake wengine nje ya ndoa k.m Maimuna na Kijakazi.

 

(v) UONEVU WA KITABAKA

– Wenye mali waliishi katika mita ya kifahari yenye taa na barabara nzuri kama Liwanzoni na  Pumziko

Tabaka la chini liliishi katika vibanda vibovu penye mitaro michafu, mavumbi, bila taa, wala barabara k.m. alikoishi Biti Sururu

 

(vii) UONEVU WA KISIASA
– Wakolon wajerumani waliwatesa wapigania ukombozi mfano ; Sakamu ya wazalendo inaonyesha viungo vilivyokatwa katikati

– Baada ya uhuru uonevu huu unaendelezwa na Maksuudi na Zanga. Wanajilimbikizia mali, majumba , magari na fedha  (zozote 5×4=20)

 

11  Akakumbuka ubeti wa shairi alilotunga karibuni katika jumla ya mashairi aliyoyakusanya

  katika kitabu alichokiita kilio cha wanyonge

 a) Muktadha

 1. Haya ni maneno ya mwandishi
 2. Anaeleza yalimpitikia inspekta Fadhili mawazoni
 3. Inspekta Fadhili yumo ukumbini mwa kakake Maksudi ambamo Maksudi amemwalika
 4. Fadhili aliwasili na akamkuta Maksudi akijizoeza kutoa hotuba, na Fadhili akashangazwa na zana zilizokuwa pale nyumbani
 5. Ndipo akakumbuka ubeti wa shairi alilotunga  Zozote 4×1=4

b) Ujumbe katika shairi

 1. Wanyonge wanalima lakini hawapati mavuno ya kazi yao
 2. Wafanya kazi walifanya kazi sana lakini walilala njaa
 3. Wanyonge na wafanya kazi walikumbwa na maradhi
 4. Walikosa elimu wakabaki ujingani
 5. Waliahidiwa shibe, matibabu na elimu na watetezi wa uhuru
 6. Lakini uhuru ulipopatikana hali yao haikubadilika
 7. Ukoloni uliondoka Afrika lakini kuacha ukolono mamboleo  TUZA Zozote 6×1=6

Onyesha Inspekta Fadhili anavyotofautiana na kakae maksudi

 1. Maksudi ni mfisadi anayejitajirisha na mali ya uma- Fadhili ni mwadhilifu na anapigana na ufisadi
 2. Maksudi anaonelea kuwa tofauti zao ni za kisiasa- Fadhili anashikilia kuwa hawafai kuwa na siasa tofauti kwasababu siasa ya nchi yao ni moja
 3. Maksudi anataka fadhili amfichilie zile habari za kesi ya magendo aliyo nayo isitoke na kumharibia kura. Fadhili anakataa kudidimisha kesi hii kwa madai kuwa yeye ni mtumishi wa umma aliyeaminiwa kulinda uhuru, haki na usalama
 4. Maksudi ana ubinafsi wa kujilimbikizia mali- Fadhili hapendezewi na ubinafsi huu ni mtumishi wa umma
 5. Maksudi anajaribu kumhonga Fadhili ili afiche habari ya kesi ya magendo – fadhili anakataa hongo yake
 6. Maksudi anamwona Fadhili kuwa mjinga kwa kukataa hongo ilhali polisi wengine wanaichukua – Fadhili anashikilia kuikataa hongo
 7. Maksudi anaamini kuwa atashinda kiti cha ubunge anachogombania- Fadhili anamweleza kuwa hawezi kushinda kwasababu watu wamechoka kudanganywa na wanafiki kama yeye
 8. Maksudi ni mnafiki- alijifanya mzuri, mcha Mungu na mtetezi wa wanyonge ili apewe cheo kisha ajitajirishe
 9. Fadhili ni mkweli na mpenda usawa na ndio sababu alipendwa na umma aliyoifanyia kazi
 10. Maksudi alichukuliwa na watu kwasababu alizingatia haki na usawa  Zozote 10×1=10

 

12.   Mwanamke kama kikwazo cha ukombozi wake

 1. Bi Farashuu anataka kulipiza kisasi kwa kifo cha bintiye (mwanasururu) kwa Bw. Maksudi. Badala ya kukabiliana na Maksudi mwenyewe, anawaharibia Maimuna na mamke maisha yao
 2. Binti Kocho, kwa ushirika na Bi Farashuu, anamchochea maimuna kutoroka kwao huku akiwa na nia ya kumharibia maisha
 3. Maimuna anapotorokea kwa Bi.Farashuu, badala ya Farashuu kumsaisia, anamsafirisha hadi kwa mama Jeni akiwa na nia ya kumwingiza katika maisha ya ukahaba
 4. Badala ya mama Jeni kama mwanamke aliyekomaa kumpa malezi mema, Maimuna ambaye yungali mchanga, anamtafutia wanaume wa kufanya naye mapenzi huku yeye mwenyewe akinufaika kwa malipo anayopewa
 5. Mama Jeni anawatumia wasichana wengine wachanga kama vile Dora kuwashirikisha ukahaba
 6. Maimuna anapotorokea kwa binti Sururu hapati afueni. Licha ya binti sururu kuendeleza ukahaba, anamfanya Maimuna kuanza kutumia pombe ambayo inamwathiri hata zaidi
 7. Kijakazi kumwonea wivu Maimuna na kumsengenya badala ya kumwona kama mwenzake katika maisha magumu ya ukahaba. Baadaye wanapigana na kuumizana vibaya
 8. Kabi anapotaka kumuoa Maimuna, Bi. Farashuu anapinga wazo hili licha ya kuwa ndiye aliyemfanya maimuna kuwa kahaba
 9. Bi. Tamima hatetei haki yake nay a bintiye. Anakubali kudhibitiwa na mumewe bila pingamizi na hata kufikia kiwango cha kumpigia magoti na kuomba msamaha licha ya kuwa hajatenda kosa lolote
 10. Bi. Kazija anakubali kutumiwa na Bi. Farashuu kulipiza kisasi kwa Bw. Maksudi. Licha ya kuwa anachukia wanaume, angetumia njia nyingine ya kujipatia pato badala ya kufanya ukahaba
 11. Selume hasaidiwi na mumewe Shoka kuikimu familia yao. Selume anafanya juu chini kutafuta chakula. Wakigombana, Shoka hutoweka nyumbani kwa muda wa wiki nzima hadi Selume amtafute. Selume angejikomboa kutokana na ndoa iliyoegemea upande mmoja

Kazija kumchukua maksudi ilhali anajua kuwa ana bibi na watoto. Anamharibia maisha ya familia yake

 

13.  (a)  – Yalisemwa na Kazija.

– Anamwambia Musa.

– Musa alikuwa mlevi huku akiropokwa kuhusu wanawake ndipo Kazija akamjibu kwa hasira.

– Kazija alikuwa amepanga njama ya kuwakutanisha Musa na babake.  (4 x 1= al. 4)

(b)  – Mwanamke hutumika kukidhi matakwa ya wanaume kama Kazija.

– Kupigwa vibaya kama Bi. Tamima na Mwanasururu walivyopigwa na Maksuudi

– Mwanamke kutalikiwa vivi hivi bila sababu k.m. Tamima na Mwanasururu.

– Wanawake kutawishwa na kunyimwa uhuru k.m. Tamima na Maimuna.

– Mwanamke kutumikishwa kikahaba k.m. Maimuna na wengine.

– Kuhiniwa mali kwa mwanasururu na Farashuu.

– Kubaguliwa hata baada ya uhuru – kuendelea kunyimwa usawa hasa ile sanamu ya mashujaa.

– Wasichana wa Farashuu kuoka mikate hadi usiku wa manane.   (Hoja zozote 4×2= al.

 

(c)- Kazija achukua hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya maksuudi.

– Anamweleza maksuudi uovu wake na kumuonya.

– Biti Kocho aonyesha kwamba umoja wao utawaangusha waovu kama Maksuudi ili

wajikomboe.

– Maimuna ajijasirisha na kutoka nje ya kasri.

– Maimuna aamua kuachana na ukahaba.

– Biti Sururu anajihusisha na uuzaji wa vileo kuibadilisha hali yake ya kiuchumi.

– Farashuu akazania ulipizaji kisasi kwa ajili ya mali yake ili kumkomesha maksuudi.

– Farashuu anashughulika na uokaji wa mikate ya kuuza.

– Biti Kocho ana mpango wa kupata kiwanja na kujenga /anakataa utumwa wa maksuudi.

– Mke wa japu anaenda kwa mkuu wa Wilaya kupata hati ya umiliki wa ardhi.

– Selume ang’ang’ania kuwakimu watoto na anamsuta mumewe shoka kwe uzohali.

 

14.  (a) MAKSUUDI

 • Anajutia kumfukuza bibiye Tamima
 • Ajutia unyama aliomtendea Mwanasururu
 • Ajutia kumtawisha Maimuna na Tamima
 • Ajutia unyang’anyi alioutendea Umma
 • Ajutia alivyotengana na mwanawe Musa
 • Ajutia kujilimbukizia mali
 • Ajutia kushiriki ufisadi
 • Ajutia mateso ya jela yaliyomponza hata akawa kilema
 • Ajutia kupoteza muda katika jela
 • Ajutia hali ya upweke/ukiwa
 • Ajutia kupoteza mali yake
 • Ajutia kuwadhulumu watu wengine (zozote 5×2=al. 10)

 

 (b) MAIMUNA anajutia;-

 • Kutoroka kwao
 • Hali yake ya ukahaba
 • Kutengana na aila yake
 • Kupapia uhuru ambao umemuumiza
 • Kifo cha babake kabla ya kutangamana naye
 • Mateso ya mamake
 • Kitendo cha kuolewa na Kabi (zozote 5×2=al. 10)

 

15.  – Mwanamke anatawaliwa na mwanaume aghalabu hupigwa na kunyanyswa mf. Bi Tamima na Mwanasururu.

– Mwanamke kama pambo na chombo cha starehe. mf. Kazija na wasichana wengine.

– Mwanamke hana sauti ndani ya familia, m.f. Bi Tamima.

– Mwanamke anatengwa na jamii katika masuala ya kisiasa na uongozi

– Mwanamke hapewi fursa ya kustosha katika masuala ya elimu mf. Maimuna

– Wasichana hawana ujasiri wa kuwashirikisha wazazi katika masuala yanayowahusu hasa ya

kimapenzi k.mf Maimuna anashindwa kumweleza Tamima hamu yake ya kutoka nje.

-Mwanamke anawajibika katika kuikimu familia hasa watoto kwa mfano zingatia Selume

anavyojitahidi kwa kila njia kutunza familia yake.

– Wanawake ndio wanafanya kazi zote za nyumbani : Rejelea kwa watumishi wa Tamima na

wasichana waokaji wa mikate kwa Farashuu

 

16.  (a) Maneno haya anayasema Bi farashuu na anamwambia mjukuu wake Kati. alikuwa

nyumbani kwa Kabi.

 

 (b)   – Anayezugumzia ni mchumba wa mjukuu wake, anaitwa maimuna .

 – Babake alimtesa mtoto wa Bi. Farashuu

 – Farashuu ana hasira na familia ya Maksundi akiwemo Maimuna

 – Hakutaka aonekane kwake akiwa salama.

 – Maimuna alikuwa chakaramu – asiyestahili kuolewa na mjukuu wake.

 – Familia ya Masuudi ilikwisha hathirika na kusambaritika

 (c)  – Takriri – neno mtoto

 – Mdokezo ….

 – Msemo – Hana siri wala fasiri

 – Swali la balagha – dondoo lenyewe

 (d) Amekuja kutambulishwa kwa mchumba wa mjukuwe Kabi

 (e) – Kabi alitoka kuwaacha nynanyake na Maimuna

 • Maimuna na Farashuu walibishana kuhusu matendo yake
 • Baadaye wakatambua mkosa yao kisha wakasameheana
 • Farashuu akawabariki Kabi na wakasameheana
 • Ndoa ikafungwa ya Kabi na Maimuna Wakahama

 

17.  (a) (i) Maneno ya Bi Farashuu

(ii) Anamwambia Biti Kocho

(iii) Ni nyumbani kwa Bi Farashuu – Madingo poromoko

   (iv) Farashuu alishangaa sababu ya Biti Kocho kuenda kumchukua ili akamsaidie

mke wa   tajiri wao

(v) Biti Kocho alimwambia haya ni kati ya njama ya kutaka kumtorosha Maimuna

  (vi) Farashuu alifurahi alipotambua kuwa lengo la Biti Kocho ni kumsaidia kulipiza

kisasi Maksundi.

(vii) Kwa uchungu mwingi alieleza maovu ya Maksundi na unafiki wake ndipo akasema

maneno haya  (8 x 1= al. 8)

(b) (i) Kazija alifanya njama ya kumfumanisha Mussa na babake.

(ii) Alimpa Mussa miadi ya kufika saa tatu na maksundi akaambiwa afike saa sita.

(iii) Maksundi alipokutana na Mussa alimpiga nusura amwue.

(iv) Mussa alilazimika kuchopeka vidole vyake kwenye macho ya babake na akafaulu kutoroka.

(v) Alipoachiliwa hakuonekana tena nyumbani kwao a hata kwa Kazija – alitengana na babake.

(vi) Alizomewa na Kazija na akalazimika kurudi nyumbani usiku wa manane kwa miguu.

(vii) Haya yote yalipangwa na Farashuu ili kukamilisha kisasi cha mateso aliyofanyiwa

Mwanasururu na Maksundi.

(viii) Usiku huo huo Maimuna alitoroka kwao na kwenda kumtafutia mamake mkunga

(anakaidi amri ya kutoka nje)

(ix) Kisha baada ya kurudi nyumbani usiku huo, alitoroka kwao ili kutafuta uhuru baada ya

kuonja uhuru wa siku moja.

(x) Maksundi anaporudi anamlaumu Tamina na kumpiga sana kisha kumtaliki.

(xi) Hatimaye Kazija anamfedhehesha katika uwanja wa uhuru

(xii) Baadaye anamtumikia kufungocha miaka miwili baada ya kupatikana na makosa ya jinai

 

(c)   (i) Mwenye bidii

(ii) Mwenye kisasi

(iii) Katili

(iv) Mnafiki

   (v) Mkarimu

   (vi) Mshirikina

(vii) Msiri

   (viii) Msamehevu

   (ix) Mpole/Mtulivu

   (x) Mwenye majuto

   (xi) Mwenye huruma  (4×1= 4)

18.  (i) Kazija kuchukia wanaume ilhali anajipamba kwa sababu yao.

 (ii) Maksundi alipofika kwake na kusikia sauti ya kitoto anakasirika badala ya kufurahi

(iii) Biti Kocho anamwambia maimuna “mjukuu wangu, dunia furahi” usemi huu ni kinyume na nia yake iliyokuwa kumtia Maimuna matatani.

 (iv) Azimio la Farashuu kuenda kumtafuta Tamina ili ashiriki katika poso ya Maimuna ni

Kinaya.

Hapoawali Farashuu alimpeleka Maimuna pumziko ili wawili hawa wasiweze kukutana

  (v) Matokeo ya Maksundi huku Rumbalola ni kinyume na matarajio yake. Alitaka kumuona

Maimuna lakini badala yake anapigwa vibaya.

(vi) Kinaya kwa Mama Jeni anapomhoji Maimuna na kudai kutojua kilichokuwa kikiendelea.

Yeye ndiye aliyemfungia kwa chumba kimoja na James.

  (vii) Kinaya kwa Maksundi na Zanga kuomba kura na kuwaambia kuwa wanahitaji viongozi

kama wao na wao ni fisadi wadhalimu.

 (viii) Kinaya Maimuna anapopewa chumba kibovu chenye mazingira mabaya na atarajiwe

apate usingizi mzito.

  (ix) Kinaya Maksundi anapojihusisha na matendo mabaya ilhali yeye ni mtu wa dini.

 (x) Kinaya Farashuu anaposema kuwa atampeleka Maimuna pumziko akapumzike.

Hatumwoni akipumzika na badala yake masabiu yake yanazidi.

  (xi) Taswira ya shoka haipendezi lakini mwandishi asema ” juu ya urembo huu kupambwa”

 (xii) Maimuna anapotoroka anatarajia maisha ya furaha na uhuru. Badala yake anaishi

maisha duni

 (xiii) Maimuna kulalamika wanakandamizwa ilhali wao wenywe wanakandamiza wenzao.

  (xiv) Maimuna alikuwa akichukiwa sana na Bi Farashuu mwishoni anaolewa na mjukuu

wake Kabi.

  (xv) Maimuna huishi uwazoni na mamake lakini hawapati liwazo lolote kutokana na dhuluma

za Bw. Maksundi.

 (xvi) Maimuna maksundi kupigania uhuru kwa dhati lakini nia yake ni kupata cheo baadaye

ili ajinufaishe.

  (xvii) Maksundi ni shehe lakini vitendo vyake ni vya uzinzi, ufisadi na dhuluma (al.10 x2= 20)

 

19.

 • Wanaume wanapenda sana kujiweka mbele katika mambo ya elimu na kuwabagua wanawake
 • Kazi yote ya nyumbani inaachiwa mwanamke k.v. kupiga pasi, kupika, kuosha n.k. Mwanaume hasaidii kwa vyovyot
 • Mwanamke hushika mamba au huza, lakini mwanaume hazai
 • Mwanamke hapati kazi nzuri kama ile inayofanywa na mwanaume
 • Mwanaume aghalabu hutoa ahadi za uongo mfano Bwana maksudi kutochaguliwa na wanawake katika auchaguzi
 • Mwanaume ni fisadi mfano maksudi na washirika wake
 • Mwanaume kuwa na kasumba ya kuwa ukahaba hutendwa na wanawake lakini sivyo kwani hutendwa na wote – wake kwa waume
 • Mwanaume ni mlaghai mfano maksudi alimlaghai Bi. Sururu mali yake
 • Mwanaume hawajibiki ipasavyo mfano shoka
 • Mwanaume ni katili Hoja 10×2=20

20.

 • Utengano wa kifamilia – Maksudi atengana na familia yake.
 • Utengano wa kijinsia – wanawake wametengana na wanaume kupitia taasubi ya kiume
 • Utengano wa watawala na watawaliwa – Bwana Maksudi ametengana sana na watu anaowatawala mfano akiwa mkuu wa wilaya
 • Utengano wa kitabaka – mtajiri kwa maskini
 • Utengano unaotokana na kifo – Bi Tamina na kitoto chake kichanga
 • Utengano wa kimaadili – Mama Jeni anafanya biashara ya danguro  Zozote 5×4=20

 

21.  a)  – Haya ni maneno ya mwandishi

– Alikuwa akieleza kuhusu Bwana Maksudi alivyombadilika

– Alikuwa anamcha Mungu sasa  

 

 b)  – Mke na watoto wake walikuwa wametoroka

– Alikuwa mgonjwa

– Alikuwa mpweke

– Hakujua cha kufanyia mali yake

– Hakuweza kufikia mali yake

– Alikuwa amefungwa jela

– Hakuwa na rafiki

 c)  – Alikuwa mfisadi

– Ni katili

– Alishiriki ngono na wanawake wengi

– Alikuwa muuaji

 d) Tashhisi – Mshibe Mungu

Kutaja alama 1 Mifano alama 1

 

22.   Mambo anayoyakashifu mwandishi

 – Ufisadi

 – Ukahaba

 – Ulevi

 – Ukatili

 – Ubaguzi wa kitabaka

 – Utawishaji

 – Ulipizaji wa kisasi

 – Taasubi ya kiume

 – Dhuluma

 – Kutowajibika

 

23.  a) Muktadha

 1. Anayezungumza ni Bwana Maksudi
 2. Anazungumza na Mr. Smith kwa simu
 3. Mr.Smith ni mshirika wa Bwana Maksudi kibiashara
 4. Mazungumzo haya ya simu yanatokea nyumbani mwa Bwana Maksudi
 5. Inspekta Fadhili alikuwa amengojea sebuleni  (Alama 4×1=4)

 

  b) Ujumbe wa shairi la “Kilio cha mnyonge”

 1. Wakulima walilima lakini hawakuona faida yao
 2. Wafanyikazi walijibidisha kazini lakini walilala njaa
 3. Wao walikumbwa na magonjwa ya kila aina
 4. Watu walikumbwa na ujinga wa kila aina
 5. Ubaguzi ulikuwepo
 6. Bara la Afrika bado linatawaliwa kupitia mlango wa nyuma
 7. Ukoloni mamboleo wa kutoka nje na ndani (Uk 71 – 72) (Alama 6×1=6)

 

c) Uovu wa mzungumzaji

 1. Fisadi – mazumgumzo baina ya Maksudi na Smith alichukua shillingi mia 200 kutoka kwa mkewe mzee Japu. Nyumba na shamba kwa mpango wa siri
 2. Mnyang’anyi – alimdanganya mwanasururu
 3. Mwenye tama mali/ ubinafsi – hakujali yeyote haswa kama kiongozi. Alitumia cheo chake ili kujitajirisha
 4. Mnafiki – Alipigania uhuru akiwa na nia ya kuchukua nafasi hiyo kujirundikia mali
 5. Katili – Alimpiga mwanasururu na kumtaliki, Alimpiga Bi. Tamina akiwa na uchungu wa uzazi, Alimpiga Mussa nusura kumuua
 6. Msherati – Alikuwa na uhusiano wa nje na Kazija
 7. Kuwatisha – Aliwafungia Tamina na maimuna
 8. Msaliti – Alisaliti imani ya wananchi kwake. Aliwasaliti wanawake aliowaoa
 9. Mwenye dharau – Alidharau wanawake/ alidharauwanawake/ alidharau watu wa tabaka la chini
 10. Mwenye taasubi ya kiume/ ubabedume, Aliamini mwanamke ni mwepesi ni mwepesi wa kuliwa , kuwatisha wanawake, kuwapiga wanawake
 11. Mwenye kiburi/ dharau
 12. Mgomvi – aligombana na Tamina, Mwanasururu, Mussa na Fadhili  Zozote 10×1=10

 

24.  a) Muktadha

 1. Msemaji ni mama Jeni
 2. Akimwambia maimuna
 3. Walikuwa kwenye mkahawa wa café Afrique
 4. Walikuwa wameenda pumziko ili Maimuna anunuliwe nguo 4×1= 4

 

  b) Sifa za aliyeelekezwa maneno

 • Mwenye kisasi – ana kisasi kwa babake kwa kumtawisha
 • Mwepesi wa hamaki – anakasirishwa na maneno ya kijakazi, pia anamsimanga James
 • Mpenda anasa (Uroda) Anaishi maisha ya anasa
 • Mkosa tahadhari – hajali hatari inayoweza kumkabili baada ya kutoroka nyumbani kwao
 • Msamehevu – anamsamehe babke na Farashuu  Zozote 4×2=8

 

  c) Mabadiliko yaliyotokea

 1. Familia ya Maksudi inabadilika baada ya usiku wa fumanizi
 2. Maksudi anapanda cheo, anakuwa mwanasiasa, anafungwa jela, afya yake inadhoofika
 3. Kiburi cha maksudi kinayeyuka, utajiri unamkwepa kisha anathamini utu
 4. Anawathamini watoto na mke wake kasha kuanza kuwatafuta
 5. Mussa anawacha tabia ya ukware anazingatia masomo na kuwa daktari
 6. Uhasama wa Mussa dhidi ya babake unaisha kasha anamhudumia hospitalini
 7. Mussa anamuoa Sihaba kinyume cha matakwa ya babke
 8. Mwanasururu ananyang’anywa mali yote na kutalikiwa akiwa mlevi, mwendawazimu na akafa
 9. Maimuna anatoroka nyumba kubwa na kuwa kahaba na kujiingiza na ulevi
 10. Maimuna anakuwa mwimbaji hodari wa nyimbo na hataki
 11. Kuna mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kimazingira n.k Zozote 8×1=8

 


 
Share this:


EcoleBooks | Maswali ya RIWAYA: UTENGANO: S.A. MOHAMMED na Majibu Yake

subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*